Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Waziri Mkuu wa Uingereza asema mlipuko wa hospitali huenda ulisababishwa na kombora lililorushwa kutoka Gaza

'Serikali ya Uingereza inaamua kwamba mlipuko huo [katika hospitali ya al-Ahli] ulisababishwa na kombora au sehemu ya moja ambayo ilirushwa kutoka Gaza. kuelekea Israeli".

Moja kwa moja

Yusuf Jumah and Ambia Hirsi

  1. Tazama video : Daraja laangushwa na mlipuko nchini Ujerumani

    Daraja la barabara kuu lililipuliwa katika mlipuko uliodhibitiwa karibu na mji wa Beselich nchini Ujerumani.

    Daraja hilo la Kerkerbachtal lenye urefu wa mita 135 (futi 443) liliporomoka ndani ya sekunde chache baada ya vilipuzi vilivyowekwa kwenye nguzo zake kulipuliwa.

    Daraja hilo, lililojengwa mwaka wa 1960, lilikuwa sehemu ya njia ya zamani inayovunjwa sasa. Barabara mpya inatengenezwa mahali pake, ikienda mbali zaidi na mji.

  2. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.

  3. Habari za hivi punde, Sunak: Idara ya ujasusi ya Uingereza inasema mlipuko wa hospitali ulisababishwa na kombora lililorushwa kutoka Gaza

    Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak anasema katika taarifa yake kwa bunge la Commons kwamba kwa msingi wa uchambuzi wa kijasusi wa Uingereza, "serikali ya Uingereza inaamua kwamba mlipuko huo [katika hospitali ya al-Ahli] ulisababishwa na kombora au sehemu ya kombora ambayo ilirushwa kutoka Gaza. kuelekea Israeli".

    Sunak anaendelea kusema kwamba kuripotiwa vibaya kwa tukio katika hospitali ya Gaza "kulikuwa na athari mbaya katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na juhudi muhimu za kidiplomasia za Marekani na mvutano wa hapa nyumbani".

    "Tunahitaji kujifunza na kuhakikisha katika siku zijazo hakuna haraka ya kutoa hukumu," analiambia bunge .

    Mamlaka ya Wapalestina inayodhibitiwa na Hamas huko Gaza mara moja iliilaumu Israel kwa mlipuko wa wiki iliyopita katika hospitali ya Al-Ahli, ikidai kuwa ni shambulio la anga la makusudi.

    Israel ilitoa ushahidi kwamba ilisema ilithibitisha Palestina Islamic Jihad, kundi jingine la wanamgambo linaloendesha shughuli zake huko Gaza, lilihusika kutokana na urushaji wa roketi.Islamic Jihad ilikanusha kuhusika na mlipuko huo.

    Sunak anasema "hakuwezi kuwa na hali ambapo Hamas inaweza kuruhusiwa kudhibiti Gaza"

    Mambo mengine muhimu sasa kutoka kwa hotuba ya Sunak Bungeni:

    • Anasema 'diplomasia inapaswa kutambua "ukweli mgumu juu ya ardhi"
    • Sunak pia anasema "tunahitaji kuwekeza kwa undani zaidi katika utulivu wa kikanda na katika suluhisho la nchi mbili" kwa mzozo kati ya Israeli na Wapalestina.
    • Pia anaongeza kuwa kunaweza kuwa "hakuna hali" ambapo Hamas inaweza kuruhusiwa "kudhibiti Gaza au sehemu yoyote ya maeneo ya Palestina"

    Anaongeza kuwa amezungumza na viongozi wengine wa ulimwengu kuhusu jinsi ya kuzuia kuongezeka kwa mzozo huo

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  4. Rwanda yatuma tani 16 za msaada huko Gaza

      • Author, Prime Ndikumagenge
      • Nafasi, BBC Great Lakes

    Serikali ya Rwanda inasema imetuma msaada wa kibinadamu kwa watu wa Palestina huko Gaza.

    Katika taarifa fupi iliyotumwa kwa BBC Idhaa ya Maziwa Makuu, naibu msemaji wa serikali, Alain Mukuralinda, alisema mchango uliotumwa kupitia Shirika la Msaada la Jordan Hashemite ‘’kuunga mkono juhudi zinazoendelea za kimataifa za uokoaji, ulipokelewa Amman leo’’.

