Watu saba wamefariki na wengine 117 kujeruhiwa wakati kombora mji wa Chernihiv nchini Ukraine
Takriban watu 117 sasa wanajulikana kujeruhiwa katika shambulio hilo, kwa mujibu wa kaimu meya wa jiji hilo.
Moja kwa moja
Kenya: Watu 6 wafariki baada ya kudumbukia ndani ya shimo la maji kabla ya harusi
Takriban watu sita waliokuwa wakipanga kuhuduria harusi wamefariki baada ya kuanguka ndani ya shimo la maji wakati walipokuwa wakicheza densi.
Ajali hiyo imetokea katika Kihunguro, Kaunti Ndogo ya Ruiru viungani mwa mji mkuu Nairobi, wakati watu hao walipokuwa wakidensi juu ya mwamba wa zege unaofunika kisima cha maji ambao uliporomoka na kuanguka nao ndani ya shimo la maji, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.
Kulingana na Msemaji wa Polisi wa Kiambu, kundi hilo la watu walikuwa wamesimama katika nyumba ya rafiki yao Jumamosi ili kujiburudisha wakati takriban 11 kati yao walikufa maji baada ya zege hilo la mfuniko wa shimo la maji kuporomoka.
Polisi wanasema lazima kisima hicho kilibomoka kutokana na uzito wa watu waliokuwa wamesimama juu yake.
Shughuli ya uokoaji ikiongozwa na kikosi cha zima moto na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Kihunguro ilianza baadaye na watu 6 walipatikana wakiwemo wakiwa wamefariki akiwemo mtoto mmoja.
Hata hivyo, polisi wamethibitisha kuwa mmoja wa watoto hao, msichana alithibitishwa kufariki.
Waliookolewa wamepelekwa katika hospitali ya Ruiru.
Kesi za Michael Jackson zinazodai unyanyasaji wa kingono zinaweza kufufuliwa, mahakama ya rufaa ya Marekani inasema

Chanzo cha picha, CHANNEL 4
Maelezo ya picha, Wade Robson, aliyepigwa picha na Jackson katika miaka ya 1990, anadai mwimbaji huyo alimnyanyasa kingono. Wade Robson, aliyepigwa picha na Jackson katika miaka ya 1990, anadai mwimbaji huyo alimnyanyasa kingono.Na Aoife WalshHabari za BBC
Wanaume wawili wanaodai walinyanyaswa kingono wakiwa watoto na Michael Jackson wanaweza kufufua kesi dhidi ya kampuni zake, majaji katika mahakama ya Marekani waliamua.
Wade Robson na James Safechuck, wote wakiwa na umri wa miaka 40, wanadai kuwa Jackson aliwanyanyasa kwa miaka mingi wakiwa wavulana.
Sasa wanaweza kufuatilia kesi zilizozuiwa hapo awali dhidi ya kampuni za mwimbaji huyo.Wanasema makampuni haya yalikuwa na jukumu la kuwalinda.
Mawakili wa Jackson, aliyefariki mwaka wa 2009, wanaendelea kusema kuwa hakuwa na hatia.
Bw Robson na Bw Safechuck wanadai walidhulumiwa na Jackson mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa 1990 walipokuwa wakiishi katika shamba lake la Neverland.
Mashtaka hayo yalionyeshwa katika filamu ya mwaka 2019 ya Leaving Neverland, ambayo familia ya Jackson ilielezea kama "unyanyasaji wa umma".

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Michael Jackson na James Safechuck mwenye umri wa miaka 10 mnamo 1988 Michael Jackson na James Safechuck mwenye umri wa miaka 10 mnamo 1988
Mnamo 2020, jaji wa Los Angeles aliamua Bw Safechuck hangeweza kushtaki biashara za Jackson, akisema kampuni hazikuwa na jukumu la kumtunza.
Mwaka mmoja baadaye, hakimu huyohuyo alitoa uamuzi dhidi ya Bw Robson kwa misingi sawa.
Lakini siku ya Ijumaa, mahakama ya rufaa huko California ilikataa, ikiamua kwamba "shirika linalowezesha unyanyasaji wa kingono kwa watoto na mmoja wa wafanyikazi wake halisamehewi jukumu la kuwalinda watoto hao kwa sababu tu inamilikiwa na mhusika wa unyanyasaji".
