Virusi vya Corona: ''Nimetukanwa kwasababu jina langu ni Corona'

Iliyochapishwa

Corona Newton amekuwa akisakamwa kwa kuwa na jina lake kwa muda mrefu sana.

Amekuwa akipata majina ya utani mengi ya bia, mwanamke huyu mwenye miaka 49-kabla hata hajabadilisha jina lake la kwanza kisheria.

"Watu walikuwa wanamuita Guinness na Budweiser," alisema. "Majina hayo yalikuwa yananifanya nichekwe mara zote.

Lakini hali ilivyo kwa sasa ni ngumu zaidi haswa wanaponifanyia na fujo."

Corona anaishi Oldham, mji ambao una idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona, idadi kubwa kurekodiwa England ya wagonjwa 100,000.

Wakazi wa mji wa Greater Manchester wamekewa masharti magumu zaidi dhidi ya corona kwa wiki kadhaa.

Corona anasema kila mtu ananichukulia kimzaa tu walipogundua jina lake la kikristo, hawezi kujiandikisha katika nyaraka za benki au zozote bila kuangaliwa kwa mshangao.

"Watu wananiambia kuwa hawawezi kumsikiliza mtu mwenye jina la virusi,"alisema.

Corona ni mama wa watoto watano amekumbwa na changamoto kubwa ya kudhihakiwa jina lake kwa kejeli za kila aina kama vile, hyo ndio vile virusi?"

Wakati alipokuwa akimpeleka binti yake kwa daktari wa meno wiki iliyopita, alipokea simu ya mwanaume ambaye alikuwa ana mtukana tu bila sababu , kwa kuwa tu jina lake ni corona.

Alisema: "Huyo mwanaume alinipigia kelele kwenye simu , ni kama janga la corona duniani limesababishwa na yeye?'"

Jina lake linampa wakati mgumu katika kipindi hiki, kama mzazi mmoja alifikiri kuwa binti yake anakasirika mwalimu anapomtaka kutaja jina la mama yake Corona.

Kwa mujibu wa takwimu za taifa, watoto wasiopungua watatu wameitwa Corona mwaka 2019 na hawajarekodiwa katika majina bora 100 ya wasichana katika kuanzia mwaka 1904-2019.

Sasa kwanini Corona limekuwa jina la kustajabiwa?

Jina hili kwa lugha ya Latin ina maanisha kuwa ni Taji na vilevile lina maana kuwa mwezi umezungukwa na nyota .

Jina hilo ni maarufu katika lugha ya Kihispaniola.

Kukua katika mji wa Drogheda, Mashariki mwa pwani ya Ireland, Corona alisema anakubali kuwa jina lake haliko kikatoliki sana ingawa alipewa jina hilo kwa kuwa mkunga mmishionari alimsaidia mama yake kujifungua alikuwa anaitwa jina hilo.

"Wazazi wangu hawakuweza kuamua kuchagua kati ya Sarah na Catherine, hivyo waliamua kuchagua Corona," alisema.

Kabla ya taarifa za habari kugubikwa na janga la corona, Corona alisema ilikuwa rahisi kwake kulishangaa jina lake kama kichekesho.

Anasema alikuwa anacheza michezo ya kutabiri jina lake na hakuna aliyeweza kupatia hivyo walibakia kumnunulia vinywaji tu.

Licha ya kuwa Covid-19 kuvurugha mipango yake ya harusi kwa sasa, pamoja na sherehe yake kubwa ya kuzaliwa ya miaka 50, Corona alisema 2020, utakuwa mwaka wa kukumbukwa.

"Katika wakati huu mgumu, kama nimeweza kumshangaza mtu kwa kuwa na jina la ajabu if I've brightened someone's day by having a funny name, so be it," she said. "At least no-one will ever forget me."