Mapigano makali yanaendelea kaskazini mwa Gaza wasiwasi ukiongezeka kuhusu watoto wachanga katika hospitali kuu
Mkuu wa WHO anasema "hali ni mbaya na hatari" baada ya kuanzisha tena mawasiliano na waliomo ndani ya Al-Shifa.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi, Dinah Gahamanyi and Asha Juma
Vyombo vya habari vya serikali ya Urusi vimeondoa ripoti ya kurudi nyuma vikosi vya nchi hiyo

Chanzo cha picha, AFP
Vyombo vya habari vya serikali ya Urusi Jumatatu vilichapisha na kubatilisha haraka ripoti za kuondolewa kwa vikosi vya nchi hiyo kutoka kwenye ukingo wa kulia (magharibi) wa Mto Dnipro.
Ripoti hizo zilinukuu wizara ya ulinzi ya Urusi ikitangaza wanajeshi wanahamishwa "kwenye nafasi nzuri zaidi" upande wa kushoto unaokaliwa na Urusi - au mashariki. Taarifa hizo zilifutwa haraka mno.
Wizara ya ulinzi ya Urusi ililaumu kuchapishwa kwa "ripoti ya uwongo" kwa "akaunti bandia" inayohusishwa na Ukraine.
Ukraine kwa upande wake ilidai kuwa tangazo hilo ni operesheni ya Urusi ya kutotoa taarifa zinazotekelezwa dhidi yake.
Marekebisho ya haraka ya Jumatatu yalifanyika karibu mwaka mmoja baada ya vikosi vya Urusi kuwaondoa wanajeshi wao kutoka kwa ukingo wa kushoto, pamoja na kutoka mji wa Kherson.
Mto huo kwa kiasi kikubwa unaendelea kutenganisha vikosi vya Ukraine na Urusi.
Katika ripoti hizo ambazo sasa zimebatilishwa, mashirika ya habari ya serikali Tass na RIA-Novosti yalisema Urusi imeweka tena wanajeshi wake katika maeneo ya mashariki mwa mto Dnipro, ili "kukomboa baadhi ya vikosi vyake, ambavyo vitatumika kwa operesheni za uvamizi katika maeneo mengine" .
Walionyesha lugha sawa na ile iliyotumiwa katika matangazo ya awali ya Urusi kurudi nyuma.
Ikulu ya Kremlin ilikataa kuzungumzia tukio hilo, ikisema ni suala la kijeshi.
Wapiganaji wenye mafungamano na Iran wauawa katika mashambulizi ya Marekani dhidi ya Syria
Marekani ilisema hapo awali kuwa ilifanya mashambulizi ya anga katika vituo viwili vinavyotumiwa na Walinzi wa Iran Revolutionary Guards nchini Syria na makundi yenye mafungamano na Iran kujibu mashambulizi yanayoendelea dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Syria na Iraq.
Shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Syria (SOHR), kundi la ufuatiliaji lenye makao yake makuu nchini Uingereza, sasa linaripoti kwamba wanachama wanane wa wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran wameuawa wengi wao wakiwa si raia wa Siria.
Inasema kuwa mashambulizi hayo yaliharibu ghala la silaha katika maeneo ya mashambani karibu na Albu Kamal na jukwaa la kurusha roketi karibu na Mayadin.
SOHR pia inasema wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran walirusha makombora katika kambi za Marekani katika uwanja wa gesi wa Conoco na eneo la mafuta la al-Omar usiku kucha. Hakukuwa na ripoti za mara moja za majeruhi yoyote ya Marekani.
Jeshi la Israel linasema wanajeshi 44 wa Israel wamefariki tangu kuanza kwa operesheni ya ardhini huko Gaza

