Balozi wa Ufaransa nchini Niger awasili Paris
Balozi wa Ufaransa nchini Niger Sylvain Itté amerejea Paris, kulingana na wizara ya Ulaya na mambo ya nje ya Ufaransa.
Moja kwa moja
Habari za hivi punde, Balozi wa Ufaransa nchini Niger awasili Paris
Balozi wa Ufaransa nchini Niger Sylvain Itté amewasili Paris, kulingana na wizara ya Ulaya na mambo ya nje ya Ufaransa.
"Balozi wetu nchini Niger amerejea Paris leo, kama ilivyoamuliwa na Rais wa Jamhuri siku ya Jumapili. Waziri wa mambo ya Ulaya na mambo ya nje alimpokea huko Quai d'Orsay ili kumshukuru kwa kazi yake pamoja na timu zinazomzunguka katika utumishi wa nchi yetu chini ya hali ngumu", wizara imesema.
Soma zaidi:
- Balozi wa Ufaransa aondoka Niger baada ya mzozo
- Kwa nini mapinduzi ya Niger yanaigusa dunia nzima?
- Kwa nini Marekani haiyaiti mapinduzi ya Niger kuwa ni mapinduzi?
- Mapinduzi Niger: Historia ya mapinduzi manne Niger tangu uhuru
Maelfu watafuta makazi shuleni huku vita vya Sudan vikiendelea

Maelfu ya watu waliolazimishwa kutoroka makazi yao kutokana na vita nchini Sudan wamekuwa wakiishi katika shule ambazo haziko kwenye hali nzuri, gavana wa eneo hilo ameiambia BBC News.
Mapigano ya miezi kadhaa kati ya jeshi la Sudan na Rapid Support Forces yamelazimisha familia 40,000 kukimbilia Darfur Kaskazini, Nimr Abdel, ambaye anasimamia jimbo hilo, amesema.
Tangu mzozo huo uanze mwezi Aprili, Darfur imeshuhudia mapigano mabaya zaidi nchini humo.
Bw Abdel aliiambia idhaa ya BBC ya Sudan Lifeline redio: "Watu wengi waliotoroka makazi yao sasa wanaishi ndani ya shule ambazo haziko katika hali nzuri.
Shule hizi hazina sifa za kuwa vituo vya makazi, kwani huduma muhimu hazipatikani huko.
"Huduma ambazo zinatolewa katika shule hizi, kama vile bafu, zilikuwa mahsusi kwa ajili ya wanafunzi, na idadi yao haikuwa sawia na idadi kubwa ya watu waliohamishwa makazi hayo."
Ikiwa mapigano yataendelea, mamlaka itaangalia kati na kujenga kambi kwa kusudi ya kukidhi hitaji hili.
Soma zaidi:
- Mgogoro wa Sudan: Jinsi watu wanavyozika miili inayoharibika mitaani huko Khartoum
Wanajeshi waokolewa baada ya kambi ya jeshi ya Mali kushambuliwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanajeshi wamehamishwa kutoka kambi ya jeshi kaskazini mwa Mali kufuatia shambulio la watu wenye silaha, jeshi la taifa hilo limesema.
Wanajeshi wa Mali waliwakabili washambuliaji huko Acharane, eneo karibu na mji wa kale wa Timbuktu, taarifa ilisema.
Bado haijabainika iwapo watu hao wenye silaha walikuwa wanamgambo wa Kiislamu au waasi wa Tuareg.
Makundi yote mawili yameongeza mashambulizi yao katika wiki za hivi karibuni - wakati ambapo walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaondoka nchini humo baada ya kuamriwa kuondoka na watawala wa kijeshi wa Mali.
Pia unaweza kusoma:
- Mali: Kipi kifuatacho kwa nchi inayotegemea Wagner kwa usalama wake?
Uingereza yaruhusu kituo cha kwanza cha matumizi ya dawa za kulevya