    Inajumuisha tani 16 za vyakula, dawa na vifaa tiba, alisema, na kuongeza ‘’Rwanda inasisitiza haja ya kusitishwa kwa mapigano ili kulinda maisha ya raia wasio na hatia.

    Rwanda ni moja ya nchi za Kiafrika zenye uhusiano wa karibu na Israel ambayo waziri mkuu wake Benjamin Netanyahu alitembelea mwaka 2016.

    Nchi zote mbili zinakabiliwa ‘’mambo yanayofanana na mauaji ya halaiki ya watu wetu wenyewe’’, Bw Netanyahu aliandika kwenye kitabu cha mgeni huyo baada ya kuzuru ukumbusho wa wahasiriwa wa mauaji ya halaiki ya 1994 nchini Rwanda.

    Zaidi ya watu 800,000 wengi wao wakiwa wa kabila la Watutsi waliuawa katika mauaji ya halaiki huku Wayahudi milioni 6 wakiuawa katika mauaji ya halaiki wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  5. Mbwa mzee zaidi duniani afariki akiwa na miaka 31

    Mbwa mzee zaidi duniani amefariki akiwa na umri wa miaka 31 na siku 165.

    Bobi, Rafeiro do Alentejo ambaye anashikilia rekodi ya dunia ya Guinness, alikufa huko Ureno siku ya Jumamosi.

    Kifo chake kilitangazwa kwenye mitandao ya kijamii na daktari wa mifugo ambaye alikutana na Bobi mara kadhaa.

    “Licha ya kuishi kuliko mbwa wote katika historia, siku zake 11,478 duniani hazingetosha kamwe, kwa wale waliompenda,” aliandika Dk Karen Becker.

    Bobi akawa mbwa mwenye umri mkubwa zaidi duniani na mbwa mzee zaidi kuwahi kutokea mwezi Februari - na kushinda rekodi ya karne ya taji hilo la mwisho.

    Mbwa wa zamani zaidi kuwahi kuishi alikuwa Bluey wa Australia, ambaye alikufa mnamo 1939 akiwa na umri wa miaka 29 na miezi mitano.

    Uzee wa Bobi ulithibitishwa na hifadhidata ya wanyama ya serikali ya Ureno, ambayo inasimamiwa na Muungano wa Kitaifa wa Madaktari wa Mifugo.

    Utambulisho wa mrithi wa Bobi kwa jina la mbwa mzee zaidi duniani bado haujafichuliwa.

  6. Hifadhi ya chakula na maji yazidi kupungua kwa wakimbizi wa Younis - Gaza

    Kila sekunde, kila dakika, unaweza kusikia sauti ya mlipuko karibu nawe," anasema Ghada Ouda, mfasiri wa kujitegemea wa Kipalestina ambaye alikimbia nyumba yake katika Jiji la Gaza hadi Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

    Katika rekodi ya sauti iliyotumwa kwa BBC, Ouda anaelezea hali ilivyo katika sehemu ya kusini ya eneo hilo.

    "Tuna hifadhi mdogo ya chakula, maji. Tunalala chini," anasema.

    Wapalestina wanaohifadhiwa huko wanaishi kwa "chakula kutoka kwa makopo, mboga, ambayo haitoshi".

    "Hata mkate ni nadra sana," anasema.

    "Tunalazimika kwenda mbali. Inakuchukua, kama, saa tano kupata mkat na hauetoshi familia mzima."

    Mgahawa wa Israel wafikiria kujenga 'mji wa mahema'

    Mamlaka ya mji wa Eilat ulioko kusini mwa Israel unafikiria kuunda mji wa mahema wa kuwahifadhi maelfu ya watu ambao wamehamia huko tangu vita kuanza, kulingana na vyombo vya habari vya Israel.

    Meya wa Eilat anasema idadi ya watu katika jiji hilo imeongezeka maradufu, huku zaidi ya watu 60,000 waliohamishwa wakiwasili.

    Kufikia sasa wamekuwa wakiishi katika vyumba 12,000 vya hoteli, sehemu 4,000 za kukodishwa kwa faragha na pia vituo maalum vya ukarimu.

    Kwa mujibu wa serikali ya Israel, zaidi ya Waisraeli 200,000 wamekimbia makazi yao tangu shambulio la Oktoba 7 - huku watu wakihama maeneo karibu na mpaka wa Gaza na Lebanon.

