Mama yake Osinachi azungumza kwa mara ya kwanza

Bi. Madu, mama Osinachi alieleza uchungu wa tukio la mwanae

Chanzo cha picha, HYACINTH OGBU

Iliyochapishwa

Mama na dada wa marehemu Osinachi Nwachukwu wamezungumza kwa mara ya kwanza tangu mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili alipofariki siku ya Ijumaa tarehe 2 mwezi Aprili.

Ndani ya mahojiano na mwandishi wa kujitegemea wa BBC Hyacinth Ogbu akiwa na familia ya Osinachi, wameeleza maumivu yao na kueleza kuhusu hali mbaya aliyopitia na mume wa Osinachi, Peter Nwachukwu.

Bi. Madu, mama Osinachi alieleza uchungu wa tukio la mwanae.

"Ninaumia kwa ajili ya huyu mkwe wangu, alikuja hapa kutaka kumuoa mwanangu na nikampatia ushirikiano, lakini sasa amechukua uhai wake'' anasema Mama wa Osinachi.

Lakini ripoti za awali zilisema kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 alikuwa akiugua saratani ya koo, lakini familia yake inakanusha hilo, ikidai kuwa alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani.

Mumewe Peter Nwachukwu bado hajatoa maoni yake kuhusu shutuma hizo dhidi yake.

Msemaji wa polisi alisema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha kifo chake.

Mama wa marehemu aliongeza pia tangu ndoa hiyo ifungwe hakuwa na amani, wala mtoto wake hakuwa na amani.

"Tangu aolewe hakuwa na amani, na mimi pia sikua na amani.''

Mama wa Osinachi anaongeza pia baada ya binti yake kuolewa hakuonana naye hadi ilipopita miaka minane.

Muimbaji huyo mahiri wa injili hakuwaambia familia yake yale yote anayopitia kwenye ndoa yake.

Chanzo cha picha, Instagram

Hata alipopata watoto yeye alisikia tu kwa watu na mume wake hakumwambia mama mkwe wake huyo kama wamepata watoto.

Mwanzoni Muimbaji huyo mahiri wa injili hakuwaambia familia yake yale yote anayopitia kwenye ndoa yake.

Lakini mama yake huyo anadai alikua akipokea taarifa kutoka kwa watu wa nje kuwa mwanae anapata shida katika ndoa yake.

Mama yake Osinachi maarufu kama Madam Madu alisema siku moja alipokea simu kutoka kwa bintiye wakati huo huo Osinachi ambaye ametoka kujifungua mtoto wake wa tatu, alisema Osinachi anateseka na hakuna mtu anayemtunza na jinsi Peter anavyomtendea anapata tabu sana''

Mama Madu anaongeza kuwa Peter aliwapigia simu na kuwaambia kuwa ikiwa mtoto wao ''hatorudi akiwa hai basi atarudi akiwa amekufa''

Baada ya hapo dada yake mkubwa wa Osinachi, Favour Mmadu ,alienda kumchukua na kurudi nae kwa baba yao.

Marehemu Osinachi alikaa kwa baba yake kwa zaidi ya mwaka mmoja yeye na watoto wake. Baadaye mumewe Peter alikuja kuomba mkewe arudi nyumbani waendelee kuishi kama familia.

Mama Madu anasema hakutaka kabisa mwanae arudi kwa mume wake, alitaka aendelee na maisha yake na atafute mume mwingine wa kumuoa.

Marehemu Osinachi

Chanzo cha picha, PETER NWACHUKWU/FACEBOOK

"Anampigia simu baba yake kumwambia niseme, Peter alimwambia kwamba ikiwa hatarudi nyumbani akiwa hai, atakufa."

Hayo yalimfanya dada yake mkubwa, Favour Mmadu, kusafiri hadi Abuja kumchukua Osinachi ili kurejea nyumbani.

Alikaa mwaka mmoja na miezi mitatu nyumbani kwa baba yake kabla ya Peter Nwachukwu kwenda kumuomba mke wake kwenda nyumbani.

Madam Madu hakutaka binti yake arudi kwenye ndoa.

Mara baada ya kurudi, vipigo na manyanyaso vikaendelea katika ndoa hiyo.

Dada yake anasema alikosana na Osinachi kwasababu ya ndoa yake na Peter.