Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Hospitali ya Gaza Kusini 'yapoteza udhibiti' baada ya kuzidiwa na mapigano

Mkurugenzi wa hospitali: 'Tumepoteza udhibiti' juu ya idadi kubwa ya waliofariki na waliojeruhiwa huku Israel ikiimarisha mashambulizi ya mizinga na vifaru

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangao yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. Uturuki yatoa hati ya kukamatwa kwa mtoto wa rais wa Somalia kutokana na ajali mbaya ya barabarani

    Uturuki imetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa mtoto wa rais wa Somalia, baada ya kudaiwa kumgonga msafirishaji wa pikipiki, ambaye alifariki baadaye.

    Ripoti ya polisi ilisema Mohammed Hassan Cheikh Mohamud aligongana na mtu huyo mchana mjini Istanbul.

    Polisi wanasema alikuwa akiendesha gari ambalo inasemekana lilikuwa la ubalozi mdogo wa Somalia nchini humo.

    Uturuki iliweka marufuku ya kusafiri kwa Bw Mohamud lakini maafisa wanaamini kuwa tayari ameikimbia nchi.

    Katika chapisho kwenye X ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, meya wa Istanbul Ekrem İmamoğlu alishirikisha umma picha za CCTV za tukio hilo lililotpkea tarehe 30 Novemba.

    Gari linaonekana likigonga nyuma ya pikipiki kwenye makutano ya barabara yenye njia nyingi.

    Mwendesha pikipiki, baba wa watoto wawili Yunus Emre Göçer, 38, alipelekwa hospitalini lakini alifariki kutokana na majeraha yake siku sita baadaye.

    Ripoti ya awali ya polisi ilisema kuwa Bw Göçer alikuwa na makosa na hivyo Mohamud aliachiliwa, kulingana na wakili wa Bw Göçer aliyenukuliwa na vyombo vya habari vya Uturuki.

    Lakini uchunguzi wa picha za usalama ulisema kunaweza kuwa na maelezo mengine.

    Bw Mohamud, ambaye ni mtoto wa Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, hajazungumza lolote.

    Hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Bw Mohamud ilitolewa na mwendesha mashtaka wa Uturuki siku ya Ijumaa.

    Hii ilikuwa baada ya polisi kumtembelea nyumbani kwake na kukuta kwamba hakuwepo kwa takriban wiki moja, shirika la habari la AFP linasema, likinukuu ripoti za ndani.

    Uturuki na Somalia awali zilieleea kuboreka kwa uhusiano wa kidiplomasia katika muongo mmoja uliopita, huku Uturuki ikiwekeza katika miundombinu, mafunzo ya kijeshi na misaada ya kibinadamu nchini Somalia.

  3. Israel inaishutumu Hamas kwa kutumia shule na msikiti kufanya mashambulizi

    Jeshi la Israel limelishutumu kundi la Hamas kwa kutumia "miundombinu ya raia" kama chanzo cha operesheni zake.

    Limemesema kundi hilo limetumia shule ya Shirka la misaada la Umoja wa Mataifa -UNRWA na msikiti mmoja uliopo eneo la Beit Hanoun kaskazini mwa Gaza kuwafyatulia risasi wanajeshi wake.

    Juliette Touma, mkurugenzi wa mawasiliano wa UNRWA, aliiambia BBC kuwa hawezi kuthibitisha madai hayo kwa sababu eneo linaloizunguka "lililipuliwa mara kwa mara", lakini akakiri kwamba shule zinapaswa "kulindwa wakati wote" na "kamwe hazipaswi kutumiwa kwa shughuli za kijeshi au mapigano”.

  4. Mafuriko Manyara: Idadi ya watu waliopoteza maisha yafikia 85

    Idadi ya watu waliopoteza maisha yao kufuatia mafuriko ya Hanang Manyara nchini Tanzania imefikia 85, imesema taarifa ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali

    Taarifa hiyo imesema miili iliyopatikana ni yote imeshatambuliwa na ndugu zao na kuchukuliwa. ‘’Idadi hii iko katika mchanganuo ufuatao: Watu wazima 49 (wanaume 20 na wanawake 29); na watoto 36 (kiume 16 na kike 20).’’ Imefafanua taarifa hiyo.