  7. Kasisi wa kanisa katoliki nchini Kenya aoa baada ya kujiunga na kundi lililojitenga

    Kasisi mmoja wa Kanisa Katoliki nchini Kenya amechukua hatua isiyo ya kawaida ya kufunga ndoa.

    Kulingana na mila za Kikatoliki, makasisi wanapaswa kujitolea kuishi maisha ya useja lakini Padre Edwin Gathang'i Waiguru sasa amejiunga na kundi lililogawanyika, linalojulikana kama kanisa la Catholic Charismatic.

    Askofu Patrick Mulau wa Kanisa la Kirinyaga Charismatic aliendesha sherehe ya harusi Jumapili katika kaunti ya Kiambu, kaskazini mwa mji mkuu, Nairobi.

    Akiwa amesimama karibu na bibi harusi wake, Margaret Wanjira Githui, Waiguru alisema "inawezekana kumtumikia Mungu na kuwa na familia na kuwa na mke mzuri".

    "Mungu hakufanya makosa alipoumba mwanamume na mwanamke na akasema si vyema mtu awe peke yake."

    Mamia ya familia na marafiki wa wanandoa hao walienda kushuhudia sherehe hiyo isiyo ya kawaida, runinga ya NTV nchini humo inaripoti.

  8. Mlipuko unaoshukiwa kuwa wa kipindupindu umekumba majimbo matatu ya Sudan

    Takriban visa 817 vinavyoshukiwa kuwa kipindupindu vimerekodiwa katika majimbo matatu ya Sudan, vikiwemo vifo 35, vyombo vya habari vya nchini vinaripoti.

    Visa hivyo viliripotiwa katika majimbo ya Gedaref, Kordofan Kusini na Khartoum, tovuti ya habari inayomilikiwa kibinafsi ya al-Rakoba iliripoti, ikinukuu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).

    Wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulisema kuwa miezi kadhaa ya migogoro nchini Sudan imewaacha mamilioni ya watu katika hatari ya kipindupindu, dengue, surua, malaria na magonjwa mengine bila uwezo wa kutosha wa kujizuia.

    WHO pia imeonya kwamba maisha ya zaidi ya wagonjwa 9,000 wa figo yako hatarini kutokana na idadi ndogo ya vituo vya kusafisha damu nchini.

    Hospitali za Sudan zimeathiriwa pakubwa na mzozo kati ya jeshi na kikosi cha kijeshi, huku nyingi zikisimamisha shughuli huku kukiwa na mapigano.

    Mzozo huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 9,000 na wengine karibu milioni sita kuyahama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

    • Malema atoa wito wa kususia bidhaa za Israel nchini Afrika Kusini

        • Author, Nomsa Maseko
        • Nafasi, BBC News, Johannesburg

      Chama cha tatu kwa ukubwa wa kisiasa nchini Afrika Kusini, Economic Freedom Fighters, kimefanya maandamano nje ya ubalozi wa Israel katika mji mkuu, Pretoria.

      Kiongozi wa chama Julius Malema kwa mara nyingine tena alitoa wito wa kufungwa kwa ubalozi huo baada ya kusema kuwa serikali ya Israel "haiheshimu ubinadamu".

      Bw Malema pia aliwataka wauzaji reja reja nchini kuondoa bidhaa zinazozalishwa na Israel kwenye rafu zao kufikia mwisho wa Oktoba.

      "Ikiwa hawataondoa bidhaa kutoka Israel, tutaziondoa wenyewe. Hatutaki bidhaa za Israel ziuzwe Afrika Kusini, hatutaki chakula kutoka kwa watu ambao wana damu ya watu wasio na hatia mikononi mwao," Alisema Bw Malema.

      Chama tawala cha African National Congress (ANC) kilifanya maandamano kama hayo nje ya ubalozi wa Israel siku ya Ijumaa.

      Naibu Katibu Mkuu wa ANC Nomvula Mokonyane alitoa wito kwa Waafrika Kusini kususia uagizaji bidhaa kutoka Israel kwa mshikamano na Wapalestina.

      Bi Mokonyane pia alisisitiza wito wa Afrika Kusini wa kusitisha mapigano mara moja katika Mashariki ya Kati.

      Wiki iliyopita, msemaji wa Umoja wa Wanawake wa ANC alijiuzulu, akishutumu chama hicho kwa kushindwa kuelewa "upande wa hadithi ya Wayahudi" katika mzozo wa Israel na Palestina.

      Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mzozo wa Israel na Palestina:Nini cha hivi punde?

      • Watu 436 wameuawa Gaza katika muda wa saa 24:Maafisa wa Palestina katika wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas wanasema zaidi ya watu 430 wameuawa huko Gaza tangu jana asubuhi - na kufanya jumla kuwa zaidi ya 5,000 tangu Oktoba 7, wanasema.
      • Israel yasema malengo 320 yameshambuliwa:Jeshi la Israel linasema linalenga miundo mbinu ya Hamas, ikijumuisha mahandaki na maeneo ya kurusha roketi.
      • Uvamizi wa Israel ndani ya Gaza:Israel inasema vikosi vyake viliingia ndani ya Ukanda wa Gaza siku ya Jumapili ili kuondoa magaidi na silaha eneo hilo, huku mwanajeshi mmoja wa Israel akiuawa.Msemaji wa IDF Daniel Hagari alisema Israel ilifanya uvamizi zaidi huko Gaza usiku kucha "kuua vikosi vya magaidi ambao wanajiandaa kwa hatua inayofuata ya vita" na "kupata taarifa za kijasusi juu ya waliochukuliwa mateka".
      • Idadi ya mateka yaongezeka:Israel inasema watu 222 wanajulikana kuwa mateka huko Gaza
      • Mwanajeshi wa Uingereza na Israel auawa:Yosef Guedalia, 22, alikuwa mwanajeshi katika kitengo cha kupambana na ugaidi na aliuawa alipokuwa akikabiliana na wapiganaji wa Hamas huko Kibbutz Kfar Aza tarehe 7 Oktoba, familia yake inasema.
      • Waziri Kiongozi wa Scotland:Waziri wa Kwanza wa Uskoti Humza Yousaf anasema mama mkwe wake na mumewe wanaishi kwa "mateso" huku wakisalia kukwama huko Gaza, katika nyumba yenye watu 100.

      Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Tiba mpya ya saratani ya shingo ya kizazi katika miaka 20 yapongezwa

      Wanasayansi wanasema huenda wamepata mafanikio makubwa zaidi katika jitihada za kutafuta tiba ya saratani ya shingo ya kizazi katika miaka 20, kwa kutumia dawa zilizopo na za bei nafuu kabla ya matibabu ya kawaida ya radiotherapy.

      Matokeo ya majaribio, yaliyotolewa katika mkutano wa matibabu wa ESMO, yanaonyesha mbinu hiyo ilipunguza hatari ya wanawake kufa kutokana na ugonjwa huo au saratani kwa 35%.

      Utafiti wa Saratani Uingereza, ambao ulifadhili kazi hiyo, uliita matokeo "ya kushangaza".

      Inatumai kliniki zitaanza kufanya vivyo hivyo kwa wagonjwa hivi karibuni.

      Saratani ya shingo ya kizazi huathiri maelfu ya wanawake kila mwaka nchini Uingereza, wengi wao wakiwa mwanzoni mwa umri wa miaka ya 30.

      Dk Iain Foulkes, kutoka Chuo cha Utafiti wa Saratani nchini Uingereza, alisema: "Wakati ndio kila kitu unapotibu saratani.

      "Ushahidi unaoongezeka unaonyesha thamani ya tiba za ziada za chemotherapy kabla ya matibabu mengine kama upasuaji na radiotherapy katika saratani zingine kadhaa, Sio tu kwamba inaweza kupunguza uwezekano wa saratani kurudi, inaweza kutolewa haraka kwa kutumia dawa ambazo tayari zinapatikana kote duniani.

      Pia unaweza kusoma:

    • Habari za hivi punde, Wizara ya afya ya Gaza inasema idadi ya walioaga dunia inapita 5,000

      Wizara ya afya ya Palestina huko Gaza, inasema idadi ya watu waliouawa huko Gaza tangu 7 Oktoba imeongezeka hadi 5,087 - ongezeko la 436 tangu jana.

      Hiyo inajumuisha watoto 2,055, wanawake 1,119, na wazee 217, wanasema zaidi ya watu 15,273 wamejeruhiwa.

      Familia ya Uingereza na Israel inasema jamaa yao amefariki

      Raia mwingine wa Uingereza-Israel amethibitishwa kuuawa katika mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel.

