Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mahusiano: Kwanini mahusiano ya utofauti mkubwa wa umri ni 'aibu'
Kadri siku zinavyoenda watu wengi sasa wanakubali kwamba upendo unaweza kuwa wa aina nyingi.
Lakini kwa nini kuna watu bado wanalaani mapenzi ya watu wenye utofauti mkubwa wa umri?
Kuna katuni ambazo zimekuwa zikisambaa mtandaoni tangu mwaka 2019 ambapo zikionesha historia ya mahusiano ya muigizaji Leonardo DiCaprio.
Mtumiaji wa Reddit aliona mahusiano ya DiCaprio yakipata umaarufu mtandaoni: Wakati huo, alikuwa na umri wa miaka 44, lakini alionekana anamchumbia wanawake wenye umri wa miaka 25 au chini ya umri huo, kila mara alikuwa akiachana na wapenzi kabla hawajafikisha miaka 26.
Majibu kwenye chati yalikuwa na utata.
Wengine walimpongeza DiCaprio kwa uwezo wake wa kuvutia wanawake wadogo, huku wengine wakimkosoa muigizaji huyo wakimtaka atafute mtu aliye karibu na umri wake.
Hata miaka mitatu baadaye, chati hiyo huibuka tena kila mara, watu wanapofuatilia kwa karibu uhusiano wa sasa wa DiCaprio na muigizaji na mwanamitindo wa Argentina Camila Morrone - ambaye sasa ana umri wa miaka 24.
Uchumba wa muigizaji huyo unaibua maoni mbalimbali juu ya maoni yake ya utata kuhusu mahusiano kati yake na watu walio na utofauti mkubwa wa umri.
Wengine huwa wanapongezwa na wanakuwa chanzo cha wengine kuiga; kuna wengine huwa hawayakubali au kuyapenda mahusiano ya watu ambao wana uhusiano na wenzi wadogo zaidi yao.
Kutoka kwa Demi Moore na Ashton Kutcher hadi George na Amal Clooney, uhusiano kati ya watu maarufu wenye tofauti kubwa ya umri, daima umesababisha maoni mengi.
Mnamo mwaka 2014, wastani wa utofauti wa umri katika uhusiano wa jinsia tofauti nchini Marekani ulikuwa mdogo - kati ya miaka miwili au mitatu - lakini utofauti wa umri kwa wapenzi wengi ni kubwa zaidi.
Katika nchi za Magharibi, karibu 8% ya wapenzi wa jinsia tofauti wana utofauti wa umri wa kati ya miaka 10 au zaidi.
Asilimia hii imeongezeka hadi 25% katika mahusiano ya kimapenzi wa jinsia moja kati ya wanaume na hadi 15% kati ya wanawake.
Na katika baadhi ya matukio, pengo hilo ni kubwa zaidi—data zinaonesha kwamba takribani 1% ya wapenzi wa jinsia tofauti nchini Marekani wana pengo la umri la miaka 28 au zaidi.
Maoni yetu kuhusu uhusiano kati ya watu walio na utofauti wa umri mkubwa yanasababishwa na utofauti wa kitamaduni.
Katika miaka mia moja iliyopita, mabadiliko ya kiuchumi na usawa mkubwa wa kijinsia yamebadilisha utofauti wa umri kuchukuliwa kuwa "kawaida" na harakati za hivi karibuni za haki za kijamii zimeongeza ukosoaji wa mienendo ya nguvu katika uhusiano wa utofauti wa umri.
Wapenzi wa aina hii mara nyingi hukabiliana na hukumu - na baadhi ya wataalam wanaamini kwamba inaweza kubadilika hivi karibuni, wengine wanasema kwamba kiwango cha kutoidhinishwa kwa vijana wa leo katika mapenzi na umri ni mkubwa zaidi kuliko ile ya vizazi vilivyotangulia.
Matokeo ya mabadiliko hayo
Watu ambao hawakubaliani na mahusiano ya Leonardo DiCaprio wana historia yake.
Kuchukiwa kwa mahusiano kati ya watu wa umri tofauti ni jambo la kawaida sana na huwa kitu kisichokubalika kwa maelfu ya watu tofauti na jinsi hali ilivyo kwa sasa.