"Itakuwa potofu kupata kutowajibika kwa msingi wa mshtakiwa wa shirika kuwa na mbia mmoja tu," hukumu ya mahakama ilisema."Na kwa hivyo tunabadilisha hukumu zilizowekwa kwa mashirika."
Vince Finaldi, wakili wa Bw Safechuck na Bw Robson, alisema kuwa mahakama ilibatilisha "maamuzi yasiyo sahihi ya hapo awali katika kesi hizi, ambayo yalikuwa kinyume na sheria ya California na ingekuwa imeweka mfano hatari ambao ulihatarisha watoto".
Jonathan Steinsapir, wakili wa mali ya Jackson, alisema "anajiamini kabisa" Jackson hakuwa na hatia, akisema madai hayo "yanakwenda kinyume na ushahidi wote wa kuaminika na uthibitisho huru".
Somalia: Mapigano makali yaibuka baina ya polisi na kundi la wanamgambo

Chanzo cha picha, Reuters
Kumekuwa na makabiliano makali katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu kati ya polisi na kundi la wanamgambo linaloongozwa na mwanajeshi wa zamani.
Polisi wanasema wanamgambo hao walikuwa wakiwaibia raia katika mji huo.
Mapigano hayo yalizuka Ijumaa jioni na kuendelea hadi Jumamosi asubuhi na kusababisha afisa mmoja na wanamgambo wawili kuuawa.
Rais wa Somalia hivi karibuni alitangaza operesheni ya kuimarisha usalama katika mji mkuu.
Mhariri wetu wa kikanda wa Afrika, Will Rossanasema kwa miaka mingi mitaa ya Mogadishu ilikuwa imejaa watu wenye silaha nzito - wengi hawakuwa sehemu ya jeshi la Somalia au jeshi la polisi.
Sauti ya milio ya risasi ilikuwa ya kawaida na wakati mwingine raia waliuawa wakati silaha zilipofyatuliwa ili kuondoa msongamano wa magari. Lakini mambo yanabadilika.
Rais Hassan Sheikh Mohamud amepiga marufuku silaha nzito katika mji huo na anataka kuimarisha usalama.
Wakati polisi jana usiku walipojaribu kuwanyang'anya silaha wanamgambo wakiongozwa na mwanajeshi wa zamani anayejulikana kama Jenerali Sheegow , ufyatuaji risasi huo ulidumu kwa zaidi ya saa kumi.
Msemaji wa polisi amesema operesheni hiyo ilifanikiwa na kiongozi huyo wa wanamgambo alikamatwa pamoja na wapiganaji wake ishirini na wanne.
Habari za hivi punde, Chernihiv: Idadi ya waliojeruhiwa katika shambulio la Urusi imeongezeka hadi 117
Takriban watu 117 sasa wanajulikana kujeruhiwa katika shambulio hilo, kwa mujibu wa kaimu meya wa jiji hilo.
Akiandika kwenye telegramu, Oleksandr Lomako amesisitiza kwamba watu saba wamefariki.
Hapo awali, wizara ya mambo ya ndani ilisema watu 90 wamethibitishwa kujeruhiwa, huku 25 kati yao wakipelekwa hospitalini.
Chernihiv: Shambulizi la kombora la Urusi laua watu watano, Ukraine inasema

Chanzo cha picha, Reuters
Watu watano waliuawa na 37 kujeruhiwa wakati kombora la Urusi liliposhambulia mji wa Chernihiv kaskazini mwa Ukraine, wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine ilisema.
Watoto 11 walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa. Jumba kuu la mraba, jengo la chuo kikuu na ukumbi wa michezo vimeripotiwa kuharibiwa.
Rais Volodymyr Zelensky alichapisha video fupi inayoonyesha magari yaliyoharibika na jengo kuu la chuo kikuu likiwa limejaa uchafu wa vifusi. Mwili mmoja pia unaweza kuonekana.
Mji wa Chernihiv uko karibu na mpaka wa Belarusi.
