Mamluki wa Wagner wanaweza kujifanya kama wahamiaji kuingia EU - Waziri Mkuu wa Poland
Baadhi ya mamluki wa Urusi wako karibu na mji wa Grodno, karibu na Poland na Lithuania, Bw Morawiecki anasema.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Mapinduzi ya Niger: EU yasitisha ushirikiano wa kiusalama na misaada ya kibajeti

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Rais wa Niger Mohamed Bazoum Muungano wa Ulaya (EU) umesitisha ushirikiano wote wa kiusalama na Niger baada ya jeshi la nchi hiyo kuchukua mamlaka kupitia mapinduzi.
Haya yanajiri baada ya Marekani kutangaza "uungaji mkono wake usio na kikomo" kwa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum - anayeonekana kama mshirika mkuu wa Magharibi katika vita dhidi ya wanamgambo wa kijidihadi.
Siku ya Ijumaa mkuu wa kitengo cha walinzi wa rais Jenerali Abdourahmane Tchiani alijitangaza kuwa kiongozi mpya wa Niger. Alisema ukosefu wa usalama, matatizo ya kiuchumi na rushwa vilimfanya aingie madarakani.
Lakini sasa kuna wasiwasi katika nchi za Magharibi kuhusu nchi ambazo kiongozi huyo mpya ataungana nazo.
Majirani wa Niger, Burkina Faso na Mali, wote wameegemea Urusi tangu mapinduzi yao wenyewe.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alijiunga na Marekani na Ufaransa kukataa kuwatambua viongozi wa mapinduzi na kusema ushirikiano wa kiusalama na misaada ya kibajeti unasitishwa kwa muda usiojulikana.
Mapema Jumamosi Umoja wa Afrika ulitoa wito kwa jeshi la Niger kurejea kambini ndani ya siku 15.
Mohamed Bazoum - kiongozi wa kwanza wa Niger kuchaguliwa kumrithi mtangulizi wake tangu uhuru mwaka 1960 - kwa sasa anafikiriwa kuwa na afya njema, na bado anashikiliwa na walinzi wake.
Maelezo zaidi:
Serikali ya Iran yajitenga na kashfa ya kanda ya ngono

Chanzo cha picha, Getty Images
Kanda ya ngono iliyoibuka mtandaoni nchini Iran imemfanya afisa anayesimamia idara ya ikuzaji maadili ya Kiislamu kusimamishwa kazi - na mamlaka kukanusha kuwa na ufahamu wowote kuhusu mienendo yake ya mawali kama inavyodaiwa.
Video iliyowekwa mtandaoni inadaiwa kumuonyesha mkuu wa utamaduni na mwongozo wa Kiislamu katika jimbo la Gilan, Reza Tsaghati, akifanya mapenzi na mwanamume mwenzake. Utambulisho wao na uhalisi wa video haujathibitishwa.
Bw Tsaghati ameondolewa kwenye wadhifa wake huku mamlaka ikichunguza tukio hilo.
Kushiriki mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Iran, huku jumuia ya LGBT+ ikikabiliwa na hatari ya kunyanyaswa.
Video hiyo - ambayo imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii - imezua taharuki mtandaoni.
Bw Tsaghati ndiye mwanzilishi wa kituo cha kitamaduni kinachoangazia uchaji Mungu na hijabu.
Siku ya Jumamosi, waziri wa utamaduni wa Iran Mohammad Mehdi Esmaili alisema hakuna ripoti mbaya zinazohusiana na Bw Tsaghati zilizokuwepo kabla ya kuchapishwa kwa video hiyo.
Baadhi wamesema kuondolewa kwa Bw Tsaghati kwenye wadhifa wake kulionyesha tofauti ya jinsi maafisa wa Iran wanavyochukuliwa wanaposhtakiwa kwa uhalifu ikilinganishwa na jamii ya LGBT+, au wanawake wasiozingatia sheria za Kiislamu.
Chini ya sheria ya Iran, ambayo msingi wake ni Sharia, mahusiano ya jinsia moja yanatazamwa kama uhalifu ambao adhabu ya juu zaidi ya kifo.
Adhabu hii kali ihaijakuwa ikitumiwa sana, lakini jumuiya ya LGBT+ inakabiliwa na ubaguzi wa kila siku.
Ligi ya Saudia imebadilisha soko - Guardiola