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Jeshi la Israel IDF Jeshi la Israel limesema siku ya Jumatatu kuwa wanajeshi wengine wawili wamefariki wakati wa mapigano kaskazini mwa Gaza.
Kulingana na vyombo vya habari vya Israel, idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa tangu kuanza kwa operesheni ya ardhini imeongezeka hadi 44.
Jeshi la Israel limesema kuwa linaendelea na mashambulizi kwenye viunga vya kambi ya wakimbizi ya Al-Shati magharibi mwa Mji wa Gaza.
Waasi wa Colombia wajaribu kuhalalisha utekaji nyara wa babake kiungo wa Liverpool Luis Díaz

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Luis Manuel Díaz (wa tatu kushoto) aliachiliwa tarehe 9 Novemba kwa usaidizi wa wajumbe wa Umoja wa Mataifa na Kanisa Katoliki. Raia wa Colombia wamejawa na hasira baada ya kiongozi wa waasi wa Colombia, ambao walimshikilia babake mwanasoka wa Liverpool Luis Díaz, kujaribu kuhalalisha utekaji nyara wake.
Jeshi la Ukombozi wa Kitaifa (ELN) lilisema lililazimika kumteka nyara ili kupata pesa kwa sababu lilikuwa "maskini".
Kundi hilo limekuwa likifanya mazungumzo ya amani kwa karibu mwaka mmoja.Kutekwa nyara kwa babake Luis Díaz, kocha mahiri wa mpira wa miguu, kumezua shaka juu ya kujitolea kwake kwa mazungumzo.
Wazazi wa mwanasoka huyo, Luis Manuel Díaz na Cilenis Marulanda, walikamatwa kwa mtutu wa bunduki tarehe 28 Oktoba katika mji alikozaliwa wa Barrancas, kaskazini mwa jimbo la La Guajira.
Watekaji nyara walimwachilia Bi Marulanda ndani ya gari saa chache baadaye huku vikosi vya usalama vya Colombia, wanajeshi na polisi, wakiwakaribia watekaji nyara.
Lakini waasi hao walimshikilia Luis Manuel Díaz mwenye umri wa miaka 58 kwa siku 12 kabla ya kumwachilia kwa ujumbe unaojumuisha maafisa kutoka Umoja wa Mataifa na Kanisa Katoliki.
Kamanda wa waasi wa ELN Antonio García amesimama kidete kwenye msimamo wa ELN kuhusu utekaji nyara tangu Luis Manuel Díaz aachiliwe.
Kamanda wa waasi alisisitiza kuwa utekaji nyara kwa ajili ya fidia sio ukiukaji wa usitishaji mapigano ambao kundi lake lilikuwa limetia saini, ambao ulianza kutumika mnamo Agosti.
Bwana García hapo awali alidai kwamba kulengwa kwa babake mwanasoka huyo maarufu lilikuwa "kosa".
"Hakuna makubaliano yoyote ambayo ELN imejitolea kujizuia na shughuli za kifedha, ikiwa ni pamoja na kumnyima mtu uhuru wake kwa sababu za kiuchumi," aliandika katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Israel haipaswi kukaa kwa muda mrefu Gaza - mkuu wa zamani wa Mossad
Danny Yetom, ambaye alikuwa mkuu wa Mossad wakati Israeli ingali na wanajeshi na walowezi wa Kiyahudi huko Gaza, anaiambia BBC Israel haipaswi kukaa muda mrefu katika Ukanda wa Gaza.
Anaendelea kusema kuwa Israel haitaweza kuondoka Gaza hadi "wote waliotekwa nyara wamerejeshwa na tumeshinda vita dhidi ya Hamas".
Anafafanua kushinda kama "kuanguka kwa Hamas kama chombo, na kupoteza uongozi wake".
Unaweza pia kusoma:
- Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
- Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
- Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
- 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
- Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
Chama cha Labour: 'Waziri wa zamani wa Uingereza amerudi kama mwokozi wa Sunak'