Ulichukuliwa na Urusi mwanzoni mwa uvamizi, lakini ukachukuliwa tena na askari wa Ukraine.
"Kombora la Kirusi lilipiga katikati mwa jiji, katika Chernihiv yetu. Chuo kikuu cha polytechnic, na ukumbi wa michezo," Rais Zelensky alichapisha kwenye Telegram.
"Jumamosi ya kawaida, ambayo Urusi imeigeuza kuwa siku ya maumivu na hasara. Kuna wafu, kuna waliojeruhiwa," aliongeza.

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Maeneo ya katikati mwa mji yamefungwa kwa muda ili kuruhusu ufikiaji wa huduma za dharura Kituo cha jiji kimefungwa kwa kiasi ili kuruhusu ufikiaji wa huduma za dharura
Kwingineko, Urusi imedai kuwa ndege isiyo na rubani ya Ukraine iligonga uwanja wa ndege wa kijeshi kaskazini magharibi mwa mkoa wa Novgorod, na kusababisha moto ambao ulizimwa haraka.
Ndege moja iliharibika lakini hakuna hasara iliyoripotiwa, iliongeza.
Ukraine haijazungumza lolote kuhusu shambulio hilo linalodaiwa kuwa la ndege zisizo na rubani.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Makasisi wa Jimbo Katoliki la Cologne na wafanyakazi walitumia kompyuta za kazini kutazama ponografia

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Kanisa kuu la Cologne, Makao makuu ya Askofu Mkuu wa Cologne Makasisi na wafanyakazi wa Jimbo Kuu la Cologne nchini Ujerumani walijaribu kuvinjari ponografia kwenye Kompyuta za kazi, Askofu wake mkuu amethibitisha.
Vyombo vya habari vya Ujerumani vilisema karibu majaribio 1,000 ya kutazama tovuti zilizozuiliwa yaliwekwa wakati shirika liliendesha majaribio ya mwezi mmoja kwenye mifumo yake ya usalama ya Teknolojia ya Mawasiliano(IT).
Angalau mshiriki mmoja mkuu wa kidini alikuwa miongoni mwa watu 15 waliotambuliwa, gazeti la Kölner Stadt-Anzeiger liliripoti.
Askofu mkuu, Rainer Maria Woelki, alisema ameagiza uchunguzi ufanyike kwa waliohusika.
Kutazama ponografia kwenye kompyuta za jimbo kuu ni marufuku kabisa, kama vile kupata nyenzo za dawa za kulevya na vurugu.
Shughuli nyingi za kutiliwa shaka zilihusu tovuti za ponografia, kulingana na Kölner Stadt-Anzeiger.
Katika taarifa iliyotolewa kwa BBC na dayosisi kuu, Kadinali Woelki alisema "amesikitishwa ... kwamba wafanyakazi walijaribu kupata tovuti za ponografia".
Uchunguzi ulikuwa umeanzishwa ili waliohusika washughulikiwe, kwani ilikuwa "muhimu kwangu sio kila mtu kuwekwa chini ya mashaka ya jumla sasa", aliongeza.
Jimbo kuu lilisema habari iliyorejelewa katika ripoti ya vyombo vya habari vya Ujerumani ilikusanywa wakati wa kuangalia uwezo wake wa usalama wa Teknolojia ya Mawasiliano ( IT) kuzuia ufikiaji wa tovuti ambazo "zinahatarisha (vurugu, ponografia, dawa za kulevya, nk)".
Iliongeza kuwa "hakuna tathmini ya yaliyomo nyuma ya URLs" zinazohusika, lakini "hakuna dalili za tabia inayofaa ya uhalifu".
Vipimo hivyo vilivyofanywa kati ya Mei na Juni mwaka jana, havikulenga hasa kuchunguza tabia za wafanyakazi au makasisi, ilisema.
Habari za hivi punde, Vita vya Ukraine: Milipuko inasikika katika moja ya wilaya za Kyiv
Vyombo vya habari vya Uukreni na njia za telegramu vimeandika kuhusu milipuko na moshi katika mji mkuu wa Ukraine Kyiv, na kuchapisha picha na video za mashahidi walioshuhudia tukio hilo.