      Yosef Guedalia, 22, alikuwa mwanajeshi katika kitengo cha kupambana na ugaidi na aliuawa wakati akikabiliana na wapiganaji wa Hamas huko Kibbutz Kfar Aza waliposhambulia tarehe 7 Oktoba.

      Kaka yake Asher alisema alisaidia kuwahamisha raia waliojeruhiwa kabla ya kurejea kupambana na wapiganaji wa Hamas.

      Kuna video ya Yosef akimfanyia huduma ya kwanza raia aliyejeruhiwa ambaye sasa anapata nafuu hospitalini Asheri anasema.

      Ndugu yake anaongeza:

      ' Aliokoa watu dakika chache kabla hajapigwa risasi.Alifanya kwa ushujaa na dhamira, aliendelea kupigana na hakujifikiria mwenyewe au kusita ... aliingia katika uokoaji wa raia wengi iwezekanavyo kabla ya kuuawa majumbani mwao na kuua magaidi wengi kadiri alivyoweza."

      'Aliokoa watu dakika chache kabla ya kupigwa risasi.Alifanya kwa ushujaa na dhamira, aliendelea kupigana na hakujifikiria mwenyewe au kusita ... aliingia katika uokoaji wa raia wengi iwezekanavyo kabla ya kuuawa majumbani mwao na kuua magaidi wengi kadiri alivyoweza."

      Asheri aliendelea kusema alikuwa na uhakika kwamba kaka yake alielewa "huenda asirudi kwa mke wake na familia yake lakini huo ndio wito wake. Huyo ndiye shujaa tuliyekuwa naye kwa miaka 22".

      Yusufu alikuwa karibu kusherehekea kumbukizi yake ya kwanza ya harusi.

      Waingereza kumi na moja sasa wanajulikana kuuawa na Hamas.Mmoja ametekwa nyara.Takriban wanne bado hawajulikani walipo

      Waziri kiongozi wa Uskoti: Familia yangu huko Gaza ina chupa sita za maji kwa watu 100

      Waziri Kiongozi wa Uskoti Humza Yousaf anasema mama mkwe wake na mumewe wanaishi kwa "mateso" huku wakisalia kukwama huko Gaza.

      "Zimepungua hadi chupa sita za maji safi ya kunywa katika nyumba ya watu 100 akiwemo mtoto mchanga wa miezi miwili," Yousaf aliwaambia waandishi wa habari wakati wa ziara ya Brechin.

      Aliondoka ili kupokea simu yake na kusema kwamba familia haiwezi kujua kama "itafanikiwa kutoka usiku mmoja hadi mwingine," huku makombora, milio ya roketi na ndege zisizo na rubani zikiendelea usiku kucha.

      Wakwe wa Yousaf walikuwa Gaza wakitembelea familia wakati uhasama ulipopamba moto.Alisema anaiomba serikali ya Uingereza kwa niaba yao kutaka kufunguliwa kwa kivuko cha Rafah na kusitishwa kwa mapigano.

      Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mamia ya wanajeshi wa Ufaransa waondoka kambi ya Niger kuelekea Chad

      Takriban wanajeshi 200 wa Ufaransa wameondoka katika mji wa Ouallam ulioko kusini-magharibi mwa Niger huku kukiwa na uondoaji mkubwa wa vikosi vya Ufaransa unaoendelea katika taifa hilo la Sahel, kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali cha Tele Sahel kinaripoti.

      Ilisema kuwa wanajeshi 193 wa Ufaransa walioko Ouallam waliondoka kambi yao kuelekea Chad siku ya Jumapili.

      Wanajeshi hao waliripotiwa kuondoka na lori 28 pamoja na magari 24 ya kivita na magari mengine ya msaada.

      Chad ilikuwa imekubali kutoa "pengo " la kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa kutoka Niger kurudi Ufaransa.Zoezi la kujiondoa lilianza tarehe 5 Oktoba.

      Ufaransa ilituma wanajeshi 1,500 nchini Niger kusaidia kukabiliana na uasi unaozidi kuongezeka wa wanajihadi tangu 2015.

      Wanajeshi hao wa Ufaransa walikuwa na makao yake katika mji mkuu Niamey, Ouallam na Ayorou - karibu na mpaka na Mali.

      Kwengineko, Umoja wa Ulaya umeanza hatua za kuwawekea vikwazo wanachama wa utawala wa kijeshi wa Niger, miezi mitatu baada ya kuchukua mamlaka katika mapinduzi.

