Virusi vya corona: Waziri Mkuu Boris Johnson alazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amelala hospitalini katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya afya yake kuzorota kutokana na virusi vya corona.
Afisi yake imesema kwamba alipelekwa katika chumba hicho kutokana na ushauri wa madaktari wake na kwamba alikuwa akipokea uanagalizi wa karibu sana.
Bwana Johnson amemtaka waziri wa maswala ya kigeni Dominic Raab kumsaidia pale atakapoweza, msemaji alisema.
Waziri mkuu mwenye umri wa miaka 55 alilazwa katika hospitali ya St. Thomas akiwa na dalili kali za virusi vya ugonjwa huo siku ya Jumapili jioni.
Malkia amekuwa akiarifiwa kuhusu afya ya Johnson kulingana na kasri la Buckingham.
Viongozi mbalimbali duniani akiwemo rais Donald Trump na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamemtumia risala za heri njema bwana Johnson.
Mwandishi wa maswala ya kisiasa wa BBC Chris Mason alisema kwamba waziri mkuu alipatiwa oksijen baadaye siku ya Jumatatu mchana kabla ya kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Alisahamishwa kama hatua ya kuchukua tahadhari ili awekwe karibu na mashine ya kumsaidia kupumua , alisema mwandishi huyo.
Mapema Jumatatu ujumbe uliandikwa kwenye mtandao wa Twitter ukiashiria kwamba anaendelea kupata afueni.
Aliongezea kwamba yeye na wenzake walikua wanahakikisha kwamba wanatekeleza mipango ya bwana Johnson haraka iwezekanavyo.
''Kupitia njia tutaweza kuliepusha taifa zima na changamoto ya virusi vya corona''.

Chanzo cha picha, PA Media
Bwana Johnson alikuwa amepekekwa hospitalini kufanyiwa vipimo baada ya kutangaza siku 11 zilizopita kwamba alikuwa ameambukizwa virusi vya corona.
Dalili alizokuwa nazo ni pamoja na viwango vya juu vya joto na kikohozi.
Mapema siku ya Jumatatu, alituma ujumbe katika mtandao wake wa twitter akisema kwamba yuko katika hali nzuri.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Je chumba cha wagonjwa mahututi ni chumba cha aina gani?
Vymba vya wagonjwa mahutiti ni wadi maalum zilizojengwa kutoa tiba na uangalizi wa karibu kwa wagonjwa walio katika hali mahututi.
Vyumba hivyo huwa na wagonjwa wachache na madaktari wengi ili kutoa uangalizi wa moja kwa moja unapohitajika.
Vyumba hivyo hushirikisha vifaa vya uangalizi .
Kuna vitanda 4,000 vya wagonjwa mahututi katika hospitali mpya ya Nightingale.

Chanzo cha picha, PA Media
Ni nani anayehitaji uangalizi wa karibu?
Kuna sababu nyingi tofauti kwanini mtu huenda akahitaji uangalizi ka a huo. Wagonja wengi uhitaji ili kupona baada ya kufanyiwa upasuaji.
Wengine wanahitaji chumba hicho baada ya kuumia vibaya , kufuatia ajali ya barabarani kwa mfano.
Waziri mkuu amewpelekwa katika chumba hicho kwa sababu dalili zake za virusi vya corona hazijaondoka.
Virusi vya corona hushambulia mapafu na inaonekana kwamba waziri mkuu kwa sasa ana matatizo ya kupumua ijapokuwa bado hajawekwa katika mashine ya kusaidia kupumua au ventilator.
Ni uangalizi gani unaotolewa?
Sio kila mgonjwa wa virusi vya corona aliyewekwa katika uangalizi wa karibu katika chumba cha wagonjwa mahutiti anahitaji usaidizi wa kupumua.
Wengine wanaweza kuwekwa katika mashine za kusaidi kupumua kwa jina CPAP ambazo hutumia nguvu nyingi kupeleka oksijeni mwilini.
Wagonjwa wanaweza kuwa macho wakati wa shughuli hiyo ikilinganishwa na wale wanaohitaji mashine za kusaidiwa kupumua.
Wagonjwa waliopo katika chumba mahututi miili yao hunganishwa na mashine nyingi tofauti , kupitia mipira, nyaya ili kuangalia jinsi miili yao inavyoendelea.
Na wanaweza kupatiwa madawa kupitia mishipa yao ya damu
Mrithi wa waziri mkuu
Hakuna mrithi wa moja kwa moja wa waziri mkuu nchini Uingereza kwa kuwa haijaidhinishwa katika katiba ya taifa hilo.
Taifa hilo hutegemea mifano na iwapo kutakuwa na matokeo yoyote yasio ya kawaida basi uamuzi utachukuliwa baada ya tukio hilo.
Tuizuru ofisi ya waziri mkuu na maambukizi ya Virusi vya Corona mpaka sasa
March 10: Waziri wa afya Nadine Dorries alikua mbunge wa kwanza kupima virusi vya ugonjwa huo, muda mfupi baada ya kuhudhuria mapokezi ya Mtaa wa Downing.
March 27: Waziri mkuu Boris Johnson na Katibu wa Afya Matt Hancock wote wawili wakaachia video zao kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter wakisema wana uambukizo wa corona na wanajitenga.Saa kadhaa baadaye , afisa mkuu wa matibabu Profesa Chris Whitty alifichua kuwa alikuwa akijitenga na dalili.
March 30: Mshauri mkuu wa waziri mkuu Dominic Cummings naye aliarifiwa kujitenga binafsi na uambukizo wa virusi hivyo
April 2: Matt Hancock anarudi kazini baada ya watu saba kufa wakati alipokuwa kwenye karantini akiwa na ahueni kubwa.
April 3; Boris Johnson aachia video akiwa kwenye ghorofa yake ya Namba 11 akisema anaendelea kujitenga kwani bado anapata homa na inapanda.
April 4: Carrie Symonds, ni mchumba wa waziri mkuu Borisi ambaye kwa sasa ni mjamzito naye amekuwa akijitenga katika chumba chake huko Camberwell.
April 5: Waziri mkuu apelekwa hospitalini 'kwa tahadhari'.
April 6: Ofisi ya waziri mkuu yakataa kutoa taarifa wazi zaidi kumhusu na msemaji wake asema bado ana kikohozi cha 'kuendelea' na joto mwilini
April 7; Waziri mkuu Boris Johnson ahamishiwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya St Thomas na nafasi yake kukaimiwa na waziri wa Mambo ya nje Dominic Raab.













