Sheria ya Uganda dhidi ya LGBTQ inachochea unyanyasaji - mashirika ya kutetea haki
Ripoti mpya imerekodi zaidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu 300 dhidi ya jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja (LGBTQ) unaofanywa na watendaji wa serikali na wasio wa serikali kufuatia kupitishwa kwa sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda
Moja kwa moja
Mwongozo mpya kwa watangazaji vinara BBC baada ya utata kwenye mtandao wa kijamii

Chanzo cha picha, Getty Images
Watangazaji vinara wanapaswa kukubaliwa kueleza maoni yao kuhusu masuala na sera lakini hawafai kufanya kampeni za kisiasa, ripoti mpya ya BBC inaeleza.
Mwongozo mpya kwa watangazaji vinara wa BBC zimechapishwa kufuatia mvutano juu ya ujumbe wa mtandaoni wa mtangazaji Gary Lineker
Hii inajiri baada ya ukaguzi kwenye miongozo ya BBC katika utumiaji wa mitandao ya kijamii kuchapishwa na aliyekuwa mkuu wa ITN John Hardie.
Lineker alijibu kupitia mtandao wa X, zamani uliokuwa ukijulikana kama Twitter, kwa kusema miongozo mipya “yote ni yenye busara”.
Miongozo hiyo ni kwa watangazaji wa vipindi maarufu mbali na matukio yanayoendelea, ambao watakuwa na “jukumu maalu la kuheshimu maadili ya BBC hususani ya kutoegemea upande wowote, kwa sababu ya kazi zao katika katika BBC.
Wale wanaofanya kazi kwenye vipindi vya habari na matukio yanayojiri tayari wanapaswa kuzingatia kanuni kali zaidi kuhusu kutokuwa na upendeleo wanapotumia mitandao ya kijamii.
Mwongozo huo mpya unatambua umuhimu wa uhuru wa kujieleza, lakini unasema kuwa wakati kipindi kiko hewani, na kwa muda wa wiki mbili kabla na baada ya kipindi hicho, watangazaji wa vipindi maarufu hawapaswi kuidhinisha au kushambulia chama cha kisiasa.
Nyota muigizaji filamu ya Harry Potter Sir Michael Gambon afariki dunia

Chanzo cha picha, Getty Images
Muigizaji filamu ya Harry Potter Sir Michael Gambon amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82, familia yake imesema.
Alijulikana sana kwa kuigiza kama Profesa Albus Dumbledore katika filamu sita kati ya nane za Harry Potter.
Muigizaji huyo alikuwa maarufu kwa kuigiza kama Professor Albus Dumbledore kwenye filamu sita za Harry Potter.
Nyota huyo aliyezaliwa Dublin alifanya kazi katika runinga, filamu, ukumbu wa michezo pamoja na radio kwa zaidi ya miongo sita ya taaluma yake.
Alishinda tuzo nne za uingizaji filamu, Baftas.
Mjane na mtoto wake wa kiume Fergus walisema alifariki kwa amani akiwa hospitalini familia ikiwa kando yake, kufuatia ugonjwa wanimonia [pneumonia]
Familia ya Michael ilikuwa imehamia London wakati akiwa bado mtoto, lakini alifanya uigizaji wake wa kwanza ukumbini nchini Ireland, katika filamu ya Othello mjini Dublin mwaka 1962.
Alianza taalumu yake alianza kushika kasi alipoanza kuwa mmoja ya waigizaji wa kwanza katika kampuni ya uigizaji ya Laurence Olivier mjini London.
Kisha akashinda tuzo tatu za Olivier katika ukumbi wa maonyesho ya Kitaifa.
Aliyekuwa waziri mkuu wa Burundi afika mahakamani kwa mara ya kwanza baada ya miezi 5 kizuizini

