Timu ya Navalny inasema mamlaka ya Urusi 'wanaficha' mwili wake
Msemaji wa Navalny, Kira Yarmysh, ameiambia BBC kuwa timu ya Navalny inaamini Vladimir Putin aliamuru kifo cha mwanaharakati huyo, ambaye bila shaka alikuwa mkosoaji maarufu wa rais wa Urusi.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Rais Samia aongoza waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa
Maelezo ya video, Rais Samia katika msiba wa Eduard Lowassa Rais Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza mamia ya waombolezaji kwenye mazishi ya aliyekuwa waziri mkuu na mwanasiasa mkongwe Edward Lowassa kwenye makazi yake wilayani Monduli jijini Arusha.
Lowassa alifariki dunia Februari 10,2024 kwenye taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam.
Katika picha: Mazishi ya aliyekua waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa

Chanzo cha picha, Ikulu /Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu/Tanzania

Chanzo cha picha, ikuku/Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu/Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu/Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu/Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu/Tanzania

Chanzo cha picha, Ikulu /Tanzania
Timu ya Navalny inasema mamlaka ya Urusi 'wanaficha' mwili wake

Maelezo ya picha, Kira Yarmysh alizungumza na BBC Jumamosi asubuhi Timu ya Alexei Navalny imedai mwili wake unazuiliwa makusudi na serikali ya Urusi.
Msemaji wa Navalny, Kira Yarmysh, ameiambia BBC kuwa timu ya Navalny inaamini Vladimir Putin aliamuru kifo cha mwanaharakati huyo, ambaye bila shaka alikuwa mkosoaji maarufu wa rais wa Urusi.
Alisema: "Tunajua kwa hakika kwamba haikuwa kifo tu, ilikuwa mauaji.
"Wanajaribu kuficha athari, ndio maana hawatoi maiti kwa familia yake na ndio maana wanamficha tu wasimwone."
Yarmysh alisema hajui mwili ulipo na lini utatolewa kwa familia ya Navalny.
Ameeleza kuwa kwa mujibu wa sheria za Urusi, mwili wa mfungwa unapaswa kupewa jamaa ndani ya siku mbili baada ya kifo.
Hapo awali, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilisema ilikataa tathmini "za upendeleo na zisizo za kweli" kutoka Uingereza kuhusu sababu ya kifo cha Navalny.
Wachunguzi wa Urusi wamesema mwili wa Alexei Navalny hautakabidhiwa kwa familia yake hadi uchunguzi utakapokamilika, kwa mujibu wa msemaji wa mwanaharakati huyo Kira Yarmysh.
Familia haijui ni wapi mwili wake umehifadhiwa .
Unaweza pia kusoma:
- Kinachojulikana kuhusu kifo cha Alexei Navalny, mwanasiasa wa Urusi ambaye alimpinga Putin
Msomali kutoka Marekani alijiunga na ISIS na kutishia kushambulia New York - Mahakama ya Marekani

Chanzo cha picha, US DEPARTMENT OF JUSTICE
Maelezo ya picha, Harafa Hussein Abdi, mwenye umri wa miaka 41, anayeishi Minneapolis, alijiunga na ISIS. Raia wa Marekani mzaliwa wa Somalia anakabiliwa na mashtaka baada ya kushtakiwa kwa kutoa "msaada wa nyenzo" kwa kundi la kigaidi la Islamic State, alipokuwa akielekea kutoa mafunzo ya kijeshi katika kambi ya mafunzo ya Islamic State nchini Somalia, kwa mujibu wa wizara ya sheria ya Marekani
Harafa Hussein Abdi, mwenye umri wa miaka 41, anayeishi Minneapolis, alikamatwa hivi majuzi Afrika Mashariki na kupelekwa Marekani wiki hii, kwa mujibu wa ofisi ya Mwanasheria wa Marekani mjini New York.
Abdi alihama kutoka Minnesota mwaka 2015 katika jimbo la Somalia lililojitangazia uhuru wake la Puntland, na kujiunga na kundi la wapiganaji wa Daesh nchini Somalia.
Alijitokeza kwa mara ya kwanza katika mahakama ya shirikisho ya Manhattan siku ya Ijumaa.
Ameshtakiwa kwa kutoa msaada wa vifaa kwa shirika la kigaidi la kigeni haswa (ISIS) na kutoa mafunzo kwa aina ya wanajeshi ambao wameletwa Somalia.
'Ni Putin ndiye aliyemuua' - Biden asema kuhusu kifo cha Navalny