Chanzo cha picha, Reuters
Chama cha Labour nchini Uingereza kimetoa maoni yake ya kwanza tangu uteuzi wa David Cameron kama waziri wa mambo ya nje.
"Wiki chache zilizopita Rishi Sunak alisema David Cameron alikuwa sehemu ya hali iliyofeli, sasa anamrejesha kama mwokozi wake," mratibu wa kampeni ya kitaifa Pat McFadden anasema.
"Huu ndio mwisho wa kauli ya kinaya ya Waziri Mkuu ya kutoa mabadiliko kutoka kwa miaka 13 iliyofeli ya Tory."
Bw Cameron, ambaye amekuwa nje ya Bunge tangu alipojiuzulu kama waziri mkuu mwaka wa 2016, amepewa kiti katika Bunge la Juu ili kumwezesha kuchukua wadhifa wake mpya.
Soma zaidi:
Habari za hivi punde, Jeshi la Israel lasema makombora yalirushwa kutoka Lebanon hadi Israeli

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema makombora mawili yalirushwa kutoka Lebanon.
Tahadhari ilianzishwa katika eneo la Galilaya lakini makombora yalitua katika eneo la wazi, na hakuna hasara iliyoripotiwa.
Katika taarifa ya X, IDF inasema vikosi vyake vilishambulia "seli ya kigaidi yenye silaha" katika eneo la Lebanon.
Tangu mzozo wa sasa kuzuka kati ya Israel na Hamas, kumekuwa na mapigano karibu kila siku kwenye mpaka kati ya Israel na Lebanon. Hezbollah inayoungwa mkono na Iran imehusika katika mashambulizi hayo.
Rais Ruto atuma baraza zima la mawaziri kwenda kupanda miti

Chanzo cha picha, KEN MUNGAI/BBC
Rais William Ruto nchini Kenya anaongoza juhudi za upandaji miti kote nchini humo hii leo.
Lengo kuu la serikali ni kupanda miti milioni 150 ifikapo mwisho wa siku, kulingana na sikukuu ya umma iliyotangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki mnamo Novemba 7, 2023.
Kama sehemu ya mpango mkubwa wa kupanda miti bilioni 15 katika mwongo ujao, makatibu mbalimbali wa Baraza la Mawaziri watasimamia mazoezi haya katika kaunti tofauti tofauti.
Ili kuhakikisha mradi huo unafaulu, Waziri wa Mazingira Soipan Tuya Jumapili, alisisitiza kuwa serikali inategemea mwongozo wa kisayansi kubainisha aina za miti itakayopandwa.
Zaidi ya hayo, watajumuisha teknolojia mpya ili kuimarisha juhudi kubwa za upandaji.
Mpango huo wa upandaji miti utahusisha kaunti zote 47 nchini Kenya huku makatibu wa baraza la mawaziri na magavana wakisimamia mchakato huo, na kuhimiza ushiriki mkubwa kutoka kwa wananchi.
Soma zaidi:
Tazama: Video inayomuonyesha simba aliyetoroka akizurura katika mji wa Italia
Maelezo ya video, Video inaonyesha simba akirandaranda kwenye barabara ya makazi kabla ya kukamatwa. Simba ambaye alionekana akitembea Ladispoli, magharibi mwa Roma, amekamatwa na kurudishwa kwenye makazi yake alikotoroka.
Video iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha wenyeji wakishangazwa kuona simba akizurura katika mitaa ya mji wa pwani wa Italia.
Simba kwa jina Kimba, alikamatwa zaidi ya saa tano baada ya tahadhari ya awali kutolewa.
Mmiliki Rony Vassallo alisema simba huyo alikuwa anaendelea vizuri, na kwamba uchunguzi unaendelea ili kujua jinsi alivyotoroka.
Waziri Mkuu wa Uingereza amfuta kazi waziri wa mambo ya ndani