Kufikia sasa, hakuna maoni rasmi juu ya tukio hilo. Hakuna tahadhari ya uvamizi wa anga iliyokuwa imetolewa wakati wa mlipuko huo.
Kulingana na meya wa Kyiv, Vitaliy Klitschko, moto huo uliosababishwa na "milipuko isiyojulikana" ulitokea katika eneo la viwanda karibu na Barabara ya Gonga katika mkoa wa Kyiv.
Chanzo cha mlipuko huo hakijajulikana.
Taarifa kuhusu waathiriwa bado hazijapokelewa.
Tazama: Ndege ya Southwest Airlines ikiwaka moto angani katikati ya safari
Maelezo ya video, Wakati ndege ya Southwest Airlines ilipowaka moto ikiwa katikati ya safari Video kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Southwest Airlines inaonyesha moto ukiwaka karibu na injini ya Boeing 737 muda mfupi baada ya kupaa, kikiwa katika safari ya kutoka Houston kwenda Cancun Jumanne.
Ndege hiyo ilitua kwa dharura na kurejea salama katika uwanja wa ndege wa Houston.
Katika taarifa, shirika la ndege la Southwest Airlines lilisema kuwa ndege hiyo ilikuwa na "tatizo la kiufundi muda mfupi baada ya kupaa" na imezuiwa.
Utawala wa Usafiri wa Anga sasa unachunguza tukio hilo.
Albania: Italia yalipa garama kwa ajili ya watalii waliokula mlo na kutoroka

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Tukio hilo lilitokea katika mji wa kihistoria wa Berat Katika hali ya kipekee ya kidiplomasia, serikali ya Italia imekamilisha garama ya mgahawa ya watalii wanne wa Kiitaliano nchini Albania ambao walikula na kuondoka bila kulipa.
Taarifa ya watalii hao walio kula na kutoroka katika jiji la Berat ziligonga vichwa vya habari katika nchi zote mbili.
Gumzo hilo lilimfanya Waziri Mkuu wa Albania Edi Rama kuzungumzia suala hilo na mwenzake wa Italia, Giorgia Meloni, alipokuwa akiitembelea nchi hiyo.
Alijibu kwa kumwambia balozi wake "nenda naulipe bili ya wajinga hawa," aliambia gazeti la La Stampa.
Ubalozi wa Italia nchini Albania ulithibitisha katika taarifa kwamba ulilipa bili hiyo, inayoripotiwa kuwa karibu €80 (£68), kwa niaba ya raia wake.
"Waitaliano wanaheshimu sheria na kulipa madeni yao na tunatumai kuwa vipindi vya aina hii havitatokea tena," ilisema.
Waziri wa kilimo wa Italia na shemeji yake Bi Meloni, Francesco Lollobrigida, pia walikuwa katika safari ya kwenda Albania na kuliambia shirika la habari la Reuters kwamba kulipa pesa hiyo ni jambo la kujivunia.
"Watu wachache wasio waaminifu hawawezi kuliaibisha taifa la watu wenye heshima," alisema.
Haijulikani ni lini tukio hilo lilitokea lakini video ya undi hilo iliyopigwa kwenye mkahawa huo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Mmiliki wa mgahawa aliiambia televisheni ya Albania – Abania’s Report TV kwamba ilikuwa mara ya kwanza kwa wateja kuondoka kwenye mgahawawake bila kulipa na kusema Waitaliano hao wanne hata walikipenda chakula hicho.
Vita vya Ukraine: Marekani yaruhusu ndege za F-16 za Denmark na Uholanzi zihamishiwe Kyiv

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Ukraine kwa muda mrefu imekuwa ikishinikiza washirika wake kutoa ndege za kivita za hali ya juu ili kulinda anga yake dhidi ya mashambulizi ya Urusi Marekani imeidhinisha kuhamishiwa Ukraine kwa ndege za kivita za F-16 zilizotengenezwa Marekani kutoka Denmark na Uholanzi wakati marubani wa Ukraine watakapopata mafunzo kamili ya kuziendesha.
"Kwa njia hii, Ukraine inaweza kuchukua fursa kamili ya uwezo wake mpya," msemaji wa serikali ya Marekani alisema.
