Mapinduzi Niger: Raia wa waandamana kudai kufukuzwa kwa jeshi la Ufaransa

Taarifa ambazo kutoka mji wa Yamai katika Jamhuri ya Niger ni kwamba maandamano makubwa yamefanyika dhidi ya vikosi vya Magharibi.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya mubashara kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. 'Tunatuma ishara wazi kwa Urusi' Kamanda wa jeshi la wanamaji la Ujerumani

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wanajeshi wa vikosi vya majini wanatarajia kuanza mazoezi ya kijeshi katika Bahari ya Baltic yakihusisha meli 30 na zaidi ya wanajeshi 3,000 wa Magharibi kwa mara ya kwanza.

    Watatafanya mazoezi ya jinsi ya kujibu shambulio la Urusi katika eneo hilo, mkuu wa jeshi la wanamaji wa Ujerumani amesema.

    "Tunatuma ujumbe wazi wa tahadhari kwa Urusi: Sio kwenye saa yetu," Makamu wa Admirali Jan Christian Kaack aliwaambia waandishi wa habari mjini Berlin. "Kizuizi cha kuaminika lazima kijumuishe uwezo wa kushambulia."

    Mazoezi hayo ya wiki mbili ya Pwani ya Kaskazini, yanayotarajiwa kuanza Septemba 9, ambapo wanajeshi kutoka nchi zote za NATO waliopo kwenye Bahari ya Baltic, pamoja na Sweden ambayo itakuwa mwanachama hivi karibuni.

    Majeshi ya nchi washirika zisizo na vikosi vyake Baltic – Kama vile Marekani Marekani, Canada, Uholanzi, Ubelgiji na Ufaransa pia watashiriki.

    Watafanya oparesheni za mashambulio kutoka bahari hadi nchi kavu.

    Jeshi la wanamaji la Marekani litaituma kwenye mazoezi hayo meli yaMesa Verde yenye urefu wa zaidi ya mita 200 (656 ft), iliyoundwa kusafirisha na kuwasafirisha baadhi ya wanamaji 800 katika shambulio la majini, amesema Kaack.

    Vita vya Ukraine-Mengi zaidi:

    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  3. Je Afrika Mashariki inaweza kukomesha biashara ya mitumba?

    g

    Nchi za Afrika Mashariki zinazungumzia tena suala la kupiga marufuku nguo za mitumba, likichochewa na hisia kwamba hatua hiyo inaweza kulinda viwanda vichanga vya nguo, limeripoti Gazeti la East African.

    Lakini ukweli wa gharama kubwa ya uzalishaji wa nguo bado unaweza kutoa fursa kwa wauzaji bidhaa wa bei nafuu kama vile Uchina, ambayo imekuwan ikiongeza mauzo yake ya nguo.

    Na hilo limeibua maoni yaliyogawanyika kuhusu uingizaji na uuzaji wa nguo hizo zinazofahamika zaidi kama mitumba Afrika Mashariki.

    Wiki hii, Uganda imekuwa nchi ya pili baada ya Rwanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kupiga marufuku mitumba, huku Rais Yoweri Museveni akisema anaendeleza sera ya taifa ya “Nunua Uganda Ijenge Uganda”.

    Wakati akizindua viwanda 16 katika Hifadhi ya Viwanda ya Sino Iliyoko Katika wilaya ya Mbale -Mbale City, Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema uingizaji wa mara kwa mara wa nguo zilizotumika hukwamisha maendeleo ya viwanda vya ndani vya nguo.

    Kupiga marufuku mitumba kunaweza kusikika kuvutia kisiasa kwa nguo za ndani lakini ni jambo ambalo halijaweza kufaulu.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mitumba Kenya: Kwanini nguo za mitumba zimezua mjadala Kenya?
    • Rwanda hatarini kuadhibiwa na Marekani juu ya nguo za mitumba
    • Rwanda yaongeza ushuru kwa mitumba
  4. Habari za hivi punde, Mapinduzi Niger: Raia wa waandamana kudai kufukuzwa kwa jeshi la Ufaransa

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Maandamano hayo yalianza jana baada ya swala ya Ijumaa

    Taarifa ambazo tunazipata kutoka mji wa Yamai katika Jamhuri ya Niger ni kwamba maandamano makubwa yanafanyika dhidi ya vikosi vya Magharibi.