Maelezo ya picha, Chumba cha matumizi ya dawa za kulevya vya Ureno kiko ndani ya mkakati wa nchi hiyo 'kupunguza madhara' ya dawa za kulevya. Kituo cha kwanza rasmi cha matumizi ya dawa za kulevya nchini Uingereza ikiwa ni pamoja na heroini na kokeini kimeidhinishwa na mamlaka huko Glasgow.
Kituo hicho kinaungwa mkono na serikali ya Scotland kama njia ya kukabiliana na janga la vifo vinavyotokana na dawa za kulevya nchini humo.
Mpango huo wa majaribio utakuwa katika kituo cha afya mwisho wa mashariki wa Glasgow.
Itashuhudia watumiaji wakichukua dawa zao wenyewe chini ya usimamizi wa wataalamu wa afya wenye ujuzi.
Bodi ya Pamoja ya Glasgow, ambayo inaleta pamoja NHS na maafisa wa baraza, iliidhinisha mipango hiyo kwenye mkutano wa mtandaoni Jumatano asubuhi.
Dk Saket Priyadarshi, mkurugenzi msaidizi wa matibabu wa huduma za urejeshaji pombe na dawa za kulevya Glasgow, aliambia mkutano huo, mradi "utapunguza madhara yanayohusiana na dawa za kulevya" kwa watu binafsi na pia kuwapa "fursa za matibabu, matunzo na kupona".
Pia unaweza kusoma:
Azerbaijan yamkamata kiongozi wa zamani wa Nagorno-Karabakh

Chanzo cha picha, STATE BORDER SERVICE OF AZERBAIJAN/HANDOUT VIA REU
Azerbaijan imemkamata kiongozi wa zamani wa Nagorno-Karabakh alipokuwa akijaribu kuondoka katika eneo hilo kuelekea Armenia, maafisa wanasema.
Ruben Vardanyan, mfanyabiashara ambaye aliongoza serikali inayotaka kujitenga kutoka Novemba 2022 hadi Februari, alikuwa miongoni mwa maelfu ya watu wanaojaribu kuondoka.
Kwa jumla, Waarmenia wa kabila 47,115 sasa wamekimbia Nagorno-Karabakh, ambayo ilitekwa na Azerbaijan wiki iliyopita.
Mkewe Bw Vardanyan aliomba usaidizi ili kuhakikisha kuachiliwa kwake salama.
"Ruben amesimama na watu wa Arsakh wakati wa kizuizi cha miezi 10 na ameteseka nao katika mapambano yao ya kuishi," Veronika Zonabend alisema.
Mamlaka yya mpakani ya Azerbaijan ilisema alipelekwa katika mji mkuu, Baku, na kukabidhiwa kwa mashirika mengine ya serikali.
Walipokuwa wakivuka mpaka siku ya Jumanne, maelfu ya Waarmenia wa kabila walikuwa chini ya ukaguzi mkali kutoka kwa Idara ya udhibiti wa mpaka wa Azerbaijan.
Mamlaka ya Azerbaijan ilidai kuwatafuta washukiwa wa "uhalifu wa kivita", na chanzo kimoja cha serikali kiliambia shirika la habari la Agence France Presse kwamba nchi hiyo inakusudia kuomba "msamaha kwa wapiganaji wa Armenia walioweka silaha chini Karabakh".
Soma zaidi:
- Kwa nini India inaiuzia Armenia silaha?
- Nagorno Karabakh: Mambo 5 ya kuyajua kuhusu mgogoro wa tangu enzi ya Soviet
Wakala wa Victor Osimhen atishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Napoli

