Marekani inaweza kusambaza ndege za kivita kwa Israel kutoka Uholanzi

Serikali ya Uholanzi haitalazimiki kusimamisha usambazaji wa sehemu zavifaa vinavyounda ndege za kivita za F-35 kutoka katika ghala linaloendeshwa na Marekani nchini Uholanzi.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi and Yusuf Jumah

  1. Somalia yajiunga rasmi na jumuiya ya Afrika Mashariki kama mwanachama wa nane

    w

    Chanzo cha picha, AFP

    Somalia imejiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wiki tatu baada ya nchi wanachama kukubali kuingia katika jumuiya hiyo ya kikanda.

    Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alitia saini mkataba wa kuipatia nchi hiyo uanachama kamili wa umoja huo siku ya Ijumaa, katika hafla iliyoongozwa na mwenyekiti wa sasa wa EAC, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, nchini Uganda.

    Nchi hiyo ilikubaliwa kuingia EAC tarehe 24 Novemba, na kuwa mwanachama wa nane wa jumuiya hiyo baada ya Burundi, DR Congo, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania, Rwanda na Uganda.

    Rais Mohamud siku ya Ijumaa alisema kuwa kurasimishwa kwa ushirikiano wa Somalia katika umoja huo ni "mwanga wa matumaini kwa mustakabali uliojaa matumaini" na kwamba nchi yake inatazamia kuchangia maendeleo ya eneo hilo.

  2. Marekani inaweza kusambaza ndege za kivita kwa Israel kutoka Uholanzi

    Serikali ya Uholanzi haitalazimiki kusimamisha usambazaji wa sehemu zavifaa vinavyounda ndege za kivita za F-35 kutoka katika ghala linaloendeshwa na Marekani nchini Uholanzi.

    Mahakama huko The Hague imechapisha hukumu kujibu pingamizi la kisheria lililoletwa na idadi ya mashirika yasiyo ya kiserikali - Oxfam Novib, peace movement PAX Uholanzi na Rights Forum

    Mashirika yasiyo ya kiserikali yalisema Uholanzi inakiuka sheria za kimataifa kwa kuipatia Israel sehemu zilizokusudiwa kwa ajili ya vifaa vya kivita, kulingana na makundi hayo serikali ya Uholanzi inajua kuwa Israel inakiuka kanuni za msingi za sheria ya vita.

    Mawaziri wa Uholanzi walisema wamepima hali hiyo pamoja na haki ya Israeli ya kujilinda.

    Jaji alifikia hitimisho kwamba serikali ilikuwa imefanya maamuzi ya busara kuruhusu usambazaji wa sehemu hizo kuendelea.

  3. Ruto: Wakenya 2,500 kupata ajira nchini Saudi Arabia

    w

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kenya imefikia makubaliano ya kusafirisha wafanyakazi zaidi ya 2000 hadi Saudi Arabia, Rais wa nchi hiyo William Ruto anasema.

    Chini ya makubaliano yaliyofikiwa siku ya Alhamisi, Kenya itatuma wauguzi na wafanyakazi wengine wenye ujuzi katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati, huku wafanyakazi 2,500 wakipangwa kutumwa kwa mara ya kwanza.

    "Hapo awali, tulituma wafanyakazi wa nyumbani pekee, lakini sasa tunaweza kusafirisha wafanyakazi wenye ujuzi hadi Saudi Arabia na nchi zingine," Rais Ruto alisema Ijumaa, akiongeza kuwa wafanyakazi hao watapokea mshahara wa kila mwezi wa shilingi 200,000 za Kenya (dola 1,300; pauni 1,000).

    Tangazo hilo linakuja karibu wiki moja baada ya wizara ya kazi ya Kenya kusema itatuma wafanyakazi 1,500 nchini Israel "na mapato ya uhakika [ya mwezi]" ya $1,500. Mwezi uliopita, Rais Ruto alisafiri hadi Ujerumani kufanya mazungumzo ya kupata ajira 200,000 kwa Wakenya.

    Bw Ruto anasema amekuwa akitafuta nafasi za ajira kwa Wakenya, ambao alisema wanasifika duniani kote kwa bidii yao.

