Wanajeshi wa Burkina Faso wajiunga na wenzao Niger kukabili wanamgambo
Majeshi ya Burkina Faso na Niger yameua idadi isiyojulikana ya wanamgambo katika operesheni za pamoja, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.
Moja kwa moja
Wanajeshi wa Burkina Faso wajiunga na wenzao Niger kukabili wanamgambo

Chanzo cha picha, AFP
Majeshi ya Burkina Faso na Niger yameua idadi isiyojulikana ya wanamgambo katika operesheni za pamoja, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.
Shambulio hilo linawadia wiki moja baada ya bunge la Burkina Faso kuidhinisha kutumwa kwa wanajeshi nchini Niger ili kupambana na uasi wa Kiislamu kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hizo.
Kituo cha Televisheni cha RTB kinachomilikiwa na serikali ya Burkina Faso kilisema Jumapili kwamba uvamizi huo ulianza baada ya wanajeshi kuona "safu ya magaidi" wakiondoka Niger kuelekea Burkina Faso.
Vikosi vya pamoja "viliwazuia washambuliaji hawa wawili wawili kwenye pikipiki 100 na kuharibu vifaa vyao vingi" katika eneo la Kantchari mashariki mwa Burkina Faso, kituo kiliongeza.
Mapema mwezi huu, Burkina Faso, Niger na Mali zilianzisha mkataba wa ulinzi, uliopewa jina la Muungano wa Nchi za Sahel, kwa nia ya kusaidiana dhidi ya uasi wowote wa kutumia silaha au uvamizi wa nje.
Pia unaweza kusoma:
- Mali, Burkina Faso kutuma ujumbe nchini Niger
Ufaransa yageukia kipindi cha TV cha Uingereza 'Sex Education' kwa elimu ya ngono

Chanzo cha picha, SAMUEL TAYLOR/NETFLIX
Shirika la upangaji uzazi la Ufaransa limeanzisha kampeni ya kuwahimiza vijana kuzungumza kuhusu ngono, iliyochochewa na kipindi maarufu cha TV cha Uingereza kwa Elimu ya Ngono.
Le Planning Familial ilisema inatangaza nambari yake ya usaidizi bila malipo na Netflix kama sehemu ya "vita vyake vya kufikia elimu ya ngono kwa wote"
Mabango yanaelezea maswali yaliyochochewa na kipindi hicho yanayoulizwa na vijana wa miaka 15-25.
Kipindi cha nne na mwisho cha mchezo wa kuigiza wa vichekesho kilizinduliwa kwenye Netflix wiki iliyopita.
Kipindi hicho kimesifiwa sana kwa uaminifu wake, utofauti na uwakilishi wa masomo magumu.
Nchini Ufaransa, elimu ya ngono ilifanywa kuwa ya lazima mwaka 2001. Lakini Le Planning Familial inasema vijana wana maswali na majibu kidogo sana.
Shirika hilo lilisema ushirikiano huo unawadia "wakati ambapo upatikanaji wa habari za kuaminika na za kipekee kuhusu ngono uko hatarini".
Sarah Durocher, rais wa Le Planning Familial, alisema kipindi hicho kimekuwa chanzo cha habari na msukumo katika suala la maswali ambayo vijana walikuwa wakiuliza kupitia huduma yao.
Soma zaidi:
Mwanamume ashtakiwa kwa kuwapiga watoto wake watatu hadi kufa