Chanzo cha picha, Reuters
Wakala wa Victor Osimhen Roberto Calenda ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Napoli baada ya klabu hiyo kumkejeli mshambuliaji huyo kwenye mitandao ya kijamii.
Napoli walishirikisha video kwenye akaunti yao ya TikTok ikimuonyesha mshambuliaji huyo akikosa penalti dhidi ya Bologna, huku sauti iliyosikika kwa juu ikisema ''gimme penalty please".
Video hiyo imeondolewa mtandaoni.
"Tuna haki ya kuchukua hatua za kisheria kumlinda Victor," Calenda aliandika kwenye mtandao wa X.
"Kilichotokea leo kwenye wasifu rasmi wa Napoli katika jukwaa la TikTok hakikubaliki.
"Video ya kumdhihaki Victor iliwekwa kwa umma lakini sasa imefutwa. Ukweli mtupu ambao unasababisha madhara makubwa kwa mchezaji na ni kama kuongeza chumvi kwenye kidonda kwani amekuwa na wakati mgumu katika kipindi kilichopita kati ya madai ya vyombo vya habari na habari za uwongo."
Osimhen alionekana akimhoji meneja Rudi Garcia alipotolewa nje dakika ya 86 katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Bologna.
Mchezaji wa kimataifa wa Nigeria Osimhen alijiunga na Napoli kwa rekodi ya euro milioni 81.3 katika msimu wa joto wa 2020.
Na alikuwa muhimu kuwasaidia kushinda taji la kwanza la Serie A katika miaka 33 msimu uliopita, akifunga mabao 26 katika mechi 32 za ligi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 - ambaye alihusishwa pakubwa na Chelsea na Manchester United msimu huu wa joto - amefunga mabao matatu katika mechi sita msimu huu.
Pia unaweza kusoma:
- Tetesi za soka Ulaya Jumatano 27.09.2023
Habari za hivi punde, Travis King yuko chini ya ulinzi wa Marekani baada ya kufukuzwa Korea Kaskazini

Chanzo cha picha, Reuters
Mwanajeshi wa Marekani Travis King, ambaye alikimbilia Korea Kaskazini mwezi Julai, yuko chini ya ulinzi wa Marekani baada ya kufukuzwa na Pyongyang, maafisa wanasema.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Marekani, King alihamishiwa chini ya ulinzi wa Marekani nchini China.
Mwanajeshi huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa katika ziara ya kuongozwa alipojitenga na kundi hilo na kukimbia kuvuka mpaka.
"Chombo husika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea kimeamua kumfukuza mwanajeshi wa Marekani Travis King, ambaye aliingia kinyume cha sheria katika eneo la jamhuri hiyo, kwa mujibu wa sheria za jamhuri," ilisema.
Alikuwa katika ziara ya kuongozwa ya Eneo lisilo na Jeshi (DMZ), ambalo linatenganisha Korea mbili, wakati aliondoka kwenye kikundi na kukimbia kuvuka mpaka.
Nchi hizo mbili ni kama bado ziko vitani baada ya Vita vya Korea kumalizika na mapigano kusitishwa katika miaka ya 1950.
Makumi ya maelfu ya wanajeshi wa Marekani wamesalia Kusini.
Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya raia wa Marekani ambao waliingia kinyume cha sheria Korea Kaskazini - bila kujumuisha wale waliopatikana na hatia ya uhalifu huko - wameachiliwa ndani ya miezi sita.
King ni mtaalamu wa upelelezi ambaye amekuwa jeshini tangu Januari 2021 na alikuwa Korea Kusini kama sehemu ya zamu yake.
Hapo awali alikuwa ametumikia kifungo cha miezi miwili nchini Korea Kusini kwa mashtaka ya shambulio kabla ya kuachiliwa mnamo Julai 10 na alipaswa kurudishwa nyumbani kuadhibiwa kabla ya kuvuka mpaka hadi Korea Kaskazini.
Soma zaidi:
- Tunachofahamu kuhusu mwanajeshi wa Marekani anayezuiliwa Korea Kaskazini kufikia sasa
- Kimya cha Korea Kaskazini kuhusu mwanajeshi wa Marekani aliyevuka mpaka
Uganda yawasimamisha kazi wafanyakazi 11 kwa tuhuma za uuzaji wa vibali feki vya sokwe

Chanzo cha picha, Reuters
Mamlaka ya wanyamapori nchini Uganda imewasimamisha kazi wafanyikazi wake 11 kwa tuhuma za uuzaji wa vibali feki vya sokwe.
Shirika la serikali, ambalo huuza tikiti kuruhusu watalii kuona sokwe kwa karibu, lilisema limepata hitilafu katika shughuli zake za mtandaoni.
Bashir Hang, msemaji kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Uganda, alisema uwezekano kwamba wafanyakazi na waendeshaji watalii walishirikiana kufanya udanganyifu unachunguzwa.
Shirika hilo liliongeza kuwa bado halijabaini ni pesa ngapi limepoteza kwa tuhuma za ulaghai.
Baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Wanyamapori wanatarajiwa kuhojiwa kuhusu kashfa hiyo, gazeti la serikali la New Vision limesema.
Sokwe huzalisha mapato makubwa ya utalii kwa Uganda, na baadhi ya pesa huenda kwenye shughuli za uhifadhi wa wanyamapori.
Pia unaweza kusoma:
- Utafiti: Binadamu na Sokwe wanaelewa lugha moja
Balozi wa Ufaransa aondoka Niger baada ya mzozo

