Rayan: Jinsi Morocco ilivyosubiri kwa hofu wakati mtoto alipotumbukia ndani ya shimo

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Shuguli ya kumuokoa mtoto mvulana mwenye umri wa miaka mitano Rayan Oram baada ya kutumbukia ndani ya shimo iliwaunganisha Wamorocco kwa siku kadhaa katika matumaini yao na maombi kwamba angepatikana akiwa bado hai.

Baba yake alikuwa akifanyia ukarabati shimo hilo katika mji mdogo wa kaskazini mwa Morocco unaoitwa Tamorot uliozingirwa na milima wakati Rayan alipotumbukia ndani yake Jumanne asubuhi. Kampeni ya mtandao ya #SaveRayan ilisambaa katika nchi nyingi, hata katika mahasimu wa Morocco, Algeria.

BBC haihusiki na dhana za mitandao ya nje yake

Mtangazaji maarufu wa televisheni ya Morocco Rachid Allali hata alikatiza kipindi chake kwa ushirikiano na Rayan. Maelfu walikusanyika katika eneo la tukio kuwatia moyo waokoaji waliokuwa wakifanya kazi hiyo saa 24 wakitumia taa za mwanga mkubwa nyakati za usiku.

Operesheni hiyo ilikuwa ngumu kutokana na mchanganyiko wa mwamba, udongo wa mchanga katika eneo hilo, ambavyo vilimaanisha kuwa kuingiliwa kokote kwa shimo hilo kungesababisha kuporomoka kwa udongo.

Wahudumu wa dharura, wakiwemo wazima moto, walisaidia kufukua shimo kubwa pembeni mwa mlima kabla ya kuchimba handaki tofauti la mlalo kuelekea kwenye shimo katika jaribio la kumuokoa Rayan, aliyekuwa amekwama 32 kwenda chini (au futi 104) kupitia shimo hilo ambalo lilikuwa jembamba saa.

Unaweza pia kusoma:

Miongoni mwa waokoaji, mwanaume mmoja alichaguliwa na kusifiwa kwa namna ya kipekee kwa jina Ba (Uncle) Ali Sahrawi, ambaye alijitolea kutumia ujuzi wake kusaidia kuchimba ili kumuokoa Rayan kwa kutumia shoka, baada ya kubainika kuwa ni hatari sana kutumia machine nzito.

Wahudumu wa uokoaji hatimaye walimfikia Rayan siku ya Jumamosi jioni, siku nne baada ya kutumbukia. Ambilansi iliyomchukua kwanza ilipokelewa na kelele za shangwekutoka kwa umati watu kabla ya taarifa ya Mfalme Mohammed VI wa Morocco kuthibitisha kifo chake . Baadaye aliwapigia simu wazazi wa rayan kuwapa rambirambi.

Timu ya waokoaji ilishiikana mikono wakati wazazi wa Rayan walipoondoka kwenye eneo la tukio huku mwili wake ukichukuliwa.