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Polisi wanasema mwanamume huyo anadai kuwa na historia ya ugonjwa wa akili - na hakuweza kuvumilia watoto wake wakilia Polisi nchini Thailand wamemshtaki mwanamume mmoja kwa kumpiga hadi kumuua bintiye wa miaka miwili na wanawe wawili wachanga wakiume.
Wanashuku kuwa Songsak Songsaeng pia aliwaua watoto wengine wawili wa kiume kutoka kwa ndoa yao ya awali.
Mashtaka hayo yanafuatia kugunduliwa wiki iliyopita kwa mwili wa msichana wa miaka miwili uliozikwa chini ya sakafu ya jikoni.
Polisi wanasema Bw Songsak anadai kuwa na historia ya ugonjwa wa akili - na kwamba aliwaua watoto wake kwa sababu hakuweza kuvumilia sauti ya kilio chao.
Mkewe pia ameshtakiwa kwa kifo cha binti yao wa miaka miwili.
Na mke wake wa zamani ameshtakiwa kwa vifo vya wavulana hao wawili.
Wote watatu wamekamatwa. Bw Songsak ameoa mara nne.
Polisi walitahadharishwa kwa mara ya kwanza kuhusu uwezekano wa kisa cha unyanyasaji wa nyumbani katika wilaya ya Bang Khen mjini Bangkok mapema mwezi huu.
Majirani wa Bw Songsak waliripoti kuwa binti zake wawili, wenye umri wa miaka 12 na minne, walikuwa wakidhulumiwa kimwili.
Polisi waliwaokoa binti hao wawili walipokuwa nyumbani peke yao.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 aliwaambia polisi kwamba wazazi wao walimpiga dadake mwenye umri wa miaka miwili, jambo ambalo lilisababisha kifo chake.
Pia alisaidia polisi kufuatilia mwili huo hadi ulipozikwa chini ya sakafu ya jikoni kaskazini-magharibi mwa Thailand wiki iliyopita.
Polisi wa Thailand pia wamemshtaki Bw Songsak kwa mauaji ya wana wengine wawili wa kiume aliokuwa nao na mke wake wa tatu baada ya DNA yake kufanana na ya watoto wawili wachanga, ambao miili yao ilifukuliwa miaka 10 iliyopita.
Mkewe wa tatu alisema kuwa aliwaua wana wao wachanga wanne na kuwaonyesha polisi mahali ambapo wawili walizikwa.
Polisi wanaamini kwamba wengine wawili huenda walizikwa chini ya eneo ambalo sasa kipo kituo cha mafuta.
Pia unaweza kusoma:
- India: Watuhumia wawili wanazuiliwa kwa kuwaua watoto waliofanya 'haja kubwa hadharani'
Wanamgambo wa Al-Shabab wauawa katika uvamizi baada ya bomu la lori - Somalia

Chanzo cha picha, Waziri wa Ulinzi wa Marekani/X
Serikali ya Somalia inasema kuwa vikosi vyake vimewaua wanamgambo wengi wa al-Shabab siku moja tu baada ya bomu lililotegwa kwenye lori kuua takriban watu 10 katika mji wa kati wa Beledweyne.
Naibu Waziri wa Habari Abdirahman Al-Adalah anasema jeshi la Somalia na wapiganaji wa eneo hilo walishambulia kambi ya wanamgambo katika kijiji cha Caad katika jimbo la Galmudug.
Idadi ya wapiganaji wa al-Shabab waliouawa haikuweza kuthibitishwa mara moja na kundi hilo halijatoa tamko lolote kuhusu madai ya serikali.
Serikali pia inasema vikosi vyake vimechukua tena vijiji kutoka kwa wanajihadi hao katika mkoa wa Hiiraan magharibi.
Haya yanajiri wakati Rais Hassan Sheikh Mohamud alipokutana na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin nchini Djibouti kujadili mapambano dhidi ya kundi hilo lenye uhusiano na al-Qaeda, ambalo limeendesha uasi nchini Somalia kwa zaidi ya miaka 15.
Katika miezi ya hivi karibuni, serikali ya Somalia imezidisha kampeni yake ya kijeshi dhidi ya al-Shabab lakini hivi karibuni imekabiliwa na vikwazo katika mapigano katikati mwa Somalia.
Somalia inapokea msaada wa kijeshi, kibinadamu na mafunzo kutoka kwa Marekani, ambayo vikosi vyake pia vinasaidia wanajeshi wa Somalia kwa kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya al-Shabab.
Bw Austin yuko katika ziara ya mataifa matatu barani humo.Tayari amezuru Djibouti, ambapo alikutana na Rais Ismail Omar Guelleh na kujadili usalama wa kikanda.
Anatarajiwa kufika katika mji mkuu wa Kenya siku ya Jumatatu kutia saini makubaliano ya ulinzi na kisha kuhitimisha ziara yake nchini Angola.
Mapigano makali yaripotiwa katika mji wa kihistoria wa Ethiopia