Chanzo cha picha, RTNB
Maelezo ya picha, Jenerali Alain Guillaume Bunyoni Jenerali Alain Guillaume amefika mahakamani akiwa na wenzake sita katika kesi iliyowasilishwa ndani ya gereza lao katika mji mkuu wa Burundi Gitega.
Yeye na washtakiwa wenzake wawili walikuwa na mawakili wa utetezi, wanne waliosalia hawakuwa nao na walisema hawakuwahitaji.
Kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwa kesi hii, mashtaka dhidi ya washtakiwa hayakusomwa, kwa hivyo hawakujibu kesi inayowakabili.
Jenerali Bunyoni alijitolea kulipa pesa za Burundi milioni mia tatu (karibu na $100,000) kama dhamana akisema anaugua kisukari cha aina B.
Lakini upande wa mashtaka uliiomba mahakama kukataa ombi lake ukisema anaandamwa kwa makosa makubwa.
Ndivyo ilivyokuwa hoja ya upande wa mashtaka kuhusu maombi ya dhamana ya washtakiwa wengine wawili.
Ulinzi ulikuwa mkali ndani ya gereza hilo na pia kwa watu wote walioingia ndani ya chumba cha mahakama wakiwemo waandishi wa habari hawakuruhusiwa kubeba kalamu, miwani, simu wala kamera.
Kesi hiyo iliahirishwa kwa ajili ya majadiliano ya uamuzi katika ''siku inayokuja'', mahakama ilisema. Jenerali Bunyoni alituhumiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na kuhujumu usalama wa taifa na uchumi.
Alikamatwa mwezi Aprili baada ya kufutwa kazi na rais Evariste Ndayishimiye zaidi ya nusu mwaka iliyopita.
Soma zaidi:
- Burundi yathibitisha kutoweka kwa waziri mkuu wa zamani Jenerali Alain Guillaume Bunyoni
- Mfahamu Alain-Guillaume Bunyoni, Waziri Mkuu mpya wa Burundi
Msumbiji yamfunga afisa wa polisi kwa ‘kupanga njama ya mapinduzi’

Msumbiji imemhukumu afisa mmoja wa polisi kifungo cha miaka 13 jela kwa mashtaka ya kuchochea mapinduzi, shirika la habari linalomilikiwa na serikali Lusa liliripoti jana.
“Mahakama ya jimbo la Inhambane kusini mwa Msumbiji, Jana Jumatano imemhukumu afisa wa Kitengo cha kushughulikia mambo ya dharura miaka 13 jela kwa uchochezi wa mapinduzi na uasi,” ilisema ripoti hiyo.
Kulingana na hakimu, mahakama hiyo ilikuwa imepunguza hukumu hiyo kutoka adhabu ya kifungo cha miaka 24 hadi 13 baada ya kuzingatia baadhi ya mambo katika kesi hiyo.
Mshtakiwa anatuhumiwa kwa kutumia mtandao wa kijami wa ‘WhatsApp’kusambaza ujumbe kuhamasisha baadhi ya mafisa wa polisi kuasi kwa sababu ya kuchelewa kulipwa mshahara na “kumuondoa amiri-jeshi mkuu [Rais Filipe Nyusi] kutoka ikulu ya uraias.”
Mshtakiwa huyo amekanusha madai dhidi yake na kusema kwamba alituma tu ujumbe huo baada ya kuupokea kutoka kwa mkuu wa polisi Bernardino Rafael kumuonya dhidi ya kupanga njama.
Pia unaweza kusoma:
Sheria ya Uganda dhidi ya LGBTQ inachochea unyanyasaji, mashirika ya kutetea haki yanasema

