Virusi vya corona: Victor Wanyama anaelezea jinsi Corona ilivyoathiri mipango
Iliyochapishwa
Janga la virusi vya Covid-19, limesababisha athari nyingi. Licha ya kusababisha vifo na kuugua, limesababisha watu kushindwa kuendelea na mipango yao ya kimaisha kama inavyotakikana. Mojawapo ya watu walioathiriwa na janga hili ni wachezaji wa Afrika wanaocheza soka la kulipwa nchi za ng’ambo. Mmojawapo ni Victor Wanyama mchezaji soka kutoka Kenya ambaye si muda mrefu amehamia katika timu ya Montreal Impact Canada. Ameiambia BBC jinsi corona ilivyoathiri maono yao...