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Wanamgambo wa eneo hilo wanaojulikana kama Fano wamekuwa wakipigana na vikosi vya serikali katika mji wa kihistoria wa Gondar (Picha kutoka maktaba) Mapigano yameendelea kuripotiwa katika eneo lenye utulivu la Amhara nchini Ethiopia kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa eneo hilo huku mji wa kihistoria wa Gondar ukishuhudia mapigano makali mijini siku ya Jumapili.
Wanamgambo wa eneo hilo wanaojulikana kwa jina la Fano waliingia katika jiji hilo ambalo ni mojawapo ya miji mikubwa zaidi katika eneo hilo na kusababisha makabiliano makali na jeshi.
Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Facebook wa Jeshi la Ulinzi la Taifa la Ethiopia (ENDF) ilithibitisha mapigano hayo na kuongeza kuwa vikosi vya usalama vya serikali vilizuia mashambulizi ya wanamgambo yaliosababisha vifo vya zaidi ya watu 50.
Mapigano pia yanaripotiwa katika maeneo mengine mengi katika eneo hilo huku wanaharakati na vyombo vya habari wenye kuhusishwa na wanamgambo wakidai kupata udhibiti wa baadhi ya maeneo na kukamata makumi ya wanajeshi.
BBC haijaweza kuthibitisha kwa uhuru madai hayo.
Viunga vya Lalibela, mji mwingine katika mkoa huo ambao ni nyumbani kwa makanisa maarufu, ulishuhudia vurugu wiki iliyopita ambazo zilijumuisha silaha nzito.
Mashambulizi mengi ya ndege zisizo na rubani yameripotiwa katika wiki za hivi karibuni katika maeneo kadhaa.
Kongamano la kila mwaka la ngazi ya juu la amani lililopangwa kufanyika mwezi Oktoba katika mji mkuu wa mkoa huo, Bahir Dar, limetangaza kuahirisha mkutano wake hadi Aprili mwaka ujao likisema ni kutokana na "hali zisizotarajiwa".
Kucheleweshwa kwa mkutano huo, ambao washirika wake ni pamoja na Umoja wa Afrika na UN, kunaweza kuhusishwa na ukosefu wa usalama katika eneo hilo.
Wakati huo huo shirika huru la kutetea haki za binadamu, Baraza la Haki za Kibinadamu la Ethiopia, limeshutumu mamlaka kwa kuendelea kukamata watu kiholela katika mji mkuu, Addis Ababa, ambao ulianza baada ya hali ya hatari kutangazwa mwezi Agosti kukabiliana na ghasia huko Amhara.
Soma zaidi:
- Kwa nini wanamgambo wa Amhara nchini Ethiopia wanapambana na jeshi?
Messina Denaro: Kiongozi maarufu wa mafia Italia afariki dunia

Chanzo cha picha, Reuters
Messina Denaro: Kiongozi maarufu wa mafia Italia afariki dunia
Kiongozi wa mafia wa Italia Matteo Messina Denaro, ambaye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakisakwa zaidi nchini humo hadi alipokamatwa mapema mwaka huu, amefariki dunia.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 61 alidhaniwa kuwa kiongozi wakundi maarufu la mafia na alitoroka kwa miaka 30 kabla ya kukamatwa na kuzuiliwa mnamo mwezi Januari.
Alikuwa akitibiwa saratani wakati wa kukamatwa kwake na alihamishwa kutoka jela hadi hospitali mwezi uliopita.
Denaro alidhaniwa kuhusika na mauaji mengi.
Alishtakiwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela bila kuwepo mahakamani mwaka 2002 kwa makosa ya jinai ikiwa ni pamoja na kuhusika katika mauaji ya mwaka 1992 ya waendesha mashtaka waliopinga kundi lao Giovanni Falcone na Paolo Borsellino na aliwahi kujigamba kuwa anaweza "kujaza kaburi" na waathiriwa wake.
Pia aliendesha shughuli za ulaghai, utupaji taka kwa njia haramu, utakatishaji fedha na ulanguzi wa dawa za kulevya kwa kundi la uhalifu uliopangwa la Cosa Nostra.
Ingawa alikuwa mtoro tangu 1993, Messina Denaro alidhaniwa kuwa bado alikuwa akitoa maagizo kwa wasaidizi wake kutoka maeneo mbalimbali ya siri.
Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, alipoteza fahamu siku ya Ijumaa katika hospitali moja katikati mwa jiji la Italia la L'Aquila, baada ya kuomba asipewe matibabu yoyote ya kulazimishwa.
Soma zaidi:
- Video: Tazama wakati bosi wa mafia Matteo Messina Denaro alipokamatwa
- Messina Denaro: Kiongozi wa 'Mafia' aliyeitisha serikali kwa ukatili wake
Hisia kali kuhusu pendekezo la kurefusha muhula wa rais wa Kenya

