Faith Kipyegon ni bingwa wa mbio za mita 1500 duniani upande wa wanawake
Faith Kipyegon alivunja rekodi ya michezo ya Olimpiki mjini Tokyo alipotetea taji lake la mbio za mita 1500m aliloshinda mjini Rio de Jeniro 2016. Mkenya huyo alitoa ushindi huo kwa bintiye mwenye umri wa miaka mitatu, ambaye anamsifu kwa kumpa motisha zaidi baada ya kuchukua mapumziko ya miezi 21 kutoka kwa mchezo huo.
Kujitolea kwake kulikuwa muhimu zaidi kwani Kipyegon ni mwanariadha wa tatu pekee kuhifadhi taji la Olimpiki baada ya kujifungua kati ya Michezo (pamoja na Shirley Strickland wa Australia, mwaka wa 1956, na Francoise Mbango wa Cameroon, mwaka wa 2008).
Kabla ya onyesho lake huko Japani, alikuwa ameweka muda bora zaidi duniani wa 3:51.07 - mara ya nne kwa kasi zaidi katika historia - na huko Monaco mnamo Julai katika mashindano ya Diamond League, hafla ambayo alitawazwa bingwa wa mwaka huo mnamo Septemba.
Baada ya rekodi yake ya Olimpiki, sasa analenga rekodi ya dunia.