Je Urusi ilipuuza onyo la Marekani kuhusu shambulio la Crocus?

Chanzo cha picha, Reuters
Baada ya kila shambulio la kigaidi, maswali yasiyoepukika hutokea. Sababu kwa nini haikuzuiwa au kugunduliwa.
Hata hivyo, mashambulizi ya hivi majuzi huko Moscow yanazua maswali magumu hasa kwa Vladimir Putin huku kukiwa na mvutano wa kimataifa na kutoaminiana, kutokana na ujumbe wa onyo kutoka Washington.
Mnamo Machi 7, Marekani ilitoa onyo kwa raia wake, kwamba kulikuwa na uwezekano wa vikundi vya "itikadi kali" kushambulia mikusanyiko mikubwa huko Moscow, haswa katika matamasha.
Aliwashauri raia wa Marekani waliopo Urusi kuepuka au kutoshiriki katika matukio kama hayo katika muda wa saa 48 zijazo.
Ingawa muda unaweza usilingane vizuri, matukio na eneo la shambulio la jana pamoja na onyo lililotolewa ni sawa katika maeneo mengi.
Inaonekana wazi kwamba Washington ilijua au kupokea taarifa za kijasusi kuhusu IS, kundi lililodai kuhusika na shambulio la Moscow.