    Kuhusu majeruhi taarifa hiyo imesema Hadi sasa jumla ya majeruhi na wagonjwa waliopokelewa tangu maafa yatokee ni 139 lakini waliopo hospitalini ni 51na kuongeza kuwa ‘’Idadi hii iko katika mchanganuo ufuatao: Watu wazima 77 (wanaume 38 na wanawake 39); na watoto 62 (kiume 28 na kike 34). Jumla ya majeruhi 86 wamepata nafuu na kuruhusiwa kurejea nyumbani huku wawili wakifariki’’, imeelezea taarifa hiyo.

    Maafa ya Hananga Manyara yalitokana na Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jumapili Novemba 3, na kusababisha sehemu ya mlima Hanang kumeguka hivyo kutokea maporomoko ya udongo uliozalisha tope liliharibu makazi ya watu na mali nyingine.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mafuriko Manyara: Idadi ya watu waliopoteza maisha yafikia 65, makazi zaidi ya 1000 yakiathiriwa na mafuriko Tanzania
    • 'Tope lilizidi, nikawaambia njooni mtoboe choo, ndio wakatoboa tukatoka'
    • Mafuriko Manyara: 'Hakuna kilichobaki, watoto wetu wote wamekwenda'
  5. Mkurugenzi wa hospitali: Hospitali ya Gaza Kusini yazidiwa kutokana na idadi kubwa ya waliofariki na majeruhi

      • Author, Rushdi Abu Alouf
      • Nafasi, Akiripoti kutoka Istanbul

    Nimesikia kutoka kwa mkurugenzi wa Hospitali ya Nasser huko Khan Younis, Nahed Abu Taima.

    Aliniambia: "Tumepoteza udhibiti kutokana na idadi kubwa ya watu waliojeruhiwa waliofika hospitalini.

    "Mamia ya waliojeruhiwa na wafia imani wanafika katika idara ya dharura.

    "Kwa kuendelea kwa mashambulizi ya Israel katika maeneo kadhaa huko Khan Younis, tunalazimika kuwatibu waliojeruhiwa wakiwa wamelala sakafuni na kwenye korido za idara kutokana na ukosefu wa vifaa vya matibabu."

    Soma zaidi:

    • Gaza huenda isiweze kupona tena kwa maafa yanayosababishwa na vita - Mkuu wa Umoja wa Mataifa
    • Hamas ilipanga unyanyasaji wa kijinsia kama silaha ya vita - mwanaharakati wa Israeli
    • Mzozo wa Gaza: Israel yasema imepata moja ya hifadhi kubwa ya silaha za Hamas
  6. Vifaru vya Israel vinasonga mbele kwenye barabara kuu ya Khan Younis

      • Author, Rushdi Abu Alouf
      • Nafasi, Akiripoti kutoka Istanbul

    Eneo la pili muhimu la operesheni ya Israeli Gaza ni kusini, na Khan Younis.

    Asubuhi ya leo, takriban watu 50 wameuawa katikati mwa Gaza na kusini mwa Ukanda wa Gaza.Wizara ya afya, inayoendeshwa na Hamas, inasema haiwezi kuhesabu idadi ya watu waliouawa kaskazini.

    Mji wa Khan Younis umezungukwa na mizinga ya Israeli kutoka pande za mashariki na kaskazini.

    Mizinga hiyo inasonga polepole kuelekea Mtaa wa Jalal, ambao ni mojawapo ya barabara kuu zinazoelekea katikati mwa jiji.

    Na sasa watu wengi waliohamishwa baadaye tarehe 13 Oktoba - kutoka kaskazini hadi Khan Younis - wanapaswa kuondoka tena kwenda Rafah.

