Rivaldo: Kigogo wa Brazil na Barcelona ambaye umaskini wa utotoni ulimnyima ndoto ya kung’aa

Rivaldo

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Gwiji wa Brazil na Barcelona - Mtazamo wa Rivaldo ulibainishwa na malezi yake
Iliyochapishwa

Mapema miaka ya 1991, kijana wa miaka 18- alisimama ndani ya duka la kuoka mikate huko Paulista, eneo la Recife kaskazini mashariki mwa Brazil, akisubiri kuhojiwa na vyombo vya habari vya ndani. Alionekana mdogo sana kama mchezaji wa soka.

Hivi majuzi aligonga vichwa vya habari baada ya kufungia bao Santa Cruz kwa kutumia kichwa. Kutokana na hilo, ripota wa Televisheni alimtafuta ikwa nia ya kujadali matarajio yake ya kazi.

"Ndoto yangu tayari inatimia; kuchezea Santa Cruz. Natumai kufanikiwa zaidi na kuwa mtu anaye enziwa zaidi na mashabiki wa kalabu hii."

Sasa anaweza kutazama kazi ambayo sio tu ilizidi matarajio yake mwenyewe, lakini pia kupinga imani kwamba lazima tuwe na ndoto kubwa ili kupata mafanikio makubwa.

Ndani ya mwongo mmoja baada ya mahojiano hayo, alishinda tuzo ya Ballon d'Or, kutajwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa Duniani na kufungia Barcelona kile wengi hukiona kuwa hat-trick bora zaidi wakati huo.

Kufikia 2002, alikuwa amebeba Kombe la Dunia kama kiungo muhimu katika kikosi cha Brazil cha soka kilichoogopwa- Ronaldo, Ronaldinho, Rivaldo. Mwaka mmoja baadaye aliongeza taji la Champions League akiwa na AC Milan.

Kuwa na ndoto kubwa, wanasema. Isipokuwa wakati ambapo malezi yako hayakuruhusu.

Short presentational grey line

"Inabidi uishi katika umaskini ili kujua umaskini ni nini," Rivaldo aliambia jarida la soka la Argentina El Grafico mwaka 1999.

"Unafanya kazi siku nzima na kupata malipo sana, au kukosa kazi kabisa na kualala njaa, kuteseka."Mjini Paulista ni vigumu kuota."

Rivaldo Vitor Borba Ferreira alikulia viungani mwa Recife eneo ambalo watalii hawakupenda kukaa na wenye ndoto walipachukulia kuwa masikini.

Alipokuwa mvulana mdogo aliwasaidia wazazi wake siku za weekend kulima katika shamba lao dogo nyumbani na kuuza peremende katika fukwe maarufu za mji. Siku za mechi alienda kutazama soka katika uwanja wa nyumbani wa Estadio do Arruda, makao makuu ya klabu yake pendwa ya Santa Cruz.

Walimu wa Rivaldo walimuelezea kama kijana muoga ambaye alichelea hata kusoma kwa sauti darasani, lakini alikuwa na nidhamu kuliko kaka zake wawili wakubwa. Alipendelea kucheza mpira wa miguu bila viatu, akiwaenzi wachezaji soka kama vile Zico na Diego Maradona.

Marafiki zake wa utotoni wanakumbuka jinsi alivyokuwa na uwezo mkubwa wa kucheza soka, akiudhibiti mpira kana kwamba umekwama kwenye miguu yake na kuupiga kwa nguvu za kushangaza kwa mtoto mdogo kama huyo.

Akiwa na miaka 13, Rivaldo alipokea zawadi ya kwanza ya vya kucheza mpira kutoka kwa baba yake Romildo. Mwaka mmoja baadaye alialikwa kwa majaribio ya kuichezea Santa Cruz, baada ya kufanya mazoezi na ya mara kwa mara alipokuwa katika timu ya chipukizi ya klabu hiyo.

Wiki mbili kabla ya majaribio hayo, Romildo aligongwa vibaya na basi. Mwanawe alifadhaika sana, alikuwa tayari kuacha mchezo na kujisalimisha kwa mazingira yake, akijiambia kuwa furaha na mafanikio sio ya wavulana kutoka eneo lake.

Rivaldo alibadili mtazamo huo wa maisha baada ya mama yake Marlucia kusema naye. Alimkalisha chini na kumwambia: "Baba yako hangetaka chochote zaidi ya wewe kuwa mwanasoka wa kulipwa. Fanya hivyo."

Na bila shaka alifanya hivyo.