Chanzo cha picha, Reuters
Seneta mmoja ambaye ni mwanachama wa muungano unaotawala nchini Kenya amependekeza kuongezwa kwa ukomo wa muhula wa urais kutoka miaka mitano hadi saba na hivyo kuzua hisia kali nchini humo.
Seneta wa Nandi Samson Cherargei anasema Rais William Ruto, ambaye amekuwa afisini kwa takriban mwaka mmoja, huenda akakosa muda wa kutosha kutekeleza manifesto yake ya kampeni.
Hata hivyo, pendekezo hilo limezua hisia kali miongoni mwa baadhi ya Wakenya huku upinzani ukishutumu serikali kwa kupanga njama ya kuondoa ukomo wa mihula ya urais.
"Inafaa kwa kweli ipunguzwe hadi miaka minne kila muhula .Hii ndiyo njia pekee ya uhakika ya kuleta uwiano wa kitaifa na kuzuia maslahi binafsi kujikita wenyewe, hivyo kuruhusu utii wa katiba kutekelezwa kikamilifu," alisema. Mtumiaji wa X .
"Iwapo kiongozi yeyote hawezi kutekeleza manifesto yake katika kipindi cha miaka 10, kuna haja gani ya kuongeza minne zaidi?"mtumiaji mwingine alishangaa.
Novemba mwaka jana, Rais Ruto alitupilia mbali pendekezo la mbunge mwingine wa UDA la kuondoa ukomo wa mihula ya urais nchini.
Katiba ya Kenya imeweka ukomo wa mihula miwili ya urais na mabadiliko yoyote yatahitaji kura ya maoni.
Somaliland yaapuuzilia mbali pendekezo la Uganda la mazungumzo ya kuungana na Somalia

Chanzo cha picha, Reuters
Somaliland imesema "haina mpango wa mazungumzo kujadili umoja" baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kutoa pendekezo la kuwa mpatanishi kati ya nchi inayojiita jamhuri na serikali ya shirikisho ya Somalia.
Rais Museveni siku ya Jumamosi alisema "amekubali kuchukua jukumu la mratibu wa amani kati maeneo hayo mawili " baada ya kukutana na mjumbe wa serikali ya Somaliland katika mji wa Entebbe nchini Uganda.
Alisema Uganda haikuunga mkono kujitenga kwa jamhuri ya Somaliland "kwa sababu kimkakati, ni makosa".
Lakini katika taarifa,wizara ya mambo ya nje ya Somaliland ilisema kuwa mazungumzo yoyote na serikali mjini Mogadishu"haitajadili umoja, lakini jinsi nchi mbili zilizoungana hapo awali zinaweza kusonga mbele kila moja kwa njia tofauti".
"Kwa hiyo, Jamhuri ya Somaliland kwa mara nyingine tena inathibitisha kwa Umoja wa Afrika na jumuiya nyingine ya kimataifa kwamba haina mpango wa mazungumzo ya kujadili umoja na Somalia", iliongeza.
Somaliland ilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991 na tangu wakati huo imekuwa ikitafuta kutambuliwa kimataifa bila mafanikio.
Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yamekuwa yakiendelea kwa miaka, na majadiliano kuanzia usimamizi wa anga na harakati za kuvuka mpaka hadi mahitaji ya Somaliland ya kutambuliwa kama nchi huru.
Rais wa zamani wa Zambia apigwa marufuku kufanya mazoezi hadharani

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Polisi walitaja mazoezi ya asubuhi ya Edgar Lungu kama harakati za kisiasa Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu, ameonywa dhidi ya matukio yake ya kukimbia hadharani, huku polisi wakielezea mazoezi yake kama "harakati za kisiasa".
Katika taarifa yake polisi ilisema vikao vya mazoezi vya Bw Lungu huku akisindikizwa na wanachama wa chama chake cha Patriotic Front (PF) na bila maafisa wake wa usalama vimefikia kiwango cha kuwa "kusanyiko lisilo halali".
Mkuu huyo wa zamani wa nchi aliamriwa kuwaarifu polisi mapema wakati wa kupanga mazoezi yake katika siku zijazo "kuhakikisha usalama wa umma na usimamizi wa trafiki".
"Bw Lungu anapaswa kuzingatia kikamilifu itifaki za usalama na ajiepushe na aina yoyote ya harakati za kisiasa," msemaji wa polisi Rae Hamoonga alisema.
Haya yanajiri siku chache baada ya Bw Lungu kupeleka serikali mahakamani baada ya kudaiwa kumzuia kusafiri kwenda Korea Kusini kwa mkutano. Baadaye aliondoa kesi hiyo mahakamani.
Baada ya kuwa mamlakani kwa miaka sita Bw Lungu alishindwa katika uchaguzi wa urais wa 2021 na Hakainde Hichilema.
Anaaminiwa kuwa anapanga kurejea katika uchaguzi wa 2026.
Kwa picha: Hoteli iliyoharibiwa kwa mashambulizi ya Urusi karibu na kituo cha bahari eneo la Odessa