    Ruto alisema hapo awali kwamba anataka Wakenya zaidi kutafuta kazi nje ya nchi ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini na kutuma pesa za kusaidia na kupungua kwa akiba ya fedha za kigeni nchini Kenya, ambayo imedhoofisha sana shilingi ya Kenya katika miezi ya hivi majuzi.

  4. Tanzania yalikaribisha Bunge la EU kukagua Ngorongoro

    w

    Siku moja baada ya Bunge la Umoja wa Ulaya kulaani kuhamishwa jamii za watu wanaoishi katika Hifadhi ya Ngorongoro, serikali ya Tanzania imetoa wito kwa Bunge hilo kwenda kukagua eneo hilo.

    Katika taarifa iliyotolewa leo na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Mobhare Matinyi inaeleza kuwa Tanzania inalikaribisha Bunge la Ulaya kwani “serikali haina kitu cha kuficha na inahakikisha wakati wote haki za binadamu zinaheshimiwa.”

    Kwa upande mwingine, Matinyi ameweka wazi kuwa Serikali ya Tanzania inatambua kwamba shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi elimu na utamaduni (UNESCO), litapeleka wataalamu wake mwezi Januari 2024 kufanya ukaguzi.

    Tanzania imeendelea kukanusha madai ya kuhamishwa jamii hizo kwa nguvu, ikisisitiza kuwa wanahama kwa hiari kwenda katika maeneo ambayo serikali imewajengea miundombinu yote muhimu.

    Msemaji wa serikali aliongeza kuwa Tanzania haikaliwi kutokana na makabila ya watu.

    ''Eneo la Ngorongoro lina makabila zaidi ya moja na Serikali haitambui watu wake kwa makabila na kila mtu wa kabila lolote nchini ana haki ya kuishi popote nchini. Kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yetu hakuna kabila au kundi la watu lenye hadhi ya “watu wa asili” (indigenous people) bali watu wote ni sawa na huishi popote katika nchi ya Tanzania.

  5. Gazeti la Mirror laamriwa kumlipa Prince Harry £140,600 kwa kudukua simu yake

    gg

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mahakama Kuu imeamuru gazeti la Mirror kumlipa fidia ya £140,600 Prince Harry kwa kuwa ni mwathirika wa udukuzi wa simu za mkononi uliofanywa na gazeti hilo.

    Jaji Fancourt anasema kwamba simu yake binafsi ililengwa kati ya 2003 na 2009 na makala 15 kati ya 33 zilikuwa "matokeo ya udukuzi wa simu ... au matokeo ya ukusanyaji habari kinyume cha sheria."

    "Nimegundua kuwa makala 15 kati ya 33 zilizojaribiwa zilikuwa matokeo ya udukuzi wa simu yake ya mkononi au simu za mkononi za washirika wake, au matokeo ya ukusanyaji wa habari usio halali.

    Fancourt anasema ingawa kiasi hicho ni kidogo, kinaonesha pia uchungu alioupata mwanamfalme kwa sababu ya gazeti la Mirror kuficha kosa hilo.

    Anasisitiza kwamba aligundua pia washirika wa Harry walilengwa kinyume cha sheria na MGN (Mirror Group Newspapers).

    Katika taarifa, msemaji wa gazeti hilo inasema: "Tunapokea uamuzi wa leo ambao unaipa biashara uwazi unaohitajika ili kusonga mbele kutokana na matukio yaliyotokea miaka mingi iliyopita.

    "Pale ambapo makosa ya nyuma yalifanyika, tunaomba msamaha bila shaka, tunawajibika kikamilifu na kulipa fidia inayostahili."

  6. Ecowas yasimamisha rasmi uanachama wa Niger kwa sababu ya mapinduzi

    nnn

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) imesimamisha uanachama wa Niger baada ya serikali kuu ya kijeshi kukataa kumrejesha madarakani Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum.

    Bazoum alipinduliwa katika mapinduzi ya kijeshi mwezi Julai.

    Ecowas ilisema katika taarifa Alhamisi kwamba mkutano wa hivi karibuni wa viongozi wake nchini Nigeria "ulitambua" kwamba serikali ya Bw Bazoum "ilipinduliwa kikamilifu katika mapinduzi ya kijeshi".

