Wanajeshi na raia wa Israeli watekwa nyara katika shambulio la wanamgambo wa Palestina
Wanamgambo wa Kipalestina walishambulia vituo kadhaa vya kijeshi - picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanamgambo ndani ya kambi isiyojulikana, wakichoma moto magari ya Israel 4kikiwemo kifaru cha jeshi aina ya Merkava.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Netanyahu awaalika wapinzani kuunda serikali ya dharura
Waziri Mkuu wa Israel amewaalika viongozi wa upinzani - Yair Lapid na Benny Gantz - kuunda serikali ya dharura ya umoja wa kitaifa. Chama cha Netanyahu cha Likud kimetoa taarifa kwa umma juu ya mwaliko huo.
Awali, Bwana Lapid aliviambia vyombo vya habari vya Israeli kuwa yupo tayari kushirikiana na Netanyahu ambaye ni hasimu wake kisiasa kuunda serikali ya dharura.
“Muda mfupi uliopita nimekutana na Waziri Mkuu Netanyahu. Nimemueleza kuwa katika hali hii ya dharura inayoendelea Nipo tayari kuunda serikali ya dharura itakayokuwa ndogo na yenye weledi. Netanyahu anajua wazi kuwa hawezi kuendesha vita kwa hali ya sasa na kwa jinsi wizara ya ulinzi ilivyoparaganyika,” amesema
Yair Lapid, kiongozi wa chama cha upinzani cha Yesh Atid.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa Lapid na Gantz kwa sasa wapo kwenye mkutano wa kujadiliana na kupanga masharti yao ya kuingia kwenye serikali ya dharura.
naweza pia kusoma:
- Je! Ujasusi wa Israel ulishindwa vipi kuzuia mashambulizi makubwa kutoka Gaza?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Habari za hivi punde, Idadi ya waliofariki Gaza yaongezeka hadi watu 232
Afisa wa wizara ya afya wa Palestina ameiambia BBC kuwa takriban watu 232 wameuawa Gaza tangu mashambulizi ya Israel yaanze asubuhi ya leo.
Takriban watu 1,790 walijeruhiwa, kulingana na wizara ya afya.
Unaweza pia kusoma:
- Je! Ujasusi wa Israel ulishindwa vipi kuzuia mashambulizi makubwa kutoka Gaza?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Habari za hivi punde, Hamas: Tumerusha roketi 150
Hamas inasema wamerusha makombora 150 kujibu mashambulizi ya anga ya Israel kwenye Mnara wa Palestina, jengo la gorofa 11 katikati mwa mji wa Gaza.
Milio ya milipuko inaweza kusikika kote Gaza.
Mashambulio ya Gaza: Nini kimetokea hadi sasa?

Chanzo cha picha, Reuters
Huu hapa ni muhtasari wa matukio ya hivi punde:
- Israel inasema vikosi vyake maalum vinahusika katika hali mbili za mateka - katika kibbutzes ya Ofakim (iliyowekwa alama kwenye ramani hapa chini) na Be'eri.
- Wanajeshi na raia wa Israel wamechukuliwa mateka na wanamgambo wa Kipalestina
- Inafuatia shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa kutoka Gaza, ambapo makumi ya watu wenye silaha walijipenyeza Israel.
- Wanamgambo wa Kipalestina pia walirusha maelfu ya maroketi huko Israel kama sehemu ya shambulio hilo
- ·Zaidi ya Waisraeli 150 wameuawa , na karibu 1,000 wamejeruhiwa, maafisa wa Israel wamesema.
- Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu asema: "Tuko vitani"
- Israel imejibu mashambulizi ya anga katika ukanda wa Gaza
- Takriban watu 200 wameuawa huko, maafisa wa Palestina wanasema

Unaweza pia kusoma:
- Je! Ujasusi wa Israel ulishindwa vipi kuzuia mashambulizi makubwa kutoka Gaza?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Israel yakata usambazaji wa umeme Gaza - waziri wa nishati wa Israel
Waziri wa nishati na miundombinu wa Israel Katz amesema kuwa Israel inakata usambazaji wake wa umeme katika Ukanda wa Gaza.
"Nimetia saini agizo la kuagiza kampuni ya umeme ya Israel kusitisha usambazaji wa umeme huko Gaza," Katz alisema katika taarifa yake.