Chanzo cha picha, Reuters
Suella Braverman amefutwa kazi kama waziri wa mambo ya ndani, baada ya kukaidi serikali kwa kushutumu polisi wa jiji la London kwa upendeleo katika maandamano.
Bi Braverman alishutumiwa kwa kuchochea mvutano kabla ya maandamano mjini London mwishoni mwa juma.
James Cleverly ametangazwa kuchukua nafasi yake, huku waziri mkuu wa zamani David Cameron akichukua nafasi yake kama waziri wa mambo ya nje bila kutarajiwa.
Alisema kuhudumu kama waziri wa mambo ya ndani ilikuwa "bahati nzuri zaidi ya maisha yangu".
Kufutwakazi kwa Bi Braverman kunapelekea mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rishi Sunak huku akiunda upya timu yake ya juu kabla ya Taarifa ya Msimu wa Pukutizi wiki ijayo.
Msemaji rasmi wa Waziri Mkuu alisema: "Mabadiliko haya yatampa waziri mkuu timu imara ya kuleta mabadiliko ambayo nchi hii inahitaji kwa muda mrefu."
Bw Cameron, ambaye amekuwa nje ya Bunge tangu alipojiuzulu kama waziri mkuu mwaka wa 2016, amepewa kiti katika Bunge la Juu ili kumwezesha kuchukua wadhifa wake mpya.
Chama cha Liberal Democrats kinataka uteuzi wa Bw Cameron kuzuiwa, kikirejelea ushawishi wake kwa kampuni ya fedha ya Greensill Capital iliyoporomoka.
Ivory Coast: Aliyekuwa Waziri Mkuu aliyejipeleka uhamishoni anapanga kurejea nyumbani

Chanzo cha picha, AFP
Waziri Mkuu wa zamani wa Ivory Coast Guillaume Soro, ambaye alijipeleka uhamishoni mwaka wa 2019, anasema anapanga kurejea nyumbani licha ya kuwa na hatia mbili za uhalifu.
Alisema Jumapili kwamba alitaka kurejea kwa sababu ilikuwa vigumu "kuishi mbali na mababu zangu... ardhi ya Afrika".
Aliongeza kuwa anataka "kuchangia maridhiano" ya nchi.
Mnamo 2021, mahakama ya Ivory Coast ilimhukumu Soro ambaye hayupo kifungo cha maisha kwa kudhoofisha usalama wa taifa.
Mwaka uliotangulia, alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa mashtaka yanayohusiana na ubadhirifu wa fedha za umma.
Hukumu zote mbili zilitokea wakati Soro alikuwa uhamishoni wa kujilazimisha, ambao ulianza Desemba 2019.
Lakini Soro Jumapili alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulikuwa Twitter, kwamba "hakuwa na hatia ya uhalifu wowote".
Aliongeza kuwa jaribio la kumkamata lilifanyika dhidi yake katika uwanja wa ndege nchini Uturuki tarehe 3 Novemba, katika jaribio la kumrejesha nchini Ivory Coast.
Ingawa Soro hakutaja tarehe ya kurejea kwake, alikuwa ametangaza mnamo mwezi Mei kwamba ana nia ya kugombea uchaguzi wa urais wa 2025 nchini Ivory Coast.
Azma yake ya awali ya kuwania urais katika uchaguzi wa 2020 ilisitishwa na uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba.
Soro, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi lililokuwa likiendesha shughuli zake kaskazini mwa Ivory Coast mwanzoni mwa miaka ya 2000, alikuwa mshirika mkuu wa Rais wa sasa, Alassane Ouattara.
Alitoa usaidizi wa kijeshi kwa Bw Ouattara wakati wa mzozo wa kuwania madaraka dhidi ya Rais wa wakati huo Laurent Gbagbo kufuatia mzozo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa 2010, ambao ulisababisha vya muda mfupi vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua karibu watu 3,000.
Iliisha wakati Bw Gbagbo alipokamatwa Aprili 2011.
Rais wa Israel akanusha kuwa hospitali ya Gaza imeshambuliwa