Chanzo cha picha, Mark Kerrison/In Pictures via Getty Images
Maelezo ya picha, Uganda hivi majuzi ilipitisha mojawapo ya sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja Ripoti mpya imerekodi zaidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu 300 dhidi ya jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja (LGBTQ) unaofanywa na watendaji wa serikali na wasio wa serikali kufuatia kupitishwa kwa sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja nchini Uganda.
Ripoti hiyo ilitolewa na kundi la mashirika ya haki chini ya Kuitisha Usawa.
Kati ya Januari na Agosti 2023 "watu wanaojihusisha na wanaodhaniwa kuwa wa LGBTIQ+ waliteswa, kupigwa, kukamatwa, kufukuzwa nje na kuteswa kimwili, kingono na kisaikolojia, ikiwa ni pamoja na kulazimishwa kufanyiwa vipimo katika sehemu ya haja kubwa, kufukuzwa na kukashifiwa, kupoteza ajira na kukatizwa huduma za afya", makundi hayo yanasema.
Hizi zilichangia jumla ya ukiukaji wa haki za binadamu na dhuluma kesi 306 kulingana na visa vya dhulama za kijinsia na utambulisho.
Kulikuwa na visa 179 vya mateso, ukatili na unyanyasaji wa kinyama ambavyo vilijumuisha vipimo vya lazima 18 katika njia ya haja kubwa kulikoamriwa na polisi ambavyo vilirekodiwa.
Waandishi hao wanatoa wito wa kulindwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na kukomeshwa kwa athari ya sheria dhidi ya mapenzi wa jinsia moja ambayo wanasema hazijashughulikiwa na mamlaka.
Wanabainisha wanasiasa na viongozi wa kidini "wanachochea uwezekano wa vurugu na ubaguzi zaidi, na kuendeleza mateso ya kimwili na ugumu wa kiuchumi kwa Waganda wa jamii ya LGBTIQ+".
Ripoti hiyo pia inaonyesha kuongezeka kwa kesi za afya ya akili kama vile mawazo ya kujiua, na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaotafuta hifadhi.
"Kama mataifa mengine ya Afrika yanazingatia sheria zinazofanana ambazo sio tu zinaongeza muda wa kifungo kwa tabia ya mapenzi ya jinsia moja lakini zinaharamisha haki halali za binadamu na afya ya umma, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kwa wafadhili wa kimataifa na wafanyabiashara kutetea kikamilifu kanuni za kutobagua na maendeleo ya kipekee kiuchumi katika maneno na matendo yao," Frank Mugisha wa Jumuiya ya Wachache wa Kijinsia Uganda na mratibu mwenza wa masuala ya Usawa.
Ilikuwa vigumu kutoa maelezo ya kina kuhusu unyanyasaji huo, ilitahadharisha ripoti hiyo, kwani baadhi ya waathiriwa walisita kushirikisha mateso wanayopitia kwa sababu ya kuogopa hatua za kulipiza kisasi.
Wakati BBC ilipotoa maoni yake, msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo alisema nchi hiyo ina mashirika ya kiraia mahiri na redio za jamii za FM ambazo wanaharakati wangeweza kuripoti visa hivyo.
Alisema hakuna vikundi vya haki vilivyoripoti kesi hata moja tangu sheria hiyo ianze kutekelezwa.
Soma zaidi:
- Sheria dhidi ya LGBT Uganda: Simulizi za waathiriwa wanavyopigwa na kulazimishwa kutoroka
Majeshi ya wanamaji ya China na Saudia kufanya mazoezi ya pamoja

Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi la wanamaji la China litafanya mazoezi ya pamoja na lile la Saudi Arabia mwezi ujao, Wizara ya Ulinzi ya China amesema.
Hii ni mara ya pili katika historia kwa China na Saudi Arabia kufanya mazoezi ya kijeshi pamoja.
Katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimeongeza kwa kiasi kikubwa ushirikiano katika masuala mbali mbali.
Beijing imetangaza kwamba zoezi hilo kwa jina. “Blue Sword 2023”, litafanyika katika maji ya Guangdong mnamo mwezi wa Oktoba.
Guangdong ni mojawapo ya maeneo ya China yaliopo karibu na Hong Kong.
“Zoezi hili la pamoja litajumuisha kufanya mazoezi kuhusu oparesheni dhidi ya magaidi baharini, “alisema Wu Qian, msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa China.
Kulingana na Bw. Wu, shughuli kama kuelekeza boti, kutua kwa helikopta pamoja na oparesheni za uokoaji zitakuwa miongoni mwa mambo yatakayofanyika katika mazoezi hayo
Nchi hizi mbili zilifanya mazoezi ya kwanza ya kijeshi pamoja mwaka 2019, kwa mujibu wa shirika la habari la Saudi Arabia.
Kenya: Polisi wasimamisha mkutano wa injili wa Mchungaji Ezekiel Odero

