MLRS: Kwanini Ukraine inazitaka 'kwa udi na uvumba' Silaha hizi?

Chanzo cha picha, DEFENSE.GO
Siku ya Jumamosi, Rais Volodymyr Zelensky alitoa wito kwa washirika yanayotoa silaha Kyiv wasiogope kuamua kukabidhi mifumo ya makombora ya MLRS kwa Ukraine. Hii sio mara ya kwanza kwa maafisa wa ngazi ya juu wa Ukraine kusisitiza juu ya silaha hizi na kukosoa mataifa ya magharibi kwa kutozitoa kwa Ukraine.
Siku moja kabla, mkuu wa ofisi ya rais, Andriy Yermak, alizungumza juu ya haja ya mifumo hii."Suala la kuipa Ukraine mifumo ya makombora ya M142 HIMARS na M270 MLRS ni muhimu sana," Zaluzhny alisema wakati huo.
Ni mifumo inayopaswa kusaidia Ukraine kukabiliana na Urusi. Hata hivyo, Ukraine bado haijapokea taarifa hizo. Wiki hii, Politico iliripoti, ikinukuu vyanzo vyake, kwamba utawala wa Biden haukuwa na haraka ya kuipatia Ukraine vifaa vingi vya kivita vikiwemo vya kudungua roketi kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa chapisho hilo, Marekani inahofia kwamba upande wa Ukraine unaweza kutumia mifumo hiyo kushambulia ardhi ya Urusi, hatua ambayo inatishia kuongezeka kwa mzozo huo.
"Matarajio ni makubwa" kwa Ukraine

Chanzo cha picha, EPA
Mnamo Mei 21, Rais Zelensky alizungumzia juu ya mifumo ya MLRS.
"Nitasema kwa uaminifu kwamba tuna matarajio makubwa - ningeiita mchakato uliosubiriwa kwa muda mrefu ... Tunatarajia maoni mazuri juu ya usambazaji wa MLRS," alisema katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Ureno Antonio Costa huko Kyiv.
Shukrani kwa mifumo hii, Zelensky anasema, "Ukraine itaweza kuchukua hatua na kukomboa eneo lake."
Alisisitiza: Kyiv inaomba msaada huu kwa sababu "hatuwezi kulipa gharama - makumi, mamia ya maelfu ya watu."
"Haipaswi kuwa hivyo"
Siku moja kabla, mkuu wa ofisi ya rais, Andriy Yermak, alisisitiza kuwa "bado tunakosa silaha nzito."
"Na muhimu sana, bado tunasubiri MLRS. Nimejifunza mengi, kama ilivyo kwa Waukraine wengi, bado tunasubiri," alisema.
MLRS ni nini na kwa nini Urusi inaziogopa?
M270 MLRS (Multiple Launch Rocket System) ni mifumo ya silaha inayoweza kufyatua roketi zisizoongozwa kwa umbali wa hadi kilomita 45, makombora ya M30 na M31 umbali wa hadi kilomita 70, na muhimu zaidi - makombora ya ballistic hadi kilomita 300.
Kama mifumo ya kombora aina ya M142 HIMARS, M270 MLRS hutumiwa kwa madhumuni mahususi.

Chanzo cha picha, Defense.Gov
Ikiwa unataka kulenga mahali fulani katika umbali mrefu, basi mifumo hii inafaa kutekeleza jukumu la OTRK na ni ina nguvu zaidi.
Vyombo vya habari vya kijeshi vya Urusi vina wasiwasi mkubwa juu ya matarajio ya Ukraine kupokea silaha hizo. Wanatarajia kwamba kwa kupewa msaada kama huo jeshi la Kiukreni linaweza kuvuka kikwazo cha eneo la Crimea.
Uwezo na nguvu kubwa ya mifumo ya HIMARS, ambayo inaweza kuwa ya maslahi kwa jeshi la Kiukreni sasa, ni uwezo wake wa kufyatua makombora ya kibalistiki ya aina ya ATACMS.
Kwa njia hii, jeshi la Kiukreni linaweza kupata "nguvu kubwa kijeshi" kwa vikosi vyake vya makombora, ambavyo kwa sasa vinatumia "Dots-U" ya Soviet yenye kiwango cha juu cha kushambulia hadi kilomita 120 kwa mashambulizi ya masafa marefu.