Rais wa Israel Isaac Herzog amekanusha kuwa Israel inashambulia hospitali kubwa zaidi ya Gaza.
Ripoti kutoka kwa wafanyikazi wa Al-Shifa zinaonyesha kuwa kituo hicho kinachohifadhi maelfu ya Wapalestina hakina umeme.
Lakini Bw Herzog alisema "kila kitu kinaendelea" hospitalini.
Akizungumza na mwandishi wa BBC Laura Kuenssberg pia alisema nakala ya kitabu cha Adolf Hitler kwa jina Mein Kampf kilipatikana kwenye mwili wa mpiganaji wa Hamas kaskazini mwa Gaza.
Bw Herzog alisema nakala iliyotafsiriwa kwa Kiarabu ilipatikana "siku chache tu zilizopita" katika chumba cha watoto ambacho "kimegeuzwa kuwa kituo cha operesheni ya kijeshi cha Hamas".
Ilani ya kiongozi wa Nazi ya kupinga Uyahudi ilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1925.
Akitafuta nakala yake kaskazini mwa Gaza, Bw Herzog alisema, ilionyesha kwamba baadhi ya Hamas "walijifunza tena na tena itikadi ya Adolf Hitler ya kuwachukia Wayahudi".
Awali, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema limepoteza mawasiliano na hospitali ya Al-Shifa, huku wafanyakazi na wagonjwa wakiwa wamenaswa na mapigano nje.
Mkuu wa WHO Dkt Tedros Ghebreyesus baadaye alisema kwamba mawasiliano yamerejeshwa lakini alionya kuhusu hali "mbaya" inayoendelea huko ndani. Alirudia wito wa kusitishwa kwa mapigano na kusema hospitali haina umeme wala maji kwa siku tatu.
Madaktari na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza wamesema kukosekana kwa mafuta kunamaanisha wagonjwa hawawezi kufanyiwa upasuaji na mashine za kuangulia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati haziwezi kufanyakazi. Lakini rais amepinga hili.
"Tunakataa hili kabisa, kuna mzunguko mwingi wa Hamas... lakini kuna umeme huko Shifa, kila kitu kinaendelea," Bw Herzog alisema.
Israel imesema kuwa Hamas ina kambi chini ya jengo la hospitali - madai ambayo yamekanushwa na Hamas.
Daktari wa upasuaji Marwan Abu Saada aliambia BBC Jumamosi kwamba hospitali hiyo imekosa maji, chakula na umeme.
Alisema sauti za risasi na mabomu zilisikika hospitalini "kila sekunde".
Msemaji wa jeshi la Israel Rear Admiral Daniel Hagari alisema Israel ingesaidia kuwahamisha watoto wachanga kutoka Al-Shifa kufuatia ombi kutoka kwa uongozi wa hospitali.
Kikundi cha madaktari kilisema Jumamosi kwamba watoto wawili waliozaliwa kabla ya wakati tayari walikuwa wamefariki.
Unaweza pia kusoma:
- Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
- Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
- Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
- 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
- Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
Wakenya wapata likizo ya kupanda miti ili kupanda miche milioni 100
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Basillioh Rukanga
- Nafasi, BBC Nairobi