Chanzo cha picha, EPA
Alexei Navalny ni mmoja wa wanasiasa mashuhuri wa upinzani wa Urusi katika siku za hivi karibuni.
Rais wa Marekani Joe Biden anasema Rais wa Urusi "alimuua" mwanasiasa mpinzani, kufuatia ripoti kwamba amefariki.
Jeshi la magereza katika eneo ambalo Alexei Navalny alikuwa akitumikia kifungo chake lilitangaza kifo chake Ijumaa.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 47, mkosoaji mkubwa wa Rais Putin, alifungwa nchini Urusi tangu 2021, kwa mashtaka yanayoaminika kuwa ya kisiasa.
"Kilichotokea ni ushahidi mwingine wa ukatili wa Putin," Biden alisema.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron alisema kuwa "hakuna mtu anayepaswa kuwa na shaka yoyote kwamba utawala wa Putin nchini Urusi ni mbaya sana baada ya kile kilichotokea".
Ufaransa ilisema Navalny alijitolea maisha yake kwa kusimama na "ukandamizaji", wakati waziri wa mambo ya nje wa Norway alisema mamlaka ya Urusi ilihusika katika kifo chake.
Navalny 'alikufa bila kuvunjwa moyo na ukatili – Obama

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amemtaja Alexei Navalny kuwa "mtetezi asiye na woga wa imani yake ambaye alikufa bila kuvunjwa moyo na ukatili alioupinga".
Obama amesema : "Alipambana na ufisadi, alihamasisha mamilioni ya watu na kamwe hakutetereka katika msisitizo wake wa uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria, na Urusi inayowajibika kwa watu na sio dikteta.
"Alikufa katika kutetea maono yake ya mustakabali bora kwa nchi yake - maono, na mfano wa ujasiri, ambao hautakufa kamwe.
Viongozi wa Afrika wakutana Adis Ababa huku bara likikumbwa na vita na ukosefu wa usalama

Viongozi wa nchi za Afrika wanakutana katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa kwa mkutano wa siku mbili wa kila mwaka wakati bara hilo likiendelea kukumbwa na vita, ukosefu wa usalama na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Elimu ni ajenda kuu lakini masuala mengine ikiwemo mgogoro wa Gaza- yanatarajiwa kujadiliwa.
Kuanzia Sudan , Senegal hadi eneo la Sahel, hali ya utulivu na mivutano ya kisiasa imekumba sehemu za bara hilo wakati Umoja wa Afrika ukianza mkutano wake wa kila mwaka.
Kinyume na shamra shamra ambazo huambatana na mkutano wa viongozi wa bara, Afrika bado inakabiliwa na changamoto ya umaskini na mabadiliko ya tabia nchi.
Na fursa nyingine ya jumuiya hiyo ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa kutokuwa na meno katika kushughulikia matatizo ya Afrika.
Karibu miezi miwili baada ya mkutano wa mwaka jana, Sudan ilitumbukia katika mgogoro mkubwa – inasubiriwa kuangalia iwapo mkutano wa mwaka huu utatoa suluhisho.
Suala moja ambalo huenda likawa katika ajenda ya mwaka huu ni vita vya Gaza. Katika miezi ya hivi karibuni, Umoja wa Afrika umekuwa ukipaza sauti katika kuilaani Israel, lakini nchi wanachama zimegawanyika katika suala hilo.
FGM: Mwanamke afungwa jela kwa kupeleka mtoto Kenya kukeketwa