Chanzo cha picha, t.me/OdessaDumskayaNet

Chanzo cha picha, t.me/OdessaDumskayaNet

Chanzo cha picha, t.me/OdessaDumskayaNet

Chanzo cha picha, t.me/SJTF_Odes
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Vita vya Ukraine: Urusi yaishambulia Odessa kwa makombora na ndege zisizokuwa na rubani

Chanzo cha picha, t.me/SJTF_Odes
Maelezo ya picha, Jengo la kituo cha baharini huko Odessa lilipata uharibifu mkubwa Jeshi la Urusi limefanya mashambulizi dhidi ya eneo la Odessa kwa ndege 19 zisizo na rubani na makombora mawili ,vyombo vya habari vya Ukraine viliripoti.
Aidha, silaha za Calibers 12 zilizifyatuliwa katika mikoa mbalimbali ya Ukraine.
Miundombinu ya bandari ilimeharibiwa kufuatia mashambulizi hayo.
Vikosi vya ulinzi vya Kusini mwa Urusi vilisema katika eneo la Onyxes waliharibu maghala ya nafaka, wakitoa picha zinazoonyesha athari za mashambulio hayo.
"Hoteli katika kituo cha baharini cha Odessa ilikuwa ukumbusho muhimu na wa kushangaza kwa kila mtu ambaye amewahi kufika katika jiji letu.leo Urusi iliiharibu,” Huduma ya Dharura ya Serikali ilisema.
Kulingana na mkuu wa utawala wa kijeshi wa mkoa, Oleg Kiper, ghala na nyumba ya kibinafsi katika mkoa wa Odessa pia viliharibiwa.
Raia mmoja mwanamke pia alijeruhiwa baada ya kuangukiwa na vifusi vya majengo.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Vita vya Ukraine: Mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani yapiga Kursk na maeneo mengine ya Urusi
Magavana wa mikoa ya Kursk na Bryansk wametangaza mapema leo asubuhi mashambulizi ya ndege zisizo na rubani; taarifa zao baadaye zilinakiliwa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, bila kutoa, kama kawaida, maelezo yoyote.
"Mifumo ya ulinzi wa anga ilinasa magari mawili ya anga ya Ukraine ambayo hayakuwa na rubani katika eneo la Kursk, na UAV mbili zaidi za Kiukreni ziliharibiwa katika eneo la mkoa wa Bryansk," ripoti ya wizara hiyo inasema.
Gavana wa Bryansk Alexander Bogomaz alifafanua hapo awali kwamba ndege mbili zisizo na rubani zilidunguliwa katika wilaya ya Surazhsky, "hakukuwa na majeruhi au uharibifu."
Mkuu wa mkoa wa Kursk, Roman Starovoit, aliripoti kwenye chaneli yake ya telegraph baada ya saa saba asubuhi kuhusu droni mbili - moja ilianguka katikati ya Kursk, nyingine nje kidogo ya jiji.
Katika tukio la kwanza, kulingana na gavana, "ulinzi wa anga ulifanya kazi"; kuhusiana na tukio la piili, Starovoit hakutaja ulinzi wa anga.
Katika mkoa wa Kursk, droni iliyoanguka ilisababisha uharibifu mkubwa wa kkatika jengo la ghorofa, na "kulikuwa na uharibifu katika makazi kadhaa ya kibinafsi na paa la jengo la utawala."
Mkuu wa mkoa hakuandika hili ni jengo la utawala la aina gani. Siku moja kabla, Kursk ilishambuliwa angalau mara mbili na droni, na uharibifu wa jengo la utawala pia uliripotiwa. Vyanzo vya Ukraine vilisema , ndege isiyo na rubani ilishambulia kiwanda cha kusafisha mafuta karibu na uwanja wa ndege.
Wakuu wa mkoa wa Tula pia waliripoti kwamba shambulio la UAV juu ya eneo la mkoa wa Tula lilizuiwa usiku uliopita; usiku, vizuizi vya ndege viliwekwa tena kwenye viwanja vya ndege vya Moscow.
Asubuhi, Wizara ya Ulinzi pia iliripoti ndege nne zisizo na rubani za Ukraine zilizotunguliwa kwenye Bahari Nyeusi na katika eneo la Crimea lililokaliwa Urusi.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
'Ninataka kuwatia moyo' – Ndayishimiye kuhusu 'uvumi' wa Mapinduzi ya serikali

