Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Namna gani unaweza kujitengenezea bahati ?
"Bado ni mzima!" alisema afisa polisi alipomkuta katika gari lililoharibika vibaya kutokana na ajali.
Ingawa miaka mingi imepita, Christian Busch anakumbuka maneno hayo ambayo wakati alipoapata ajali iliyombadilisha maisha yake.
Busch ni mhadhiri katika chuo kikuu cha New York na shule ya uchumi ya mjini London (LSE)
Kama mtafiti aliangazia ujasiriamali pamoja na masuala ya kijamii, ubunifu na kukua kwa masoko.
Alijumuishwa kati ya watu 99 wenye ushawishi zaidi duniani katika jarida la Diplomatic Courier, "watu wenye mawazo ya uchumi katika The Economist na "Davos 50".
Katika kitabu alichokichapisha hivi karibuni kinachoitwa: 'The Art & Science of Creating Good Luck ' kimeangazia umuhimu wa kufanya kitu sahihi kwa kutumia fursa ambazo hata hazikuwa zinatarajiwa, si kwa upande wa taaluma pekee bali hata binafsi.
"Watu wengi wanahofia uwezo wa kutumia fursa ya nafasi iliyopo.
Lakini waliangalia takwimu na kuona wazi kuwa vitu ambavyo havitarajiwi huwa vinatokea tu kila wakati, hivyo ni sawa kuwa tayari kwa ajili ya chochote kile .
Leo hii si kawaida kwa kampuni kuanzisha nafasi kama ya kugundua kile ambacho hakikutarajiwa.
"Mjerumani mwenye asili ya Mexico"
Busch alikuwa nchini Ujerumani na kusoma pamoja na kufanya kazi katika nchi mbalimbali zikiwemo Urusi, China, Kenya, na Mexico ambako aliishi muda mwingi mpaka sasa.
Kwa mujibu wa Busch, mara nyingi watu tunaowaita wana bahati huwa wamepitia mlolongo mrefu wenye ubunifu wa aina yake na kukabiliana na hali ambazo hawakutarajia kukutana nazo.
Je kuna watu kwa asili tu kuwa ni zaidi ya wengine, au wanaona fursa zaidi ya wengine katika hali ambazo hazikutarajiwa?
"wanafanya vitu tofauti, " alijibu. "Changamoto kubwa ambayo ni muhimu ni kukubali kuwa hatuwezi kupanga kila kitu."
" Kukubali makosa kuwa sehemu ya maisha yetu kwamba makosa yanaweza kutokea kwa bahati mbaya."
Haya hapa ni majibu ambayo yalitolewa kwa BBC.
Kabla ya kupata ajali alijiona kuwa ana uwezo wa kufanya mambo mengi sana lakini alipogundua ni rahisi kiasi gani kupoteza maisha, na kutojiamini sana kupita kiasi.
Aliainisha suala la kuwa dunia inabadilikabadilika na ujuzi ambao unatengenezwa ni kuwa na bahati.Je ni namna gani bahati inaweza kutengenezwa.
Covid-19 imeweza kutukumbusha historia ya mchakato wa namna binadamu anavyokuwa tegemea jambo ambalo halifahamiki.
Licha ya kuwa mbali kutokana na janga la corona , lazima kutafuta namna ya kuhusiana kwasababu fursa na mawazo yanaweza kutokana na kuhusiana.
Katika wakati huu wa janga la corona,maisha yetu ya kila siku yamebadilika , na tumeshuhudia jinsi watu walivyokuja na ubunifu wa aina mbalimbali.
Kwa mfano Ujerumani, pombe zilipopigwa marufuku ,vitakasa mikono 'sanitizers' zikaanza kuuzwa kwa bei nafuu.
Mtu ambaye amehusiana si tu kwa yale ambayo ni muhimu sana kwao lakini bado pia kwa watu ambao wana thamani katika maisha yao.
Katika wakati wa majanga, jitihada za namna hii huwa zina msukumo wa uhitaji . Lakini utafiti na sayansi ya jamii unaonesha kuwa fursa huwa zinakuja bila kutarajia na huwa ni matokeo ya mambo ambayo hayakupangwa au kufanyiwa maamuzi.
Bahati nzuri 'smart luck' ina utofauti na bahati ya mtu ambaye haoni 'blind luck lakini huwa inatokea tu labda katika familia .
Inatokea tu labda kwenye tukio dogo na kubadili maisha au hata kubadili dunia kabisa.
Kuna mifano mingi katika sayansi na dawa katika suala la bahati.
Mara nyingine dawa hiyohiyo inaweza kumponya mtu na kwa mwingine ikasababisha madhara.
Kwa mujibu wa mtafiti, inawezekana kwa mtu kujitenenezea bahati nzuri .
Lakini unawezaje kutengeneza bahati nzuri?
Kile ambacho tunaweza kukifanya ni kufanya mambo ambayo yataleta matokeo chanya. Kuweka fikra zetu kuruhusu bahati nzuri ijengeke katika maisha yetu.
Nini kinachofanya wengine kuwa na bahati zaidi ya wengine.
Katika utafiti wetu tumebaini kuwa watu ambao wenye maendeleo makubwa na ushawishi katika maeneo mengi duniani, wengi wao huwa wanatengeneza fikra zao kuwa wako tayari na hali hiyo inawafanya wawe wabunifu zaidi na kupata msukumo wa kutaka kufanikiwa na kubadili dunia.