Darya Dugina ni nani?

Darya Dugina

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Kifo cha Darya Dugina, binti wa miaka 29 wa mwana itikadi za kitaifa wa Urusi Alexander Dugin, kilihamisha mwelekeo wa vita vya Ukraine kutoka uwanja wa vita hadi vitongoji vya Moscow, ambapo gari la Dugina lililipuliwa, na kumuua papo hapo.

Idara ya Usalama ya Urusi (FSB) ilisema Ukraine ndiyo iliyohusika na mauaji hayo na mshukiwa – anadaiwa kuwa raia wa Ukraine, alimfuata Dugina na babake kwenye tamasha katika mkoa wa Moscow na hatimaye kutekeleza shambulio hilo lakini baadaye alitorokea nchi jirani ya Estonia, kabla ya kizuiliwa.

Hata hivyo, maafisa wa Ukraine wamekejeli nadharia hii na kukana kuhusika, huku mshauri wa rais Mykhailo Podolyak akielezea taarifa ya FSB ya mauaji hayo kama "propaganda zilizobuniwa na Urusi".

Badala yake, Kyiv inasema mapigano ya kisiasa ya ndani ya Urusi ndiyo yalisababisha shambulio hilo.

Rais Putin alilaani "uhalifu huo mbaya na wa kikatili" na kumtunuku Bi Dugina heshima ya raia ya ujasiri. Siku ya Jumanne katika ibada ya kumuaga mjini Moscow baba yake mwenye umri wa miaka 60 Alexander Dugin alimpongeza akisema: "Alikufa kwa ajili ya Urusi. kwenye mstari wa mbele. Na mstari wa mbele uko hapa."

Yeye ni nani?

Darya Dugina

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Dugina alijitokeza kwenye Runinga ya Urusi akionyesha maoni yanayopinga Ukraine

Darya Dugina hakuwa jina kubwa nchini Urusi lakini yeye na haswa baba yake walikuwa na uwepo mkubwa kwenye vyombo vya habari, wakitoa maneno ya kupinga Ukraine na dhidi ya wanabropaganda wa nchi za magharibi.

Baba yake, Alexander, wakati mwingine huelezewa kama "ubongo wa Putin" na kwa muda mrefu ameelezea falsafa dhidi ya Magharibi, ambayo imemfanya kuwa mtu muhimu huko Moscow - licha ya kutokuwa na wadhifa wowote wa kisiasa.

Alikuwa mwanzilishi wa wa kinachojulikana kama harakati za Eurasian, maoni yake ni maarufu miongoni mwa wasomi wa kisiasa wa Urusi.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kiini cha nadharia ya jiografia ya Dugin ni kwamba dhamira ya Urusi ni kupinga ubabe wa Marekani duniani, kwa msaada wa Iran, na vyama vinavyounga mkono ajenda za ulaya.

Wengi nchini Urusi wanaamini kwamba Alexander Dugin ndiye alikuwa mlengwa halisi wa shambulio hilo la mwishoni mwa juma, kwani alikusudiwa kusafiri kwa gari moja na binti yake lakini akabadili nia dakika za mwisho.

Wakati huo huo Darya mwenyewe alikuwa sauti hai ya maoni ya baba yake, mgeni wa mara kwa mara kwenye vituo vingi vya Runinga vya Urusi na YouTube.

Pia aliandika kwa idadi ya machapisho yanayoiunga mkono serikali na alikuwa akifanya kazi kwenye mitandao ya kijamii.

Pamoja na itikadi za baba yake, alizungumza juu ya kurejesha "Nafasi Kubwa" ya Urusi kote Eurasia, akianza na umoja wa Slavic wa Mashariki, unaojumuisha Urusi, Ukraine na Belarus.

Dugina aliyezaliwa mwaka 1992, alijiunga na idara ya filosofia ya Chuo Kikuu cha kifahari katika Jimbo la Moscow.

Vyombo vya habari vya Urusi vinawanukuu waalimu wake ambao wanasema alipata sifa kama mwanafunzi mwenye kipawa na akili.

Mwaka 2012 hadi 2013 alijiunga na Chuo Kikuu cha Bordeaux III nchini Ufaransa, ambako alijikita katika falsafa ya mwanafilosofia wa zamani wa Ugiriki Plato, ambaye kazi zake zilikuwa mada ya tasnifu yake ya mwisho na pia lengo la utafiti wake wa uzamili.