      Baraza la EU lilitangaza Jumatatu kwamba "limepitisha mfumo" ambao utaliruhusu kuweka vikwazo dhidi ya "watu binafsi na vyombo vinavyohusika na vitendo vinavyotishia amani, utulivu na usalama wa Niger".

      Baraza hilo pia lilisema kuwa vikwazo hivyo vitawekewa watu binafsi ambao wanahujumu utaratibu wa kikatiba wa Niger, demokrasia au utawala wa sheria, pamoja na watu binafsi wanaohusika naukiukaji wa haki za binadamu.

      Vikwazo hivyo vitajumuisha marufuku ya usafiri, kufungia mali na kupiga marufuku utoaji wa fedha kwa watu waliowekewa vikwazo.

      Unaweza pia kusoma

    • Je! tunajua nini kuhusu uvamizi wa Israeli ndani ya Gaza?

      Asubuhi ya leo tumekuwa tukifahamu zaidi kuhusu uvamizi ambao wanajeshi wa Israel wamekuwa wakifanya ndani ya Gaza kwa muda wa saa 24 zilizopita.Haya ndio tunayoyajua

      Jumapili:

      • Israel inasema vikosi vyake vilienda magharibi mwa Ukanda wa Gaza siku ya Jumapili, kufanya operesheni ya kuwaondoa magaidi na silaha katika eneo hilo, na kujaribu kutafuta mateka.
      • Kulingana na IDF,makombora yalirushwa kwao na Hamas - na mwanajeshi mmoja wa IDF aliuawa na wengine watatu kujeruhiwa
      • Mrengo wenye silaha wa Hamas unasema ilitokea mashariki mwa Khan Younis kusini mwa Gaza, na kwamba wanajeshi wa Israel walivuka ua "kwa mita kadhaa"
      • Mrengo wa kijeshi wa Hamas unasema"walijihusisha na nguvu iliyoingia" na kudai waliharibu tingatinga mbili na tanki.Wanasema wanajeshi wa Israel waliacha magari yao na kukimbia mashariki mwa ua kwa miguu

      Jumatatu:

      • Msemaji wa IDF Daniel Hagari anasema Israel ilifanya uvamizi zaidi Gaza usiku kucha
      • Hagari alisema: "Wakati wa usiku kulikuwa na uvamizi wa vikosi vya vifaru na wanajeshi wanaotembea kwa miguu. Mashambulizi haya ni mashambulizi ambayo yanaua vikosi vya magaidi wanaojiandaa kwa hatua inayofuata ya vita. Haya ni mashambulizi ambayo yanaingia ndani kabisa, hadi kwenye mstari wa mwisho wa makabiliano .pia tanafuta na chochote tunachoweza kupata katika suala la ujasusi juu ya mateka".

      Lakini - sio mara ya kwanza tumejua kuwa wanajeshi wa Israeli kuvuka Gaza.

      Katika wiki ya kwanza ya mzozo huu,Israel ilisema wanajeshi na vifaru viliingia Ukanda huo li kufanya uvamizi na kupigana na Hamas kwa lengo la kujaribu kutafuta Waisraeli waliopotea.

      Israel inasema wanachama 37 wa Hamas walikamatwa katika Ukingo wa Magharibi usiku kucha

      Pia mbali na Gaza, Jeshi la Ulinzi la Israel linasema limewakamata takriban Wapalestina 800 wanaosakwa katika Ukingo wa Magharibi - ikiwa ni pamoja na zaidi ya 500 wanaoshirikiana na Hamas - tangu shambulio la Israel tarehe 7 Oktoba.

      Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Jeshi la Israel linasema lilishambulia ' seli nane za kigaidi' nchini Lebanon

      Tumekuwa tukiangazia leo asubuhi juu ya kile kinachotokea kusini mwa Israeli na Gaza - lakini pia kuna vurugu kwenye mpaka na Lebanon.

      Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari anasema kuwa IDF ilishambulia "vikundi vinane vya magaidi" nchini Lebanon katika muda wa saa 24 zilizopita.

      Saba kati ya hizo zilipigwa kabla ya kufanikiwa kurusha makombora na makombora ya vifaru, alisema.

      Hagari pia alisema seli 20 za Hezbollah zimeshambuliwa tangu mapigano yalipozuka kwenye mpaka mapema mwezi huu.