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Miti inapandwa kwa uangalifu kwa kuzingatia upandaji mahali pazuri inapofaa kupandwa Wakenya wamepewa likizo maalum ya kupanda miti milioni 100 kama sehemu ya lengo la serikali kupanda miti bilioni 15 katika kipindi cha miaka 10.
Likizo hiyo inaruhusu "kila Mkenya kumiliki mpango huo", kulingana na Waziri wa Mazingira Soipan Tuya.
Kila Mkenya anahimizwa kupanda angalau miche miwili, hivyo basi kufikia lengo la milioni 100.
Takriban miche milioni 150 imepatikana katika vitalu vya umma.
Serikali itakuwa ikitoa miche hiyo bila malipo katika vituo vya wakala wa misitu ili Wakenya waipande katika maeneo maalum ya umma.
Lakini pia imewahimiza Wakenya kununua angalau miche miwili ili kuipanda katika ardhi yao wenyewe.
Rais William Ruto anaongoza zoezi hilo eneo la Makueni mashariki mwa nchi. Mawaziri wametumwa katika mikoa mingine kuongoza shughuli hiyo pamoja na magavana wa kaunti.
Upandaji miti utafuatiliwa kupitia programu (app) ya mtandao, ambayo inafuatilia zoezi hilo kwa kuruhusu watu binafsi na mashirika kurekodi shughuli, ikiwa ni pamoja na aina ya mimea, nambari na tarehe iliyopandwa.
Programu ya Jaza Miti pia itasaidia watu kupanda miche inayofaa kwa kulinganisha eneo la ardhi na spishi zinazofaa, kulingana na wizara ya mazingira.
Bi Tuya aliaambia televisheni ya Citizen nchini humo siku ya Jumapili usiku kwamba muitikio uilikuwa "wa kushangaza" na tayari kulikuwa na usajili milioni mbili kwenye programu kufikia Jumapili.
Hata hivyo alisema upandani wa miche hiyo hautafanyika katika eneo la kaskazini-mashariki, ambako kumekuwa na mafuriko.
Kwa sasa nchi inakabiliana na mvua kubwa ya El Niño ambayo imeiwaua makumi ya watu, maelfu ya watu kuyahama makazi yao na kuharibu miundombinu - huku eneo la kaskazini likiathirika zaidi.
Wakenya wameitikia kwa kiasi kikubwaupandaji miti huku pia wakibainisha baadhi ya changamoto.
Mwanamazingira Teresa Muthoni aliambia BBC kwamba mpango huo ulikuwa "wazo zuri sana", lakini zoezi hilo halikuandaliwa kwa njia ambayo ingehakikisha kila mtu yuko nje akipanda miti.
Alisema "watu wengi wanapaswa kuendelea na kazi zao za kuweka chakula mezani... inakuja wakati uchumi wetu hauendi vizuri hivyo watu wengi wanatatizika kifedha".
Pia alibainisha kuwa "miti mingi kati ya milioni 150 inayopatikana" katika vitalu vya umma ilikuwa ya migeni. "Ni muhimu sana kupanda miti inayofaa mahali pazuri," alisema.
Serikali pia imekosolewa kwa kutetea upandaji miti huku ikishindwa kudhibiti ukataji haramu wa miti katika misitu ya umma - hivi majuzi iliondoa marufuku ya ukataji miti.
Lakini siku ya Jumapili, waziri alitetea uamuzi huo, akisema ni misitu iliyotengenezwa kwa madhumuni ya kibiashara pekee ndiyo iliyoathiriwa - karibu 5% ya jumla ya misitu yote.
Mzozo wa Israel na Hamas: Haya ndiyo yanayojiri hivi punde