Kukatika kwa umeme ni jambo la kila siku mjini Gaza.
Mamlaka ya nishati ya Gaza inasema asilimia 80 ya vifaa vya umeme vya Gaza vimefungwa kufuatia tangazo la Israeli.
Kabla ya kauli ya Katz, wakaazi wa Gaza walikuwa tayari wanaripoti kukatwa kwa umeme mara kwa mara tangu mashambulio ya Israeli kuanza asubuhi ya leo.
Ukanda huu unapata nishati zake nyingi kutoka kwa Israeli pamoja na michango zaidi kutoka kwa mtambo pekee wa kuzalisha umeme wa Gaza na kiasi kidogo kutoka Misri.
Kiwanda cha kuzalisha umeme na jenereta za watu wengi hutegemea mafuta ya dizeli, na vifaa vinavyoletwa kupitia Israel.
Unaweza pia kusoma:
- Je! Ujasusi wa Israel ulishindwa vipi kuzuia mashambulizi makubwa kutoka Gaza?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Vikosi vya Ulinzi vya Israeli: Tunapigana katika maeneo 22 ndani ya Gaza
Zaidi kutoka kwa Jeshi la Ulinzi la Israeli, ambao wamethibitisha kuwa wanajeshi wao wanapigana katika maeneo 22 katika taarifa.
"Hakuna jamii ya kusini mwa Israeli ambako hatuna nguvu," inasema.
Imeonge kuwa Israel itatumia 'njia nzito' dhidi ya wanamgambo.
"Malengo yetu ni kwamba magaidi wote watauawa, kwamba jamii zote zitaondokana na magaidi," taarifa ya Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) imesema.
Pia iliwaonya watu wanaoishi Israel karibu na Ukanda wa Gaza kusalia ndani hadi wakati huo.
Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa IDF inaendesha mashambulizi ya anga huko Gaza na baadaye itaendelea na "njia nzito za ardhini"
Unaweza pia kusoma:
- Je! Ujasusi wa Israel ulishindwa vipi kuzuia mashambulizi makubwa kutoka Gaza?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Habari za hivi punde, Idadi ya Waisraeli waliopoteza maisha yafikia takriban watu 150 - maafisa
Wizara ya afya ya Israel imetoa nambari mpya kwa vyombo vya habari vya Israel kuhusu wahanga wa shambulio la Hamas tangu mapema Jumamosi.
Idadi ya vifo sasa inaripotiwa kuwa takriban 150 na idadi ya watu waliopelekwa hospitalini ni 985.
Mtangazaji wa umma Kan anasema makumi ya wale wanaotibiwa wako katika hali mbaya.
Idadi ya majeruhi inatarajiwa kuongezeka zaidi
Tazama: Mlipuko mkubwa huku magorofa marefu yakiharibiwa na jeti Gaza
Maelezo ya video, Tazama:Mlipuko mkubwa katika eneo la Gaza ulivyoharibu jengo Ndege za kivita za Israel zimepiga majengo kadhaa katikati mwa mji wa Gaza, likiwemo jengo la gorofa 11 liitwalo Palestine Tower.
Gorofa hili lina vituo vya redio vya Hamas juu ya paa na pia lina ukumbi wa sinema.
Israel imefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika ukanda wa Gaza, maafisa wa huko wanasema, baada ya shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa katika eneo la Israel na wanamgambo wa Kipalestina mapema Jumamosi.
Unaweza pia kusoma:
- Je! Ujasusi wa Israel ulishindwa vipi kuzuia mashambulizi makubwa kutoka Gaza?
- Fahamu chanzo cha uhasama kati ya Israel na Palestina
Habari za hivi punde, Vikosi maalum vimehusika katika hali mbili za mateka - jeshi la Israeli
Katika taarifa yake, jeshi la Israel pia linathibitisha kwamba kuna hali ya utekaji nyara katika kibbutzes ya Ofakim na Be'eri.
Inasema vikosi maalum vinahusika na "vita vya risasi" vinavyoendelea.
Aidha jeshi hilo linathibitisha kuwa wanajeshi wa Israeli wameuawa, lakini halitoi idadi.
Waisraeli watekwa nyara katika shambulio la wanamgambo wa Palestina

Chanzo cha picha, Reuters
Wanamgambo wa Kipalestina walishambulia vituo kadhaa vya kijeshi - picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanamgambo ndani ya kambi isiyojulikana, wakichoma moto magari ya Israel kikiwemo kifaru cha jeshi aina ya Merkava.