"Katika tamaduni nyingi, haikubaliki kupendana na mtu ambaye ni mdogo sana au mkubwa kuliko wewe," anasema Elena Touroni, mshauri wa saikolojia na mmoja wa waanzilishi wa Kliniki ya Saikolojia ya Chelsea huko London.
"Kwa mtazamo wa mabadiliko yanayoonekana sasa , matamanio ya kuanzisha familia inaweza kuathiri uchaguzi wa mtu ambaye anataka kuwa naye katika uhusiano, wote kutoka kwa mtazamo wa kibiolojia, lakini pia ili wazazi wote wawili wawe hai kulea watoto wao. ," alisema.
Kwa wanaume na wanawake, uzazi huelekea kupungua baada ya takriban miaka 35.
Ingawa wanawake hupoteza uwezo wao wa kupata watoto kwa haraka zaidi, inaleta maana kwamba tumebadilika ili kuvutiwa na watu wa rika sawa.
Ingawa kuna data kidogo kuhusu umri katika mahusiano ya jinsia moja, tunajua kwamba tofauti za umri kati ya wapenzi wa jinsia moja ni za kawaida zaidi, labda zinaonesha ushawishi wa uwezo wa kibaiolojia kuhusu jinsi tunavyotafuta mpenzi.
Lakini sio kwasababu ya uzazi peke yake.
Utafiti unaonesha kuwa kuoana na mtu wa rika sawa huongeza uwezekano wa uhusiano wako kudumu kwa muda mrefu.
Wataalamu wanaamini hii ni kwa sababu wanandoa hawa huwa wanapitia hatua na changamoto za maisha katika misimu iliyokaribiana na kwa hivyo wanaweza kuendelea kuelewana kwasababu kuna vitu wanavipenda wote.
"Katika miaka 10 ya kwanza ya ndoa, watu huripoti viwango vya juu vya kuridhika kwa ndoa ikiwa wenzi wao ni mdogo," asema Grace Lordan, profesa wa sayansi ya tabia katika Shule ya Uchumi ya London, ambaye kwa sasa anatafiti uhusiano kati ya umri na furaha.
"Lakini baada ya muda, kuridhika kwa ndoa kwa wanandoa wenye utofauti mkubwa wa umri hupungua zaidi kuliko wapenzi wa umri sawa," alisema. "Uwezekano wa talaka kati ya wanandoa wa umri sawa pia ni mdogo."
Lakini licha ya mambo haya yanayotushawishi kuchagua wapenzi wanaolingana na umri, hali za kijamii na kiuchumi wakati mwingine zinaweza kuzuia msukumo wa mageuzi.
Mnamo miaka ya 1900, tofauti ya wastani ya umri kati ya wanandoa ilikuwa karibu mara mbili ya tofauti katika miaka 2000. Kihistoria, watu (hasa watu wa tabaka la kati na tabaka la juu) wangekuwa na uwezekano mkubwa wa kuolewa na mtu mdogo zaidi au mkubwa zaidi kuliko wao.
Sababu ya hali hii ni za kibiolojia na kiuchumi. Ikiwa mwanaume mwenye umri wa miaka 50 anataka kupata watoto, hatakuwa na nia ya kuoa mwanamke wa umri sawa, ambaye ana uwezekano mdogo sana wa kuzaa.
Katika jamii ya enzi hizo ambapo wanaume wana mamlaka ya kiuchumi, chaguo la kuoa mwanamke mdogo zaidi lingeweza kupatikana kwake zaidi.
Katika karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, wanawake wengi walitengwa na wafanyakazi, kwa hivyo ilikuwa na maana kwao kutanguliza ndoa kwa mtu ambaye tayari ameanza kupata kipato.
Kwa upande wa wanaume, ilikuwa na maana kujiimarisha kiuchumi kwanza, na kisha kuhangaikia ndoa - baada ya yote, kutokana na uwezo wao mkubwa wa kijamii, wangeweza kupata wake wadogo ambao walikuwa na uwezekano mkubwa wa kupata watoto.