Chanzo cha picha, PASTOR EZEKIEL ODERO/FACEBOOK
Polisi eneo la Kilifi nchini Kenya wamesimamisha mkutano wa injili wa Mchungaji Ezekiel Odero wa New Life International Ministry.
Akithibitisha hilo, Kamanda wa Polisi wa Kilifi Kaskazini Kenneth Maina, amesema mhubiri huyo hakujulisha polisi juu ya mkutano wake kwa wakati unaofaa.
‘’Hatukuweza kumruhusu mchungaji Ezekiel Odero kuendelea na mkutano wake kwa sababu alitujulisha ndani ya kipindi kifupi. Inahitajika kujulisha polisi ndani ya saa 72, lakini atafanya mkutano wake wiki ijayo,’’ alisema.
Bwana Maina aliongeza mkutano huo ulitarajiwa kuanza Jumatano.
‘’Alikuwa ameomba siku tano, na mkutano huo wa injili uanze Jumatano, kwahiyo, bado utafanyika kwa kipindi hicho hicho wiki ijayo,’’ aliongeza.
Siku za nyuma, mkutano kama huo uliwahi kufutwa huko Arusha nchini Tanzania
Soma zaidi:
Kama wewe ni abiria unapenda kuendeshwa na dereva mwanamke ama mwanaume?
Maelezo ya video, Kama wewe ni abiria unapenda kuendeshwa na dereva mwanamke ama mwanaume? Kikundi kimoja cha madereva wa pikipiki wanawake mkoani Mwanza kanda ya Ziwa, kimepata umaarufu mkubwa kutokana na aina yake ya uendeshaji inayotajwa kuwa rafiki kwa abiria.
Ni kina dada wadogo ambao wameamua kujikita kutoa huduma kwa jamii baada baada ya kuona mwanya uliokuwepo kwa madereva pikipiki wanaume.
Mwandishi wa BBC David Nkya ametembelea mkoa huo na kutuandalia makala hii.
Pia unaweza kutazama:
Video inayoonesha ajali ya ndege ya jeshi la anga ya Mali

Chanzo cha picha, @JacdecNew
Kanda ya video imeibuka ikionyesha jinsi ndege inayoaminiwa kuwa ya jeshi la anga la Mali ilivyo pata ajali na kuteteketea moto katika uwanja wa ndege wa Gao, Kaskazini mwa Mali, Juma mosi iliyopita.
Kumekuwa na fununu kwamba mamluki wa kundi la Urusi Wagner huenda walikuwa miongoni mwa abiria katika ndege hiyo, lakini madai hayo bado hayajathibitishwa.
Ndege hiyo inaonekana ikitua lakini gurudumu zake zinaonekana kuchelewa kugusa ardhini, kabla ya risasi kuanza kushuhudiwa kwenye njia ya ndege kwa kasi ya ajabu.
Kisha inafulululiza na kupita kile kinachoonekana kuwa vizuizi kabla ya kuanguka chini ya tuta kwenye shimo na baadaye kuanza kuteketea.
Picha inayoonyesha ndege hiyo ikiwa imeanguka pia imesamba katika mitandao, ikionyesha sehemu kubwa ya ndege hiyo ikiwa imeunguwa.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Jeshi la Mali bado halijatoa tamko lolote kuhusu ajali hiyo. Kulingana na Shirika la habari AFP, serikali ya junta imetoa risala za rambi rambi kwa kanali mmoja ambaye jamaa zake wanadai alifariki katika ajali hiyo.
Vikosi vya Mali, mamluki wa kundi la Wagner pamoja na vikosi vya Umoja wa mataifa vya kulinda amani nchini Mali kwa pamoja hutumia uwanja wa ndege wa Gao.
Mali imekuwa ikishuhudia ongezeko la mashambulio kutoka kwa makundiyaliojihami yanaojidai kuwa ya kiislamu pamoja na waasi wa kabila la Tuareg kaskazini mwa nchi hiyo
Pia unaweza kusoma:
Salva Kiir yuko nchini Urusi kwa mazungumzo na Putin

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Salva Kiir akiwa New York mapema mwezi huu akihutubia Umoja wa Mataifa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir yuko Moscow kwa mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Ziara hiyo inakuja wakati ambapo Urusi na mataifa yenye nguvu ya Magharibi yanajaribu kuvuta uungwaji mkono wa Afrika kutokana na uvamizi wa Ukraine.
Bw Kiir aliwasili katika mji mkuu wa Urusi siku ya Jumatano na kupokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Andrey Rudenko Yurevich, kulingana na taarifa kutoka kitengo cha habari cha rais.
Ofisi ya Bw Kiir inasema mkutano na rais wa Urusi siku ya Alhamisi utajikita katika matarajio ya maendeleo ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili katika maeneo mbalimbali, pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa.
Imeongeza kuwa ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kuchunguza maeneo mengine ya ushirikiano katika biashara, fursa za uwekezaji na usalama.
Viongozi hao wawili pia watajadili kuondolewa kwa vikwazo vya silaha na vikwazo vilivyolengwa vilivyowekwa kwa watu binafsi nchini Sudan Kusini, taarifa hiyo iliongeza.
Mwezi Mei, Urusi ilijizuia katika kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kurejesha vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Sudan Kusini, ambavyo ni pamoja na marufuku ya kusafiri na vikwazo vya silaha.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
ISW: Urusi itaweza kununua makombora kutoka Iran baada ya Oktoba 18