Ukraine ilisifu uamuzi ambao imekuwa ikiushinikiza kwa bidii tangu mwaka jana.Lakini inatarajiwa kuwa itachukua miezi kadhaa kabla ya Kyiv kuweza kutumia ndege za F-16 kujaribu kukabiliana na ubora wa anga wa Urusi.
Waholanzi wanafikiriwa kuwa na takriban ndege 24 za F-16 zinazofanya kazi ambazo zimeratibiwa kuondolewa kazini na nafasi yake kuchukuliwa na ndege za juu zaidi za vita.
Denmark pia inapanga kuboresha ndege zake 30 za F-16.
Marekani na washirika wake hapo awali walikataa kutoa F-16 kwa Ukraine, wakihofia kwamba hii ingesababisha kuongezeka kwa mashambulizi zaidi ya Urusi ambayo ina silaha za nyuklia.
Urusi - ambayo ilianzisha uvamizi kamili wa Ukraine mnamo Februari 2022 - hadi sasa haijatoa maoni yoyote ya umma juu ya suala hilo.
Denmark na Uholanzi zilikuwa zimepewa "hakikisho rasmi" la kuhamisha ndege zao za vita za F-16, msemaji wa serikali ya Marekani alisema.
Msemaji huyo aliongeza kuwa hii itafanyika "mara tu marubani wa kwanza watakapomaliza mafunzo yao".
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Wopke Hoekstra aliafiki uamuzi wa Marekani, akisema kuwa "hii ni alama muhimu kwa Ukraine kutetea watu wake na nchi yake".
"Sasa tutajadili zaidi mada hiyo na washirika wetu wa Marekani," aliandika kwenye chapisho kwenye X, zamani ikijulikana kama Twitter.
Waziri wa Ulinzi wa Denmark Jakob Ellemann-Jensen aliunga mkono maneno yake.
"Serikali imesema mara kadhaa kwamba mchango ni hatua ya kawaida baada ya mafunzo. Tunaijadili na washirika wa karibu," aliliambia shirika la habari la Ritzau la Denmark.
Nchini Ukraine, Waziri wa Ulinzi Oleksii Reznikov aliuelezea uamuzi wa Marekani kama "habari kuu".
"Jeshi letu limethibitisha kuwa limejaa wanafunzi wa haraka. Hivi karibuni tutathibitisha kwamba ushindi wa Ukraine hauwezi kuepukika. Asante kwa washirika wetu wote na marafiki nchini Marekani, Uholanzi na Denmark. Tuendelee kwa Ushindi!" aliandika kwenye X.
Muungano wa wanachama 11 wa washirika wa Ukraine katika nchi za Magharibi unatarajiwa kuanza kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine baadaye mwezi huu na wanatarajiwa kuwa tayari mwaka ujao.
Mapema wiki hii, msemaji wa Jeshi la anga la Ukraine Yuriy Ihnat alikiri kwamba Kyiv haitaweza kuendesha ndege za F-16 msimu huu wa vuli na baridi kali.
F-16 Fighting Falcon inachukuliwa kuwa mojawapo ya ndege za kivita zinazotegemewa zaidi duniani.
Inaweza kuwa na makombora na mabomu yanayoongozwa kwa usahihi na inaweza kuruka kwa kasi ya mita1,500 kwa saa(2,400km/h), kulingana na Jeshi la Anga la Marekani.
Uwezo wa kulenga wa F-16 ungeiwezesha Ukraine kuvishambulia vikosi vya Urusi katika hali zote za hewa na usiku kwa usahihi zaidi.
Ukraine inaaminika kuwa na makumi ya ndege za kivita - nyingi zikiwa ni MiG - zote zilitengenezwa enzi ya Usovieti, na nchi hiyo kwa sasa imezidiwa vibaya na Urusi angani.
Kyiv inahitaji ndege za kisasa za kivita ili kusaidia kulinda anga lake dhidi ya mashambulizi ya mara kwa mara ya makombora ya Kirusi na ndege zisizo na rubani, na pia kusaidia mashambulizi yake ya kukabiliana na mashambulizi ya kusini na mashariki mwa Ukraine ambayo hadi sasa yametoa matokeo machache.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo tarehe 19.08.2023