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Hasira imetokana na Ufaransa kukataa kuitambua serikali mpya ya kijeshi Balozi wa Ufaransa nchini Niger ameondoka nchini humo mwezi mmoja baada ya watawala wa kijeshi kuamuru afukuzwe.
Nchi hizo mbili zilikuwa washirika wa karibu hadi Rais Mohamed Bazoum alipoondolewa madarakani mwezi Julai.
Ufaransa imekataa kuwatambua viongozi wa mapinduzi na imepuuza agizo la kumuondoa mjumbe wake.
Siku ya Jumapili, Rais Emmanuel Macron alisema balozi Sylvain Itté ataondoka ndani ya siku chache.
Pia alisema wanajeshi wote wa Ufaransa wataondoka Niger ifikapo mwisho wa mwaka.
Unaweza pia kusoma:
- Kwa nini mapinduzi ya Niger yanaigusa dunia nzima?
- Kwa nini Marekani haiyaiti mapinduzi ya Niger kuwa ni mapinduzi?
- Mapinduzi Niger: Historia ya mapinduzi manne Niger tangu uhuru
Kenya: Shule yapigwa faini kwa kuchapisha picha za wanafunzi bila idhini
Mdhibiti wa dijitali nchini Kenya ameitoza shule faini ya $31,000 (£25,000) kwa kuchapisha picha za wanafunzi mtandaoni bila idhini ya wazazi wao.
Hii ni hatua ya kwanza ya aina yake kuchukuliwa na Ofisi ya Kamishna wa Ulinzi wa Data.
Klabu ya usiku na kampuni ya mikopo pia imetozwa faini ya $12,500 na $20,000 mtawalia.
Kulingana na mdhibiti, klabu hiyo ilichapisha picha ya mteja kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii bila idhini yake.
Kampuni ya mikopo iliwatishia wateja kupitia simu na ujumbe kwa kutumia taarifa zilizopatikana kutoka kwa wahusika wengine.
Faini hizi zimezua mjadala wa umma kuhusu haki ya faragha, hasa katika vilabu vya pombe na baa.
Baadhi ya taasisi hizo sasa zimechapisha ilani kwamba mtu yeyote anayeingia kwenye eneo lao awe amekubali kupigwa picha, au kurekodiwa bila kulipwa fidia na kwamba wale ambao hawakubaliani na sheria zao hawapaswi kuingia.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa X, mdhibiti huyo alisema ana matumaini kuwa faini hizo zitapeleka ujumbe kwa taasisi wa kufuata sheria za ulinzi wa takwimu za nchi zikiwemo zinazowataka kuomba ridhaa kabla ya kuweka picha za watu mtandaoni.
Marekani yasitisha msaada kwa Gabon kufuatia mapinduzi