    Imeisimamisha Niger katika vyombo vya kufanya maamuzi vya Ecowas hadi "utaratibu wa kikatiba utakapo rejeshwa nchini humo".

    Hali ya nchini Niger awali ilichukuliwa na Ecowas kama jaribio la mapinduzi, na hivyo kusababisha kuchelewa kusimamisha uanachama wa nchi hiyo.

    Ecowas iliweka vikwazo na hata kutishia kuingilia kijeshi baada ya mapinduzi.

  7. Ajali ya treni ya chini ya ardhi Beijing yasababisha majeruhi zaidi 100

    w

    Chanzo cha picha, WEIBO

    Ajali ya treni kati ya treni mbili za chini ya ardhi mjini Beijing imesababisha watu 102 kuvunjika mifupa, vyombo vya habari vya serikali ya China viliripoti.

    Zaidi ya watu 500 walipelekwa hospitalini baada ya tukio hilo, lililotokea takriban saa 19:00 kwa saa za huko (11:00 GMT) siku ya Alhamisi.

    Treni hizo ziligongana wakati wa theluji nyingi zikishuka kwenye njia ya chini ya ardhi ya Changping. Kufikia Ijumaa asubuhi, watu 423 wameruhusiwa kutoka hospitalini.

    Ingawa ajali kama hizo si za kawaida kwenye mtandao wa usafiri wa mji mkuu wa China, dhoruba za theluji ziliripotiwa kusababisha njia kuwa na utelezi. Hili basi lilisababisha "uharibifu wa alama za treni" ambao ulisababisha treni ya kwanza kusimama ghafla, gazeti la China Daily liliripoti, likinukuu mamlaka ya usafiri ya Beijing.

    Treni iliyofuata haikuweza kushika breki kwa wakati ilipokuwa ikishuka kwenye njia zenye barafu, na kusababisha kugonga nyuma ya treni ya kwanza.

    Athari hiyo ilisababisha mabehewa mawili ya mwisho ya moja ya treni kukatika. Haijulikani ni treni gani ilitenganishwa.

    Picha na video zilizochapishwa mtandaoni zinaonyesha wasafiri wakiwa wamejazana kwenye magari, wakiachwa gizani kutokana na kukatika kwa umeme. Wachache walionekana wakitumia nyundo za dharura kuvunja madirisha ili kupata hewa safi. Katika video iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii wa China Weibo, mwanamke ambaye anaonekana kuzirai anaonekana akiwa amelala kwenye viti vingi vya treni. Watu 67 wamesalia hospitalini kwa matibabu, huku 25 wakiwa "chini ya uangalizi", ripoti zilisema. Hakukuwa na vifo.

    Tukio hilo lilizua maoni ya hasira kutoka kwa watumiaji wa mtandao wa China. Baadhi walishangazwa na idadi ya majeruhi, huku wengine wakilalamikia usumbufu uliosababishwa na ajali hiyo.

  8. Waangalizi wa uchaguzi DRC waonya mwenendo wa uchaguzi mkuu wa wiki ijayo

    w

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waangalizi huru wa Uchaguzi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameonya kuwa masuala kama vile wapiga kura kukosa kadi zinazotambulika za kupigia kura, kuwazuia wapinzani kutumia usafiri wa ndege wakati wa kampeini na kuchelewesha kwa toleo la sajili rasmi ya wapiga kura hauenda ikahujumu uchaguzi mkuu unaopangiwa wiki ijayo.

    Kwa miezi kadhaa tume ya uchaguzi CENI imekuwa ikanusha madai kuwa haina uwezo wa kuandaa uchaguzi huru na wa haki, licha ya kuiandikia serikali ya DRC na Umoja wa Matifa kuipa misaada ili kuiwezesha kusafirisha vifaa vya kupigia kura hasa katika maeneo ya mashambani, ambayo haina mifumo nzuri ya usafiri.

