Mashahidi waripoti milio ya risasi hospitalini Al – Shifa huku Israel ikisema vikosi maalum vinaisaka hospitali hiyo

Wanajeshi wa Israel wanaendelea kufanya msako katika ghorofa moja hadi nyengine katika hospitali ya Al - Shifa , wakati mamia ya wagonjwa na wafanyikazi wa matibabu wakisalia hospitalini humo

Moja kwa moja

  1. ANC yaunga mkono wito wa kutaka ubalozi wa Israel mjini Pretoria ufungwe

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Waafrika kusini wakifanya maandamano ya kutaka ubalozi wa Israel kufungwa nchini humo

    Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimesema kitaunga mkono hoja ya upinzani bungeni "ya kufunga ubalozi wa Israel nchini Afrika Kusini na kusimamisha uhusiano wote wa kidiplomasia na nchi hiyo hadi ikubali kusitishwa kwa mapigano".

    ANC pia imesema inatarajia Israel "kujitolea kuheshimu mazungumzo yaliyowezeshwa na Umoja wa Mataifa".

    Chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) pia kinatoa wito wa kusitishwa kwa uhusiano wote wa kidiplomasia na Israel kwa mshikamano na watu wa Palestina.

    Huruma ya Afrika Kusini kwa mapambano ya Wapalestina kwa ajili ya taifa huru ilianza katika siku za kiongozi wa kupinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela.

  2. Bunge la Kenya launga mkono askari wa Kenya kupelekwa Haiti licha ya kesi mahakamani

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Polisi wa Kenya

    Bunge la Kenya limeidhinisha mpango tata wa serikali kupeleka takriban maafisa 1,000 wa polisi nchini Haiti kusaidia kukomesha ghasia za magenge.

    Hii ni licha ya amri ya mahakama inayozuia askari hao kutumwa nchini haiti, ikisubiri matokeo ya pingamizi la kisheria mahakamani.

    Wabunge wa upinzani walilaani kura hiyo, lakini chama tawala kilitumia wingi wake kuunga mkono serikali kufuatia mjadala mkali.

    Haiti ilikuwa imeomba msaada wa kimataifa ili kukabiliana na ongezeko la uvunjaji sheria.

    Ofa ya Kenya ilipata kibali cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi uliopita, lakini mpango huo umepingwa na chama kikuu cha upinzani.

    Takriban magenge 300 yanafanya kazi nchini Haiti na asilimia 80 ya mji mkuu, Port-au-Prince, uko chini ya udhibiti wa magenge hayo.

    Makundi haya yamechukua udhibiti mkubwa wa mji huo tangu mauaji ya rais wa nchi hiyo mnamo 2021 yalipoiweka Haiti katika mzozo wa kisiasa.

    Katika upigaji kura wa Alhamisi katika bunge la Kenya, wabunge wanaounga mkono hoja hiyo walisema kuwa nchi hiyo ni sehemu ya jumuiya ya kimataifa na haiwezi kupuuza maombi ya kuomba msaada kutoka kwa mataifa mengine.

    Pia walisema kuwa taifa hilo la Afrika Mashariki lina historia ya misheni za kulinda amani kama vile Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sierra Leone.

    Bunge liliidhinisha mpango huo katika muda mfupi wa kupiga kura kabla ya Mahakama Kuu kuanza kusikiliza kesi hiyo.

    Chama kidogo cha upinzani, Thirdway Alliance, kimeongoza changamoto hiyo ya kisheria, kikisema mpango huo haukuwa wa katiba kwa sababu ni wanajeshi pekee wanaoweza kutumwa nje ya nchi.

    Serikali imekataa hoja hiyo, na inatetea kesi hiyo.

  3. Marekani na China zakubali kuanza tena mawasiliano ya kijeshi baada ya mkutano

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais Joe Biden na mwenzake wa China Xi jinping

    Marekani na china zimekubaliana kuendelea na mawasiliano ya kijeshi katika juhudi za kupunguza wasiwasi uliopo, rais Joe Biden amesema.

    "Tumerudi katika mawasiliano ya moja kwa moja, na yalio wazi," alisema kufuatia mkutano nadra na Rais wa China Xi Jinping huko California Jumatano.

    Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wawili hao kuzungumza ana kwa ana kwa zaidi ya mwaka mmoja.

    Lakini bado kulikuwa na dalili za mvutano kati ya wawili hao - Bw Biden alirudia maoni yake kwamba Bw Xi ni dikteta.

    Wizara ya mambo ya nje ya China baadaye ilikosoa matamshi hayo, lakini hayaonekani kuwa yameondoa kile ambacho pande zote mbili zinaonyesha kama mkutano wenye mafanikio makubwa.

    Bw Biden pia alisema viongozi wote wawili wamekubaliana kuanzisha njia ya moja kwa moja ya mawasiliano kati yao.

    Katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano huo, ambao ulifanyika katika eneo la kihistoria la nchi karibu na San Francisco, Bw Biden alisema ukosefu wa mawasiliano ni "jinsi ajali zinavyotokea" na akaongeza kuwa marais wote wawili sasa wanaweza "kuchukua simu na kusikilizwa moja kwa moja. "

  4. Jaribio la dawa latoa matumaini kwa wagonjwa wenye TB sugu

    Majaribio mawili muhimu ya kimatibabu yameonyesha kuwa dawa za antibiotic zinaweza kuzuia kifua kikuu sugu (MDR-TB) miongoni mwa watoto na watu wazima.

    Watafiti kutoka Kituo cha TB cha Desmond Tutu katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch nchini Afrika Kusini walitangaza mjini Paris kwamba dawa, aina ya levofloxacin, inayotolewa mara moja kwa siku kwa watoto zaidi ya miezi sita, ilikuwa salama sana.

    Zaidi ya watu nusu milioni hupata MDR-TB kila mwaka. Ni vigumu kutibu kwa dawa za sasa na gharama ni kubwa.

    Watafiti wa mojawapo ya tafiti hizo mbili wanasema wamepata njia ya kuwalinda watoto kwa usalama wakati mtu mzima nyumbani anaugua maradhi hayo.

    Katika jaribio la TB-CHAMP lililofanywa nchini Afrika Kusini, watoto 453 ambao walikuwa wameambukizwa na mtu mzima TB walipewa levofloxacin. Ni watano tu ndio waliopata ugonjwa huo.

    Utafiti wa pili, wa majaribio ya V-QUIN, uligundua kuwa levofloxacin ilipunguza hatari ya watu wazima na vijana kupata MDR-TB kwa 45%.

  5. Habari za hivi punde, Israel inasema wanajeshi wake wanasaka ghorofa hadi ghorofa katika hospitali ya Al-Shifa

    Kama ambavyo tumekuwa tukiripoti, mtu aliyeshuhudia tukio hilo ameripoti ufyatuaji wa risasi katika hospitali ya Al-Shifa ya Gaza.

    Tumekuwa na taarifa mpya kutoka kwa afisa kutoka Jeshi la Ulinzi la Israeli.

    • Wanasema wanajeshi kutoka kikosi maalum "wanaendelea kufanya operesheni" katika hospitali hiyo. Operesheni hiyo inaelezwa kuwa "tata na inayoendelea"
    • Afisa huyo pia anasema kwamba "askari wanaendelea kufanya msako katika ghorofa moja hadi nyengine, wakati mamia ya wagonjwa na wafanyikazi wa matibabu wakisalia kwenye eneo hilo".
    • Afisa huyo huyo anakariri madai ya IDF kwamba kuna "miundombinu ya kigaidi iliyofichwa katika eneo hilo" - jambo ambalo Hamas inakanusha.
    • Na tena wanasema wamepata silaha na "nyenzo za kijasusi" - pamoja na "vituo vya amri na udhibiti na vifaa vya mawasiliano" mali ya Hamas.
  6. Habari za hivi punde, Shahidi mmoja katika hospitali ya Al-Shifa asema kuwa wanajeshi walifyatua risasi

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Hospitali ya Al Shifa

    Mawasiliano ya ripota wetu huko Gaza anasema kumekuwa na ufyatuaji risasi katika hospitali ya Al-Shifa.