Baba mzalendo

Alexander Dugin

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alexander Dugin anasifiwa kwa kuunda mtazamo wa ulimwengu wa Rais Vladimir Putin

Wakati huo baba ya Darya, ambaye tayari anajulikana sana kwa itikadi yake ya utaifa na mpinzani wa Ukraine, alikua maarufu zaidi.

Mnamo 2014 video iliibuka ikimuonyesha Bw Dugin akisema kwa Kirusi: "Nadhani, kuua, kuua na kuua [Waukraine], hakuwezi kuwa na mazungumzo mengine yoyote."

Maoni hayo yalikasirisha Warusi wengi - ombi la kutaka aondolewe katika nafasi yake kama mkuu wa idara ya sosholojia na uhusiano wa kimataifa katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Moscow lilitiwa saini na zaidi ya watu 10,000, na kusababisha kufukuzwa kwake.

Mnamo 2015 aliwekewa vikwazo na Marekani na Canada kwa jukumu lake katika unyakuzi wa Crimea.

Muda mfupi baadaye, marafiki zake wanasema, Darya Dugina alivutiwa na dini ya Othodoksi ya Urusi, ambayo ilishangaza baadhi ya marafiki zake wa Moscowwenye misimamo ya kimagharibi na urafiki kupoa.

"Polepole akawa mfuasi wa mawazo ya baba yake na hapo ykakatiza mawasiliana," - alielezea rafiki mmoja, aliyenukuliwa na tovuti ya Meduza.

Kuunga mkono unamizi wa Ukraine

Mwishoni mwa miaka ya 2010, Darya Dugina alianza kuonekana kwenye vituo mbali mbali za Televisheni za Urusi, na pia kuandika kwenye wavuti zinazounga mkono serikali, mara nyingi akitoa maoni juu ya siasa za Uropa na kuelezea kuunga mkono nguvu za kisiasa alizoelezea kama "haki mpya" na kutabiri ushindi wao dhidi ya waliberali.

Mnamo mwaka wa 2018 katika tahariri ya Urusi leo (RT), vyombo vya habari vinavyoeneza propaganda ya serikali ya Urusi, Dugina aliandika juu ya kifo cha Emmanuel Macron kama rais wa Ufaransa, na alionyesha kumuunga mkono sana mwanasiasa wa mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen.

Wakati wa uchaguzi wa rais wa Ufaransa mnamo 2017 na 2022 aliandika juu ya matarajio yake ya ushindi wa Le Pen.

Katika maonyesho hayo yote ya vyombo vya habari, Dugina alitumia jina la kalamu "Platonova", inasemekana lilihusishwa na mapenzi yake kwa mwanafalsafa Plato wa Ugiriki ya Kale.

Wachunguzi wa Urusi wakiwa kwenye eneo la mlipuko wa gari

Chanzo cha picha, Kamati ya Uchunguzi ya Shirikisho la Urusi

Maelezo ya picha, Wachunguzi wa Urusi wakiwa kwenye eneo la mlipuko wa gari

Novemba mwaka jana, baada ya Urusi kuanza kupeleka askari wake kwenye mpaka na Ukraine, Dugina alielezea Ukraine kama "mpaka wa usafi" kati ya Urusi na nchi za Magharibi.

Baada ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi, Dugina aliunga mkono kwa kauli moja, akiandika kwamba ilikuwa "ufahamu wa ufalme".

Mnamo Julai aliwekwa kwenye orodha Uingereza ya watu waliowekewa vikwazo kama "mchangiaji wa mara kwa mara wa habari potofu kuhusiana na Ukraine".

Katikati ya mwezi wa Juni alitembelea viwanda vya chuma vya Azovstal mara baada ya jiji lililozingirwa kwa muda mrefu la Mariupol kudhibitiwa kikamilifu na vikosi vya Urusi.

Kabla ya kuuawa kwake, alikuwa akishirikiana na shirika la mrengo wa kulia la uchapishaji la Kirusi "The Black Hundred" kwenye uchapishaji ujao wa "Kitabu cha Z", kilichoelezwa na wachapishaji kama "mkusanyiko wa shuhuda na hadithi za washiriki na mashahidi".

Herufi "Z" ikawa ishara ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, huku magari ya kijeshi na sare za wanajeshi zikiwa na herufi hiyo katika kipindi chote cha miezi sita iliyopita.