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Jeshi la Gabon lilimpindua rais tarehe 30 Agosti Marekani inasitisha msaada wake kwa Gabon kufuatia mapinduzi ya mwezi uliopita.
"Tunasitisha programu fulani za usaidizi wa kigeni ambazo zinanufaisha serikali ya Gabon wakati tukitathmini uingiliaji kati usio wa kikatiba wa wanajeshi wa nchi hiyo," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema katika taarifa yake.
Imesema hatua hiyo ya muda inaendana na hatua zilizochukuliwa na Jumuiya yakikanda ya Afrika ya Kati, Umoja wa Afrika (AU) na washirika wengine wa kimataifa kufuatia mapinduzi hayo.
Uanachama wa Gabon katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (Ecowas) na AU ulisitishwa kufuatia mapinduzi hayo.
Uamuzi wa kusimamisha msaada kwa Gabon utabaki "huku tukitatmnini hali ya mambo nchini humo", Wizara ya Mambo ya Nje ilisema.
Hata hivyo wizara hiyoilisemakuwa inatambua shughuli nchini humo zinaendelea, ikiwa ni pamoja na shughuli za kidiplomasia na kibalozi kuwasaidia raia wa Marekani.
Tarehe 30 Agosti, viongozi wa kijeshi wa Gabon walimpindua Rais Ali Bongo baada tu ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi.
Rais Bongo amekuwa madarakani tangu 2009. Alimrithi babake, Omar Bongo, ambaye alikua rais kwa mara ya kwanza mwaka wa 1967.
Serikali ya Gabon imeahidi kuandaa uchaguzi huru na wa haki lakini haijaweka ratiba.
Waziri mkuu mpya aliyeteuliwa na junta aliambia BBC mapema mwezi huu kwamba nchi hiyo itafanya uchaguzi mpya ndani ya miaka miwili ijayoo
Kenya ina imani polisi wake watamaliza vita vya magenge ya Haiti

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Magenge kwa kiasi kikubwa yamewazidi nguvu polisi nchini Haiti Kenya inasema ina uhakika kutumwa kwa mamia ya polisi wake hadi Haiti kufikia Januari kutamaliza vita vya magenge huko.
Mwaka jana serikali ya Haiti iliomba msaada kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge.
Magenge kwa kiasi kikubwa yamewazidi nguvu polisi na sasa yamedhibiti zaidi ya robo tatu ya mji mkuu.
Hapo awali maafisa wa Kenya walizungumza kuhusu maafisa 1,000 wanaokwenda Haiti kutoa mafunzo kwa polisi wa eneo hilo na kusaidia kulinda mitambo muhimu huko.
Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Alfred Mutua anasema kuwa kitakuwa kikosi cha kuingilia kati kuwapokonya silaha wale aliowaita "majambazi na magenge".
Katika mahojiano na BBC Alfred Mutua alisema polisi wa Kenya watawaachilia raia wa Haiti ambao walikuwa wametekwa nyara na kuwaachia huru wanawake waliokuwa wakibakwa.
Alisema hakutarajia kungekuwa na vurugu nyingi.
Baadhi wameelezea mashaka kuhusu kutuma maafisa umbali wa kilomita 12,000 (maili 7,500) hadi Haiti.
Hasa kwa vile kuna changamoto nyingi za sheria na utulivu nchini Kenya na mashirika ya kutetea haki yamekuwa yakishutumu polisi kwa ukatili ikiwa ni pamoja na mauaji na mateso.
Habari za hivi punde, Moto Iraq: Maharusi wote wawili wapoteza maisha yao - Afisa wa afya
Wanandoa hao wapya wote walipoteza maisha katika moto uliowaka katika karamu ya harusi nchini Iraq, kulingana na Ahmed Dubardani, naibu mkuu wa kurugenzi ya afya ya Ninawi.
Takriban watu 100 wamefariki na wengine 150 kujeruhiwa baada ya moto kuzuka kwenye harusi kaskazini mwa Iraq, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Akizungumza na wanahabari hapo awali katika mkutano na wanahabari, aliongeza kuwa takriban watu hamsini wako katika hali mbaya, na angalau nusu yao wameungua.
"Wengi wa waliojeruhiwa waliungua kabisa. Na wengine asilimia 50 hadi 60 ya miili yao iliungua. Hii si nzuri hata kidogo," alisema.
Aliongeza kuwa wengi wa waliojeruhiwa walikuwa vijana wa kiume na wa kike - hakuna aliyeruhusiwa kuondoka hospitali kufikia sasa.