Chanzo cha picha, NTARE RUSHATSI
Maelezo ya picha, Rais Ndayishimiye aliwasili Burundi Jumanne usiku baada ya wiki ziara ya siku mbili katika mataifa ya Cuba na Marekani Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi, amekanusha uvumi kuhusu mapinduzi nchini mwake alipokuwa ziarani katika mataifa ya kigeni kwa muda wa wiki mbili.
Kuanzia tarehe 10 mwezi huu wa Julai (9) nimefurahi kwamba alikwenda Havana, Cuba kwa mkutano wa G77+China na kisha akaenda New York kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Chini ya wiki moja baada ya kuondoka kwake, tetesi zilienea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kupinduliwa kwa userikali yake, uvumi ambao haujulikani ulitoka wapi.
Katika hotuba yake alipofika nchini Jumanne, Rais Ndayishimiye alisema: “Unaona wanasema ‘Waburundi huacha kulima lakini hawaachi kuongea’, ambapo wanaweza kusema naweza kuwazuia kufanya kazi na wote wanakaa kwenye uvumi , halafu mnakaa na kuwapiga uvumi, kisha wanaacha kufanya kazi na kufa njaa hadi kesho.
Ndayishimiye alisema kuwa uvumi huu uliletwa na wale ambao siku zote wanataka "kuichafua Burundi kwa sababu wanaona ina sauti tena duniani".
Alisema, “Kwa hiyo hao ndio utawakuta wakisema ‘kwa hiyo tufanye nini? Nitaudanganya walimwengu yale ambayo huwa tunawadanganya hata kama ni uongo kwao, tuwavunje mioyo ya watu wa Burundi."
Mbali na na kile kilichosemwa na Rais Ndayishimiye, Jumatatu Wizara ya Ulinzi na Usalama iliyoa ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X kulaani uvumi huo ulioanza kuonekana baada ya wiki moja.

Chanzo cha picha, RTNB
Aliongeza kusema kuwa “…Ninataka kuwatia moyo kwani mkiendelea na hayo, mkisikiliza hayo kesho tutakuwa na njaa tukiendelea kukaa...”
Burundi ni mojawapo ya nchi zenye historia ya mapinduzi mengi zaidi barani Afrika - imekumbwa na mapinduzi 11 kwa jumla.
Unaweza pia kusoma:
- 'Afrika mashariki inamaslahi zaidi DRC kuliko UN'- Evariste Ndayishimiye
- Evariste Ndayishimiye: Mfahamu rais wa Burundi
Msichana mweusi anyimwa medali Ireland huku wenzake wazungu wakituzwa

Chanzo cha picha, Twitter
Shirika la michezo ya viungo nchini Ireland limeingia kwenye mzozo wa ubaguzi wa rangi baada ya video kuonyesha mshindani mchanga mweusi akinyimwa medali huku wenzake wazungu wakipewa kila mmoja wao.
Bingwa wa Olimpiki nchini Marekani Simone Biles alilaani kisa hicho cha 'kuhuzunisha' na kusema alikuwa ametuma video ya kumuunga mkono msichana huyo mdogo baada ya wazazi wake kuwasiliana naye.
Mchezaji huyo wa Timu ya Marekani alikuwa miongoni mwa alama za mtandaoni zilizolaani kitendo cha afisa huyo, akiandika kwenye X:
'Hakuna nafasi ya ubaguzi wa rangi katika mchezo wowote hata kidogo!!!!'
Video hiyo iliyochukuliwa Machi mwaka jana, inaonyesha wachezaji wa mazoezi ya viungo wakisubiri tuzo zao, huku msichana mdogo akisubiri medali yake kwa shauku kabla ya kunyimwa.
Baada ya kuonekana tena kwa picha za tukio hilo kusambaa mitandaoni wiki hii, Shirika la michezo ya viungo nchini Ireland liliomba radhi kwa umma kwa tukio hilo, baada ya wazazi wa msichana huyo kusema kuwa kitendo hicho cha kukerwa kilitokana na ubaguzi wa rangi.
Shirika la michezo la Ireland lilidai kuwa suala hilo lilitatuliwa mwezi Agosti, lakini mamake msichana huyo amekanusha hilo, akidai kuwa familia hiyo haikupokea msamaha.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Mwanaume ashambuliwa na fahali hadi kufa kwenye tamasha la Uhispania