    Khader, mwandishi wa habari ndani ya Al-Shifa, alipigiwa simu na mwandishi wa BBC Rushdi Abualouf - ambapo alisema: "Askari wako kila mahali, wakipiga risasi kila upande."

    Alisema wanajeshi "wamevamia idara zote" za hospitali hiyo, na kuharibu sehemu ya kusini ya ukuta wa jengo hilo na makumi ya magari.

    Tunasubiri taarifa zaidi kuhusu hatua hiyo ilioripotiwa. BBC haikuweza kuithibitisha kwa uhuru.

    Wanajeshi wa Israel waliingia hospitalini zaidi ya saa 36 zilizopita. Jana usiku, walisema walikuwa "wanaendelea na operesheni sahihi na iliyowalenga Hamas"

  7. Mbwa anusurika wiki 10 katika milima ya Colorado kando ya mmiliki wake aliyekufa

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Milima

    Mbwa ambaye alipatikana akiwa hai kando ya maiti ya mmiliki wake wiki 10 baada ya kutoweka katika milima ya Colorado alinusurika kwa kuwinda wanyama wadogo, waokoaji walisema.

    Rich Moore, 71, pamoja na Jack Russell terrier, Finney, walikuwa wamepanga kupanda Blackhead Peak tarehe 19 Agosti, lakini hawakurudi nyumbani.

    Mwili wa Bw Moore ulipatikana tarehe 30 Oktoba, na Finney kando yake.

    Waokoaji walisema ni "hadithi nzuri ya kunusurika".

    Delinda VanneBrightyn, wa kikundi cha kujitolea cha Taos Search and Rescue, alisema waokoaji walifanya msako usio na mafanikio wa siku nyingi katika upande wa magharibi wa mlima huo

    Wiki kadhaa baadaye mwindaji mmoja alipata mwili wa Bw Moore katika Milima ya San Juan - takriban maili 1.5 (2.5km) mashariki mwa kilele - huku Finney akiwa bado hai lakini akiwa na uzani wa takriban pauni sita, karibu nusu ya uzito wake wa awali.

    Kikosi cha uokoaji kilisafirishwa siku iliyofuata. Finney alipelekwa kwa daktari wa mifugo na sasa yuko na familia ya Bw Moore.

  8. Mshauri wa zamani anasema Marekani inabadilisha jinsi inavyoichukulia Israel

    Msaidizi mkuu wa zamani wa kisiasa wa Marekani anasema ameona "urekebishaji" katika wiki chache zilizopita kwa jinsi utawala wa Biden unavyomchukulia mshirika wake Israeli.

    Ben Rhodes, ambaye alikuwa naibu mshauri wa usalama wa taifa chini ya Rais Obama, alipendekeza utawala wa sasa hapo awali ulitumai kuwa unaweza kuwa na athari katika operesheni ya kijeshi ya Israel kwa "kumkumbatia" Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu na serikali yake.

    Lakini hili halijathibitishwa, aliiambia BBC Radio 4 asubuhi ya leo. Rhodes alibainisha kuwa Marekani iliomba kusitisha vita ili kuruhusu misaada ya kibinadamu lakini Israel "imepuuza kwa kiasi kikubwa ushauri huo".

    Rhodes alipendekeza hii ilionyesha tofauti iliopo kati ya nchi hizo mbili, ingawa alisema Marekani "bado inaunga mkono kwa ujumla".

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  9. Israel yaonya watu kuondoka maeneo ya kusini mwa Gaza

    Vikosi vya Israel vilidondosha vijikaratasi katika eneo la Khan Younis kusini mwa Gaza usiku kucha, vikiwaonya watu katika miji minne kuhama makazi yao na kuelekea kwenye hifadhi, Reuters na Times of Israel yanaripoti.

    Vikaratasi hivyo vilionya watu kutafuta usalama katika maeneo ya Bani Shuhaila, Khuzaa, Abassan na Qarara - miji ambayo ilikuwa na watu zaidi ya 100,000, kabla ya kusini kuzidiwa na idadi ya watu waliokimbia makazi.