Chanzo cha picha, IRANIAN ARMY/GETTY IMAGES
Urusi na Iran zinaweza kufikia makubaliano juu ya uuzaji wa ndege zisizo na rubani na makombora baada ya Oktoba 18, wakati vikwazo vya Umoja wa Mataifa juu ya silaha za Iran vitakapomalizika, kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Vita (ISW).
Mnamo tarehe 20 Septemba, Brigedia Jenerali Amir-Ali Hajizadeh, kamanda wa Kikosi cha Wanaanga cha IRGC, alimpleleka Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu ziara ya kuchunguza ghala la Iran la ndege zisizo na rubani, makombora na ulinzi wa anga.
Shoigu pia alijadiliana na Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani kuhusu kumalizika kwa vikwazo dhidi ya Iran kuhusiana na makombora na silaha nyinginezo chini ya Azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Baada ya Oktoba 18, Iran itakuwa huru kusafirisha makombora na teknolojia zinazohusiana bila udhibiti wa kimataifa, kuruhusu kukidhi mahitaji ya kijeshi ya Russia, inasema taasisihiyo.
Katika ziara hiyo, Shoigu Hadjizade alionyesha kombora la kusafiri la Paveh, makombora ya balestiki ya Ababil na Fattah, pamoja na vifaa vingine vya kijeshi, kikiwemo kifyatuzi kipya cha drone cha Shahed-136.
Mnamo tarehe 5 Septemba, Ashtiani alisema Wizara ya Ulinzi ya Iran iko tayari kuendeleza uhusiano wa kiulinzi na wa kimkakati na "nchi zote huru na washirika" baada ya kumalizika kwa vikwazo.
Mnamo Disemba 2022, maafisa wa Marekani na Uingereza walionya kwamba Urusi ilikuwa inataka kununua makombora kutoka Iran ili kushughulikia silaha zake zinazopungua, ISW inakumbuka.
Kulingana na ujasusi wa Ukraine na Israeli, Urusi inavutiwa kimsingi na makombora ya Irani ya Fateh-110 na Zolfaghar, ambayo yanaweza kupigaeneo lillilopo kilomita 300 au zaidi.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Moto kwenye harusi ya Iraq: Jinsi moto ulivyotokea
Maelezo ya video, Moto wa harusi ya Iraq: Jinsi moto ulivyotokea Takriban watu 94 walikufa na wengine 100 kujeruhiwa baada ya moto kuzuka wakati wa harusi katika Ukumbi wa al-Haitham, ukumbi mkubwa wa hafla uliopo nje kidogo ya mji wa kaskazini wa Qaraqosh.
Wachunguzi wanajaribu kubaini chanzo cha moto huo, lakini walioshuhudia walisema moto huo ulianza wakati fataki kadhaa zilipowashwa wakati wa harusi.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameieleza BBC kuwa matukio ya kutia kutisha na wasi wasi mkubwa wakati moto huo ukishika kasi.
Justin Trudeau aomba msamaha baada ya mkongwe wa Nazi kupewa heshima bungeni

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Waziri Mkuu Justin Trudeau alisema Bunge lilikuwa "halijui muktadha" Waziri Mkuu Justin Trudeau ameomba msamaha kwa niaba ya Canada baada ya mwanaume mmoja wa Ukraine aliyepigana katika kitengo cha Nazi kupigiwa makofi kimakosa bungeni.
"Hili ni kosa ambalo liliaibisha sana bunge na Canada," Bw Trudeau alisema Jumatano.
Spika Anthony Rota, ambaye alichukua jukumu la kumwalika Yaroslav Hunka, mwenye umri wa miaka 98, alijiuzulu Jumanne.
Tukio hilo limelaaniwa kimataifa.
Bw Trudeau pia aliomba msamaha moja kwa moja kwa kiongozi wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye alikuwa akiizuru Canada na kuhudhuria bungeni, akisema: "Canada inasikitika sana."
Kiongozi huyo wa Ukraine alikuwa miongoni mwa wale waliopigwa picha wakimshangilia Bw Hunka, picha ambayo imekuwa ikitumiwa katika propaganda za Urusi.
Haikun: Taiwan yazindua nyambizi mpya ili kujilinda dhidi ya China