    Picha na video kutoka eneo la tukio zinaonyesha jinsi mamia ya waandamanaji wanavyojaribu kuingia kwenye Uwanja wa Ndege wa Escadrille, ambapo wanajeshi wa Ufaransa na wa kigeni wamewekwa.

    Lakini wanajeshi wa nchi hiyo ambao wanaonekana kuwa ni wachache ikilinganishwa na idadi ya watu, wanajaribu kuwazuia.

    Katikati ya wiki, makundi yanayounga mkono jeshi lililofanya mapinduzi yaliitisha maandamano makubwa na kuwasihi watu kukaa ndani kwa siku tatu ili kuwafukuza wanajeshi wa Ufaransa nchini humo.

    Unaweza pia kusoma:

    • Je, Ufaransa ndio wa kulaumiwa kwa mapinduzi ya kijeshi Afrika Magharibi?
    • Kwa nini mapinduzi ya Niger yanaigusa dunia nzima?
    • Mapinduzi Niger: Historia ya mapinduzi manne Niger tangu uhuru
    • Kwa nini mapinduzi ya Niger yanaigusa dunia nzima?
  5. Wafungwa wawaachilia huru walinzi 57 wa magereza wa Ecuador baada ya kuwateka nyara

    f

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Maafisa wanasema shughuli za kawaida zimeanza tena katika vituo hivyo sita.

    Wafungwa katika magereza sita ya Ecuador wamewaachilia walinzi 50 na maafisa saba wa polisi waliokuwa wamewateka , idara ya magereza (SNAI) imesema.

    Mateka 57 walioachiliwa "wanafanyiwa tathmini ya matibabu" lakini wanaonekana kuwa na afya njema, kulingana na SNAI.

    Maafisa wanasema utekaji nyara huo uliongozwa na magenge ya wahalifu waliokasirishwa na majaribio ya kudhibiti mamlaka yao.

    Mabomu mawili ya gari yaliyolipuka karibu na majengo ya polisi katika mji mkuu, Quito, pia yameripotiwa kutekelezwa na magenge hayo.

    Mamlaka zinaamini kuwa moja ya tukio hilo linaweza kuwa kulipiza kisasi kwa msako wa polisi wa kutafuta silaha katika jela moja kubwa nchini humo.

    Mamia ya maafisa wa polisi na wanajeshi walifanya msako katika jela ya Cotopaxi lililopo Latacunga, takriban maili 55 (88km) kusini mwa Quito, kama sehemu ya juhudi za kuzuia ghasia zaidi katika gereza hilo siku ya Jumatano.

  6. Habari za hivi punde kuhusu Mohamed Salah na kuhamia kwake Saudi Arabia

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Katika saa chache zilizopita, kumekuwa na maneno mengi kuhusu uamuzi wa mwisho wa nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, huku ikiaminika kwamba atahamia huko na kwenda Saudi Arabia.

    Kwa hivyo vyombo vya habari vya kimataifa vya michezo viliandika nini kuhusu habari za hivi punde zinazohusiana na Salah?

    Al-Ittihad wako tayari kutoa dau la pauni milioni 200 kumnunua mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, 31, kabla ya dirisha la usajili la Ligi ya Saudia kufungwa Septemba 7.(Barua inasema hivyo)

    Liverpool tayari ina mbadala wa Salah waliopangwa na wanaweza kumnunua winga wa PSV Eindhoven raia wa Ubelgiji Johan Bakayoko, 20, mwezi Januari iwapo mshambuliaji huyo wa Misri ataamua kuondoka.( Express iliandika)

    Huku soko la uhamisho la Saudia halijafungwa hadi Septemba 7, mara moja ilisemekana kuwa Al-Ittihad wanaweza kurejea kwenye ofa hiyo.

    Kwa upande mwingine, Klopp akizungumzia tena kuhusu Mo Salah na Al Ittihad alisema "Kwa mtazamo wangu, sioni cha kuwa na wasiwasi, Mohamed amedhamiria sana"."Kweli anafanya mazoezi kikamilifu hapa. Kila kitu ni kizuri," alisema kocha wa timu ya Liverpool.

