Picha za hospitali ya Gaza zinaonyesha misururu ya maiti huku Israel ikizidisha mashambulizi ya mabomu

Tunataka kuonyesha uzito wa mzozo huu, na madhara yake kwa raia, huku tukiwa makini kuhusu kile ambacho wewe, hadhira, unakabiliana nacho.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya mubashara kwa leo , tukutane tena hapo kesho majaaliwa.

  2. Tazama: Video fupi ya Hamas ikionyesha kuachiliwa kwa mateka mama na binti yake Wamarekani

    Maelezo ya video, Video ya Hamas inaonyesha kuachiliwa kwa mateka kwa mama na binti yake Wamarekani

    Video iliyoshirikishwa mitandaoni na Brigedi za al-Qassam - tawi la kijeshi la Hamas - lilionyesha wakiwaachilia huru mateka wawili.

    Raia wa Marekani Judith Raanan na bintiye Natalie walikuwa miongoni mwa takriban watu 200 waliotekwa nyara wakati wa mashambulizi mabaya ya Hamas dhidi ya Israel.

    Wafanyakazi waliovalia sare za Tume ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) walionekana wakiandamana na mateka walioachiliwa.

    Mjomba wa Natalie, Avi Zamir, alisema familia hiyo "ilikuwa na furaha sana" na Rais wa Marekani Joe Biden alisema alikuwa na furaha kubwa kwa kuachiliwa kwao - akithibitisha kuwa alizungumza na Raanan kwa simu.

  3. Nyota wa Muziki wa Nigeria wazoa tuzo nyingi za Trace, huku Diamond akiendelea kuwa mbabe A. Mashariki

      • Author, Yves Bucyana
      • Nafasi, BBC Swahili
    g
    Maelezo ya picha, Mwanamuziki David Adedeji Adeleke maarufu Davido

    David Adedeji Adeleke maarufu Davido na mwanamuziki mwenzake Divine Ikubor maarufu REMA wote wa Nigeria kila mmoja ameshinda tuzo mbili za TRACE 2023 ,huku Diamond Platinamuz akiendelea kuwa mbabe wa Afrika Mashariki.

    Kongamano la muziki mjini Kigali liliwashirikisha wasanii mashuhuri wa muziki wa kiafrika kutoka sehemu mbali mbali duniani – Zaidi ya wasanii 60 wameshiriki tamasha la muziki kwenye uwanja wa BK Arena ambapo pia tuzo mbali mbali zimetolewa kwa wasanii bora wa mwaka 2023 ,Album iliyoshinda nyingine,Wazalishaji bora wa muziki na wadau wengine katika tasnia ya muziki.

    g
    Maelezo ya picha, Diamond Platinamz ameshinda tuzo ya msanii bora wa Afrika Mashariki

    Davido,30 ameibuka kuwa msanii bora wa kiume ,tuzo nyingine ikiwa ni ya wimbo bora wa mwakaulioshirikisha wasanii wengine.

    Rema,23 msanii wa miondoko ya Afropop ameibuka mshindi wa msanii Bora wa Kimataifa-Best Global artist na pia tuzo yawimbo bora wa mwaka, wimbo wake ‘’Calm down’’uliokonga nyoyo za wengi.

    Naye Diamond Platinamz ameshinda tuzo ya msanii bora wa Afrika Mashariki,katka ghafla ya kutoa tuzo hizo ameimba kwa kushirikiana na mwenzake wa Tanzania Juma Jux.

    h
    Maelezo ya picha, Namchebo kutoka Afrika Kusini amepata tuzo ya mwanamuziki Bora Afrika -na wimbo wake Jerusalema pamoja na Rema

    Ushindani katiya wasanii wa Afrika magharibi na Afrika mashariki bado unaonekana katika ghafla za utoaji tuzo –kwa msanii wa Tanzania FID Qambaye pia ni katibu mkuu wa shirikisho la wasanii ,Afrika muziki wa afrika mashariki bado unakosa utambulisho kama vile wenzao wa pande nyingine za Afrika.

