Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
India: Wanawake walivyokasirishwa na kulazimishwa kueleza na kwanini wanavaa hijabu
Nabeela Shaikh alikuwa na umri wa miaka 30 alipoanza kuvaa hijabu. Alikuwa wa mwisho kati ya dada watatu kuzaliwa.
Muzna ambaye ni mkubwa, alivaa kwanza alipokuwa na umri wa miaka minane, alivutiwa na binamu yake. Alikuwa akivaa hijabu kulingana na watu ambao walikuwa karibu yake mpaka alipogundua kuwa asingeweza "kumfurahisha kila mtu".
Mdogo zaidi kati yao Sarah, alifikia "hatua ya mwisho kabisa" maishani mwake wakati ndoto yake ya kuwa daktari wa upasuaji ilipozima baada ya kupata alama za chini za mtihani. "Ilianza na mambo kama vile kuomba kwa wakati," anasema. "Nilikuja kuanza kuvaa hijabu baadaye na ilikuja kama kitu cha asili tu."
Wazazi wao wote wakiwa ni madaktari , ndugu hao walikulia katika jiji kuu la pwani la India, Mumbai.
Mama yao havai hijabu au kufunika kichwa chake. Lakini wanapofanya hivyo, watu wanasema, wanadhani wanalazimishwa.
Hijabu huvaliwa sana nchini India, ambapo kwenye maonesho ya hadharani ya imani ni ya kawaida - lakini mwezi uliopita, wasichana wa shule katika jimbo la Karnataka walipinga kuzuiwa kuivaa hijabu darasani tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Swali ni - iwapo wasichana wa Kiislamu wana haki ya kuvaa hijabu darasani - sasa liko mahakamani. Mzozo huo umezua ghasia, kugawanya mabweni ya vyuo vikuu na kuwazuia wasichana kadhaa wa Kiislamu huko Karnataka kushindwa kuhudhuria madarasani.
BBC ilizungumza na wanawake wa kiislamu katika maeneo mbalimbali nchini India ambapo wanasema wanahisi hasira kuhusu "hali ya kuingilia masuala yao ya asili" kuwa mjadala.
"Tunakumbushwa kila mara kwamba ili tukubaliwe, ni lazima tuache dini yetu," alisema mwanamke mmoja kutoka Delhi. Kilio kikubwa cha umma, wanasema hili ni chaguo la mtu kibinafsi.
Wale wanaochagua kuvaa hijabu wanasema sio uamuzi wa kidini pekee, bali ni mtu aliyezaliwa kutokana na kutafakari. Na wale wanaochagua kutovaa wanasema nywele zao sio kipimo cha imani yao.
'Sijaonewa'
"Watu hawaelewi ni jinsi gani mtu anaweza kuhisi kutaka kuvaa hijabu," Nabeela anasema, huku akicheka. "Inawachanganya ili watuhukumu."
Kuonewa ni neno ambalo kwa kawaida hutolewa kwa wanawake wanaovaa hijabu - lakini wengi wanaeleza kuwa kukataa kutilia maanani kwa nini wanafanya hivyo pia si kuwakomboa, na wala sio kuwazuia wasichana kwenda shule kwa sababu wanakataa kuiondoa.
"Wanawake vijana wa Kiislamu wako nje mitaani wakipambania haki zao. Na bado unaniambia kuwa wanawake hawawezi kujifikiria wenyewe?" Alisema Naq mwenye umri wa miaka 27 kutoka mji wa kusini wa Bangalore, ambaye anatumia jina lake la kwanza pekee.
Wakati Naq alipoamua kuvaa hijab miaka mitano iliyopita, anasema alikumbana na hisia za"kushangaza zaidi".
"Pazia langu lilifunua mawazo mengi ya watu," anasema. "Watu walinizomea: Je, umeonewa? Je, unahisi joto? Unatumia shampoo gani? Watu wengine waliniuliza ikiwa hata nilikuwa na nywele - walifikiri nina saratani."
Kwake, hijabu pia ilikuwa jaribio la kinadharia - anaona uzuri katika kila muonekano na rangi.
"Watu wanafikiri hijabu yangu inakinzana na nguo zangu za kisasa na vipodozi. Lakini sivyo," anasema. "Ikiwa nitaingia kwenye chumba, nataka watu waniangalie na kufikiria, huyo ni mwanamke wa Kiislamu anayefikia malengo yake, anasafiri ulimwengu, na anavutia."
Wanawake wengine wa Kiislamu - kama vile Wafa Veeksha, mwanasheria katika mji wa kusini wa Mangalore - wanasema kutovaa hijabu haiwafanyi kuwa Waislamu.
"Sikuvaa kwa sababu haiendani na mimi - na hakuna mtu anayeweza kuniambia niivae," anasema. "Lakini kama hivyo, hakuna mtu anayeweza kuniambia sipaswi kuvaa pia."
Mama yake Wafa hakuwahi kuvaa hijabu pia - lakini anasema alikua na imani katika mazingira yake, kusikiliza hadithi za sio tu za Mtume bali pia za wanawake katika Uislamu.