    Unaweza pia kusoma:

    • Taarifa za uhamisho: Usajili uliofanyika siku ya mwisho
    • Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 02.09.2023
    • Siku ya mwisho ya uhamisho 2023: Primia Ligi yavunja rekodi kwa matumizi ya mabilioni ya pesa
  7. Tazama:Video yaonyesha polisi wakimpiga risasi mwanamke mweusi

    Maelezo ya video, Tazama: Video yaonyesha polisi wakimpiga risasi mwanamke mweusi

    Polisi katika jimbo la Ohio wametoa kanda za video zinazomuonesha afisa mmoja akimpiga risasi mwanamke mweusi aliyekuwa mjamzito.

    Ta'Kiya Young, mwenye umri wa miaka 21, alifariki tarehe 24 Agosti wakati alipopigwa risasi akiwa ndani ya gari lake nje ya duka la vyakula la Kroger lililopo eneo la Blendon Township, kitongoji cha Columbus.

    Picha za video zinaonyesha maafisa wakijaribu kumhoji kwa madai ya kuiba bidhaa za duka.

  8. Tazama:Kimbunga Saola chapasua miti huku Hong Kong ikikabiliana na dhoruba

    Maelezo ya video, Tazama:Kimbunga Saola chapasua miti huku Hong Kong ikikabiliana na dhoruba

    Tahadhari ya juu zaidi ya dhoruba inatumika huko Hong Kong wakati kimbunga Saola kinakaribia.

    Huenda ikawa dhoruba kali zaidi kuwahi kutokea katika eneo hilo kwa miongo kadhaa, huku Shirika la Uangalizi la Hong Kong likionya kuhusu upepo wenye kasi ya wastani ya 118 km/h.

    Makumi ya mamilioni ya watu huko Hong Kong na maeneo ya karibu ya China Bara wamejificha.Makao ya dharura yamekuwa yakifunguliwa katika mji wa Shenzhen.

  9. Mohamed Al Fayed: Mmiliki wa zamani wa Harrods afariki akiwa na umri wa miaka 94

    f

    Mohamed Al Fayed, bosi wa zamani wa Harrods ambaye mwanaye Dodi aliuawa katika ajali ya gari pamoja na aliyekuwa Bintimfalme Wales Diana, amefariki akiwa na umri wa miaka 94.

    Mohamed Al Fayedambaye ni mzaliwa wa Misri, alijenga himaya ya biashara katika Mashariki ya Kati kabla ya kuhamia Uingereza katika miaka ya 1970.

    Hata hivyo, hakuwahi kutambua azma yake ya kupata pasipoti ya nchi aliyoasili.

    Amekuwa akihoji kwa miaka hali ya vifo vya mwanaye Dodi na Diana.

    Bw Al Fayed alikuwa amebaki nje ya umaarufu wa umma katika muongo mmoja uliopita, akiishi katika jumba lake la kifahari la Surrey na mkewe Heini.

    Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, familia yake ilisema: "Bi Mohamed Al Fayed, watoto wake na wajukuu wanataka kuthibitisha kwamba mume , baba na babu yao mpendwa, Mohamed, ameaga dunia katika hali ya amani siku ya Jumatano Agosti 30, 2023 kutokana na uzee wake.

  10. Aditya-L1: India tafanikiwa kuanza uchunguzi wake wa kwanza kuhusu Jua

    h

    Chanzo cha picha, ISRO

    Maelezo ya picha, Ujumbe wa India unaolenga kulichunguza jua ulijiondoa kutoka kwa uwanja wa uzinduzi huko Sriharikota Jumamosi asubuhi

    India imeanzisha safari yake ya kwanza yenye lengo la kulichunguza Jua, siku chache tu baada ya nchi hiyo kuweka historia kwa kuwa ya kwanza kutua karibu na ncha ya kusini ya Mwezi.

    Aditya-L1 alijiinua kutoka uwanja wa uzinduzi huko Sriharikota Jumamosi saa tano na dakika 50 asubuhi Ujumbe wa India unaolenga kulichunguza jua ulijiondoa kutoka kwa uwanja wa uzinduzi huko Sriharikota Jumamosi asubuhikwa saa za India

    Itasafiri kilomita milioni 1.5 (maili 932,000) kutoka duniani - 1% ya umbali wa Dunia-Jua.

    Shirika la anga za juu la India linasema itachukua miezi minne kusafiri umbali huo.

    Ujumbe wa kwanza wa anga za juu nchini India unaolenga kujifunza mfumo wa jua umepewa jina la Surya - mungu wa Kihindu wa Jua ambaye pia anajulikana kama Aditya.

  11. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara ikiwa leo ni tarehe 02.09.2023