    ‘’wasanii wa afrika mashariki wanatakiwa kutafuta utambulisho wa nyimbo zao,mfano ukisikiliza ‘amapiano’utatambua kwamba ni wa Afrika kusini na ukisikia ‘ Afribeat’ utaelewa kwamba ni Nigeria au Ghana’’

    ‘’Tuzo za TRACE ni miongoni mwa tuzo kubwa zinazotolewa Afrika kila mwakanaituo cha televisheni cha TRACE na kuwaleta pamoja wanasanii wa muziki bora Zaidi wenye asili ya kiafrika –lengo likiwa ni kuwasaidia kuonyesha vipaji vyao na kukuza tamaduni za nyimbo za kiafrika kote ulimwenguni.

    b
    Maelezo ya picha, Hafla hiyo pia imehudhuriwa na wanamitindo kutoka sehemu mbali mbali duniani
  4. Netanyahu: Hezbollah itafanya 'kosa katika maisha yake' ikiwa itaingia vitani

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Netanyahu alikuwa akizungumza na wanajeshi kaskazini mwa Israel, karibu na mpaka na Lebanon

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameionya Hezbollah - kikosi chenye nguvu zaidi cha kijeshi cha Lebanon - dhidi ya kuvuka na kuingia mstari wa pili wa vita na Israel.

    Itakuwa inafanya "kosa la maisha yake" ikiwa itafanya hivyo, alisema wakati akizungumza na wanajeshi wa Israeli karibu na mpaka na Lebanon.

    Alisema itasababisha mashambulio ya kivita ya Israeli ya kiwango "kisicho kufikirika" ambayo yatasababisha "uharibifu" kwa Lebanon.

    Israel na Marekani tayari zimeionya Hezbollah inayoungwa mkono na Iran - ambayo imetajwa kuwa shirika la kigaidi na Uingereza, Marekani na nchi nyingine - dhidi ya kuanzisha mapambano mengine kwenye mpaka wa kaskazini wa Israel.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  5. Mamlaka za Gaza zinasema watu 4,651 wameuawa

    Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema takriban watu 4,651 wameuawa katika Ukanda huo tangu tarehe 7 Oktoba.

    Inaongeza kuwa watu 14,245 wamejeruhiwa.

    Wizara hiyo pia inasema katika taarifa yake kwamba Wapalestina 266 wameuawa katika muda wa saa 24 zilizopita, wakiwemo watoto 117.

  6. Wananchi wa Gaza wakiomboleza kando ya mistari ya miili iliyofunikwa ndani ya ua wa hospitali

    Tahadhari: Taarifa hii lina maelezo ambayo baadhi ya watu wanaweza kupata ya kuhuzunisha.

    Tuliripoti mapema juu ya picha zinazoonyesha miili ya watoto waliokufa katika hospitali ya Al Aqsa katikati mwa Gaza .

    Tuliandika kwamba picha zilionyesha miili ya watoto 11 na watoto wawili.

    Sasa tumeona picha nyingine, kutoka kwa mpiga picha huyo anayefanya kazi na shirika la habari la AFP, inayoonyesha mwili wa mtoto wa 12.

    Kwa mara nyingine tena, tunaamua kutoonyesha picha hii.

    Tunataka kuonyesha uzito wa mzozo huu, na madhara yake kwa raia, huku tukiwa makini kuhusu kile ambacho wewe, hadhira, unakabiliana nacho.

    Lakini kuna picha zingine zilizochukuliwa hospitalini ambazo tunaweza kuonyesha, ambazo unaweza kutazama hapa chini.Mmoja wao anaonyesha kile kinachoonekana kuwa mtoto aliyevikwa sanda na kubebwa na mwanamume.

    Mwili ndani ya sanda hauonekani.

    Kama ilivyo kwa picha za watoto, hatujui ni lini au wapi watu kwenye picha hizi walikufa.

    Hospitali hiyo iko katika mji mdogo wa Deir Al Balah, ambao umekumbwa na migomo ya Israel katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

    Mji huo uko nje ya eneo la kaskazini la Gaza ambalo Israel imewaambia raia kuondoka na kukimbilia kusini - inaendelea kushambulia kwa mabomu katikati na kusini mwa Gaza.

