Virusi vya Corona: Hali mbaya ya hewa inapochanganyika na janga la Corona

Evacuated people sit in a temporary cyclone relief shelter as Cyclone Ampha

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Kimbunga cha Ampha
Iliyochapishwa

Matukio ya hali ya hewa yamelazimisha watu kutofuata taratibu za kukabiliana na mlipuko wa corona kwa kukaa kwa umbali, kwa mujibu wa shirikisho la kimataifa la Msalaba mwekundu(Red cross) na wakala wengine wa masuala ya kibinadamu.

“ Watu kukaa kwa umbali limekuwa jambo gumu kufuatwa kwa sababu watu ambao wamepoteza makazi yao kutokana na mvua imebidi wakae katika kituo", Marshal Makavure, mratibu wa operesheni za dharura wa IFRC mashariki mwa Afrika BBC.

“Watu wanalazimishwa kuvunja taratibu za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa corona kutokana na hali hiyo kujitokeza.”

BBC imezungumza na watu ambao wanaishi katika maeneo ambayo matukio ya hali ya hewa imesababisha hali ya maisha kuwa ngumu na watu kupoteza makazi yao.

India

Subrat Kumar Padhihary, mkulima mwenye umri wa miaka 38-kutoka jimbo la Odisha fukwe za mashariki ya India, ana hofu.

Maofisa wa India wametoa angalizo kuhusu kimbunga cha Amphan, kupiga Magharibi mwa Bengal na Odisha siku ya Jumatano, inaonekana kusababisha dhoruba kubwa zaidi.

Kijijini kwake Subrat, ambako ni takribani kilomita 40 kutokea eneo la bahari.

Nyumba yake ambayo alikuwa akiishi na mke wake, mabinti zake watatu na mama yao ilikuwa imeharibika vibaya sana na kimbunga cha Fani kilichotokea mwaka jana, hivyo ana hofu kama wataweza kuhimili dhoruba la sasa la kimbunga Amphan.

Lakini hata kama nyumba yake ikipona kipindi hiki, anahofia kuwa wanapaswa kuhama kijiji hicho kama mamlaka itasema kuwa wanapaswa kuondoka ili wasije kupata athari na hali hii.

Subrat anahisi kuwa hali inaweza kuwa hatari zaidi.

Subrat Kumar Padhihary and his family

“Hofu yangu ni kuwa tutahamishiwa katika shule za karibu ambazo zimegeuzwa kuwa makazi ya karantini kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya corona.

“Hakuna vituo vingi katika kijiji chetu na hali hiyo inaweza kusababisha watu watumie kwa pamoja sehemu za watu ambao wanaweza kuwa na virusi vya corona na hiyo ni hatari zaidi.”

“Magharibi mwa jimbo la Bengal limekuwa likiangaika na janga la ugonjwa wa Covid-19 na sasa hofu imehamia kwenye kimbunga,” kwa mujibu wa Siddarth Srinivas, kutoka shirika la Oxfam barani Asia.

“hapo nyuma, baadhi ya majimbo nchini India waliwaokoa watu na kuwaweka katika shule na majengo ya umma lakini wazo kubwa lilikuwa ni kuwalinda na mlipuko wa ugonjwa wa corona.”

Uganda

Magharibi mwa Uganda ni miongoni mwa maeneo ambayo mafuriko yalipiga hivi karibuni huku watu wapatao mia moja wakiwa wamebaki bila maeneo ya kuishi.

Joseline Kabugho ana ujauzito wa miezi sita.

Mwanamke huyo mwenye miaka 23 amelazimika kuhama makazi yake yeye pamoja na watoto wake wawili na kuhamia kwenye shule ambayo ilibadilishwa kuwa kambi katika wilay hiyo.

Anakaa katika makazi hayo licha ya kwamba yanaweza kuwa hatari kutokana na hali yake ya ujauzito na yuko katika kundi hatari la watu ambao wanaweza kupata maambukizi ya virusi vya corona.

Kuna watu zaidi ya 200 ambao mafuriko yalisababisha wahame makazi yao.

The school-turned temporary shelter where nearly 200 people displaced by floods in a village of Kasese district of Uganda are taking shelter

Chanzo cha picha, Jokus, Red Cross

“Sisi ni watu ambao hatujiwezi sasa,” alisema akiwa anaishi katika darasa amalo wanaishi na familia nyingine tatu, haya ndio makazi yangu ya muda. “Siwezi kukaa mbali na watu wengine kwa sababu ya eneo kuwa dogo.