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Taiwan imezindua manowari yake ya kwanza kutengenezwa nchini katika mji wa bandari wa Kaohsiung Taiwan imezindua manowari yake ya kwanza iliotengenezwa nchini humo huku ikiimarisha ulinzi wake dhidi ya shambulio linalowezekana la China.
Rais Tsai Ing-wen aliongoza hafla ya uzinduzi katika mji wa bandari wa Kaohsiung siku ya Alhamisi.
Maafisa wa Marekani wameonya kuwa China inaweza kuwa na uwezo wa kijeshi kufanya uvamizi ndani ya miaka michache ijayo.
Taiwan ni kisiwa kinachojitawala ambacho China inakichukulia kama jimbo lililoasi na imeapa kukirudisha siku moja.
Waangalizi wengi wanaamini kuwa China haitashambulia kisiwa hicho mara moja, na Beijing imesema inatafuta "kuungana tena" kwa amani na Taiwan.
Lakini wakati huo huo imeonya dhidi ya Taiwan kutangaza rasmi uhuru na msaada wowote wa kigeni.
Hatahivyo imeendelea kuweka shinikizo kwenye kisiwa hicho kwa mazoezi yake ya kijeshi katika Mlango-Bahari wa Taiwan, yakiwemo kadhaa yaliyofanywa mwezi huu.
Manowari hiyo yenye thamani ya dola bilioni 1.54 (£1.27bn) inayotumia umeme wa dizeli itafanyiwa majaribio kadhaa na itawasilishwa kwa jeshi la wanamaji kufikia mwisho wa 2024, kulingana na maafisa wa kijeshi.
Unaweza pia kusoma:
- China-Taiwan: Jinsi Beijing inavyobadilisha majibu yake kuhusu kinachofanyika Taiwan
- China yafanya mazoezi ya kushambulia 'maeneo muhimu' Taiwan
Upasuaji salama wa ubongo kwa kutumia Akili Mnemba(AI) inawezekana ndani ya miaka miwili

Upasuaji wa ubongo kwa kutumia akili ya bandia unaweza kufanyika ndani ya miaka miwili, na kuuanya uwe salama na wenye ufanisi zaidi, daktari bingwa wa upasuaji wa neva anasema.
Madaktari wa upasuaji wanaofunzwa wanafanya kazi na teknolojia mpya ya Akili Mnemba (AI), ili kujifunza upasuaji sahihi zaidi wa tundu la ubongo.
Teknolojia mpya Iliyobuniwa katika Chuo Kikuu cha London, inaangazia uvimbe mdogo na miundo muhimu kama vile mishipa ya damu katikati ya ubongo.
Serikali inasema hili linaweza kuwa "badiliko la kweli" kwa huduma ya afya nchini Uingereza.
Changamoto ya upasuaji

Maelezo ya picha, Daktari wa upasuaji anayetumia mkufunzi wa AI kwenye "mgonjwa" bandia Upasuaji wa ubongo ni sahihi na mchungu – na iwapo utafanyika kwa njia isiyofaa unaweza kumuua mgonjwa papo hapo.
Kuepuka kuharibu tezi ya pituitary (Inayodhibiti ukuaji ) yenye ukubwa wa zabibu, iliyopo katikati ya ubongo, ni muhimu. Tezi hii hudhibiti homoni zote za mwili - na kuathiriwa kokote kunaweza kusababisha upofu.
"Iwapo hutaenda mbali zaidi na upasuaji , basi una hatari ya kutoondoa uvimbe wa kutosha," mshauri wa Hospitali ya Taifa ya Neurology na Neurosurgery daktari wa upasuaji wa neva Hani Marcus anasema.
"Na iwapo unafanya upasuaji kwenye eneo kubwa sana, una hatari ya kuharibu miundo hii muhimu sana."
Hisia za viongozi wa Afrika Mashariki baada ya kukubaliwa kuandaa AFCON 2027