    Tunajitahidi kupata maelezo zaidi kutoka kwa hospitali kote Gaza.

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    f

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Getty Images

    Chanzo cha picha, Getty Images

  7. Tanzania yasaini mikataba ya undeshaji wa bandari na DP World

    f

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Rais Samia amesema tetesi za bandari ya Dar Es Salaam inauzwa ni potofu

    Serikali ya Tanzania imeingia mikataba mitatu mahsusi ya uwekezaji na kampuni ya uchukuzi ya DP World kutoka Dubai kuendesha bandari kuu ya nchi hiyo ya Dar Es Salaam kwa kipindi cha miaka 30.

    Mikataba hiyo ya nchi inayopokea uwekezaji, kukodisha na kuendesha sehemu ya bandari imetiwa Saini leo katika Ikulu ya Dodoma mbele ya rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

    Uwekezaji huo hata hivyo umepitia ukosoaji mkubwa kwa miezi kadhaa na kilele chake kikawa ni kufungulliwa kwa kesi mahakamani ambayo serikali ilishinda.

    Wakosoaji wa uwekezaji huo wameibua hoja na hufo kuwa uwekezaji huo hauna maslahi kwa taifa.

    Akizungumza katika hafla ya kutia Saini mkataba huo, Rais Samia amezungumzia baadhi ya hofu hizo na kusema tetesi za bandari ya Dar Es Salaam inauzwa ni potofu na kwamba lengo kuu la serikali ni kupanua bandari hiyo ili iweze kupigania nafasi bora katika eneo la Afrika Mashariki na Kati ambalo mataifa yake yanategemea zaidi bandari za Kenya na Tanzania kuingiza mizigo kutoka ughaibuni.

    Rais Samia amesema kwamba haikuwa kazi raisi kufikia makubaliano hayo: “Kila kilichokuwa kinaibuliwa tulikuwa tunakipeleka kwenye kamati yetu ya majadilino na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wakipitie na kama kina tija wakichukue… Tulipokea ushauri na kwa uhakika hakuna sauti ya kundi ambalo lilipuuzwa.’’

    ‘’Bandari hii ni sekta muhimu inayunganisha taifa hili na mataifa Jirani ambayo inategemea kupitisha bidhaa,’’ amesisita Rais Samia.

  8. Waziri Mkuu wa zamani wa Israel asema mzozo wa kibinadamu huko Gaza 'sio kazi yetu'

    g

    Naftali Bennett, Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, anasema mzozo wa kibinadamu huko Gaza "sio kazi yetu".

    Israel inadhibiti anga la juu ya Gaza na ufuo wake, na inadhibiti kwa uthabiti usafirishaji wa watu na bidhaa.

    "Ulimwengu unaweza kuja na kuwasaidia Wagaza, hiyo sio kazi yetu," aliiambia Victoria Derbyshire wakati wa Kipindi cha Jumapilicha Laura Kuenssberg, alipoulizwa kama Israel itaruhusu msaada zaidi Gaza.

    Anasema hatua za kibinadamu lazima ziwe za kuafikiana, akitoa mfano wa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

    Derbyshire ilimwambia Bw ennett kuwa ni jukumu la Israel kwani ni lazima ionyeshe mapambano yake ni dhidi ya Hamas badala ya watu wa Palestina.

    "Hatuwajibiki kwa Gaza kama vile nyinyi hamhusiki na Ufaransa," alijibu.

    "Ikiwa wengine wanataka kuwatunza Wagaza, hiyo ni kazi yao."

    Akisisitizwa zaidi kuwa Israel inadhibiti mipaka ya Gaza, Bennett alisema tahadhari ya Israel kwa Wagaza kuhamia kusini ni ushahidi wa hatua za kibinadamu.

  9. Tazama: Boti zagongana katika maji yenye mzozo ya Bahari ya China Kusini

    Maelezo ya video, Tazama: Boti zagongana katika maji yenye mzozo ya Bahari ya China Kusini

    Ufilipino imewashutumu walinzi wa pwani wa China kwa kugongana na boti ya usambazaji bidhaa kutoka Ufilipino kwenye maji yanayozozaniwa ya Bahari ya China Kusini, na kuhatarisha wafanyakazi wake.