“Nina hofu kuwa ninaweza kupata virusi na ninahofia watoto wangu na mtoto ambaye yuko tumboni,” dada huyo aliiambia BBC.

Joseline alikuwa amelala karibu na watoto wake wawili usiku wa kuamkia Mei,7 , wakati aliposikia wanakijiji wengine wakipiga kelele.

“Baadae niligundua kuwa majirani zangu walikuwa wanataka nikimbie ili niokoe maisha yangu.

Kijiji chote kilikuwa kimepigwa na mafuriko makubwa.

“Niliwashika watoto wangu wawili na kukimbia, sikuwa na muda wakubeba chochote kile."

Nilinunua nguo kidogo kwa ajili kwa ajili ya mtoto ambaye hajazaliwa kabla ya mafuriko kutokea. “Sikuweza hata kuokoa nguo hizo, mafuriko yalichukua kila kitu.

“Kila kitu tulichokuwa nacho kilienda na maji."

Joseline and her two kids in a school classroom in Uganda's Kasese district where she has taken refuge after the floods

Chanzo cha picha, Jokus, Red Cross

Mume wangu anafanya kazi katika wilaya nyingine na ameshindwa kusafiri kutokana na marufuku ya kusafiri kutokana na mlipuko wa corona.

“Sina sehemu ya kwenda na sijui nini cha kufanya baada ya hapa.”

Chama cha msalaba mwekundu kinasema kuna maelfu ya watu ambao hawana makazi na sasa wanaishi kanisani na katika shule, mara baada ya mafuriko kupiga mataifa ya Afrika mashariki na kufanya suala la watu kupata maji na sabuni kuwa jambo gumu.

Mamia ya watu wamefarki na maelfu kupoteza makazi yao kwa sababu ya mafuriko katika ,mataifa mengi.

Zaidi ya vifo 2,700 vilivyotokana na Covid-19 na wagonjwa wa corona 82,000 wamethibitika barani Afrika kwa mujibu wa chuo kikuu cha John Hopkins.

Miongoni mwa mataifa ambayo yalikumbana na athari hizo katika mataifa ya Afrika mashariki ni pamoja na Somalia ambako kuna idadi kubwa ya vifo ya watu 55 na kufuatiwa na vifo 50 nchini Kenya na 21 nchini Tanzania.

Fukwe za Pacific

Kimbunga Harold kilipiga fukwe za Pacific zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Baadhi ya nchi ambazo zimeathirika na majanga haya ziliwabidi kuachana na makatazo yaliyowekwa kuzuia maambukizi ya corona ili kuwaruhusu watu waokoe maisha yao kwa kukaa katika kambi.

Ingawa kuna watu bado katika vituo vya dharura lakini kwa sababu ya mlipuko jitihada za uokoaji zimeathirika pia.

Kimbunga kikali kupiga nchi hiyo, Vanuatu, imeongezeka katika hali ya dharura ya watu zaidi ya 92,000 kuathirika, kwa mujibu wa Unicef.

Huko Fiji, vituo vipatavyo 10 operesheni ya uokoaji inaenda taratibu kwasababu nyumba nyingi bado hazijajengwa.

“Upatikanaji wa maji bado ni changamoto kubwa wakati kimbunga kilivyopiga na kusababisha miundombinu ya kusambaza maji kuwa migumu,” alisema Vani Catanasiga, mkurugenzi wa manispaa ya huduma za Fiji.

“Bila upatikanaji wa maji, kufuatia maagizo ya kuzingatia usafi ili kuzuia maambukizi ya Covid-19 hali inakuwa ngumu sana, licha ya kwamba serikali ya Fijian imefanikiwa kukabiliana na janga la Covid-19.”

Wakala wa masuala ya kibinadamu wanasema kuwa , operesheni hiyo itakuwa rahisi kama masharti yatalegezwa.

Mfanyakazi wa msalaba mwekundu, Irene Nakasiits anagawa maji na sabuni kwa watu ambao wamehama makazi yao kutokana na mafuriko katika jamii za magharibi ya Uganda.

“Ingawa kuna changamoto katika kuhakikisha jambo hilo linafanyika, bado tunaweza kuwakumbusha jamii ambazo zimeathirika kufuata miongozo iliyowekwa ili kujizuia kupata maambukizi ya corona ” kwa mujibu wa Marshal Mukuvare kutoka IFRC.

“Tunaweza kuwa na ujumbe ulioandikwa katika chakula na misaada mingine, ambayo inapelekwa kwa wahanga wa mafuriko.

“Hali hii itasaidia watu kufanya kile ambacho wanaweza hata wakiwa katika hali ngumu inayowakabili.”