Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo Somalia: Bunge la Somalia lapiga kura kupinga mpango wa Rais Farmajo
Bunge la nchini Somalia limepiga kura kusitisha kuongeza miaka miwili ya utawala wa rais aliyepo madarakani.
Uchaguzi wa kuchagua rais mpya ulikuwa ufanyike Februari .
Hatua ambayo imepelekea migogoro ya kisiasa ambao umesababisha machafuko mjini Mogadishu na kuleta mapigano ya kijamii kati ya wanajeshi wanaomuunga mkono rais Mohamed Abdullahi Farmajo na wale wanaompinga.
Jumapili iliyopita kulikuwa na ghasia mjini Mogadishu na maelfu ya watu kukimbia makazi yao.
Kufuatia msukumo mkubwa wa kimataifa rais wa Somalia aliamua kusitisha mpango wake wa kuendelea kubaki madarakani kwa miaka mingine miwili.
Rais Mohamed Abdullahi Farmajo aliliambia bunge kuwa waziri mkuu ataongoza katika kuandaa uchaguzi.
Bunge nalo likapiga kura kufutilia mbali muswada huo ambao uliongeza muda wa rais.
Wakiwa na matumaini ya kusitisha hofu na mvutano wa kisiasa ambao ungeiweka Somalia katika vurugu kubwa kwa miaka.
Ingawa bado kuna kazi kubwa mbele ya kuandaa uchaguzi uliochelewa kufanyika.
Hata hivyo Rais Farmajo alisema pia kuwa vyombo vya usalama vinahakikisha usalama kwa raia unazingatiwa na kuzuia matukio yeyote ambayo yanaweza kupelekea taifa kuingia katika mapigano.
Huku baadhi ya raia wakiwa wamekimbia ghasia na kumekuwa na hofu ya wanamgambo wa al-Shabaab.