Chanzo cha picha, LUCY NORTH/PA
Mwanamke mmoja amefungwa jela kwa kumpeleka mtoto wa Uingereza mwenye umri wa miaka mitatu nchini Kenya kujkeketwa (FGM).
Amina Noor, 40, kutoka Harrow, kaskazini-mashariki mwa London, alisafiri hadi Kenya mwaka 2006 ambapo alimpeleka mtoto katika nyumba ya kibinafsi kwa ajili ya utaratibu huo, mahakama iliambiwa.
Mahakama ya Old Bailey, Noor alipewa kifungo cha miaka saba jela.
Alikuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa kwa kumsaidia mtu ambaye si Muingereza kufanya ukeketaji.
Tahadhari: Makala taarifa hii ina maelezo ambayo baadhi yanaweza kuwa ya kuhuzunisha
Aliiambia mahakama ya Old Bailey kwamba ukeketaji ulifanywa kwa sababu za kitamaduni na ulikuwa utaratibu ambao yeye mwenyewe alikuwa amepitia kama mtoto.
Wakati wa hukumu ya awali, Jaji Bryan alisema "uhalifu huu wa kutisha na wa kuchukiza sana" uliacha maisha ya mwuthiriwa "yamebadilika na hayaweze kubadilishwa".
Aliongeza kuwa ukeketaji ni mila ambayo ilikuwa imeenea sana nchini Somalia na Kenya.
Jaji huyo alisifu "ujasiri wa msichana huyo kuzungumza na mwalimu" na kujitokeza na kusema anatumai kuwa "ujasiri utawatia moyo wanawake wengine kufanya vivyo hivyo".
Upande wa utetezi uliiambia mahakama ya Old Bailey siku ya Ijumaa kwamba Noor "alishawishiwa wakati huo kwa imani kwamba alikuwa akifanya kile ambacho kilihitajika kukubalika na utamaduni wake".
Mwendesha mashtaka Deanna Heer KC alikubali "shinikizo la kitamaduni" lililokuwepo, lakini akasema kuwa Noor "alishindwa kuingilia kati kumlinda" msichana.
Muathiriwa alisoma taarifa mahakamani, ambayo ilisema kwamba alikuwa ameathiriwa na kesi kuwa katika "uwanja wa umma", akionyesha jinsi alivyokosa raha kwa "wageni kuujadili mwili [wake]" hadharani.
Maandamano, kutoa heshima na kukamatwa huku kifo cha Navalny kikiombolezwa kote duniani
Kifo cha Alexei Navalny katika gereza la Urusi kimesababisha maandamano na watu wamejitokeza kutoa heshima kwake kote ulimwenguni.
Wafuasi wa mwanaharakati huyo wa kisiasa mwenye umri wa miaka 47 walikusanyika nje ya balozi za Urusi na maeneo mengine katika miji mikubwa duniani kote, ikiwa ni pamoja na London, Paris, Geneva na New York.
Mjini Berlin, umati mkubwa wa watu ulipiga kelele "Putin hadi Hague" na nje ya ubalozi wa Urusi mjini London waandamanaji walishikilia mabango yaliyosema "Navalny ni shujaa wetu".
Zaidi ya watu 100 walisimama mbele ya Umoja wa Mataifa huko Geneva ambapo walishikilia picha za Navalny na kuweka maua.
Pia kulikuwa na maandamano nchini Urusi.
Picha kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha vikundi vya watu wakiweka maua kwenye makaburi ya muda huko Moscow na Saint Petersburg.
Zaidi ya watu 100 wanaripotiwa kuzuiliwa katika miji mbali mbali ya Urusi.

Chanzo cha picha, Shutterstock
Maelezo ya picha, Maua na mishumaa vimewekwa nje ya ubalozi wa Urusi mjini Zurich, Uswizi 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mjini London, umati mkubwa wa watu uliinua mabango na kuimba nje ya ubalozi wa Urusi wa jiji hilo 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Huko Paris, mfuasi wa Navalny anaweka mshumaa kwenye mkesha katika kumbukumbu yake Unaweza pia kusoma:
- Matukio: Kwa nini Navalny alikuwa mpinzani mkuu wa Putin?
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 17.02.2024