    Hali ya wasi wasi imetanda huku DRC ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa tare=he 20. Wapinzani war ais Felix Tshisekedi wamelalamika kuwa hawapewa nafasi sawa ya kufanya kampeini katika maeneo yote, na pia kuishutumu vyombo vya dola kwa kupanga njama ya kutumia ulaghai ili kuhakikisha kuwa rais wa sasa anashinda awamu ya pili.

    Hata hivyo tume ya CENI imekanusha madai haya.

    Kilicho mashakani sio tu uhalali wa utawala utakaochukua madaraka nchini DRC, lakini pia uthabiti wa DRC, kwa sababu malimbano kuhusu dosari za na uvunjifu wa sheria mara nyingi huzua ghasia nchini Kongo. Ghasia na machafuko yana weza kuwa naahdari kubwa kwa dunia nzima kwa sababu taifa la DRC ndilo taifa linaloongoza duniani kwa uzalishaji wa madini ya Cobalti madini ambayo yanatumiwa kwa utengenezaji wa betri za magari ya umeme na simu za rununu.

    Kwa sasa ni msimu wa mvua nchini DRC na tume ya uchaguzi imekabiliwa na changamoto chungu nzima kusafirisha vifa vya kupigia kura katika maeneo yote kutokana na miundo mbinu duni ya barabara.

    Aidha wagombea wa viti mbali mbali hasa kiti cha urais nao pia wamekabiliwa na matatizo kuwafikia wapiga kura, kutokana na masharti ya usafari wa ndege uliowekwa na serikali na ukosefu wa mafuta ya ndege.

    Tangu DRC, Zamani ikijulikana na Kama Zaire, ipate uhuru wake zaidi ya miaka 59 iliyopita, taifa hilo lilishuhudia mpango wa kukabithi madaraka kwa njia ya kidemokrasia kwa mara ya kwanza mwaka wa 2019, wakati Rais wa wakati huo Joseph Kabila alipomkabithi mamlaka ya nchi rais Felix Tshisekedi baada ya uchaguzi mkuu.

  9. Mvulana wa miaka 17 aliyetoweka kwa miaka sita apatikana nchini Ufaransa.

    g

    Chanzo cha picha, GREATER MANCHESTER POLICE

    Maelezo ya picha, Alex Batty mdogo, pichani kabla hajapotea

    Kijana wa Uingereza aliyetoweka nchini Ufaransa kwa miaka sita alituma ujumbe kwa nyanya yake: "Nakupenda, nataka kurudi nyumbani" baada ya kuchukuliwa na dereva.

    Alex Batty yuko katika kituo cha kijana huko Toulouse na anaweza kurejea Uingereza ndani ya saa chache, waendesha mashtaka' ofisi mjini humo iliambia BBC.

    Alex alitumia simu ya dereva kutuma ujumbe kwa nyanya yake nchini Uingereza, akisema "Nakupenda, nataka kurudi nyumbani".

    Alikuwa ametoweka tangu 2017, lakini alipatikana Jumatano asubuhi na dereva ambaye alimuona akitembea kwenye mvua karibu na Toulouse.

    Alex Batty alitoweka mnamo 2017 alipokuwa likizo nchini Uhispania na mama yake na babu yake.

    Kwa sasa Alex yuko katika kituo cha kijana huko Toulouse na anaweza kurejea Uingereza baadaye akiwa na polisi na maafisa wa ubalozi.

  10. Uchaguzi DRC 2023: Wenye kadi za kupigia kura zilizofutika wataruhusiwa kupiga kura – Tume ya Uchaguzi

    g

    Chanzo cha picha, Ceni-RDC

    Maelezo ya picha, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchinii DRC Denis Kadima

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC (CENI) Denis Kadima amesema kuwa wapiga kura wote waliosajiliwa rasmi wataruhusiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika wiki ijayo hata ikiwa kadi za kupigia kura zimeharabika.

    Kuali hiyo ya CENI imeungwa mkono na na uamuzi wa mahakama ya katiba ambayo imeyakataa madai yote ya kuahirisha uchaguzi yaliyotolewa na wagombea urais wa upinzani.

    Mahakama imesema kuwa madai yao hayana msingi na mchakato wa uchaguzi utaendelea kama ilivyopangwa.