Chanzo cha picha, Getty Images
Viongozi wa Afrika Mashariki wamepongeza kutunikiwa hadhi ya kuandaa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), 2027, baada ya ombi la pamoja la Uganda, Tanzania na Kenya kukubaliwa.
Itakuwa mara ya kwanza kwa shindano hili kuu la kandanda barani Afrika kuchezwa katika mataifa matatu kwa wakati mmoja, baada ya lile lililofanyika Ghana na Nigeria kwa wakati mmoja mwaka 2000 na Equatorial Guinea na Gabon mwaka 2012.
‘’Tunashukuru kupata fursa ya kuandaa AFCON 2027 kwa ushirikiano na Kenya na Uganda’’, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenye X (zamani ikitwa Twitter)
‘’Ninawashukuru wote walioshiriki kuhakikisha nchi yetu inapata fursa hii adhimu.’’
Sasa naiagiza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kufanya maandalizi ipasavyo ikiwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa viwanja viwili vipya Dodoma na Arusha kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa’’, aliongeza.
Naye Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema kupokea shindano hilo kutaathiri vyema uchumi wa mataifa hayo.
‘’Nilipata habari njema kwamba ombi letu la pamoja na Kenya na Tanzania la kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 limefanikiwa. Nawashukuru waandaaji kwa kuweka hoja nzuri kwa mataifa ya Afrika Mashariki. Hii itakuza nchi zetu na kuleta athari njema kwa uchumi wa mataifa yetu, hasa sekta ya utalii.’’ Bw Museveni aliandika kwenye X.
Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua pia alipeleka hisia zake kuhusu suala hilo kwenye ukuraza wa X, kuonyesha kufurahishwa kwake na hatua ya kuletwa kwa AFCON Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza tangu Ethiopia iandae shindano hilo mwaka 1976.
‘’ Inafurahisha kupokea taarifa kwamba ombi la pamoja la Kenya, Uganda na Tanzania la kuandaa AFCON 2027 limekubaliwa…na Shirikisho la Soka la Afrika.’’ Alisema Gachagua.
Carabao: Newcastle yailaza Manchester City

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe anasema timu yake ina hamu ya "kupanda nafasi moja bora" kuliko washindi wa pili wa msimu uliopita wa Kombe la Carabao baada ya timu yake kuishinda Manchester City na kufika raundi ya nne ya kampeni hii.
Alexander Isak alifunga bao la ushindi kwa kikosi cha pili cha Newcastle, ambao walipata uhai baada ya mapumziko na kuwashinda City ambao walikuwa wamebadilika kikosi chao.
Newcastle, ambao walipoteza kwa Manchester United katika fainali mwaka jana, walifanya mabadiliko 10 kutoka kwa ushindi wa 8-0 Jumapili dhidi ya Sheffield United na hawakupata kiki katika kipindi cha kwanza kilichotawaliwa na wageni.
Lakini baada ya Bruno Guimaraes na Anthony Gordon kuingia baada ya mapumziko, Magpies ilibadilika, na Isak akifunga bao kufuatia kazi nzuri kutoka kwa Joelinton.
"Tunataka kujaribu na kwenda mbele zaidi kama tunaweza lakini kuna safari ndefu katika hatua hii. Bado tuko pale tunapambana.
"Wakiwa na nidhamu lakini wazembe mbele ya utawala wa City wa kumiliki mpira, vijana wa Howe walikuwa na bahati ya kusawazisha baada ya dakika 45, huku Julian Alvarez akikosa nafasi mbili nzuri.
Pep Guardiola alifanya mabadiliko saba, akimpatia fursa ya kwanza kiungo chipukizi Oscar Bobb miongoni mwao.
Lakini wenyeji walistahili ushindi wao kutokana na mchezo mzuri katika kipindi cha pili.Kwa Guardiola mechi hiyo ilikuwa ya pili katika mechi 38 kwa klabu yake kulazwa katika michuano yote.
Matokeo Mengine
Aston Villa 1. Everton 2
Blackburn 5 Cardiff 2
Bournemouth 2 Stoke 0
Brentford 0 Arsenal 1
Chelsea 1 Brighton 0
Liverpool 3 Leicester 1
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 28.09.2023