    China ilisema Ufilipino "ilizua matatizo kimakusudi".

    Katika tukio la pili pia karibu na Second Thomas Shoal siku ya Jumapili, mamlaka ya Ufilipino ilisema meli ya wanamgambo wa China iligonga meli ya walinzi wa pwani ya Ufilipino.

    Wanajeshi wa Ufilipino wametoa picha wanazosema zinaonyesha migongano.

  10. Habari za hivi punde, Picha za kutoka Gaza zaonyesha miili ya watoto wadogo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali

    Onyo: Chapisho hili lina maelezo ambayo baadhi ya watu wanaweza kupata ya kuhuzunisha.

    Tumekuwa tukiona picha nyingi sana zikitoka Gaza asubuhi ya leo, baadhi zikionyesha miili ya watoto waliokufa katika hospitali moja katikati mwa Gaza.

    Picha kutoka hospitali ya Al Aqsa zinaonyesha miili ya watoto wasiopungua 11 - ikiwa ni pamoja na watoto wachanga wawili - na Wapalestina wengine wengi waliokufa ikiwa imefungwa kwa sanda.

    Picha hizo zinatoka kwa mpiga picha anayefanyiaa kazi na shirika la habari la AFP.

    Nyingi kati yake ni mbaya sana kwetu sisi kuzionyesha hapa.

    Tunaporipoti kuhusu mzozo huu, tunapaswa kuamua ni nini kinafaa kukuonyesha.

    Tunataka kuakisi uzito wa vita hivi, na madhara yake kwa raia, huku tukiwa makini kuhusu kile ambacho wewe, hadhira, unakabiliana nacho.

    Moja ya picha inaonyesha watoto waliokufa wakiwa wamelala kando ya wenzao kwenye karatasi, wengine wakiwa na majeraha yanayoonekana kichwani.Picha nyingine inaonyesha mtoto akiwa mikononi mwa mwanamume - wote wamekufa na mwanamume ana jeraha la wazi usoni.

    Haijabainika wazi kutoka kwa picha ni lini au wapi watu hao walikufa.

    Hospitali hiyo iko katika mji mdogo wa Deir El Balah, ambao umekumbwa na mashambulio ya Israel katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

    Mji huo uko nje ya eneo la kaskazini la Gaza ambalo Israel imewaambia raia kuondoka na kukimbilia kusini.

    Israel imeendelea kulipua eneo la kati na kusini mwa Gaza.

    Tunafanya juhudi leo ili kujua zaidi kuhusu kinachoendelea katika hospitali hii - na katika maeneo mengine kote Gaza

  11. Mzozo wa Israel na Hamas: Tazama picha za hivi punde kutoka Gaza

    Picha zinazotujia leo kutoka Gaza zinaonyesha athari zinazotokana na mzozo unaoendelea, huku majengo yakiharibiwa na watu wakitafuta manusura kwenye vifusi huku mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea.

    Pia kumekuwa na foleni nje ya maduka ya kuoka mikate huku watu wakisubiri kununua mkate huku kukiwa na uhaba wa chakula na mafuta.

    Tazama baadhi ya picha za hivi punde:

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Majengo yaliyoharibiwa yanaweza kuonekana katika kitongoji cha Al Remal cha Mji wa Gaza
    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mtoto akitazama wakati Wapalestina wakiwa kwenye foleni ya kununua mkate katika duka la mikate huko Khan Younis kusini mwa Gaza
    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wapalestina wakikagua vifusi leo asubuhi baada ya mgomo huko Rafah kusini
    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Mwanamume akimsaidia mwanamke kwenye barabara iliyoharibiwa huko Gaza
  12. Israel inasema mateka 212 wanazuiliwa Gaza

    f

    Habari za hivi karibuni zaidi kutoka katika jeshi la Israeli, ambalo zinasema jeshi hilo linaamini kuwa watu 212 wanashikiliwa mateka na Hamas huko Gaza, tofauti na makadirio ya yake ya awali ya japo jana ambapo lilitangaza kuwa ni watu 210 waliotekwa.