Chanzo cha picha, AVN
Maelezo ya picha, Wanandoa hao wote walipoteza maisha yao, alisema Ahmed Dubardani, naibu mkuu wa kurugenzi ya afya ya Ninawi Trump alihusika na ulaghai wa kodi, jaji asema katika kesi ya madai ya New York

Chanzo cha picha, Reuters
Donald Trump "mara kwa mara" hakuwasilisha kwa usahihi utajiri wake wa mamia ya mamilioni ya dola kwa benki na bima, jaji wa New York alisema katika uamuzi wake.
Uamuzi huo unasisitiza madai muhimu yaliyotolewa na mwanasheria mkuu wa New York katika kesi yake ya madai dhidi ya rais huyo wa zamani.
"Nyaraka zilizo hapa zina zinadhihirisha wazi ulaghai ambao washtakiwa walitumia katika biashara," hakimu aliandika.
Hili ni pigo kubwa kwa Bw Trump kabla ya kesi hiyo kusilikizwa Jumatatu ijayo.
Wakili wa Bw Trump aliutaja uamuzi wa jaji huyo kuwa "upotovu wa haki" katika taarifa yake Jumanne jioni.
Mwanasheria Mkuu Letitia James alimshtaki Bw Trump Septemba mwaka jana, akimshutumu yeye, wanawe wawili na Shirika la Trump Organization kwa kudanganya kuhusu thamani na mali yake kati ya 2011 na 2021.
Muigizaji wa maili 8 Nashawn Breedlove afariki akiwa na umri wa miaka 46

Chanzo cha picha, PATRICIA A BREEDLOVE
Muigizaji na rapa Nashawn Breedlove, anayejulikana kwa kupigana na Eminem kwenye vita vya rap katika filamu ya 8 Mile, amefariki akiwa na umri wa miaka 46.
Breedlove alicheza kama mpinzani wa kutisha katika Lotto -katika filamu ya 2002, kwa akiigiza maisha ya rapa Eminem, na alionekana kwenye wimbo wa sauti wa filamu ya 2001 The Wash.
Mama yake alithibitisha kifo chake kwenye mtandao wa kijamii siku ya Jumanne.
Alifariki usingizini nyumbani kwake huko New Jersey siku ya Jumapili, TMZ iliripoti.
Rapa Mickey Factz anamkumbuka kama mmoja wa watu wachache "walioshinda Eminem."
"Tutakukosa kwa ukakamavu wako na uchokozi wako," aliongeza katika ujumbe huo uliotumwa kwenye Instagram.
"Hakuna anayeweza kupinga kipaji chake," mama yake aliandika kwenye chapisho la Facebook mnamo Jumanne.
"Kuondoka kwa Nashawn katika ulimwengu huu kumeacha pengo kubwa sana maishani mwangu, ambalo maneno hayawezi kueleza kikamilifu. Siwezi kueleza kwa maneno uchungu na uchungu ninaohisi’’, aliongeza
Wengi wanaomsifu Breedlove walikumbuka tukio lake katika filamu ya 8 Mile, wakati uhusika wake kama Lotto alikichukua nafasi ya B-Rabbit ya Eminem na kuirap, "I feel bad I gotta murder that dude from Leave it to Beaver".
Filamu hii ilipokea sifa kuu na ilikuwa na mafanikio makubwa kibiashara, na kushinda Tuzo la Academy la Wimbo Bora Asili wa Lose Yourself na Eminem.
Shakira atuhumiwa kwa uhalifu wa kodi kwa mara ya pili

