Mashine inayotafsiri shughuli za ubongo katika sentensi

Mashine inayotafsiri shughuli za ubongo katika sentensi

Chanzo cha picha, SPL

Maelezo ya picha, Mashine inayotafsiri shughuli za ubongo katika sentensi
Iliyochapishwa

Wanasayansi wameweza kuongeza utaalamu zaidi wa kutambua jinsi binadamu anavyozungumza kwa kuangalia mfumo wa ubongo wake.

Wataalamu wameweza kuhamisha mfumo wa ubongo katika jinsi sentensi zinavyoundwa katika uhalisia na kupata kiwango cha makosa cha asilimia tatu katika neno.

Awali mashine ya ubongo ilikuwa ina uwezo mdogo wa kutambua vitu kwa namna hiyo.

Utafiti huo ulichapishwa katika jarida la 'Nature Neuroscience'.

Awali mfumo huo wa ubongo ulikuwa unaweza kutambua maneno ambayo yanayoongelewa kwa asilimia ndogo ya maneno.

Mtaalamu wa kusoma mashine hiyo ya ubongo Dkt Joseph Makin kutoka chuo kikuu cha California, San Francisco (UCSF), Marekani wamejaribu kuboresha kuhakikisha kuwa inasoma ipasavyo.

Watu wanne waliojitolea waliweza kusoma sentensi wakati mashine hiyo ikisoma shughuli ambazo ubongo unafanya.

Shughuli za ubongo zinaweza kuwa katika mfumo wa komputa, ambapo unaweza kuwasilisha maelezo ya takwimu Fulani.

Upande wa Lugha

Sifa ambazo zinaweza kufanya ubongo kufikia kusoma sentensi huwa inategemea muundo wa sentensi kuanzia kwenye herufi, maelekezo ya matamshi kama ni swali au amri?

Namna nyingine ambayo inafanya mashine hiyo itambue neno kwa neno mpaka sentensi inapoundwa ni idadi ya sentensi.

Mfano hotuba inaweza kunakiliwa katika mfumo huo kuanzia sentensi 30- 50.

Ingawa tunataka kufahamu pia kama mfumo huo unaweza kutambua lugha tofauti na kiingereza, watafiti wameandika bado wanafanya utafiti zaidi ili kutambua hilo.

Lakini waliongeza kuwa mashine hiyo haitambui sentensi kwa namna ilivyoundwa.

Wamelitambua hili kwa kadri walivyojaribu kuongeza sentensi.

Wanasayansi wanasema kuwa , mashine inaweza kutambua neno moja na sio sentensi. Hii ikimaanisha kuwa kuwa uwezekano wa sentensi kutotambuliwa wakati wa mafunzo yao.

Wakati mfumo wa komputa ulipopewa mafunzo ya jinsi ubongo unavyofanya kazi na maneno ya mtu kabla ya mafunzo, matokeo yake yanaonyesha kuwa kuna mabadiliko makubwa na vyema teknolojia hiyo ikatumike kwa watu wengine.