      Msafara wa tatu wa msaada waingia Gaza kutoka Misri - ripoti

      Tunasikia taarifa kuwa msafara wa tatu wa misaada umevuka hadi Gaza kutoka Misri.

      Mashirika ya habari ya Reuters na AFP yanasema malori zaidi yameingia hivi punde kupitia kivuko cha Rafah.

      Hii inafuatia msafara wa kwanza wa lori 20 siku ya Jumamosi na msafara wa pili Jumapili wa saa nane mchana . Tutakuletea maelezo zaidi kadri tutakavyokuwa nayo.

      Sio kutia chumvi kusema hali ni kama janga huko Gaza - Msalaba Mwekundu

      Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imekaribisha kuwasilishwa kwa misafara miwili ya kwanza ya misaada huko Gaza - lakini inasema ni "tone" tu la kile idadi ya watu wanahitaji.

      Akizungumza na BBC Breakfast, msemaji wa shirika la kutoa misaada Imene Trabelsi alisema kuna haja ya kuwa na mpango endelevu wa kuwasilisha vifaa - na akadokeza kwamba idadi kubwa ya watu wa Gaza walikuwa wakitegemea misaada kabla ya mzozo wa hivi punde kuzuka.

      Trabelsi anaongeza kuwa familia zilizolazimishwa kutoka kwa nyumba zao zinalala mitaani bila vitu muhimu kama vile blanketi kwa sababu makazi tayari yamejaa.

      "Siyo kutia chumvi kusema ni janga huko Gaza."Wiki iliyopita, msemaji wa IDF alipendekeza kwa BBC kuwa hakuna mgogoro wa kibinadamu huko Gaza.

      Picha za hivi punde kutoka kaskazini mwa Gaza

      Kama tumekuwa tukiripoti, Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) linasema katika saa 24 zilizopita, lilipiga shabaha zaidi ya 320 katika Ukanda wa Gaza.

      Pia tumekuwa na picha kutoka kaskazini - ambapo Israel imewaonya wakazi kuhama.

      Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Tazama: Video inaonyesha mfanyakazi wa bia wa China akikojoa kwenye tanki

      Mamlaka ya Uchina inachunguza baada ya video iliyosambaa mitandaoni ikimuonyesha mfanyakazi kutoka Tsingtao akikojoa kwenye tanki, linaloaminika kuwa na viambato vya bia yake maarufu.

      Klipu hiyo ilitazamwa na makumi ya mamilioni ya watu kwenye mitandao ya kijamii.

      Kampuni hiyo ilisema iliwaarifu polisi mara baada ya video hiyo kujulikana, na kuongeza kuwa viungo katika tanjki hilo vilikuwa vimefunikwa vizuri.

      Tsingtao ni mojawapo ya wazalishaji wakuu wa bia nchini China na muuzaji wake mkubwa nje.

      Katika klipu hiyo iliyoonekana mtandaoni siku ya Alhamisi, mfanyakazi, aliyevalia sare na kofia ya chuma, anaonekana akipanda juu ya ukuta mrefu na kuingia kwenye kontena kabla ya kukojoa ndani yake.

      Lebo ya eneo la klipu hiyo inasomeka "Kiwanda cha bia ya Tsingtao No.3", chombo cha habari nchini The Paper kiliripoti Ijumaa.

      Kituo cha biashara cha "National Business Daily" baadaye kilitaja chanzo cha ndani kikisema kuwa aliyechukua video hiyo na mtu anayeonekana ndani yake hawakuwa wafanyakazi wa moja kwa moja wa kampuni hiyo.

      Katika taarifa iliyochapishwa siku ya Ijumaa, ofisi ya usimamizi na utawala wa soko la Pingdu City, ambako kiwanda hicho kipo, ilisema walituma timu mara moja na kufanya uchunguzi kwenye eneo hilo baada ya kuiona video hiyo, na kuziba viungo vilivyoonekana kwenye video.

      Pia iliongeza kuwa ofisi hiyo itashughulikia suala hilo kwa umakini mara tu maelezo yatakapothibitishwa

      Tsingtao ilisema siku ya Ijumaa kwamba "ilishikilia umuhimu mkubwa" kwenye video ya mtandaoni, na polisi walikuwa wameanza uchunguzi.

      BBC imefikia kampuni hiyo kwa maoni.

      Mitandao ya kijamii ya Wachina imeshtushwa na klipu hiyo, kwani bidhaa hiyo inajulikana sana nyumbani na nje ya nchi.