    Siku ya Ijumaa, mateka wawili wa Kimarekani - mama na binti Judith na Natalie Raanan - walikuwa wa kwanza kuachiliwa.

    Tunafuatilia kwa karibu taarifa zozote kuhusu wale wanaozuiliwa - ikiwa ni pamoja na watu waliothibitishwa na BBC, au wanaoripotiwa kuwa walitekwa nyara na Hamas kutoka Israel.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  13. Hezbollah inacheza mchezo hatari sana, inasema IDF

    Akizungumzia kuhusu mvutano kati ya Israel na kundi la Hezbollah la Lebanon Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) Jonathan Conricus, amesema "Hadi sasa majibu yetu yamepimwa, kimbinu na yanakomea katika maeneo ya karibu na mpaka (na Lebanon)," anafafanua.

    "Hezbollah inacheza mchezo hatari sana sana," Conricus anaongeza."wanaendeleza mzozo, tunashuhudia mashambulizi zaidi na zaidi kila siku."

    Msemaji wa IDF anasema Israel imekuwa "ikijilinda tu" na "hatua za kuzuia" zimechukuliwa.

    Conricus anasema wale walio karibu na mpaka na Lebanon kaskazini mwa Israel wamehamishwa.

  14. Vita vya Israeli na Hamas: Marekani kutuma mifumo ya ulinzi wa makombora Mashariki ya Kati

    BBC
    Maelezo ya picha, Jingi mfumo wa Thaad unafanya kazi

    Pentagon inasema itatuma mfumo inayozuia mashambulio ya maeneo ya miinuko ya juu (THAAD) katika Mashariki ya Kati, pamoja na vikosi vya ziada vya mfumo wa makombora wa ulinzi wa anga wa Patriot.

    Mfumo wa THAAD umeundwa kurusha makombora ya masafa mafupi na ya kati katika awamu ya mwisho ya safari yao.

    Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin pia alisema wanajeshi wa ziada wamewekwa "kujiandaa kupeleka" maagizo katika eneo hilo, ingawa hajataja ni wangapi.

    Taarifa kutoka Pentagon inasema hii inafuatia "kuongezeka kwa hivi karibuni kwa Iran na vikosi vyake vya wakala katika eneo la Mashariki ya Kati".

    Mashambulizi dhidi ya majeshi ya Marekani nchini Iraq na Syria yameongezeka tangu mzozo kati ya Israel na Hamas kuzuka wiki mbili zilizopita.

    Kufuatia shambulio la Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba, Marekani ilipeleka shehena ya ndege , Meli na jeti mashariki mwa Mediterania – na kuahidi kuipa Israel vifaa vya kijeshi na risasi zaidi.

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  15. Wananchi wahusishwe katika vita dhidi ya waasi wa ADF- Museveni

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameliambia jeshi la Uganda (UPDF} kuwahusisha raia katika juhudi zao kuwasaka wanamgambo wa kundi la kigaidi la {Allied Democratic Force) – ADF.

    Wiki iliyopita wanamgambo hao walifanya mashambulizi katika mbuga ya kitaifa nchini humo ya Malkia Elizabeth ambapo raria wawili wa kigeni na mmoja wa Uganda waliuawa.

    Rais huyo aliyenukuliwa na vyombo vya Habari nchini humo alipotoa taarifa kwa taifa Jumapili, amesema kwamba shughuli za kuwasaka watu hao waliotelekeza shambulizi hilo bado linaendelea akiongeza kuwa msako pia unawalenga walioteketeza moto lori moja mjini Kasese.

    Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X -zamani ikiitwa Twitter, Rais Museveni anasisitiza kwamba, ‘UPDF inapaswa kuihusisha idara ya polisi, na raia (wananchi) kusaka haya makundi yanayotokea Congo ,’

    ‘‘Watu hawa sio tatizo la jeshi pekee yake, Ni jukumu la vitengo mbali mbali vya usalama kama polisi, idara ya uhjasusi na kila mmoja wetu kuhakikisha vita dhidi ya ugaidi vinafaulu, ‘ aliogeza Rais Museveni.