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Shakira alishinda tuzo ya mafanikio ya maisha katika Tuzo za Muziki za Video za MTV mapema mwezi huu Shakira alishinda tuzo ya mafanikio ya maisha katika Tuzo za Muziki za Video za MTV mapema mwezi huu
Mwanamuziki wa pop wa Colombia, Shakira amefunguliwa mashtaka ya kukwepa kulipa kodi kwa mara ya pili na serikali ya Uhispania.
Waendesha mashtaka nchini Uhispania wanadai muimbaji huyo aliilaghai serikali ya Euro milioni 6.7 ($7.1m, £5.8m) mwaka wa 2018.
Wanasema hii ilitokea aliposhindwa kutangaza mamilioni ya malipo ya awali aliyopewa katika Ziara yake ya Dunia ya El Dorado, miongoni mwa malipo mengine.
Waendesha mashtaka wa Uhispania walianza uchunguzi wa pili mnamo Julai 2023, lakini walitoa maelezo Jumanne wiki hii.
Mtandao wa Kihispania wa RTVE unasema muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 46 anafahamu mashtaka mapya, lakini shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa timu ya wanasheria ya Shakira huko Miami - anakoishi sasa - bado haijaambiwa kuyahusu.
Badala yake, "walilenga kujiandaa kwa kesi ya miaka ya fedha ya 2012-14, ambayo itaanza Novemba 20," waliliambia shirika la habari la Reuters katika taarifa.
Mashtaka mapya yanatokana na ukweli kwamba mnamo 2018, Shakira alikuwa akiishi Barcelona na nyota wa mpira wa miguu Gerard Pique na kwa hivyo alitakiwa kutoa kodi ya mapato yake yote ya kimataifa alipokuwa huko.
Shakira anakabiliwa na kesi ya uhalifu sita kuhusiana na kodi mjini Barcelona mwezi huu wa Novemba - mashtaka ambayo ameyakanusha.
Mbwa kamanda wa Biden amuuma afisa mwingine wa ujasusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Mbwa wa miaka miwili mwenye cheo cha kamanda wa familia ya Biden aina ya German Shepherd, amemng'ata wakala mwingine wa Huduna za Ujasusi.
Shambulio hilo lilitokea Jumatatu usiku na afisa huyo alitibiwa kwenye eneo la Ikulu Huduma ya Siri ilisema katika taarifa Jumanne.
Hii ni mara ya 11 kwa mbwa huyo kumng'ata mlinzi katika Ikulu ya White House au nyumba ya familia ya Biden.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Kamanda alionekana akibweka wakati Bw Biden anaondoka Ikulu mnamo 25 Juni 2022 Afisa anayehusika na waandishi wa habari wa White House hapo awali alilaumu mashambulio hayo kusababishwa na dhiki ya kuishi katika Ikulu ya White House.
"Kama mnavyojua, jumba la White House linaweza kuwa la kipekee na lenye msongo wa mawazo. Hilo ni jambo ambalo nina uhakika nyote mnaweza kuelewa," alisema Julai.
"Ni la kipekee na lina mfadhaiko kwetu sote. Kwa hivyo unaweza kufikiria kwa mbwa wa familia au wanyama wanaofugwa ndani ya familia inavyokuwa, kwa mapana zaidi."
Kamanda huyo ndiye mdogo wa mbwa aina ya Germany Sheherd wa familia ya Biden. Matukio mengine ya kuumwa na mbwa yalitokea katika nyumba ya rais na mke wa rais huko Delaware.
Moto wa Iraq: Takriban watu 100 wauawa katika karamu ya harusi Nineveh

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mfanyakazi wa huduma za dharura akiokota vifusi kwenye mabaki ya mahali ambapo sherehe ya harusi ilifanyika Takriban watu 100 wamefariki na wengine 150 kujeruhiwa baada ya moto kuzuka kwenye harusi kaskazini mwa Iraq, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Bibi harusi na bwana harusi wanaripotiwa kuwa miongoni mwa waathiriwa, kulingana na vyombo vya habari vya ndani ya nchi hiyo.
Moto huo ulitokea katika wilaya ya Al-Hamdaniya katika mkoa wa Nineveh kaskazini mwa Iraq jioni ya Jumanne.
Bado haijabainika kilichosababisha moto huo, lakini ripoti za mapema zinasema kuwa ulizuka baada ya fataki kuwashwa.
Picha iliyotumwa na shirika la habari la Iraq Nina ilionyesha makumi ya wazima moto wakipambana na moto huo, na picha kutoka kwa waandishi wa habari wa eneo hilo kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha mabaki yaliyoteketea ya jumba la tukio.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Askari na wafanyikazi wa dharura nje ya hospitali kuu ya Al Hamdaniya Walioshuhudia walisema mamia ya watu walikuwa pale wakisherehekea wakati jengo lilipowaka moto mwendo wa saa nne na dakika 45 kwa saa za eneo (19:45 GMT).
"Tuliona moto ukitokea nje ya ukumbi, waliofanikiwa walitoka na wale ambao hawakukwama, hata waliotoka walivunjika," Imad Yohana, 34, ambaye alitoroka. inferno, aliliambia shirkka la habari la Reuters.
Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara, leo ikiwa ni tarehe 27.09.2023