      "Uchungu ambao utaharibu pesa nyingi, mfanyakazi huyu amefanya uharibifu mkubwa hapa," maoni yaliyopendwa zaidi kwenye jukwaa la X-like Weibo inasoma.

      "Jambo zuri kwamba sinywi bia - lakini haiwezekani kufikiria ikiwa chapa hii itaisha kwa sababu ya hii," mtumiaji mmoja alisema.

      "Hii ni mara ya kwanza lakini?"maoni mengine yanasema.

      Hisa katika Kiwanda cha Bia cha Tsingtao zilipungua sana wakati Soko la Hisa la Shanghai lilipofunguliwa Jumatatu asubuhi lakini zilikuwa zikiuzwa kwa kiwango kikubwa kufikia alasiri.

      Soko la Hong Kong, ambapo hisa za Tsingtao pia zimeorodheshwa, lilifungwa Jumatatu kwa likizo ya Tamasha la Chung Yeung.

    • Habari za hivi punde, Watu 222 sasa wamethibitisha kutekwa na Hamas Gaza: Jeshi la Israel

      Jeshi la Israel limetoa taarifa mpya kuhusu idadi ya mateka wanaoshikiliwa Gaza - likisema watu 222 sasa wamethibitishwa kushikiliwa.

      Awali jeshi hilo lilisema idadi ya mateka waliochukuliwa na Hamas ni 212

    • Tunaishi ndani ya ua wa hospitali. Hakuna chaguo jingine

        • Author, Rushdi Abu Alouf
        • Nafasi, Akiripoti kutoka Khan Younis, Gaza

      Hospitali hii iliyoko Khan Younis sio makao ya watu waliojeruhiwa, bali na mamia ya familia zinazochukua hospitali hii kama kimbilio.

      Watu wanakaa chini ya ua wa hospitali hiyo, wamelala chini.

      Kunakuwa na hali ya baridi kidogo jioni, ni hali mbaya sana kwa watu hao - lakini hawana chaguo lingine, hawana mahali pengine pa kwenda.

      Familia yangu na mimi tunaishi katika hema hospitalini.

      Bado tuko hapa kwa sababu tulihamishwa mara nne na hakuna imani kwamba tutapata nyumba nyingine – ambayo ni itakuwa salama.

      Kwa hiyo tuliamua kukaa hospitalini. Tunajaribu kuishi kwa chakula kidogo na maji kidogo.

    • Mzozo wa Israel na Hamas: Ni nini kimetokea katika saa chache zilizopita?

      Gaza imeshuhudia mashambulio ya mabomu kutoka Israeli usiku kucha.

      Haya ndiyo yaliyotokea katika saa chache zilizopita:

      • Mashambulizi ya usiku huko Gaza yameua au kujeruhi "idadi kubwa" ya watu, kulingana na wizara ya mambo ya ndani inayosimamiwa na Hamas.
      • Pia kumekuwa na ripoti za milipuko karibu na hospitali kadhaa, ambazo baadhi ya Hamas inadai kuwa zilitokana na mashambulizi ya anga ya Israel. Msemaji wa jeshi la Israel ameiambia BBC kuwa wanachunguza madai haya
      • Mwanajeshi wa Israel aliuawa Gaza alipokuwa akiwatafuta mateka huku wengine kadhaa wakijeruhiwa, linasema jeshi la Israel
      • Viongozi wa Marekani, Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani na Italia walitumia wito wa pamoja kusisitiza uungaji mkono wao kwa "haki ya Israel ya kujilinda dhidi ya ugaidi" lakini pia wanatoa wito wa "kufuata sheria za kimataifa za kibinadamu"
      • Msafara wa pili wa misaada ya kibinadamu ukiwa na malori 14 yaliyokuwa yamebeba misaada uliruhusiwa kuingia Gaza siku ya Jumapili, na kuleta kile ambacho Martin Griffiths, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu, alikiita "mwanga mdogo wa matumaini"
      • Jeshi la Israel limesema ndege yake ilishambulia vyumba viwili vya Hezbollah ndani ya Lebanon ambavyo vilikuwa vinapanga kurusha makombora ya vifaru na maroketi kuelekea eneo la Israel.

      Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

    • Mzozo wa Israel na Hamas kwa picha: Khan Younis yaharibiwa zaidi kwa mashambulio ya Israeli