Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mateka wa Israel: IDF yasema iliwaua kimakosa wanaume watatu waliokuwa wanashikiliwa Gaza
Jeshi la Israel linasema limewaua kimakosa mateka watatu wakati wa shambulizi lake la Gaza baada ya kutambuliwa kimakosa kama "tisho".
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Habari za hivi punde, Jeshi la Israel lajibu mashambulizi kutoka kwa Hezbollah nchini Lebanon
Jeshi la Israel (IDF) linasema kuwa limejibu mashambulizi kadhaa kutoka Lebanon kuelekea Israel katika muda wa saa chache zilizopita.
IDF lilisema kuwa majengo ya kijeshi na "miundombinu ya kigaidi" mali ya Hezbollah - wanamgambo wenye nguvu wanaoungwa mkono na Iran nchini Lebanon - walikuwa wamepigwa na ndege za kivita kujibu mashambulizi.
Hezbollah imerusha mara kwa mara makombora yanayovuka mpaka tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba.
Vita vya Israel na Gaza vimesababisha kuzuka upya kwa uhasama kati ya Israel na Hezbollah kutokana na shambulio la Israel na kuwaua watu wanne, wakiwemo waandishi wawili wa habari, kusini mwa Lebanon mwezi uliopita.
Israel ilisema wakati huo ilikuwa ikijibu "tisho" katika eneo hilo.
Habari za hivi punde, Jeshi la Israel lasema mateka waliouawa walikuwa wameshikilia fimbo zenye vitambaa vyeupe
Mateka watatu wa Israel ambao waliuawa kimakosa Gaza na jeshi la Israel siku ya Ijumaa walikuwa wameshikilia kitambaa cheupe kwenye fimbo, IDF inasema.
"Mateka walipigwa risasi kinyume na sheria ya Israeli," afisa wa IDF anasema.
Waasi wa Yemen wa Houthi waliushambulia mji wa Israel kwa 'kundi la ndege zisizo na rubani'
Msemaji wa waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen anasema kuwa mji wa mapumziko wa Bahari Nyekundu wa Israel wa Eilat kwa "kundi la ndege zisizo na rubani".
Mshambulizi haya ni ya hivi karibuni zaidi zaidi katika mfululizo wa mashambulizi ya Wahouthi - walionyakua mamlaka miaka tisa iliyopita - ambao walitangaza kuliunga mkono kundi la Hamas na wanasema kuwa wamelenga meli zinazosafiri kuelekea Israel.
Bahari Nyekundu ni mojawapo ya njia muhimu zaidi duniani kwa usafirishaji wa mafuta.
Asubuhi ya leo, kikosi cha ulinzi wa anga cha Misri kimeidungua ndege inayoshukiwa kuwa karibu na mji wa Dahab katika Bahari Nyekundu.
Wakati huo huo, Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Grant Shapps, anasema meli ya kivita ya kikosi cha nchi yake -Royal Navy ilidungua ndege inayoshukiwa kufanya shambulizi katika Bahari Nyekundu.
Alisema ujasusi ulisema kuwa ndege hiyo isiyo na rubani ilikuwa ikilenga boti za wafanyabiashara.
Jana, kampuni mbili kuu za meli zilisimamisha safari za meli katika eneo hilo kwa sababu ya mfululizo wa mashambulizi ya Houthis.
Soma zaidi:
- Balozi wa Israel nchini Uingereza asema Israel haitakubali suluhisho la mataifa mawili
- Kiongozi wa Hamas: Gaza bila Hamas baada ya vita ni 'udanganyifu'
- Waandishi wa habari 17 waliuawa wakiripoti kuhusu vita vya Israel na Hamas
Serikali ya DRC yakerwa na hatua ya Kenya kuwaruhusu wapinzani wake kufanya mkutano Kenya
Serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, imeelezea kutorishishwa kwake na mpango wa viongozi wa kisasa akiwemo mkuu wa kundi la M23 waliokutana na kuhutubia kikao cha wanahabari jijini Nairobi, Ijumaa wiki hii.
Katika kikao hicho ambacho kilihutubiwa na aliyekuwa mkuu wa tume ya uchaguzi nchini DRC Cornell Nangaa, alitangaza kubuniwa kwa muungano wa kisasa unaofahamika kama, Congo River Alliance.
Kulingana na msemaji wa serikali ya Kinshasa Patrick Muyaya, hatua ya serikali ya Kenya kuridhia kikao hicho kufanyika nchini Kenya ni ukiukaji wa uhusiano mwema wa kidiplomasia kati ya Kenya na DRC.