    Watu wanaendelea kuzungumza nami kuhusu ramani iliyotolewa na Waisraeli, wakitoa onyo la mara kwa mara kwa raia kuhama. Wanasema hawawezi kuelewa utaratibu wa hili na wapi wanapaswa kwenda.

    Soma zaidi:

    • Gaza huenda isiweze kupona tena kwa maafa yanayosababishwa na vita - Mkuu wa Umoja wa Mataifa
    • Hamas ilipanga unyanyasaji wa kijinsia kama silaha ya vita - mwanaharakati wa Israeli
    • Mzozo wa Gaza: Israel yasema imepata moja ya hifadhi kubwa ya silaha za Hamas
  7. Habari za hivi punde, mzozo wa israel na Hamas: Mateka wa Israel, athibitisha kuuawa Gaza

    Mmoja wa Waisraeli wanaoshikiliwa mateka katika Ukanda wa Gaza, Sahar Baruch, mwenye umri wa mia 25, ameuawa katika eneo hilo, jamii yake ya wakulima (kibbutz) na familia za mateka zimesema katika taarifa.

    "Tutadai kurejeshwa kwa mwili wake kama sehemu ya mpango wowote wa kutolewa kwa mateka.Hatutasimama hadi kila mtu awe nyumbani,” ilisema taarifa hiyo.

    Haya yanajiri baada ya mrengo wa kijeshi wa Hamas kutoa video siku ya Ijumaa ambayo ilisema ilionyesha matokeo ya umwagaji damu ya kushindwa kwa operesheni ya Israel ya kuwakomboa mateka.

  8. Rais wa DRC Tshisekedi amlinganisha Kagame wa Rwanda na Hitler

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi Ijumaa alimlinganisha mwenzake wa Rwanda na Adolf Hitler wakati wa hotuba yake kuhusu kampeni katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo lililokumbwa na mzozo.

    Mashariki mwa DRC imekumbwa na miongo kadhaa ya ghasia zisizokwisha za makundi ya waasi, wakiwemo waasi wa M23 wanaoongozwa na Watutsi ambao wameteka maeneo mengi ya ardhi tangu kuanza mashambulizi mwishoni mwa 2021.

    Kinshasa, pamoja na mataifa kadhaa ya Magharibi yakiwemo Marekani na Ufaransa, yanasema M23 inaungwa mkono na Rwanda, ingawa Kigali imekuwa kikikanusha madai hayo.

    "Nitazungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame na kumwambia hivi: kwa kuwa alitaka kuwa na tabia kama Adolf Hitler kwa kuwa na malengo ya kujitanua (nchini DRC), ninaahidi ataishia kama Adolf Hitler," Tshisekedi aliuambia umati wa watu waliokuwa wakishangilia. katika mkutano wa hadhara Bukavu, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini.

  9. Kitendo cha ujambazi kilichofanywa na mwanamke kilichowashangaza hata majaji

    Mwanamke wa Afrika Kusini alipatikana na hatia ya kuiba dola milioni 28 kutoka kwa kampuni aliyoifanyia kazi, na alihukumiwa kifungo cha miaka 50 jela.

    Hildegard Steenkamp amekuwa akiiba pesa hizi kwa miaka 13, na kuziiba kutoka kwa kampuni ambayo alikuwa mhasibu ya huduma ya afya iliyopo Gauteng.

    Steenkamp tayari amekiri mashtaka 336 ya uhalifu.

    Alifika mbele ya hakimu ambaye alisema hajawahi kushughulikia kesi inayohusu wizi wa pesa, inayohusisha mtu mmoja pekee kwa kiasi hicho cha pesa

    Jaji Phillip Venter alielezea kushtushwa kwake na kitendo hiki akisema "kuelewa kuwa mfanyakazi mmoja aliiba pesa nyingi kiasi hiki kutoka kwa kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi ni jambo la ajabu," alisema hakimu.

    Mwanamke huyo alijitetea kwamba alilazimika kufanya hivyo baada ya kudhulumiwa na mume wake aliyefariki ambaye alimlazimisha kufanya kitendo hiki Lakini Jaji Venter hakukubaliana na hoja hiyo akasema kwamba alifanya hivyo peke yake.