Chanzo cha picha, Reuters
Ikiwa unajiunga nasi, au unahitaji muhtasari, haya hapa ni baadhi ya matukio muhimu yaliyojiri saa chache zilizopita.
- Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema hospitali ya Al-Shifa katika Jiji la Gaza "haifanyi kazi kama hospitali tena"
- ·Kuna "milio ya risasi na milipuko ya mara kwa mara" katika eneo karibu na hospitali, kulingana na mkuu wa WHO Tedros Adhanom, ambayo "imezidisha hali ambayo tayari ni mbaya"
- Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas inasema zaidi ya watu 2,000 wako ndani ya Al -Shifa, wakiwemo wagonjwa, wahudumu wa afya na waliokimbia makazi yao.
- Jeshi la Israel limekariri kuwa ''liko tayari kusaidia'' kuwahamisha watoto kadhaa kutoka hospitalini - lakini linakanusha kugonga hospitali wakati wa mapigano na Hamas.
- Madaktari wa Al-Shifa wanasema wanahofia kwamba watoto 36 waliosalia wanaohitaji matibabu ya uangalizi mkubwa wanaweza kufa huku shirika la misaada la Medical Aid kwa Wapalestina likisema bila ambulensi, vifaa muhimu au hospitali ya kuwahamisha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, "hakuna dalili ya jinsi ili linaweza kufanyika kwa usalama''
- Kwingineko, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema wakati wa mahojiano na mtandao wa NBC wa Marekani kwamba '' kunaweza kuwa '' makubaliano ya kuwaachilia mateka wa israel waliosalia Gaza - lakini hakutoa maelezo yoyote.
Israel yatoa majina ya wanajeshi wengine wawili waliouawa huko Gaza
Jeshi la Israel limetoa majina ya wanajeshi wengine wawili waliouawa kwenye mapigano huko Gaza.
Wametajwa kuw ani Isahar Nathan mwenye umri wa miaka 28 na Itay Shoam mwenye umri wa miaka 21.
Kwa hivyo, IDF tayari imepoteza wanapoteza wanajeshi wasiopungua 44 waliouawa katika vita huko Gaza.
Aidha, jeshi la Israeli linaripoti kwamba mpiganaji mmoja alijeruhiwa vibaya siku ya Jumapili.
Haiwezekani kuhamisha watoto wachanga wa Al-Shifa salama, shirika la misaada linasema

Makumi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wanaotibiwa kwa sasa katika hospitali ya Al-Shifa hawawezi kuhamishwa salama, shirika la misaada limesema.
Kufuatia jeshi la Israel kusisitiza kwamba limejitolea kusaidia kuhamisha watoto hao wachanga hadi "hospitali salama", Shirika la Msaada wa Matibabu kwa Wapalestina linasema kuwa harakati za kuwahamisha watoto wachanga walio wagonjwa mahututi ni "mchakato mgumu na wa kiufundi".
Katika taarifa yake siku ya Jumapili, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la misaada, Melanie Ward, alitilia shaka madai ya Israel na kusema "anatiwa wasiwasi sana na ripoti zisizo za kukosoaji za vyombo vya habari".
''Huku magari ya kubebea wagonjwa hayawezi kufika hospitalini - hasa wale walio na ujuzi na vifaa vinavyohitajika kuhamisha watoto hawa - na hakuna hospitali yenye uwezo wa kuwapokea, hakuna dalili ya jinsi hii inaweza kufanyika kwa usalama."
Ward anasema "chaguo pekee lililo salama" la kuokoa watoto wachanga ni kwa Israel "kusitisha mashambulizi yake na kuzingira Al Shifa, kuruhusu mafuta kufika hospitalini, na kuhakikisha kwamba wazazi waliobaki wa watoto hawa wanaweza kuunganishwa nao" .
Unaweza pia kusoma:
- Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
- Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
- Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
- 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
- Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
Netanyahu anasema kunaweza kuwa na mpango wa kuwaachilia mateka wa Israel

Chanzo cha picha, Reuters
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameulizwa kama kunaweza kuwa na makubaliano ya kuwakomboa mateka takriban 240 wa Israel waliotekwa wakati wa shambulio la Oktoba 7.
"Unnaweza kuwepo'', alikiambia kituo cha TV cha Marekani NBC.
"Kadiri ninavyozungumzia kidogo jkuhusu suala hili, ndivyo nitakavyoongeza uwezekano wa kutokea."
Bw Netanyahu hakutoa maelezo yoyote lakini alisema "jambo moja" ambalo linaweza kulazimisha makubaliano ni "shinikizo la kijeshi" ambalo jeshi lake la ulinzi lilikuwa likifanya dhidi ya Hamas.
Lakini afisa mmoja wa Marekani ambaye jina lake halikutajwa amedai kuwa muda wa usitishaji mapigano ni "muhimu" katika mzozo huo ili kuruhusu kkuachiliwa kwa mateka.
Waziri Mkuu Netanyahu amekataa wito unaoongezeka wa kusitishwa kwa mapigano na ameapa kuwa usitishaji huo utatekelezwa iwapo utaambatana na kuachiliwa kwa mateka wote.
Unaweza pia kusoma:
- Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
- Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
- Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
- 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
- Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
Wanajeshi watano wa Marekani wafariki katika ajali ya ndege ya mafunzo mashariki mwa Mediterania