Tunamlaani nani na kwanini
Kadiri wanawake walivyozidi kupata uwezo mkubwa wa kiuchumi, mvuto wa mume mwenye umri mkubwa zaidi unapungua, na kufanya mahusiano ya utofauti wa umri kuwa ya kawaida - na mara nyingi huwa hayakubaliki .
Na leo, wanandoa ambao mtu mmoja ni mkubwa zaidi kuliko mwingine bado wanakabiliwa na hukumu, hata kama jamii nyingi zinakubali mawazo yanayoendelea kuhusu upendo, mahusiano, na utajiri wa aina mbalimbali ambao unaweza kupatikana kutambulisha uhusiano wa namna hiyo.
Badala ya kukiri kwamba watu wana furaha pamoja, kuna mwelekeo wa kuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kutofautiana kwa mamlaka na kuuchukulia uhusiano huo kuwa shughuli, tukichukulia kwamba upande mmoja unatafuta kuinua hadhi yao ya kijamii au kuongeza utajiri wao.
Kwenye Kiingereza, kuna hata misemo mbalimbali ya kufafanua hukumu hii: kama vile "sugar daddy" hufafanua mwanaume mkubwa, wakati mwanamke mdogo anaweza kuwa " gold-digger".
Uhusiano kati ya Rais wa Ufaransa Emmanuel na Mke wa Rais Brigitte Macron, ambao wameoana tangu mwaka 2007, walikosolewa kwenye vyombo vya habari.
Katika miaka ya hivi karibuni, aina hii ya mahusiano yameibua misemo haswa kwa pale wanawake ndio wenzi wenye umri mkubwa zaidi.
Takwimu zinaonesha kuwa mnamo mwaka 1963 ni 15% tu ya wanawake wa Uingereza walikuwa wakubwa kuliko wapenzi wao.
Lakini kufikia mwaka 1998, idadi hiyo iliongezeka hadi 26%, na utafiti wa 2011 uligundua kuwa idadi ya wanawake walioolewa au wanaoishi na mwanaume mwenye umri wa miaka mitano au zaidi ilikuwa karibu mara tatu tangu miaka ya 1970.
Wanawake wanaoamua kuchumbiana na wanaume wenye umri mdogo wanaonekana kukabiliwa na hukumu isiyo na uwiano.
"Sisi wanadamu huhukumu kila kitu, na ikiwa jirani yetu atafanya kitu nje ya kile tunachotarajia, tunaweka uangalizi kwake," anasema Lordan.
"Wanawake wanaoolewa na wanaume wenye umri mdogo huenda kinyume na inavyotarajiwa katika simulizi zetu za ndoa. Kwa sababu hiyo, wanapata hukumu nyingi zaidi."
Tahadhari ya vyombo vya habari kuhusu ndoa ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mkewe Brigitte - mwenye umri wa miaka 24 - na utangazaji mkali wa uhusiano kati ya mwanamitindo na muigizaji Kim Kardashian mwenye umri wa miaka 41 na muigizaji na mcheshi Pete Davidson mwenye miaka 28) zinathibitisha tu.
Lakini Touroni anaamini kuwa uhusiano kati ya wanaume wazee na wanawake wenye umri mdogo hupokea lawama kubwa zaidi kuliko wanandoa ambao wanawake ni wazee kuliko wanaume.
Labda hii inahusiana, kwa sehemu, na harakati ya #MeToo, ambayo imevutia umakini wa mienendo ya nguvu katika uhusiano.
Baadhi ya watu wanahoji kwamba tofauti kubwa ya umri, pamoja na uwezo wa kijamii na kiuchumi unaotumiwa na wanaume katika jamii inayotawaliwa na wanaume, inaweza kuwaacha wanawake vijana katika hali hatarishi.
Utafiti uliofanywa muda mfupi baada ya vuguvugu la #MeToo unaonesha kuwa wachunguzi wengi wanaamini kuwa kuna kipengele cha uchunguzi wa mahusiano wa utofauti wa umri.
Watafiti waligundua kuwa vijana hasa hukataa mahusiano ambayo mwanaume ni mkubwa, labda kwa sababu wanaamini kuwa ni uhusiano wa kubadilishana - kwa mfano, watu kubadilishana ngono kwa mtindo fulani wa maisha.