    Wachunguzi waligundua kuwa Steenkamp alitumia pesa hizo kufadhili maisha yake ya kifahari ya kamari, kununua vito vya thamani na kusafiri.

    Moja ya matumizi ya pesa hizo ni $263,000 ambazo alichezesha kamari kwa usiku mmoja.

    Mahakama pia iliambiwa kuwa Steenkamp alitumia karibu $1.6m kwa safari zake za kimataifa na alitembelea Dubai mara kwa mara.

    Alifanya kazi katika kampuni hiyo kutoka 2004 hadi 2017, kabla ya kujiuzulu.

  10. Mzozo wa Israel na Hamas: Nini kilifanyika kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilipiga kura kuhusu azimio lililotaka kusitishwa mara moja kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza.

    Kabla ya kura hiyo - ambayo rasimu yake ilitayarishwa na Umoja wa Falme za Kiarabu na kufadhiliwa na mataifa 97 wanachama - mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema watu wa Gaza "wanaangalia katika shimo ka kuzimu".

    Katika kura hiyo, wanachama 13 walipiga kura ya azimio hilo , huku Uingereza ikipiga ikizuia kupiga kura. Marekani ilikuwa nchi mwanachama pekee ambayoilikataa azimio hilo, kwa kutumia hadhi yake kama mwanachama wa kudumu kupiga kura ya turufu .

    Ikizungumza baada ya kupiga kura, Marekani ilisema kwamba "karibu mapendekezo yetu yote yalipuuzwa". Uingereza, mshirika wake mkuu, ilisema haikukubali azimi hilo kwa "kutolaani ukatili uliofanywa na Hamas" dhidi ya Waisraeli tarehe 7 Oktoba.

    Marekani ilikosolewa na nchi zikiwemo Uchina na Urusi , huku Jimbo la Palestina - ambalo lina hadhi ya uangalizi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa – likitaja kushindwa kwa azimio hilo kama "kipindi cha mabadiliko katika historia", na kuongeza kuwa "mamia ya watu watauawa kufikia muda kama huu kesho" .

    Mataifa mengine katika baraza hilo mwaka huu – ambao uanachama wake huzunguka miongoni mwa wanachama 10 wasio wa kudumu - ni pamoja na Brazil, Japan na Uswizi. Israel si mwanachama kwa sasa.

    Soma zaidi:

    • Gaza huenda isiweze kupona tena kwa maafa yanayosababishwa na vita - Mkuu wa Umoja wa Mataifa
    • Hamas ilipanga unyanyasaji wa kijinsia kama silaha ya vita - mwanaharakati wa Israeli
    • Mzozo wa Gaza: Israel yasema imepata moja ya hifadhi kubwa ya silaha za Hamas
  11. Katika picha: Hali halisi ya mandhari ya kusini mwa Gaza ambako Israel inafanya mashambulizi ya nyumba kwa nyumba

    Wakati jeshi la Israel likiendelea kulenga eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza katika juhudi zake za kuwashinda Hamas, hii hapa ni baadhi ya picha kutoka humo asubuhi ya leo.

    Soma zaidi:

    • Gaza huenda isiweze kupona tena kwa maafa yanayosababishwa na vita - Mkuu wa Umoja wa Mataifa
    • Hamas ilipanga unyanyasaji wa kijinsia kama silaha ya vita - mwanaharakati wa Israeli
    • Mzozo wa Gaza: Israel yasema imepata moja ya hifadhi kubwa ya silaha za Hamas
  12. Seneta wa Marekani: Kitunguu saumu cha China ni hatari kwa usalama wa taifa

    Seneta wa Marekani ametoa wito wa uchunguzi wa serikali kuhusu athari kwa usalama wa taifa wa bidhaa za vitunguu kutoka China.

    Seneta wa chama cha Republican Rick Scott amemwandikia barua katibu wa biashara, akidai kitunguu saumu cha China si salama, akitoa mfano wa mbinu za uzalishaji zisizo safi.

