Tunachokifahamu kuhusu moto wa Mlima Kilimanjaro

Shughuli za kuzima moto Mlima Kilimanjaro bado zinaendelea mpaka leo Ijumaa ikiwa ni siku ya sita toka ulipolipuka siku ya Jumapili.
Kilimanjaro ndiyo mlima mrefu zaidi barani Afrika, na upo kaskazini mwamnchi ya Tanzania. Mlima huo ni moja ya vivutio vikubwa vya watalii kwa Tanzania, na mpaka kufikia sasa serikali ya nchi hiyo inasisistiza kuwa moto huo haujaathiri shughuli za utalii katika eneo hilo.
Miale ya moto imekuwa ikionekana kutoka mji wa Moshi umbali wa makumi ya kilomita kutoka eneo la mlima kulikotokea tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa na msemaji wa Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Paschal Shelutete inaeleza kuwa "eneo kubwa lililoathirika na moto huo limedhibitiwa."
Lakini, je ni mambo gani ambayo tnayoyafahamu kufikia sasa kuhusu moto huo.

Chanzo cha picha, TANZANIA NATIONAL PARKS
Je, chanzo cha moto huo ni kipi?
Mpaka kufukia sasa, chanzo hasa cha moto huo bado hakijafahamika na mamlaka zinaendelea na uchunguzi.
Kinachofahamika ni kuwa moto huo ulianzia katika eneo ambalo wapanda mlima hupumzika siku ya Jumapili.
Kumekuwa na taarifa kuwa kuna uwezekano kuwa moto huo ulillipuka wakati mmoja ya wasaidizi wa wapanda mlima alipokuwa akipasha moto chakula na kuenea haraka kupiti nyasi zilizokauka, hata hivyo taarifa hizo hazijathibitishwa na mamlaka kufikia sasa.

Chanzo cha picha, TANAPA
Juhudi za kuuzima zimefikia wapi?
Kufikia Jumatano ya wiki hii, mamlaka zileleza kuwa, wanakaribia kudhibiti kabisa moto huo ambao ulikuwa unawaka katika eneo dogo. Pia mamlaka zilibainisha kuwa mvua iliyonyesha usiku wa Jumanne zilisaidia jitihada zao.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Hata hivyo, siku ya Alhamisi, Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla alieleza kupitia ukuraasa wake wa Twitter kuwa upepo, nyasi kavu na vichaka vimekuwa changamoto kubwa na kuwa wataanza kutumia ndege na helikopta na ndege katika shughuli za kuzima moto huo.

Chanzo cha picha, TANAPA
Mpaka Jumatano, shughuli ya uzimaji wa moto ilikuwa ikifanywa na watu 500 wakiwemo askari wa zimamoto, maafisa wa Tanapa na raia wakujitolea kutoka vyuo na vijiji vya karibu na mlima huo.
Kufikia leo Ijumaa, Tanapa imeeleza kuwa ukaguzi wa helikopta umebainisha kuwa eneo kubwa lililoathirika na moto limedhibitiwa na kuwa maafisa kutoka idara ya zimamoto na Tanapa wapo katika meneo yote ambayo yameathirika ili kudhibiti moto huo.
Je, moto huo umeleta athari kiasi gani?
Taarifa ya Ijumaa ya Tanapa inabainisha kuwa, moto huo umeathiri eneo la kilomita 95.5 sawa na asilimia 5 la hifadhi lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1700.
Waziri Kigwangala pia ameeleza kuwa katika eneo la Horombo, moto huo umeunguza mabanda 12 ya watalii, 10 ya kawaida na mawili ya wageni mashuhuri, mitambo miwili ya umeme wa jua na vyoo viwili.
""Shughuli za kitalii zinaendelea kufanyika katika njia zote za kupanda Mlima Kilimanjaro na utafiti umeonesha hakuna njia ambayo imeathiriwa na moto huo," ameeleza Kigwangalla.