Uvamizi kama huo ulitarajiwa kutoa fursa ya kutosha kuwakamata maafisa na wanajeshi wa Israeli.
Makundi ya Wapalestina siku za nyuma yamekuwa yakiwatumia mateka kama njia ya mazungumzo ili kuhakikisha kuachiliwa kwa wanamgambo wanaoshikiliwa na Israel.
Israel illiweza kufanikiwa katika kuachiliwa kwa askari wake Gilad Shalit kwa kuwaachilia zaidi ya wafungwa 1,000 wa Kipalestina mwaka 2011.
Takriban wafungwa 200 walikuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuandaa au kutekeleza mashambulizi ndani ya Israel.
Kulingana na taarifa za hivi pundeza B'Tselem, kundi la haki za binadamu la Israel, kulikuwa na Wapalestina 4,499 gerezani kwa kile ambacho Israel ilikifafanua kama misingi ya "usalama" mwezi Juni.
Idadi hiyo ilijumuisha 183 kutoka Ukanda wa Gaza. Mamia kadhaa zaidi wanazuiliwa kwa kuwa ndani ya Israel kinyume cha sheria.
Mashambulio ya Gaza: Hamas inasema imewakamata 'maafisa wakuu'
Naibu mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Saleh al-Arouri, amedai "maafisa wakuu" wa jeshi la Israel wamekamatwa.
Aliiambia idhaa ya Kiarabu ya Al Jazeera kwamba "kile kilicho mikononi mwetu kitawaacha huru wafungwa wote" nchini Israel - ikiwa ni kumbukumbu ya Wapalestina wanaozuiliwa katika jela za Israel.
"Tulikamata maafisa wakuu kutoka jeshi la uvamizi," alisema.
"Kuna Wapalestina wengi waliouawa na Waisraeli wengi wamekufa pamoja na wafungwa, na vita bado vinaendelea."
Arouri alisema Hamas iko tayari kukutana na uvamizi wa ardhini wa Israel huko Gaza, ambao aliutaja kuwa "mazingira bora zaidi kwetu kutatua mzozo dhidi ya adui".
Hakuna madai yoyote kati ya haya yanayoweza kuthibitishwa kwa kujitegemea na BBC kwa wakati huu, na mamlaka ya Israeli haijatoa maoni yoyote kuhusu ripoti nyingi za utekaji nyara.
Habari za hivi punde, Marekani inaunga mkono haki ya Israel kujilinda, Netanyahu anasema
Tunasikia kutoka kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu sasa, ambaye anasema Rais wa Marekani Joe Biden amemwambia Marekani inaunga mkono kikamilifu haki ya Israel ya kujilinda.
Tunatarajia kusikia kutoka kwa Biden hivi karibuni na tutakuletea zaidi kadri tutakavyoyapata.
Marekani 'itajitahidi kuhakikisha Israel ina kile inachohitaji kujilinda' - Austin

Chanzo cha picha, EPA-EFE/Rex/Shutterstock
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin ametoa taarifa kuhusu mashambulizi dhidi ya Israel yanayofanywa na wanamgambo wa Kipalestina.
"Ninafuatilia kwa karibu matukio nchini Israel. Ahadi yetu kwa haki ya Israel ya kujilinda bado haijayumba, na ninatuma rambirambi zangu kwa familia za waliopoteza maisha katika shambulio hili la kuchukiza dhidi ya raia," anasema.
"Katika siku zijazo Idara ya Ulinzi itafanya kazi kuhakikisha kuwa Israel inapata kile inachohitaji ili kujilinda na kuwalinda raia dhidi ya ghasia na ugaidi usiobagua."
Habari za hivi punde, Idadi ya vifo katika Gaza yaongezeka hadi 198 - maafisa
Idadi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulizi ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza imeongezeka hadi 198, maafisa wa afya wanasema.
Idadi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulizi ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza imeongezeka hadi 198, maafisa wa afya wanasema.