Maoni yake yaliungwa mkono na raia wa nchi hiyo katika mtandao wa kijamii wa X, ambao wamekerwa na kufanyika kwa mkutano huo ambao ulitangaza muungano wa kijamii, na kijeshi ambao wahusika wakuu walitaja kwamba madhumuni yake ni ya kuleta amani hasa katika eneo la mashariki wma nchi hiyo ambalo wamedai limetengwa na kukumbwa na vita kwa zaidi ya miongo mitatu.
Baadhi waliipongeza hatua ya serikali ya DRC kukashifu Kenya na kutaka majibu ya haraka kuhusu kikao hicho, wakisema kwamba taifa hilo linahitaji amani na ushirikiano kutoka wka mataifa wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
DRC inajiandaa kwa uchaguzi mkuu katika siku tano zijazo, ambapo eneo la mashariki mwa taifa hilo linahofiwa kutoshiriki katika uchaguzi huo kutokana na hali ya usalama huko.
Wiki hii, Marekani ilisimamia makubaliano kati ya serikali za Rwanda na DRC kusitishwa kwa vita kwa siku tatu, na baadaye kuongeza muda huo hadi wiki mbili.
Ikulu ya White House: Mauaji ya mateka watatu wa Israel ni kosa la kutisha
Ikulu ya White House ilielezea mauaji hayo ya kijeshi Mateka watatu wa Israeli Waisraeli, katika Ukanda wa Gaza, waliita "kosa la kutisha."
John Kirby, msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa, aliiambia Libya White alisema Rais Joe Biden alikuwa amefahamishwa kuhusu tukio hilo.
Msemaji huyo alieleza imani yake kwamba Waisraeli watagombea Kagua na ujue jinsi hii ilifanyika.
Jeshi la Israel lilikuwa limeelezea masikitiko yake makubwa kutokana na mauaji ya wafungwa hao Zote tatu ni "kwa bahati mbaya".
Waisraeli waliuawa Watatu hao walipokuwa Shujaiya, mojawapo ya vitongoji vikubwa zaidi katika Jiji la Gaza, kaskazini mwa Ukanda huo.
Israeli inaamini kuwa kitongoji hicho ni ngome ya haarakati za mapambano ya kundi la Kiislamu la "Hamas," na kitongoji hicho kimekuwa kitovu cha mapigano kwa siku kadhaa.
Vita vikali kati ya vikosi vya Israeli vya ardhini na wapiganaji kutoka kwa mirengo ya yenye itikadi kali ya Palestina.
Soma zaidi:
- Balozi wa Israel nchini Uingereza asema Israel haitakubali suluhisho la mataifa mawili
- Kiongozi wa Hamas: Gaza bila Hamas baada ya vita ni 'udanganyifu'
- Waandishi wa habari 17 waliuawa wakiripoti kuhusu vita vya Israel na Hamas
Ndege ya shirika la ndege la Kenya KQ yalazimika kukatisha safari baada ya hitilafu angani
Shirika la ndege nchini Kenya, KQ limeeleza kwamba ndege yake nambari KQ 310 imelazimika kurejea Nairobi baada ya kukumbwa na matatizo, ilikuwa na changamoto kwenye magurudumu yake.
Ndege hiyo iliyokuwa ikielekea jijini Dubai kutoka Nairobi,iliondoka uwanja wa ndege wa Jommo Kenyatta mwendo wa saa tatu usiku, ila maafisa wa uwanja wa ndege walipokuwa wakifanya shughuli zao , walikumbana na mabaki madogo ya gurudumu yalithibitishwa kutoka kwa ndege hiyo ambayo tayari ilikuwa angani.
Tarifa kuhusu hitilafu kwenye ndege hiyo zilianza kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ya X na baadhi ya wanahabari nchini humo ambapo wakenya wengi walieleza hofu kubwa wakihoji kwamba ni kwa vipi hali ya ndege hiyo kwa muda ilikuwa haijulikani.
KQ inasema kwamba ndege hiyo ilipofika katika jimbo la Wajir uliopo kaskazini mashariki mwa Kenya, rubani wake aliombwa kuirejesha Nairobi , ambapo aliweza kutua salama katika uwanja wa JKIA mwendo wa saa tano na dakika arobaini na sita usiku wa Ijumaa bila ya tatizo kubwa.
Huku shirika hilo liliomba msamaha kwa yaliyojiri, lilitangaza pia kwamba abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo walikuwa wamepangiwa malazi kabla ya kuwekwa kwenye ndege nyingine jumamosi hii kuelekea Dubai.