Rivaldo, katika picha ya mwaka 1997 baaada ya kuhamia Barcelona

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Rivaldo, katika picha ya mwaka 1997 baaada ya kuhamia Barcelona

Jaribio lilifanikiwa, lakini changamoto mpya ziliibuka hivi karibuni. Kituo cha mafunzo cha Santa Cruz kilikuwa kilomita 15 kutoka nyumbani kwao na hakuwa na nauli ya kwenda na kurudi nyumbani kila siku. Rivaldo alilazimika kutembea kilomita 30 kwenda na kurudi kila siku. Alifika akiwa amechoka na kuondoka akiwa amechoka - matege kwenye miguu yake ilionekana zaidi.

Licha ya kujitolea kwake, sifa ilikuwa ngumu kupatikana. Alihukumiwa vikali - na hali hiyo iliendelea kuwa kwa sehemu kubwa ya kazi yake, hasa miongoni mwa Wabrazil.

Utendakazi usiokuwa wa kuridhisha uliashiria siku zake za kwanza Santa Cruz na haikuchukuwa muda alianza kutumiwa kama kisingizio cha klabu hiyo kutofanya vyema.

Baada ya kukosewa heshima, kuzomewa na mashabiki na kupuuzwa na makocha, hatimaye alitumiwa katika mkataba wa kubadilishana wachezaji na klabu ya Mogi Mirim ya daraja la pili mjini Sao Paulo. Joao Caixeiro, rais wa zamani wa Santa Cruz, baadaye alitaja hatua hiyo kuwa "mkataba mbaya zaidi katika historia ya klabu hiyo".

Rivaldo alitumia miaka minne iliyofuata kujilimbikizia sifa kedekede uwanjani lakini hakukubalika kama alivyotarajia.

Akiwa Mogi, alifanikiwa kufanya kile alichofanya gwiji wa soka Pele - Kufunga bao kutoka mbali ya lango.Alipotolewa kwa mkopo kwa klabu ya Corinthians mwaka 1993, alifunga mabao 22 katika mechi 58 alizoanza kwa njia ya ustadi wa hali ya juu na kutajwa kuwa mchezaji bora wa msimu na kufunga kwenye mechi yake ya kwanza ya kimataifa dhidi ya Mexico.

Baada ya kurejea Sao Paulo kujiunga na Palmeiras, alishinda taji la mwaka 1994 la Ligi Kuu ya Brazil na kutajwa kuwa mchezaji wa msimu wa kwa mara nyingine tena. Uthabiti kama huo ulizawadiwa na kujumuishwa zaidi kwenye timu ya taifa, lakini kocha Carlos Alberto Parreira aliamua kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa "mbinafsi sana" na "haaminiki", akimuacha nyumbani wakati Brazil ikiendelea mbele kushinda Kombe la Dunia la 1994.

Kufikia 1996 baada ya Parreira kuondoka, Rivaldo alijumuishwa katika kikosi cha kitaifa kwa Michezo ya Olimpiki ya Atlanta. Kwa mara nyingine tena, aliishia kubebeshwa lawama.

Katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Nigeria Nigeria, Brazil iliongoza kwa mabao 3-1 lakini dakika 12 kabla ya mechi hiyo kuisha alipoteza udhibiti wa mpira katika safu ya kati na kuwafanya Waafrika hao kutia kimyani bao la pili.

Nigeria ilifunga mabao mawili zaidi na kuibandua Brazil katika kinyang'anyiro hicho, kwa kuwa Rivaldo aliyepoteza nafasi ya kufunga bao hali haikuwa nzuri kabisa, baada ya mechi kuisha alifadhaika na kulia kwa masikitiko makubwa katika chumba cha kubadilisha nguo.

"Mechi dhidi ya Nigeria ilishutua kila mtu kwa sababu matarajio yalikuwa kwamba tungeshinda medali ya dhahabu," mchezaji mwenza wa zamani Luizao aliambia BBC Sport.

"Kwa bahati mbaya ulikuwa mchezo wa kawaida na kila mtu alikuwa na huzuni - Rivaldo zaidi kuliko mtu yeyote kwa sababu alipokea shutuma nyingi. Daima alikuwa mchezaji mwenye haiba kubwa, akijiamini sana."

Alipoulizwa kuhusu hilo miaka kadhaa baadaye, Rivaldo aliongeza: "Nina kumbukumbu chungu ya kipindi hicho, lakini iliniruhusu kupata motisha ya kuonyesha ukosoaji uliofanywa kwangu haukuwa wa haki."

Kocha Mario Zagallo, aliyekabidhiwa jukumu la kuiongoza Brazil katika Kombe la Dunia nchini Ufaransa mnamo 1998, alipuuza hadharani nafasi ya Rivaldo kuiwakilisha nchi yake. Lakini yeye, na wapinzani wengine wengi, hawakuwahi kufikiria ni nini kingetokea.

Short presentational grey line