    China ndiyo muuzaji mkubwa zaidi duniani wa vitunguu vibichi na vilivyopozwa na Marekani ndiyo mlaji mkuu.

    Lakini biashara hiyo imekuwa na utata kwa miaka mingi.

    Marekani imeishutumu China kwa "kumwaga" vitunguu saumu sokoni kwa bei ya chini.

    Tangu katikati ya miaka ya 1990 imetoza ushuru mkubwa au ushuru kwa uagizaji wa China ili kuzuia wazalishaji wa Marekani kutozwa bei nje ya soko.

    Mnamo 2019, wakati wa utawala wa Trump, ushuru huu uliongezwa.

    Katika barua yake Seneta Scott anarejelea wasiwasi huu uliopo. Lakini anaendelea kuangazia "wasiwasi mkubwa wa afya ya umma juu ya ubora na usalama wa kitunguu saumu kinachokuzwa katika nchi za kigeni - haswa, vitunguu vinavyokuzwa katika China ya Kikomunisti".

    Anarejelea mazoea ambayo, anasema, "yamerekodiwa" kwenye video za mtandaoni, blogi za kupikia na filamu za kumbukumbu, ikiwa ni pamoja na kupanda vitunguu katika maji taka.

    Ametoa wito kwa Idara ya Biashara kuchukua hatua, chini ya sheria ambayo inaruhusu uchunguzi kuhusu athari za uagizaji maalum kwa usalama wa Marekani.

    Ofisi ya Sayansi na Jamii katika Chuo Kikuu cha McGill huko Quebec, ambayo inajaribu kueneza na kuelezea masuala ya kisayansi, inasema "hakuna ushahidi" kwamba maji taka hutumiwa kama mbolea ya kukuza vitunguu nchini China.

    "Kwa hali yoyote, hakuna shida na hii," nakala iliyochapishwa na chuo kikuu mnamo 2017 inasema.

    "Taka za binadamu ni mbolea yenye ufanisi sawa na taka za wanyama. Kueneza kinyesi cha binadamu kwenye mashamba yanayokuza mazao haionekani kuvutia, lakini ni salama zaidi kuliko unavyoweza kufikiria."

  13. Bowen: Marekani inatumia kura ya turufu lakini shinikizo la kusitisha mapigano Gaza linaongezeka

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amezungumzia "hatari kubwa ya kudumishwa kwa amani na usalama wa kimataifa" katika mzozo wa Gaza, akitoa mfano wa kumwagika kwa mapigano katika "Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, Lebanon, Syria, Iraq na Yemen".

    Alianzisha Kifungu cha 99, na kusababisha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupiga kura siku ya Ijumaa, kwa sababu anaamini kuwa hili ni jambo la dharura sana ambalo lazima liletwe kwa baraza hilo.

    Serikali ya Israel haiupendi umoja wa Mataifa UN na wanamchukia katibu mkuu.

    Waisraeli walikataa maelezo yake, wakidai Bw Guterres ni tishio kwa amani ya dunia kwa sababu anaitambua Hamas katika kujaribu kumaliza mapigano sasa, kabla ya kazi yao ya kuharibu kundi hilo kukamilika.

    Hisia hizo mbaya hazitakuwa bora baada ya katibu mkuu pia kutaja kwamba moja ya hatari ni kwamba hali ya Gaza inaweza kuwa mbaya sana kiasi kwamba kunaweza kuwa na idadi kubwa ya Wapalestina wanaohama kwenye mpaka wa Misri – jambo ambalo pia linatia wasiwasi mkubwa kwa serikali ya Misri.

    Bwana Guterres alisema, kuna hatari kubwa ya "kuporomoka kabisa kwa mfumo wa usaidizi wa kibinadamu katika Gaza". Na Wapalestina wanasema hivyo ndivyo Israeli inavyotaka kwa sababu inataka kuwatoa Wapalestina wote kutoka Gaza.