    "Kwa usalama wako, unahitaji kuhama mara moja kwenye makazi yako na kuelekea kwenye makazi yanayojulikana. Mtu yeyote aliye karibu na magaidi au vituo vyao anaweka maisha yake hatarini, na kila nyumba inayotumiwa na magaidi italengwa," vijikaratasi hivyo vilisema, kulingana na Reuters. .

    Wiki zilizopita, vijikaratasi kama hivyo vilirushwa kaskazini mwa Gaza kabla ya mashambulizi ya ardhini.

    Pia siku ya Alhamisi asubuhi, wizara ya mambo ya ndani ya Gaza inayoendeshwa na Hamas ilisema helikopta za Israel "zimeshambulia nyumba za raia mashariki mwa Khan Younis".

    Mnamo Oktoba, idadi ya watu wa Khan Younis ilitoka kwa wakaazi 400,000 hadi zaidi ya milioni huku mamia ya maelfu wakiondoka kaskazini mwa Gaza.

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

  10. Hiki ndicho ilichopata Israel chini ya hospitali ya Al-Shifa

    .

    Chanzo cha picha, IDF

    Kama tulivyoripoti, wanajeshi wa Israel wanaendelea na msako wao katika hospitali ya Al-Shifa katika Jiji la Gaza - kituo kikubwa zaidi cha matibabu katika Ukanda wa Gaza.

    Mwishoni mwa mwezi uliopita, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilishutumu Hamas kwa kuwa na kambi yake kuu chini ya Al-Shifa. Ilitoa picha ambayo lilitumia 3D kuibua mtandao unaodaiwa kuwa na mahandaki chini ya ardhi .

    Msemaji alisema kulikuwa na uhusiano kutoka hospitali na mahandaki, na walikuwa na "ushahidi halisi" kwamba "mamia" ya wapiganaji wa Hamas walikuwa wamejificha katika hospitali baada ya mashambulizi dhidi ya Israeli tarehe 7 Oktoba.

    Marekani baadaye ilisema taarifa zake za kijasusi zilithibitisha taarifa za Israel kuhusu matumizi ya hospitali hiyo na Hamas - ingawa Hamas imekuwa ikikanusha.

    Israel ilisema wanajeshi wake waliingia katika hospitali hiyo takriban saa 36 zilizopita. Wamemruhusu mwandishi wa BBC Lucy Williamson ndani, wakionyesha vitu ambavyo wanasema wamevipata - ikiwa ni pamoja na bunduki 15, vesti za kuzuia risasi na vitu vingine ikiwa ni pamoja na kompyuta ndogo.

    IDF bado haijaonyesha ushahidi wa kituo cha Hamas au handaki chini ya hospitali kama ilivyosema awali.

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  11. Afrika Kusini yaishtaki Israel katika mahakama ya ICC

    Rhamaphosa

    Chanzo cha picha, Reuters

    Afrika Kusini imeishitaki serikali ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kufuatia jukumu lake katika mzozo wa Gaza, Rais Cyril Ramaphosa alisema Jumatano.

    "Afrika Kusini, kama nchi nyingine nyingi duniani, tumeona inafaa kuishshtaki serikali ya Israel kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Tumetuma rufaa kwa sababu tunaamini kuwa uhalifu wa kivita unafanywa huko," Rais Ramaphosa alisema

    Hakufichua nchi nyingine zilizoshtaki Israel ICC. Aliongeza kuwa hawakuunga mkono shambulio la awali la Hamas dhidi ya Israel lakini wanapinga hatua zinazoendelea za Israel, ambazo "wanaamini kwamba uchunguzi unastahili kufanywa na ICC".

    ICC ni mahakama ya kimataifa ambayo inachunguza na kuwahukumu watu binafsi wanaotuhumiwa kufanya uhalifu mkubwa unaotia wasiwasi jumuiya ya kimataifa, kama vile uhalifu wa kivita au mauaji ya halaiki.

    Afrika Kusini imekuwa moja ya wafuasi wengi wa Wapalestina katika mzozo unaoendelea na Israel.

    Viongozi kadhaa wa nchi hiyo wamewaunga mkono hadharani Wapalestina na pia kumekuwa na maandamano ya kuunga mkono Palestina.

