Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumanne 29.10.2024
Kocha wa Sporting Ruben Amorim amekubali kuwa meneja ajaye wa Manchester United kufuatia kufukuzwa kwa Erik ten Hag siku ya Jumatatu. (Manchester Evening News),
Meneja wa zamani wa Borussia Dortmund Edin Terzic ndiye anayelengwa na Manchester United, baada ya Thomas Tuchel kuteuliwa kuwa kocha wa England. (Sun,
Arsenal wanatathmini dau la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Brentford raia wa Cameroon, Bryan Mbeumo, 25. (Football Insider)
Liverpool wanafikiria kumnunua beki wa kati wa Nottingham Forest wa Brazil Murillo, 22, lakini wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea. (TeamTalks)
Meneja wa Brentford Thomas Frank ni miongoni mwa wachezaji ambao Manchester United wanafikiria kuchukua nafasi ya Ten Hag. (ESPN)
The Red Devils wamebainisha orodha fupi ya wasimamizi watano ambao wanaweza kuchukua nafasi ya Ten Hag. (Sky Sports)
United haijaondoa uwezekano wa kumtafuta Ole Gunnar Solskjaer, huku klabu hiyo ikiwekewa vikwazo vya kuteua kocha huru. (Manchester Evening News)
Mshambulizi wa Uswidi Alexander Isak, 25, anaweza kushinikiza kuondoka Newcastle United katika dirisha dogo la usajili la majira ya joto. (Football Insider),
Liverpool wanamfuatilia kiungo wa kati wa Benfica na Uturuki Orkun Kokcu, 23. (Rekodi -In Portuguese).
Arsenal wamekataa mpango wa Palmeiras kutaka kumsajili mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 27. (ESPN).
Manchester United wanavutiwa na kiungo wa kati wa Sporting Mreno mwenye umri wa miaka 17 Geovany Quenda. (A Bola – In Portuguese)
Nottingham Forest imeanza mazungumzo na mshambuliaji wa New Zealand Chris Wood mwenye umri wa miaka 32 kuhusu kandarasi mpya. (Telegraph – Subscription Required),
Mshambulizi wa Guinea-Bissau Beto, 26, anafikiria kuondoka Everton ili kutafuta soka ya kuchezea kikosi cha kwanza. (Football Insider)
Imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla