Almanusura niwe muuaji kwa misingi ya ubaguzi wa rangi

Chanzo cha picha, Jared Stapp
Katika miaka yake ya ujana, Mike akawa Mnazi. Na sasa miaka sita baadaye, yeye ni muunga mkono wa vuguvugu la Black Lives Matter - na linalomshangaza ni vile alikaribia sana kubeba bunduki yake na kupiga watu risasi. Wakati alimtaza yule mwanamume alikuwa ameanguka chini, angeelewa kuwa angekufa.
Siku tatu baada ya mauaji ya George Floyd, maandamano ya kuuunga mkono vuguvugu la Black Lives Matter yalikuwa yanazuka kote nchini Marekani. Mike alikuwa akiandamana huko Oakland, California na mpenzi wake lakini usiku ulipoingia na polisi wakaanza kufyatua risasi za mipira na vitoa machozi, waliamu kuondoka
Walikuwa wanatembea kurudi kwa gari lao, kwenye mitaa iliyokuwa imeja moshi wakati waliona gari leupe likisimama. Kisha wakaskia milio ya risasi. Baadaye Mile akafahamu kuwa mwanamume aliyekuwa amekufa alikuwa Dave Patrick Underwood, afisa wa serikali aliyekuwa analinda mahakama.
Kwa bahati Mike alikuwa anamfahamu Underwood, alikuwa akitembea siku hiyo na watu wa familia yake. Lakini pia alikuwa amemfahamu mwanamume ambaye baadaye alikuja kushtakiwa kwa kumuua- Steven Carillo, ni sajenti katika kituo cha wanahewa huko California ambapo Mike alikuwa amejisajili siku chache kabla.
Na haikutosha, Mike alikuwa na siri. Nyumbani kwenye kabati la nguo , kulikuwa na sare ya Nazi - aliiweka hilo kujikumbusha kuhusu alikuwa mtu wa aina awali. Kama Carillo, Mike alikuwa amegeuka kuwa mtu mweye msimamo mkali na kuwa mfisadi wa kikundi katili cha mrengo wa kulia.
Utotoni alikuwa amekulia kwenye mji mdogo kijiji uliokuwa umejaa wazungu. Lakini wakati Mike alifikisha umri wa miaka 12, mama yake alimtaliki baba yake wa kambo na kuhamia sehemu tofauti ya nchi.

Chanzo cha picha, Jared Stapp
Ghafla Mike alikuwa anaishi eneo lenye mchanganyiko wa watu na alichukia sana. "Kuna watu ambao hawakuwa wanaonekana kama kitu chochote nilikuwa nimekiona awali, chakula kilikuwa tofauti, maji yalikuwa na ladha tofauti, kila kitu kilikuwa tofauti."
Sasa kiwango chao cha maisha kilikuwa kimeshuka sana, na babake wa kambo hakutimiza ahadi yake ya kuja kuwatembelea. Haya yalichangia hasira za Mike na akagundua kuwa njia ya kutoa hasira hiyo na kujiunga na mrengo wa kulia.
Kwa kutiwa moyo na baba wa rafiki wake , Mike akaanza kusikiliza mwaandalizi wa kipindi cha mrengo wa kulia Sean Hannity na wakati alisaka maudhui mitandaoni, alipata video za wanachama wa mrengo wa kulia kwenye mitandao ya Facebook na Youtube.
Akaambiwa, kwa mfano, talaka ni njama za wayahudi za kuangamiza familia za watu weupe. Kisha Mike akahamia mitandao ya siri zaidi ya wazalendo wa kizungu ya 4chan na 8chan. Mitandao ilikuwa ni klabu za kibaguzi, Nazi na wazalendo wa kuzungu. Anasema.
Katika kipindi kimoja, alialikwa na rafiri yake waliyekuwa wamekutana mitandaoni kurekodi video za propaganda. Rafiki wake huyo alikuwa anamiliki kiwango kikubwa cha bunduki na baadhi ya hizo zikajazwa kwenye gari na wakaelekea milima iliyokuwa karibu.
"Tulikuwa tunafyatua risasi, tukirekodi na kukimbia huku na kule huku tukiwa tumevaa sare za Nazi," Mike anasema.
"Nilikuwa ninatafuta mahala pa kutua hasira zangu," Mike anasema, Na nikapata mahala salama.