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Matukio ya mbio za mafahali kama hili San Sebastian bado ni maarufu sana nchini Uhispania Mwanamume mmoja amefariki na rafiki yake kujeruhiwa wakati wa tamasha la mbio za mafahali mashariki mwa Uhispania, mamlaka inasema.
Mwanamume huyo, mwenye umri wa miaka 61, alipigwa ubavuni mwake na ng’ombe wakati wa hafla hiyo katika mji wa Pobla de Farnals katika eneo la Valencia siku ya Jumamosi. Alifanyiwa upasuaji wa dharura lakini alifariki Jumapili.
Rafiki yake, mwenye umri wa miaka 63, aliyeshambuliwa kwenye miguu yote miwili na fahali mmoja alitibiwa na sasa yuko katika hali nzuri hospitalini.
Vifo na majeraha wakati wa matamasha ya mbio za mafahali nchini Uhispania sio kawaida.
Kuna mamia ya matukio kama haya - ambapo mafahali hutolewa kwenye barabara za jiji huku watu wakikimbia mbele yao - kote Uhispania kila mwaka.
Mashirika ya kutetea haki za wanyama kwa muda mrefu yamekuwa yakilalamikia hatari hiyo kwa umma pamoja na wanyama.
Lakini matukio haya ya kila mwaka yameendelea kuwa maarufu.
Msimu wa mbio za mafahali hutoa huboresha sana uchumi wa Valencia.
Utafiti wa 2019 uligundua kuwa mbio hizi zilisaidia kubuni ajira 3,000 na kuingiza pato la euro milioni 300. Karibu matukio kama haya 10,000 hufanyika kila mwaka.
Vita vya Ukraine: Msimamo wa Beijing juu ya vita unapingana na kanuni za China – Kamishna wa EU

Maelezo ya picha, Valdis Dombrovskis, Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya na Kamishna wa Biashara wa EU. Msimamo wa China juu ya vita nchini Ukraine una athari mbaya kwa sura ya nchi, na kusita kwa Beijing kulaani uvamizi wa Urusi hubeba hatari kwa sifa, alisema Valdis Dombrovskis, Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya na Kamishna wa Biashara wa EU, ambaye anatembelea China.
"Uadilifu wa nchi daima umekuwa kanuni muhimu ya diplomasia ya kimataifa kwa China.
Vita vilivyoanzishwa na Urusi ni ukiukaji wa wazi wa kanuni hii, AFP inamnukuu Dombrovskis akisema huko Beijing. "China imekuwa ikisisitizia kila nchi kuwa huru kuchagua njia yake ya maendeleo."
"Kwa hivyo ni vigumu sana kwetu kuelewa msimamo wa China kuhusu vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, kwa kuwa inakiuka kanuni za msingi za China yenyewe."
Mwezi Machi, Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara rasmi nchini Urusi na kusema kuwa uhusiano kati ya Moscow na Beijing unaingia katika zama mpya. Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa kufanya ziara nchini China mwezi Oktoba.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Mapinduzi ya Niger: Macron asema Ufaransa kuondoa wanajeshi na balozi wake

Chanzo cha picha, Reuters
Rais Emmanuel Macron amesema Ufaransa itamuondoa balozi wake na kusitisha ushirikiano wote wa kijeshi na Niger kufuatia mapinduzi.
"Ufaransa imeamua kumuondoa balozi wake. Katika saa zijazo balozi wetu na wanadiplomasia kadhaa watarejea Ufaransa," Bw Macron alisema.
Aliongeza kuwa ushirikiano wa kijeshi "umekwisha" na wanajeshi wa Ufaransa wataondoka katika "miezi ijayo".
Jeshi la Junta ambalo lilichukua mamlaka nchini Niger mwezi Julai lilikaribisha hatua hiyo.
"Jumapili hii tunasherehekea hatua mpya kuelekea uhuru wa Niger," junta ilisema, katika taarifa iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP.
Kuna takriban wanajeshi 1,500 wa Ufaransa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi isiyo na bandari. Uamuzi huo wa Paris unafuatia miezi kadhaa ya chuki na maandamano dhidi ya uwepo wa Wafaransa nchini humo, na maandamano ya mara kwa mara katika mji mkuu wa Niamey.
Hatua hiyo ni pigo kubwa kwa operesheni za Ufaransa dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu katika eneo pana la Sahel na ushawishi wa Paris huko. Lakini Bw Macron alisema Ufaransa "haitashikiliwa mateka na waasi," akizungumza na vituo vya televisheni vya TF1 na France 2 vya Ufaransa.
Bw Macron alisema bado anamchukulia Rais aliyeondolewa madarakani wa Niger, Mohamed Bazoum, ambaye kwa sasa anashikiliwa mfungwa na viongozi wa mapinduzi, kama "mamlaka halali pekee" ya nchi na amemfahamisha kuhusu uamuzi wake. Alimtaja rais aliyeondolewa madarakani kuwa "mateka".
"Alilengwa na mapinduzi haya kwa sababu alikuwa akifanya mageuzi ya ujasiri na kwa sababu kulikuwa na utatuzi wa alama za kikabila na woga mwingi wa kisiasa," alisema.
Niger ni moja ya makoloni kadhaa ya zamani ya Ufaransa huko Afrika Magharibi ambapo jeshi limechukua udhibiti hivi karibuni - inafuata Burkina Faso, Guinea, Mali na Chad. Mapinduzi ya hivi punde yalikuwa nchini Gabon mwezi Agosti.
Vita dhidi ya Ufaransa vimeshamiri katika eneo hilo katika miaka ya hivi karibuni, huku wanasiasa wengi wa eneo hilo wakiishutumu Paris kwa kutekeleza sera za ukoloni mamboleo - mashtaka ambayo yamekanushwa na Ufaransa.
Pia kumekuwa na wasiwasi katika nchi za Magharibi juu ya kuongezeka kwa nafasi katika kundi la mamluki la Sahel la Russia la Wagner.
Inashutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu na imekuwa ikisaidia baadhi ya tawala mpya za kijeshi.
Jumuiya ya Kiuchumi ya Kikanda ya Afrika Magharibi (Ecowas), inayoungwa mkono na Ufaransa, imetishia kuingilia kati kijeshi nchini Niger ili kumrejesha kazini Bw Bazoum. Lakini hadi sasa haijachukua hatua.
Sheria za magari ya umeme zinaweza kuwagharimu watengenezaji mabilioni