KQ wiki hii imelazimika kujitetea baada ya vyombo vya Habari nchini Kenya kuandika tathmini ya malalamishi ya wateja kuhusu huduma zake na hatua za kampuni hiyo kuahirisha safari zake kwa wakati mfupi sana bila ya kuwapa wateja muda wa kutosha.
Tazama jinsi mhalifu alivyomvamia mpelelezi Uingereza
Polisi wametoa picha za video za mwanamume, ambaye tangu wakati huo amepatikana na hatia ya kupanga shambulio la bunduki katika Hyde Park, akimpiga mpelelezi wakati alipokuwa akihojiwa na polisi.
Edward Little alikamatwa akiwa njiani kuelekea kusini mwa London kununua bunduki.
Siku ya Ijumaa, alihukumiwa kifungo cha miaka 16 jela, baada ya kukiri kujiandaa kufanya vitendo vya ugaidi.
Mtoto apatikana akiwa hai kwenye mti baada ya kimbunga Tennessee
Mtoto mwenye umri wa miezi minne amepatikana akiwa salama "kwa neema ya Mungu" baada ya kimbunga kumchukua kutoka nyumbani kwake.
Mtoto mchanga wa miezi minne amepatikana akiwa hai "kwa neema ya Mungu" wazazi wake walisema baada ya mtoto kunyenyuliwa juu na kimbungo kutoka nyumbani kwao katika jimbo la Tennessee.
Wazazi wake walisema kimbunga kikali siku ya Jumamosi kiliiharibu nyumba yao na kuisomba beseni iliyokuwa na mtoto bado ndani yake.
Alinusurika na kugunduliwa kwenye mti ulioanguka wakati mvua ilipokuwa ikinyesha.
Mtoto huyo, kaka yake mwenye umri wa mwaka mmoja na wazazi walipata majeraha madogo ya michubuko katika tukio hilo.
Wakati kimbunga hicho kilipokaribia, mama wa watoto wawili, Sydney Moore, 22, alisema paa la nyumba yao liliezuliwa.
"Kimbunga kilishuka na kuokota beseni yenye mtoto wangu, ndani yake," Bi Moore alikiambia kituo cha habari cha eneo hilo. "Yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kupanda juu."
Mateka wa Israel: IDF yasema iliwaua kimakosa wanaume watatu waliokuwa wanashikiliwa Gaza
Kutoka kushoto kwenda kulia: Alon Shamriz, Yotam Haim na Samer Talalka
Jeshi la Israel linasema limewaua kimakosa mateka watatu wakati wa shambulizi lake la Gaza baada ya kutambuliwa kimakosa kama "tisho".
Watu hao walitambuliwa kwa majina Yotam Haim, 28, Samer Talalka, 22, na Alon Shamriz, 26.
Jeshi lilielezea majuto yake na kusema watatu hao walipigwa risasi na wanajeshi wanaoendesha harakati za kijeshi katika eneo la Shejaiya, kaskazini mwa Gaza.
Zaidi ya mateka 100 wameendelea kuwa mateka Gaza baada ya kukamatwa katika mashambulizi ya Oktoba 7 dhidi ya Israel.
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema tukio la Ijumaa linachunguzwa, na kwamba "linajutia sana tukio hilo la kusikitisha na linatuma familia hizo rambirambi zake za dhati".
"Dhamira yetu ya kitaifa ni kutafuta waliopotea na kuwarudisha mateka wote nyumbani," liliongeza.
Mamia ya watu walikusanyika katikati mwa Tel Aviv kufuatia tangazo hilo na kuandamana hadi kituo cha kijeshi cha IDF mjini humo, wakiitaka serikali kkuhakikisha inafikia makubaliano ya kuwaachilia mateka waliosalia.
Waandamanaji walishika mishumaa na kubeba mabango yaliyoandikwa "Walete nyumbani" na "Kubadilishana mateka sasa!"
Miili ya watu hao watatu imerudishwa katika ardhi ya Israel, ambapo ukaguzi ulithibitisha utambulisho wao.
Soma zaidi:
- Balozi wa Israel nchini Uingereza asema Israel haitakubali suluhisho la mataifa mawili
- Kiongozi wa Hamas: Gaza bila Hamas baada ya vita ni 'udanganyifu'
- Waandishi wa habari 17 waliuawa wakiripoti kuhusu vita vya Israel na Hamas
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa leo ni Jumamosi tarehe16.12.2023