Kundi la jihad la Kiislam ladai kuwakamata wanajeshi wa Israel
Kundi la Jihad la Kiislamu ( Islamic Jihad) ambalo linaendesha harakati zake Gaza, linadai wapiganaji wake pia wamewakamata wanajeshi "wengi" wa Israeli, Msemaji wake anayejiita Abu Hamza anasema kwenye chapisho la Telegram,
"Tunathibitisha katika Brigedi za al-Quds kwamba sasa, shukrani kwa Mwenyezi Mungu, tunamiliki askari wengi wa Kizayuni ambao ni wafungwa mikononi mwetu."
Islamic Jihad ni mojawapo ya makundi kadhaa ya wapiganaji wanaoendesha harakati zao huko Gaza.
Brigedi ya Quds ni tawi lake la silaha. Kundi hilo linashirikiana na Hamas lakini pia linadumisha uhuru.
Pia linafanya kazi katika Ukingo wa Magharibi na limefanya mashambulizi kadhaa dhidi ya Waisraeli.
Habari za hivi punde, Iran yaunga mkono mashambulizi ya Wapalestina
Tumepokea ripoti zinazosema kuwa mshauri wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei anaunga mkono shambulio la Wapalestina dhidi ya Israel.
"Tunawapongeza wapiganaji wa Palestina," Rahim Safavi amenukuliwa akisema na shirika la habari la ISNA.
"Tutasimama na wapiganaji wa Palestina hadi ukombozi wa Palestina na Jerusalem," anasema.
Tazama: Video 'inaoonyesha kifaru cha jeshi la Israel kilichotekwa mjini Gaza'
Maelezo ya video, Video ya 'Kukamatwa kwa kifaru cha jeshi la Israeli mjini Gaza' Video imeibuka inayodaiwa kuwaonyesha Wapalestina wakiruka kwenye kifaru cha Israel kilichotekwa na wanamgambo wa Hamas.
Picha hizo, ambazo shirika la habari la Reuters lilizipata, pia zinaonyesha wanamgambo wakiingia Gaza kwa kile kinachosemekana kuwa gari la kijeshi la Israel lililotekwa.
Msemaji wa jeshi la Israel alikataa kutoa maoni yake kwa waandishi wa habari kuhusu Waisraeli kukamatwa na Hamas, kulingana na Reuters.
Simone Biles: Mwanariadha aliyepambwa kwa medali zaidi duniani katika mashindano ya sarakasi

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Biles alichukua dhahabu kwa alama 58.399 Mmarekani Simone Biles amekuwa mwanariadha aliyepambwa zaidi katika historia baada ya kushinda medali yake ya pili ya dhahabu katika Mashindano ya Ulimwengu ya Sarakasi.
Baada ya kuisaidia Marekani kutwaa taji la saba mfululizo la timu mapema wiki hii, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alishinda dhahabu ya pande zote nchini Ubelgiji siku ya Ijumaa.
Amepata jumla ya medali 34 za dunia na Olimpiki ni nyingi kuliko mwanariadha mwingine yeyote, wa kiume au wa kike.
Biles alichukua dhahabu kwa alama 58.399.
Alimaliza mbele ya bingwa mtetezi Rebeca Andrade wa Brazil (56.766), huku mwenzake wa Biles' Mmarekani Shilese Jones akitwaa shaba kwa alama 56.332.
Ushindi huu ulikuwa taji lake la sita la dunia nzima hadi kufikia jumla ya medali 27 za dunia, ambazo ni pamoja na 21 za dhahabu.
Mashambulio la Palestina dhidi ya Israel: Tunajua nini kuhusu ripoti za mateka?

Chanzo cha picha, Reuters
Televisheni ya Israeli - Reshet 13 inaripoti kwamba wanamgambo wa Kipalestina wanawashikilia Waisraeli katika mji wa kusini wa Ofakim, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Hii ni moja ya ripoti za kwanza tulizo nazo kutoka kwa vyombo vya habari vya Israel kuhusu hali hiyo, baada ya kuenea kwa madai kwenye mitandao ya kijamii kuwa wanamgambo wa Kipalestina wamechukua mateka.
Video ambazo hazijathibitishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonekana kuonyesha Wapalestina wakiwachukua raia mateka na kuwahamisha kwa pikipiki hadi Gaza.
Mamlaka ya Israel wamesema hawatatoa maoni yoyote kuhusu hili na BBC hadi sasa haijaweza kuthibitisha ripoti hizo.
Hata hivyo, msemaji wa Hamas aliiambia televisheni ya Al Jazeera kwamba "sio mateka - ni wafungwa wa vita".