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Meli ya mizigo ya USS Gerald R Ford ni mojawapo ya meli mbili zilizotumwa mashariki mwa Mediterania (picha ya maktaba) Wanajeshi watano wa Marekani wamefariki katika ajali ya helikopta mashariki mwa Mediterania, jeshi la Marekani limesema.
Inasema ndege hiyo ilipata hitilafu ilipokuwa ikijaza mafuta ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya kawaida.
Marekani imeongeza operesheni zake katika eneo hilo tangu kuzuka kwa mzozo kati ya Israel na Hamas.
Rais Joe Biden alitoa pongezi kwa waathiriwa, akisema wahudumu waliweka " maisha yao kwa ajili ya nchi yetu kila siku".
"Tunasali kwa ajili ya familia za wapiganaji wetu wote waliofariki leo na kila siku," aliongeza.
Taarifa hiyo ya jeshi haikubainisha ni wapi ndege hiyo ilikuwa ikiruka au ni wapi iilikotokea ajali hiyo.
Lakini Marekani imehamisha ndege mbili za kubeba mizigo , pamoja na jeti, hadi mashariki mwa Mediterania katika kipindi cha mwezi uliopita.
Hatua hiyo inaonyesha wasiwasi wa Marekani kwamba mzozo kati ya Israeli na Hamas unaweza kuenea katika maeneo mengine ya eneo hilo.
Marekani ina nia hasa ya kuzuia vuguvugu lenye nguvu la Hezbollah la Lebanon kujiunga na mzozo huo.
Hezbollah Inaungwa mkono na Iran, ambayo pia inafadhili na kuipatia silaha Hamas.
Unaweza pia kusoma:
- Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
- Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
- Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
- 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
- Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
DRC: Wabunge wa Nord-Ubangi 'wamtimua' Gavana mjukuu wa Mobutu

Chanzo cha picha, MALO MOBUTU/X
Maelezo ya picha, Malo Mobutu alikuwa Gavana wa Nord-Ubangi tangu mwaka 2022 Wabunge katika jimbo la Nord-Ubangi kaskazini-magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepiga kura ya kumtimua Gavana Malo Ndimba Mobutu wa jimbo hilo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.
Malo Mobutu, 41, ni mjukuu wa Maréchal Mobutu Sese Seko ambaye alitawala Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) kwa miaka 32 hadi 1997, alipopinduliwa na waasi wakiongozwa na Laurent-Désiré Kabila.
Vyombo vya habari vya DRC, ikiwa ni pamoja na Radio Okapi ya Umoja wa Mataifa, vinaripoti kuwa Malo Mobutu alitimuliwa katika kura ya kutokuwa na imani iliyofanyika Jkatika Bunge la Jimbo la Nord-Ubangi Jumamosi.
Vyombo vya habari vya RTNC vya Congo viliripoti kwamba Malo Mobutu alipigiwa kura ya kutokuwa na imani na wabunge wengi 10 kati ya wabunge 18 wa bunge la mkoa.
Habari zinasema kuwa wabunge hao walimshutumu kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na ubadhirifu wa fedha nukiwemo ubadhirifu wa baadhi ya fedha zilizokusudiwa kwa ajili ya kazi za umma katika jimbo hilo.
Malo Mobutu hajatangaza hadharani chochote kuhusu uamuzi huo na mashtaka dhidi yake. Inasemekana hakuwapo bungeni wakati kura dhidi yake ilipopigwa.