  12. Tazama: Ufyatuaji wa mizinga ya heshima kwa ajili ya sherehe ya miaka 75 ya kuzaliwa ya Mfalme charles III

    Maelezo ya video, Tazama: ufyatuaji wa mizinga ya bunduki ya heshma kwa ajili ya sherehe ya miaka 75 ya kuzaliwa ya Mfalme charles III

    Kasri la Buckingham liliadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa kwa Mfalme Charles III kwa kufyatua mizinga ya bunduki 41. Tukio hilo lilitekelezwa na Kikosi cha Wanajeshi wa Kifalme cha Kivita cha London Green Park.

    Itakuwa mojawapo ya salamu za bunduki siku ya Jumanne kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mfalme, ikiwa ni pamoja na milio 62 katika Mnara wa London (Tower of London)

    Mfalme Charles atatumia siku hiyo kufanya shughuli za umma, na baadaye ataandaa hafla ya mamia ya wauguzi na wakunga, kama sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Huduma ya Kitaifa ya Afya.

  13. Malawi yasitisha safari zote za kiserikali nje ya nchi

    Rais wa Malawi aliagiza mawaziri wote walio nje ya nchi kurejea nyumbani

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amesitisha safari zote za kimataifa zinazomhusisha yeye na maafisa wote wa serikali.

    Pia amewaagiza mawaziri wote walioko nje ya nchi kwa sasa kurejea nyumbani.

    Akihutubia taifa kupitia televisheni Jumatano usiku, pia alitangaza vikwazo vya usafiri wa ndani na kupunguza kwa nusu ya mgao wa mafuta kwa mawaziri na maafisa wakuu wa serikali.

    Hatua hizo zitadumishwa hadi mwisho wa mwaka wa fedha mnamo Machi 2024.

    Baadhi ya hatua kama hizo za kubana matumizi pia zilitangazwa wakati wa janga la Covid lakini zilikuwa na athari ndogo kwani hazikutekelezwa kikamilifu.

    Rais alimtaka waziri wa fedha kuweka masharti ya nyongeza ya mishahara kwa watumishi wote wa umma katika mapitio yajayo ya bajeti.

  14. Biden 'ana matumaini kidogo' kuhusu kuachiliwa kwa mateka wa Gaza

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa Marekani Joe Biden anasema "ana matumaini kidogo" kuwa kutakuwa na mpango wa kuwakomboa zaidi ya watu 200 wanaoshikiliwa mateka Gaza.

    Aliuambia mkutano na waandishi wa habari California hapo awali kwamba hakutaka kuzungumza kabla ya wakati wake lakini kwamba Marekani imeona "ushirikiano mkubwa" kutoka kwa Qatar, ambayo imekuwa ikiongoza mazungumzo yanayoendelea kati ya Israel na Hamas.

    Akizungumzia operesheni ya hivi karibuni ya Israel katika hospitali kubwa zaidi ya Gaza - Al-Shifa - rais huyo wa Marekani anasema Hamas ilifanya "uhalifu wa kivita" kwa kuwa na kituo chini yake.

    Israel imeonyesha kile inachodai kuwa ni silaha na vifaa vingine vya Hamas ambavyo vilipatikana kutoka hospitalini.

    Hamas inakanusha kuwa inatumia vituo vya matibabu kama ngome ya harakati zake za kijeshi dhidi ya Israel.

    Biden anasema Marekani imeitaka Israel kuwa makini , kuhakikisha kuwa raia wanakuwa salama wakati wa kuzisaka ngome za Hamas.

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  15. Polisi Washington wajeruhiwa katika maandamano ya uungaji mkono wa Wapalestina

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Polisi wa mjini Washnton Marekani wakijaribu kuwaondoa waandamanaji kutoka makao makuu ya DNC wakati wa maandamano

    Polisi wanasema kuwa takriban maafisa sita wamejeruhiwa baada ya waandamanaji wengi kukabiliana na mamlaka nje ya ofisi za Kamati ya Kitaifa ya Kidemokrasia (DNC) mjini Washington.

    Maafisa waliokuwa wamevalia zana za kudhibiti ghasia walitumia pilipili ili kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wakitaka kusitishwa kwa shughuli za kijeshi za Israel Gaza.