  14. Cristiano Ronaldo: Afikisha mechi 1,200 katika maisha yake ya soka rasmi

    Cristiano Ronaldo alifikisha mechi ya 1,200 katika maisha yake ya soka rasmi kwa kufunga bao moja na kusaidia jingine kwa klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 aligonga krosi ya Sadio Mane na baadaye akamtengenezea mwenzake Otavio katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Al-Riyadh.

    Ronaldo aliwashukuru wale wote ambao wamemsaidia kufikia alama hiyo - lakini akaongeza kuwa "bado hajamaliza".

    Mshambuliaji huyo wa Ureno ndiye mfungaji bora wa Saudi Pro League akiwa amefunga mabao 16 katika michezo 15 msimu huu.

    Kipa wa zamani wa England Peter Shilton anakubalika kuwa ndiye anayeshikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi za kulipwa katika mchezo wa wanaume akiwa na 1,387.

    The Saudi Pro League ilithibitisha kwenye mitandao ya kijamii kwamba Ronaldo amefikia hatua hiyo na mchezaji huyo baadaye akachapisha kwenye Instagram: "Pointi tatu zaidi! Asante kwa wachezaji wenzangu wote walionisaidia kufikisha mechi yangu ya 1,200. Ni safari gani, lakini bado haijakamilika."

    Ronaldo pia alifikisha mechi yake ya 1,000 kwa wakubwa kwa kufunga mnamo Februari 2020, akiifungia Juventus kwenye Serie A.

    Mnamo Juni, alikuwa mchezaji wa kwanza wa wanaume kucheza mechi 200 za kimataifa alipoichezea Ureno dhidi ya Iceland, na pia ndiye mfungaji bora wa kimataifa akiwa na mabao 128.

    Miongoni mwa rekodi zake za maisha ya klabu, Ronaldo anaongoza orodha ya kucheza mara zote kwenye Ligi ya Mabingwa (183), ambayo aliwakilisha Manchester United, Real Madrid na Juventus.

    Pia amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia kufunga mabao 800 ya kiwango cha juu katika maisha yake ya soka alipoipita jumla ya mabao hayo aliyoichezea Manchester United mwezi Desemba 2021 na tangu wakati huo amevunja mabao 850.

    Al-Nassr wanasalia nafasi ya pili kwenye jedwali, pointi saba nyuma ya viongozi Al-Hilal.

    • Jinsi Ronaldo alifikisha michezo 1,200
    • Sporting - 31 michezo
    • Manchester United - michezo 346
    • Real Madrid - michezo 438
    • Juventus - michezo 134
    • Al Nassr - michezo 46
    • Ureno - michezo 205
  15. Mapigano ya nyumba kwa nyumba yaripotiwa kusini mwa mji wa Gaza

    Mjini Gaza, wakaazi wanaripoti mashambulio mpya ya vifaru vya Israeli kaskazini mwa eneo hilo, huku mapigano makali yakiendelea kusini.

    Mashambulizi ya jeshi la Israel dhidi ya Hamas mjini Gaza yanaendelea kwa nguvu zote, licha ya shinikizo linaloongezeka la kutaka juhudi zaidi zifanyika ili kupunguza vifo vya raia.

    Kusini, vikosi vya Israel vimefanya mashambulizi zaidi dhidi ya Khan Younis, huku mapigano yakitokea nyumba hadi nyumba.

    Jana usiku, mrengo wenye silaha wa Hamas ulitoa video ambayo inasema inaonyesha matokeo ya kushindwa kwa operesheni ya Israel ya kuwakomboa mateka.

    Inaonyesha picha za mwili uliojaa damu unaoonekana kuwa wa mateka. Video haijathibitishwa kwa kujitegemea.

    Msemaji wa jeshi la Israel amesema wanajeshi wawili wamejeruhiwa vibaya wakati wa operesheni za kuwaachilia mateka huko Gaza lakini hakuna aliyeachiliwa.

  16. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja ya leo tarehe 09.12.2023