Chanzo cha picha, Getty Images
Sheria mpya za biashara baada ya kuondoka kwa Uingereza katika Muungano wa Ulaya au Brexit, zinazohusu magari ya umeme zinaweza kuwagharimu watengenezaji wa Ulaya pauni bilioni 3.75 katika miaka mitatu ijayo, shirika la tasnia limesema.
Sheria hizo zinakusudiwa kuhakikisha kuwa magari ya umeme yanayozalishwa na Umoja wa Ulaya yanatengenezwa kwa kutumia vipuli vingi vinavyotoka ndani.
Lakini watengenezaji wa pande zote wanasema hawako tayari.
Jumuiya ya Watengenezaji Magari ya Ulaya (ACEA) pia ilionya kua hatua hizo zinaweza kupunguza mapato kutoka kwenye viwanda vya EU kwa magari 480,000.Na walisema wateja watalipia gharama.
Tatizo kuu liko katika kile kinachoitwa "sheria za asili" ambazo zinaanza kutumika Januari. Zinatumika kwa usafirishaji wa magari kote chini ya masharti ya mkataba wa Brexit, Mkataba wa Biashara na Ushirikiano wa Uingereza na EU.
Watahakikisha kwamba magari ya umeme yatahitaji kuwa na betri zinazozalishwa nchini Uingereza au EU.
Magari ambayo hayatimizi vigezo yatatozwa ushuru wa 10% yanaposafirishwa kupitia vituo vya safari za magari katika pande zote mbili.
Kosovo na Serbia zazozana juu ya makabiliano ya bunduki katika nyumba ya watawa

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Polisi wa Kosovo walifunga eneo karibu na nyumba ya watawa iliyopo katika eneo la Banjska Kosovo na Serbia zinazozana katika mzozo mbaya kati ya washambuliaji wa kabila la Waserb na polisi kaskazini mwa Kosovo.
Polisi mmoja na watu watatu wenye silaha waliuawa wakati shambulio dhidi ya nyumba ya watawa wa dini ya Orthodox ya Serbia katika kijiji cha Banjska siku ya Jumapili.
Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti aliishutumu Serbia kwa kuunga mkono kundi hilo lenye silaha.
Rais wa Serbia Aleksandar Vucic alisema maafisa wa Kosovo waliwajibika kwa vifo hivyo.
Alisema washambuliaji watatu waliouawa walikuwa Waserbia wa Kosovo.
Mapigano ya Jumapili yanaashiria moja ya hali mbaya zaidi nchini Kosovo kwa miaka, na yanafuatia miezi kadhaa ya mvutano unaoendelea kuongezeka kati ya pande hizo mbili.
Kosovo ilijitangazia uhuru wake mwaka 2008 lakini Serbia - pamoja na washirika wakuu wa Belgrade -China na Urusi - hawaitambui.
Waserbia wengi wanaiona Kosovo kama mahali pa kuzaliwa kwa taifa lao. Lakini kati ya watu milioni 1.8 wanaoishi Kosovo, 92% ni wa jamii ya kikabila ya Waalbania na 6% tu ni wa kabila la Waserbia.
