Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 06.04.2022: Pogba, Mbappe, Bale, Nunez, Carvalho, Foden, Antony, Laimer

Real Madrid wana uhakika wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, kutoka PSG msimu huu wa joto, licha ya ripoti kuonyesha kuwa anakaribia kukubali mkataba mpya wa kusalia Paris. (90min)
Paris St-Germain wametoa ofa kwa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 29, wakati anaingia miezi ya mwisho ya kandarasi yake Manchester United - lakini klabu hiyo ya Ligue 1 imetoa pesa kidogo kuliko United. (MEN)

Mshambulizi wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 28, atakuwa na hamu ya kutaka kusikiliza ofa yoyote kutoka kwa Manchester United msimu huu wa joto kabla ya kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake wa muda mrefu. . (The Athletic - subscription required)
Crystal Palace itasikiliza ofa kwa mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 29(Mail)
Mshambulizi wa Wales Gareth Bale, 32, ataondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu huu, lakini hakuna uamuzi wowote ambao umefanywa kuhusu hatma yake ya baadaye, ajenti wake amesema. (Deportes Cuatro, via Mirror)
Manchester United na Atletico Madrid ni miongoni mwa timu kadhaa zinazofikiria kumnunua mshambuliaji wa Benfica wa Uruguay Darwin Nunez, 22. . (Telegraph - subscription required)
Liverpool tayari wanakaribia kusajili wachezaji watatu wapya. The Reds wamefikia makubaliano ya kuwachukua kiungo wa kati wa Fulham Mreno Fabio Carvalho, 19, winga wa Celtic raia wa Scotland Ben Doak, 16, na winga wa Derry City, 15, Muireland, Trent Kone-Doherty. (Football Insider)

Manchester City wana matumaini ya kusaini mkataba mpya na kiungo wa kati wa Uingereza Phil Foden, 21, kabla ya mwisho wa msimu huu. (90min)
Uteuzi unaowezekana wa Erik ten Hag kama meneja wa Manchester United unaweza kumfanya mlinzi wa Uholanzi, Jurrien Timber, 22, na winga wa Brazil Antony, 22, wakifuata kutoka Ajax msimu huu wa joto. (Mike Verweij, via Express)
Meneja wa muda wa United Ralf Rangnick anaweza kutumia fursa ya mawasiliano yake na RB Leipzig kumleta kiungo wa kati wa Austria Konrad Laimer, 24, Old Trafford. (Bild, via Express)
Msako wa Manchester United wa kutafuta meneja mpya katika upo katika hatua ya juu zaidi, huku uamuzi wa mwisho ukiwa kati ya kocha wa Ajax Ten Hag na Mauricio Pochettino wa PSG. (The National)
Newcastle United wako tayari kumuuza fowadi Mfaransa Allan Saint-Maximin, 25, msimu wa joto. (90min)

Newcastle wamemfanya mshambuliaji wa Reims Mfaransa, Hugo Ekitike, 19, kuwa mshambulizi wao mkuu msimu huu. (Football Insider)
The Magpies wameweka orodha ya wachezaji saba wanaotamani kuhama ambayo pia inajumuisha mshambuliaji wa Everton na Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 25. (Mirror)
Lakini Newcastle wanatazamiwa kukosa lengo moja kwani AC Milan wamekubaliana na mlinzi wa kati wa Lille Mholanzi Sven Botman mwenye umri wa miaka 22 kufuatia mazungumzo ya wiki iliyopita. . (90min)

Licha ya kutakiwa na Manchester United na Liverpool, mlinzi wa Uruguay Ronald Araujo, 23, anakaribia kuafikiana mkataba mpya wa muda mrefu na Barcelona, wakala wake amethibitisha. (ESPN)
Tottenham wanatarajiwa kuanzisha chaguo lao la kumsajili winga wa Uswidi Dejan Kulusevski, 21, kutoka Juventus katika nafasi ya kwanza msimu huu wa joto. (Mail)
Spurs wanaweza kutumia kipengele cha kumsajili Kulusevski kwa mkataba wa kudumu kwa pauni milioni 25, badala ya kusubiri hadi mkopo wake umalizike, wakati chaguo hilo linaweza kugharimu pauni milioni 33.5. (Times - subscription required)
Winga wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 23, amepuuzilia mbali uvumi unaomhusisha na kuondoka Stamford Bridge. (Metro)