    Mwishoni mwa wiki iliyopita, jeshi la UPDF lilitekeleza ushambulizi katika kambi ya kundi la kigaidi la ADF katika eneo la magharibi mwa DRC ambapo jeshi la Uganda linasema kambi kuu ya ADF ililengwa na kuharibiwa.

  16. Waisraeli zaidi waondoshwa mbali na mpaka wa Lebanon huku hali ya wasiwasi ikiongezeka

    g

    Chanzo cha picha, AFP

    Wakati vita vya Israel dhidi ya Hamas vikizidi kupamba moto, hali ya wasiwasi nayo inaongezeka katika mpaka wa kaskazini mwa nchi hiyo na Lebanon.

    Katika muda wa wiki chache zilizopita, makombora kutoka Lebanon yameshambulia vijiji vya Israel, na jeshi la Israel limelionya kundi la wanamgambo wa Hezbollah - jeshi lenye nguvu zaidi la Lebanon - kwamba linacheza "mchezo hatari sana".

    Hezbollah, kama Hamas, imetajwa a kuwa shirika la kigaidi na Uingereza, Marekani na nchi nyinginezo.

    Sasa, wakaazi wa Israeli wanaoishi katika makazi 14 karibu na mpaka wa Lebanon wanahamishwa, taarifa ya pamoja kati ya Wizara ya Ulinzi ya Israeli na jeshi lake inasema.

    Makazi 14 ni Snir, Dan, Beit Hillel, She'ar Yashuv, Hagoshrim, Liman, Matzuva, Eylon, Goren, Gornot HaGalil, Even Menachem, Sasa, Tziv'on na Ramot Naftali.

    Wanajiunga na Jamii 28 ambazo zilihamishwa siku ya Jumatatu ili "kupunguza madhara kwa raia" na kuwapa wanajeshi wa Israel "uhuru wa kuchukua hatua iwapo itahitajika".

    Wakazi wa jamii zilizohamishwa wanaishi katika nyumba za wageni zinazofadhiliwa na serikali.

    g

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  17. Israel yaapa kushambulia kwa mabomu zaidi Gaza huku Hamas ikisema watu 55 waliuawa usiku kucha

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Iwapo unajiunga nasi tu, karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja ya na taarifa za hivi punde katika vita vya Israel-Gaza. Haya ndiyo yaliyojiri

    • Jeshi la Israel (IDF) linasema lilishambulia "nyumba ya magaidi" huko Jenin katika Ukingo wa Magharibi , ambayo inadaiwa kuwa ni pamoja na seli ya Hamas ndani ya msikiti.
    • Inakuja baada ya operesheni ya awali ya vikosi vya usalama vya Israel katika kambi ya wakimbizi ya Nur Shams katika Ukingo wa Magharibi kuwaua watu 13, wakiwemo watoto watano, kulingana na UN.
    • ·Msemaji wa IDF, Daniel Hagari, aliambia mkutano wa waandishi wa habari Jumamosi kwamba jeshi la Israeli "litaongeza" na "kuongeza" mashambulizi yake huko Gaza.
    • Malori ya kwanza yaliyokuwa yamebeba msaada katika Ukanda wa Gaza wenye wakazi wengi zaidi yaliingia kutoka Misri siku ya Jumamosi, yakiwapelekea Wapalestina chakula, maji na vifaa vya matibabu vinavyohitajika sana - lakini sio mafuta.
    • Kuongezeka kwa hali ya wasiwasi kufuatia shambulio la Hamas dhidi ya Israel zaidi ya wiki mbili zilizopita na kuua zaidi ya watu 1,400.
    • ·Tangu wakati huo Israel imeanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi ya anga . Zaidi ya watu 4,300 wameuawa huko Gaza tangu Oktoba 7, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas
    g

    Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza:

  18. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo ikiwa ni Jumapili tarehe 22.10.2023