Chanzo cha picha, Jared Stapp
Mwaka mmoja baadaye, Mike akamaliza shule ya upili na akasafiri kwenda London kuendelea na masomo yake.
Alitarajia kuona kofia za bakuli na waungwanan lakini mambo yalikuwa ni tofauti kabisa. Chuo chake kilikuwa eneo la Whitechapel, eneo lenye watu wengi waumini wa kiislamu.
"Nilikuwa umri wa miaka 18 mzalendo wa kizungu niliyechukia uislamu," anasema. Sikuona mchanganyiko huko kama kitu kizuri..
Wakati akiwa London, Mike akazama kabisa kwenye uzalendo wa uzungu huku akiwashambulia mitandaoni watu mashuhuri wa mrengi wa kushoto nchini Marekani.
Jioni moja Aprili mwaka 2017, alikuwa ameabiri treni kwenda kukutana na marafiki kwenye baa. Wakati abiria waliambiwa kuwa kituo cha Westminster kilikuwa kimefungwa kwa sababu ya oparesheni wa polisi.
Gari lilvurumisha kwenye njia ya muguu na kuwagonga watembea kwa miguu. Kisha dereva akatoka nje na kumchoma kisu afisa wa polisi. Watu sita walikufa akiwemo mshambuliaji, na 50 kujeruhiwa.
Mike alishuka kutoka kwa treni na kushuhudia hofu iliyotanda. Picha ya watoto wawili waliokuwa wamefungwa mablanketi bado iko akilini mwake. IS lililokuwa kundi lenye nguvu mashariki ya kati, lilisema lilihusika kwenye shambulizi hilo.
Baada ya wiki kadhaa Mike alikuwa amerejea California na kujiunga na jeshi la wanahewa na Marekani.
"Nilikuwa na msukumo, naamananisha sikuwa na shaka akilinia mwangu kuwa nilitaka kwenda nchi ya mtu mwingine, iwe Iraq au Afghanistan, nivae sare na nichukue bundukli na niwaue."
Wiki chache kabla ya kuanza mafunzo, alichukua masaa mengi kwenye karakana yake huku akinywa na kuvuta sigara, akijaswa na hasira.
"Karibu kila wakati nilikuwa na bunduki," anasema. Na nilikuwa katika hali ambayo iwapo mtu angeniambia nifanye kitu, ningekifanya."

Chanzo cha picha, Jared Stapp
Februari mwaka huu makao makuu ya jeshi yalitangaza hatua dhidi ya misimamo mikali - amri kwa viongozi kote jeshini kutatua tatizo la misimamo mikali ndani ya vikosi vyao. Wakati huo pia, waziri wa ulinzi Lloyed Austin alibuni kundi la kutambua vitisho vya ndani na kusema kuwa wale watachaguliwa kujiunga na jeshi watakaguliwa iwapo wana mashirikiano na misimamo mikali.
Hatua hizi zilijiri baada ya uchunguzi wa awali dhidi ya walke waliokamatwa kwenye maandamano ya Capitol Hill Januari 6 kubaini kuwa wengi wao walikuwa wanajeshi wakati au wa zamani.
Lakini la kushangaza ni kwamba kwa Mike jeshi limekuwa mwanzo wa safari yake kuachana na kuunga mkono kundi la mrengo wa kulia.Mwaka 2017 alikuwa katika mwezi wake wa pili wa mafunzo katika misitu ya Missouri.
"Nilikuwa nimekwama eneo ambalo lilikuwa na mkusanyiko wa kila aina ya watu kutoka kote Marekani, wakiwemo watu weusi, wayahudi, mtu kutoka Guam aliyenifunza kumchoma samaki mkuki," anasema. Nilikuwa nafanya urafiki na watu ambao awali sikutarajia kuwa wangekuja kuwa marafiki.
Alipata kuishi kambini kuwa jambo gumu. Udhibiti wa wakubwa wake kwa kila alichokifanya - ilikuwa hali ngumu kwake.
Akajaribu kuacha mara sita katika kipindi cha wiki nane. Alipomuona ameketi peke yake siku mmoja, muajiriwa mweusi alipendekeza waombe pamoja.Wiki chache zilizofuatia, maujiriwa huyo pamoja na mwanamume mwingine Myahudi wangemsadia Mike wakati ya nyakati ngumu.
Kwenye kambi ya mafunzo hakuwa na muda kuingia mitandano na bila ya kuwepo kwa propaganda alizokuwa anaziona kila siku, chuki yake ikaanza kupungua.Baada ya kupewa likizo ya kiafya kutoka jeshi la wanahewa kutokana na kudhoofika afya yake ya akilia, Mike akaanza kufanya kazi kwenye ukumbi wa muziki.
Hii ndilo alilihitaji kutoa hasira zilizokuwa zimejirundika tangu utotoni muziki wa punk ukawa mkombozi wake.
Wakati likizo yake ilifikia mwisho, Mike hakurudi jeshini na akatangwa kwa mtu aliyelihama jeshi bila likizo . Kisha Disemba iliyopita kwa mshangao aliruhusiwa kuondoka jeshini kwa heshima.Lakini wakati akijitoo kwa misimamo mikali, aliona baadhi ya Wamarekani wakizama kabisa, Waandamanaji wa Black Lives Matters walijeruhiwa kwenye miji kadhaa na Mike akatishwa sana na shambulizi la huko Capitol Hill.
Mike anataka watu waelewe ni rahisi vipi nchini Marekani leo hii, itikadi za misimamo mikalia zinaweza kuteka maisha ya mtu.
"Kile ninataka watu wajue ni kuwa nilikuwa Mnazi, Na sio wa mwaka 1939 lakini kwenye Marekani ya saa.