    Kumękuwa na wasi wasi kuwa idadi kubwa ya wapiga kura huenda wasishiriki uchaguzi baada ya maelezo kwenye kadi zao kufutika.

    Tume ya uchaguzi imekuwa ikiendesha shughuli ya kuwapa wapiga kura wałiosajiliwa kadi mpya ikiwa kadi żao zimeharika łakini zoezi lenyewe limekuwa likienda pole pole kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza ili kupata kadi mpya.

    Kadima ameongeza kuwa hadi sasa hawajafanikiwa kupata ndege za kutosha kusafirisha vifaa vitakavyotumika wakati wa uchaguzii hadi maeneo yote.

    Siku mbili zilizopita CENI iliiandikia serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa kuipa misaada ya ndege ili kufanikisha shughuli ya kusafirisha vifaa vya kupigia kura.

    Licha ya hayo amesema kuwa CENI Inafanya kila Liwezalo ili uchaguzi mkuu uendelee kama ilivyopangwa.

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchinii DRC Denis kadima amesema kuwa wapiga kura wote waliosajiliwa rasmi wataruhusiwa kushiriki Karola uchaguzi mkuu utakaofanyika Wiki ijayo hata ikiwa kadi ZSP za kupigia kura zimerabika.

    Kumę kuwa na wasi wasi kuwa Idadi kubwa ya wapiga kura huenda wasishiriki baada ya Maelezo kwenye kadi zao kufutika. Tume ya uchaguzi imekuwa ikiendesha shughuli ya kuwapa wapiga kura wałiosajiliwa kadi mpya ikiwa kadi żao zimeharika łakini zoezi lenyewe limekuwa likienda pole pole kutokana na Idadi kubwa ya watu waliojitokeza ili kupata kadi mpya.

    Kadima ameongeza kuwa hadi sasa hawajafanikiwa kupata Ndege za kutosha kusafirisha vifaa vitakavyotumika wakati wa uchaguzii hadi Maeneo yote. Siku mbili zilizopita CENI iliandikia serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa kuipa misaada ya ndege ili kufanikisha shughuli ya kusafirisha vifaa vya kupigia kura.

    Licha ya hayo amesema kuwa CENI inafanya kila liwezalo ili uchaguzi mkuu uendelee kama ilivyopangwa.

    Uchaguzi 2023 DRC: soma zaidi

    • Uchaguzi wa Urais DRC: mwongozo kamili wa kuuelewa uchaguzi wa Disemba 2023
    • Uchaguzi wa DRC 2023: "Tusifikirie kuwa kazi ya makanisa ni kupinga utawala uliopo" - Mchungaji Eric Senga
    • Uchaguzi wa DR Congo:‘Kama ungekuwa uamuzi wetu, tungepiga kura kupata amani
    • Uchaguzi wa DRC 2023: Félix Tshisekedi, mwanafikra aliyetaka kuibadilisha DRC kuwa nchi ya ndoto
    • Uchaguzi wa DRC 2023: Unachohitaji kujua
    • Martin Fayulu, Mwanasiasa wa upinzani wa DRC asiyetetereka
  11. Worldcoin inafanya mazungumzo na Kenya ili kurejesha shughuli zake

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Kenya ilisitisha shughuli za Worldcoin mwezi Agosti kwa sababu ya masuala ya ufaragha wa data

    Mradi wenye utata wa matumizi ya crypto Worldcoin unafanya mazungumzo ya kina ili kurejesha shughuli zake nchini Kenya, zaidi ya miezi minne baada ya mamlaka hiyo kusimamisha shughuli zake nchini humo.

    Operesheni hizo zitaendelea chini ya kanuni mpya na kali zaidi ambazo zitawekwa na bunge, ripoti za vyombo vya habari vya ndani imesema.

    Inasemekana kuwa kampuni hiyo inatarajiwa kupanua shughuli zake hadi maeneo mengi zaidi nchini na itaendelea kuwalipa watumiaji posho.

    Worldcoin - mradi wa kampuni ya ujasusi bandia ya Marekani OpenAI – ulisimamishwa nchini Kenya mwezi Agosti kutokana na masuala ya faragha za data.