"Mke wa kwanza wa Mtume alikuwa mfanyabiashara, na wa pili alipanda ngamia kwenda vitani. Kwa hiyo, je, kweli tunaonewa jinsi ulimwengu unavyotaka tuamini?" anauliz
'Kuna ubaya gani kuwa Muislamu?'
Kulikuwa na wakati ambapo Falak Abbas alichukia wazo la kufunika nywele zake, chaguo lisilo la kawaida huko Varanasi, jiji la kaskazini la kihafidhina.
Lakini alikuwa na umri wa miaka 16 alipomwona Malala Yousafzai, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Pakistani kwenye TV na akabadili mawazo yake.
"Kichwa chake kilifunikwa, lakini alionekana kuwa na nguvu sana. Nilipata msukumo na niliamua kufunika kichwa changu pia."
Shule yake ya kidini ilipinga, ikisema hijabu iligongana na sare, ambayo ilikuwa kanzu ndefu na suruali.
Falak anadai kwamba kwa siku tatu alizuiliwa kutoka darasani - hata alikosa mtihani wa biolojia. Alipokataa, shule iliita wazazi wake na kumshutumu kwa utovu wa nidhamu.
"Walisema nikivaa hijabu itaniletea matatizo si kwangu tu lakini hata kwa shule kwani kila mtu atagundua kuwa mimi ni Muislamu," anakumbuka. "Kuna ubaya gani kuwa Muislamu?"
Lakini alikubali baada ya wazazi wake kumwambia "asihatarishe elimu yake juu ya hijabu".
Miaka minane kuendelea, akitazama matukio kutoka Karnataka, anasema kwa mara nyingine tena ameingiwa na "hasira kali".
Khadeeja Mangat, kutoka jimbo la kusini la Kerala, pia amekasirishwa na uchunguzi huo.
Shule yake ilipiga marufuku vazi la hijabu usiku kucha mwaka 1997 - marufuku hiyo ilibatilishwa baadaye, lakini Khadeeja anashangaa kitakachotokea Karnataka.
"Kila kitu kiko mbele yenu - katiba, maadili yake na sauti zetu," anasema. "Hata hivyo tumefanywa kujilinda bila kuchoka, hata kwa gharama ya elimu yetu."
'Jinsi watu wanavyokuona inaweza kuwa mbaya sana'
Wakati kikao cha mahakama kinalenga zaidi kuvaa hijabu darasani, wanawake wa Kiislamu wana wasiwasi kuhusu jinsi hukumu hiyo itakavyotekelezwa katika nchi yenye mgawanyiko mkubwa chini ya serikali ya Kihindu ya Waziri Mkuu Narendra Modi.
Simeen Ansar, kutoka mji wa kusini wa Hyderabad, anasema hijabu inageuzwa kuwa ishara ya uasi kwa "mafanikio ya kisiasa".
"Nilikua na wasichana wa Kihindu ambao walifunika miguu yao ndani ya sketi zao za shule, jambo ambalo lilionekana kuwa la kushangaza kwangu wakati huo kuliko kna wavulana wa Sikh wamevaa vilemba," asema.
"Lakini linapokuja suala la vazi la hijabu, wanawake wa Kiislamu wanawekewa vikwazo katika vazi hilo. Mimi ni wa kitamaduni na ninadhulumiwa ikiwa nitavaa moja, ya kisasa na niko huru ikiwa sitavaa." cha ajabu kwangu wakati huo kuliko kuona wavulana wa Sikh wamevaa vilemba," anasema.
"Lakini linapokuja suala la hijabu, wanawake wa Kiislamu wanazuiwa. Mimi ni mtu wa kitamaduni na ninadhulumiwa ikiwa nitavaa moja, ya kisasa na nitakuwa huru iwapo sitavaa."
Anasema yeye na dada yake walianza kuvaa hijabu, lakini waliiacha mara moja kwa sababu chaguo lao halikukubaliwa kabisa.
Wakati dada yake akikabiliwa na ubaguzi kazini, Simeen anasema watu walikuwa wanamshangaa katika maeneo ambayo hawakutarajia kumuona mwanamke aliyevalia hijabu - ukumbi wa mazoezi, baa au katika sherehe.
Na hii ni hofu inayosisitizwa na wanawake wengi wa Kiislamu - kwamba sasa kuliko wakati mwingine wowote, hijabu ndiyo yote ambayo watu wataona.
Ni mahangaiko ambayo yanamfanya Wafa, ambaye havai hijabu, afuatilie kwa karibu.
"Hata nikiwa kazini huwa naweka vikiliza sauti na kusikiliza kinachoendelea," anasema.
Ana wasiwasi jinsi hii itaathiri marafiki na familia ambao huvaa hijabu.
"Unachukua hijabu yangu, nini kinafuata? Jina langu bado ni Kiarabu. Je, nitalazimika kubadilisha hilo pia ili kupata heshima kutoka kwako?"