    Takriban mtu mmoja amekamatwa hadi sasa, polisi walisema.

    Mbunge wa California Brad Sherman alikuwa miongoni mwa wale ambao walilazimika kuhamishwa kutoka kwa DNC.

    "Waandamanaji walikua na vurugu, wakiwapulizia pilipili maafisa wa polisi na kujaribu kuingia ndani ya jengo hilo," aliandika kwenye mtandao wa kijamii.

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  16. Farasi alivyoilazimisha ndege kurudi kwenye uwanja wa ndege baada ya kutoroka kwenye kibanda

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Farasi, ambaye hayupo kwenye picha hii, alitoroka wakati ndege hiyo ikisafiri umbali wa futi 30,000 (picha ya faili)

    Ndege ya mizigo aina ya Boeing 747 imelazimika kugeuka, baada ya farasi kutoroka kutoka kwenye kibanda chake ndani ya ndege na kusababisha vurugu wakati ndege hiyo ikisafiri kumbali wa futi 30,000 (9,144m) angani.

    Ndege hiyo ilikuwa ikitoka New York kuelekea Ubelgiji lakiniilibidi ilazimike kurudi baada ya farasi aliyekuwemo ndani ya banda lake kwenye ndege kutoroka takriban dakika 90 baada ya ndege hiyo kupaa.

    Sauti ya udhibiti wa usafiri wa anga ilimrekodi rubani akisema: "Tuna mnyama hai, farasi, kwenye ndege. Farasi ametoroka.""Hatuwezi kumrejesha farasi salama."

    Rubani wa ndege ya Air Atlanta Icelandic 4592 aliwaambia waongozaji wa safari ya ndege hali ilikuwa swari, lakini farasi aliyeruka ndiye aliyekuwa na wasiwasi.

    Kisha alimuomba daktari wa mifugo kukutana na ndege hiyo mara tu ilipotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F Kennedy.

    Bado haijafahamika ni kwa jinsi farasi Houdini alivyoweza kutoka ndani ya kibanda chake na kutoroka.

    Ndege hiyo ilipaa baadaye siku hiyo hiyo na kufanikiwa kufika katika Uwanja wa Ndege wa Liege Ijumaa asubuhi, kulingana na FlightRadar24.

  17. Jeshi la Ulinzi la Israel limeripoti tena mashambulizi ya anga dhidi ya Hezbollah.

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Israel imepeleka makombora kwenye mpaka wake na Lebanon

    Katika ujumbe wa X ( zamani ikiitwa Twitter), jeshi la Israel limesema lilishambulia maeneo kadhaa katika ardhi ya Lebanon Jumatano.

    Limesema miongoni mwa maeneo hayo ni pamoja na ghala la silaha, miundombinu ya kijeshi, vituo vya uchunguzi na maeneo ambayo wanamgambo wa Hezbollah walirusha makombora katika ardhi ya Israel.

    g

    Chanzo cha picha, X

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  18. Ikiwa ndio kwanza unautembelea mtandao wetu, huu ndio muhtasari wa habari kuu za dunia

    • Israel imeahidi itatoa ushahidi wa kuthibitisha madai yake kuwa wanamgambo wa Hamas wana kituo chao kikuu cha kuratibu operesheni zao katika hospitali ya Al Shifa,hospitali kubwa zaidi Gaza.
    • Mpaka sasa jeshi hilo halijatoa ushahidi madhubuti unaothibitisha kuwa chini ya majengo ya Al Shifa kuna mahandaki ya Hamas lakini imeonesha video ambazo haziwezi kuthibitishwa kuwa walipata silaha ndani ya hospitali hiyo. Hamas mara kwa mara imeakanusha madai hayo.
    • Baaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linalotaka kusitishwa na kurefushwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa misingi ya kiutu katika Ukanda wa Gaza.
    • Rais wa Marekani Joe Biden ameyataja mazungumzo yake na kiongozi wa China Xi Jinping mjini San Francisco kama yenye tija zaidi kuwahi kufanyika kati yao.
    • Raia wa Madagascar leo wanapiga kura katika uchaguzi wa rais unaokuja baada ya wiki kadhaa za maandamano.
  19. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 16.11.2023