    Mamlaka nchini Kenya zilianzisha uchunguzi kuhusu mradi huo.

    Mbunge wa eneo hilo alidai kuwa mwanga wa infra-red unaotumiwa na orbs za kuangalia macho za Worldcoin ulidhuru macho ya baadhi ya watumiaji, na hivyo kusababisha uchanganuzi wa kitaalamu kwenye orb.

    Wordcoin, hata hivyo, aliiambia BBC kwamba orb ni salama na inafuata masharti ya viwango vya kimataifa.

  12. Nyota wa Brooklyn Nine-Nine Andre Braugher alifariki kutokana na saratani ya mapafu

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Muigizaji aliyeshinda tuzo ya Emmy mara mbili Andre Braugher alifariki kutokana na saratani ya mapafu baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa huo miezi kadhaa iliyopita, msemaji wake ameithibitishia BBC.

    Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 61 alifariki siku ya Jumatatu.

    Braugher alijulikana sana kwa majukumu yake kama Kapteni Ray Holt katika kipindi chaBrooklyn Nine-Ninena Detective Frank Pembleton kwenye Homicide: Life on the Street.

    Alishinda Emmy kwa uigizaji wakewaHomicide mnamo 1998 na lingine mnamo 2006 kwa kazi yake katika filamu ya ‘Thief’.

  13. Vita vya Ukraine: Hungary yazuia €50bn za ufadhili wa EU kwa Ukraine

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban mjini Brussels siku ya Alhamisi

    Hungary imezuia €50bn ($55bn; £43bn) ya msaada wa EU kwa ajili ya Ukraine saa chache baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kuanzisha mazungumzo kuhusu uanachama.

    "Muhtasari wa usiku: kura ya turufu ya pesa za ziada kwa Ukraine," Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban alichapisha kwenye mitandao ya kijamii baada ya mazungumzo mjini Brussels.

    Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamesema mazungumzo kuhusu msaada kwa Ukraine yataanza tena mapema mwaka ujao.

    Ukraine inategemea sana ufadhili wa Muungano wa Ulaya na Marekani huku ikiendelea kupambana na kukaliwa kimabavu na majeshi ya Urusi.

    Kuzuia msaada kulitangazwa na Bw Orban muda mfupi baada ya viongozi wa EU wa kuamua kuanzisha mazungumzo ya uanachamawa Ukraine na Moldova na kutoa hadhi ya Georgia kuwania uanachama wa muungano huo.

    Hungary kwa muda mrefu imekuwa ikipinga uanachama wa Ukraine katika EU lakini haikuwahi kuipigia kura ya veto hatua hiyo.

    Bw Orban aliondoka kwenye chumba cha mazungumzo kwa muda kwa kile maafisa walichoeleza kama ‘’uamuzi uliochukuliwa awali na wenye kujenga’’, huku viongozi wengine 26 wakiendelea kupiga kura yao.

    Msemaji wa Charles Michel, rais wa Baraza la Ulaya, alisema makubaliano hayo yamekuwa ya kauli moja.

    Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alisifu uamuzi wa Muungano wa Ulaya kuhusu mazungumzo ya uanachama wa nchi yake akiutaja kama "ushindi".

  14. Gautam Singhania: Madai ya unyanyasaji wa nyumbani yanatishia mali ya tajiri wa India

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Makubaliano ya juu ya talaka kati ya mfanyabiashara maarufu wa nguo wa India, Gautam Singhania, na mkewe, Nawaz Modi, yanaweza kumfanya apoteze 75% ya utajiri wake wa $1.4bn (£1.1bn).

    Wote wawili Bw Singhania na Bi Modi ni wanachama wa bodi na wanahisa wakuzaji wa Raymond Group iliyoorodheshwa katika soko la hisa , mojawapo ya chapa zinazojulikana zaidi za watumiaji India.

    Mkewa mfanyabiashara huyo ambaye anafahamika kwakupenda bot za kifahari , magari ya kasi na ndege za kibinafsi - hataki kukubalia kiasi cha chini cha fedha, chanzo kilicho karibu na Bi Modi kimeiambia BBC, na kukanusha ripoti za habari kwamba wanandoa hao walikuwa wameanza. Mazungumzo ya kukubaliana kuhusu kiasi chenye"uhalisia"Zaidi ili kupata suluhu .

    Wanafamilia wawili kutoka pande zote mbili wanapatanisha mzozo huo na asilimia 75 bado iko mezani, duru zimeiambia BBC.

    "Anasema amekubali 75% mbele ya watu wengi - marafiki, wapatanishi, wanasheria na wahasibu wa kukodi. Hakuna kurudi nyuma juu yya hilo," chanzo kimoja kilisema, kikiongeza kuwa Bi Modi alisisitiza kwamba wakfu maalum unafaa kuundwaambapo mali hiyo itahamishwa na kukabidhiwakwa binti zake wawili baadaye wakiwa watu wazima .

  15. Mzozo wa Essequibo: Venezuela na Guyana zakubali kutotumia nguvu

    g

    Chanzo cha picha, AFP

    Guyana na Venezuela zimekubali "kutotumia nguvu" kusuluhisha mzozo wao kuhusu eneo lenye utajiri wa mafuta la Essequibo.

    Baada ya kukutana na Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Rais wa Guyana Irfaan Ali alithibitisha ahadi yake ya kuleta amani katika eneo hilo.

    Lakini alisema Guyana ilikuwa na haki ya kutumia eneo lao kwa njia huru ili kujiendeleza .Katika taarifa yake kupitiaX, Bw Maduro alisema imekuwa "siku bora ya mazungumzo".

    Bw Ali na Bw Maduro walikutana huko St Vincent na Grenadines.

    Katika tamko la pamoja la kurasa tatu, nchi hizo zilikubaliana "hazitatishia au kutumia nguvu dhidi ya kila mmoja wao kwa hali yoyote" na "kuendelea na mazungumzo".

    Pia walikubaliana kuunda tume ya pamoja ya mawaziri wa mambo ya nje kushughulikia masuala yoyote yanayotokana na eneo linalogombaniwa, na watakutana tena Brazil kujadili Essequibo.

    Guyana inasema suala hilo litatatuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki, huko The Hague, lakini Venezuela haitambui mamlaka ya mahakama hiyo.

    Essequibo, eneo la msitu lenye ukubwa wa kilomita za mraba 160,000, linasheheni theluthi mbili ya eneo la Guyana.

  16. Vita vya Israel na Hamas: Netanyahu aapa tena kuangamiza Hamas

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Benjamin Netanyahu akikutana na Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema tena vita dhidi ya Hamas vitaendelea "hadi ushindi kamili" upatikane.

    Mara hii , matamshi hayo ya Netanyahu yametolewa alipokutana na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani, Jake Sullivan, ambaye anaizuru Israel.

    Kauli hiyo inajiri huku ukiongezeka wa kusitishwa kwa mapigano Gaza huku kukiwa na ongezeko la vifo na hali mbaya ya kibinadamu ikizidi.

    Tangu kuanzisha vita hivyo vilivyolenga kujibu mashambulizi ya Oktoba 7 yaliyotekelezwa na Hamas, Netanyahu ameapa kuliangamiza kundi hilo.

    Maeneo makubwa ya Gaza yamegeuzwa kuwa magofu na zaidi ya watu 18,000 wameuawa, kulingana na mamlaka ya afya ya eneo hilo, wakiwemo watoto karibu 7,000.

    Mamia ya maelfu ya wengine wameyakimbia makazi yao, na sasa wanatatizika kuishi huku kukiwa na uhaba mkubwa wa vifaa vya msingi.

    Sullivan alikuja Israel kujadili ratiba inayowezekana ya kumalizika kwa mzozo huo. Lakini je Israel inakaribia kutokomeza Hamas?

    Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant alimwambia Sullivan kwamba kuangamiza kundi hilo kutachukua "zaidi ya miezi kadhaa". Maafisa wa jeshi la Israel wameripotiwa kusema bado wanahitaji wiki kadhaa kabla ya kumaliza operesheni kali.

    Soma zaidi:

  17. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 15.12.2023