Chanzo cha picha, reu
Uwezo wa kifedha wa Ligi ya Saudia "umebadilisha soko" la uhamisho wa wachezaji wa soko na vilabu vya "vinahitaji kufahamu kinachoendelea", anasema mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola.
Baada ya kumnasa nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo hadi Saudi Arabia mwezi Disemba, ligi hiyo imevutia wachezaji kadhaa wenye majina makubwa msimu huu wa joto.
Kundi hilo linajumuisha Riyad Mahez wa Algeria, ambaye aliondoka City na kujiunga na Al-Ahli.
"Saudi Arabia imebadilisha soko," alisema Guardiola. "Miezi michache iliyopita wakati Cristiano [Ronaldo] peke yake aliyeondoka, hakuna aliyefikiria kuwa wachezaji wengi wa hadhi ya juu zaidi wangecheza kwenye ligi ya Saudia.
"Katika siku zijazo kutakuwa na zaidi na ndio maana vilabu vinapaswa kufahamu kinachoendelea.
"Riyad alipata ofa ya ajabu na ndiyo maana hatukuweza kumzuia 'kuondoka'." City walikubali kumuuza Mahrez kwa mkataba wa hadi £30m huku Allan Saint-Maximin akitarajiwa kuwa mchezaji anayefuata kuondoka Ligi ya Premia kwenda Saudi Arabia atakapojiunga na Mahrez huko Al-Ahli.

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Al-Ahli walifikia mkataba wa hadi £30m na Manchester City ili kumsajili winga Riyad Mahrez Mchezaji wa Bayern Munich Sadio Mane yuko kwenye mazungumzo juu ya uwezekano wa kuhamia, baada ya kupokea ofa kutoka kwa Al-Nassr, huku mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or Karim Benzema akiwa tayari amemfuata mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid Ronaldo kwenda Saudi Arabia.
Mapema wiki hii, mtendaji mkuu wa Ligi Kuu ya Uingereza Richard Masters alisema "hana na wasiwasi" kuhusu kuongezeka kwa ushawishi wa Saudi Arabia katika soka.
Wagner wanaweza kujifanya kama wahamiaji kuingia EU - Waziri Mkuu wa Poland

Chanzo cha picha, reu
Wapiganaji wa Wagner nchini Belarus wanaweza kujifanya wahamiaji na kuingia EU, Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki ameonya.
Wagner pia wanaweza kunaweza kuchangia uhamiaji haramu kutoka Belarus, ambayo Poland inaelezea kama "vita vya mseto", anasema.
Takriban wapiganaji 100 wa Wagner wamehamia karibu na mji wa Grodno, karibu na mpaka wa Poland na Lithuania, Waziri Mkuu aliongeza.
Baadhi ya wanajeshi wa Wagner wamehamia Belarus chini ya makubaliano ya kumaliza maasi ya muda mfupi nchini Urusi mwezi Juni.
Kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko hapo awali alipinga kuzusha mzozo wa wahamiaji barani Ulaya kwa kuwarubuni wahamiaji wanaotarajiwa kuingia kwenye mipaka yake na mataifa ya EU.
Lakini Bw Morawiecki alisema Jumamosi kwamba zaidi ya wanachama 100 wa kundi la Wagner walihamia Belarus kaskazini-magharibi karibu na pengo la Suwalki - mpaka wa Poland wa maili 60 (95km) na taifa la EU la Lithuania, ambalo linatenganisha Belarus na Urusi ya Kaliningrad.
Alidai kuwa mamluki hao wanaweza kujifanya kama walinzi wa mpaka wa Belarus ili kuwasaidia wahamiaji kuvuka EU, au hata kujifanya wahamiaji wenyewe na kuingia katika umoja huo.
"Hali sasa inazidi kuwa hatari," aliambia mkutano wa waandishi wa habari kwenye ziara ya kiwanda cha silaha huko Gliwice, kusini mwa Poland.
"Hakika hii ni hatua kuelekea mashambulizi zaidi mseto katika eneo la Poland," aliongeza.
Maelfu kadhaa ya wapiganaji wa Wagner wamehamia Belarus tangu maasi ya muda mfupi ya kundi hilo dhidi ya Kremlin mwezi Juni.
Walipewa chaguo la kujiunga na jeshi la kawaida la Urusi au kwenda nchini Belarus, mshirika wa karibu wa Urusi.
Bw Morawiecki alisema kumekuwa na majaribio 16,000 ya kuvuka mpaka kati ya Belarus na Poland kufikia sasa mwaka huu.
Kulingana na shirika la udhibiti wa mpaka wa EU Frontex, kulikuwa na majaribio 2,312 ya kuvuka mpaka wa kuingia EU kutoka Belarus kati ya Januari na Juni.
Wanne hawajulikani walipo baada ya helikopta ya kijeshi ya Australia kupata ajali

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Helikopta ya MRH-90 Taipan, sawa na hii (pichani) hapa 2021, ilianguka wakati wa mazoezi ya kijeshi ya usiku. Mabaki ya helikopta ya kijeshi ya Australia iliyoanguka katika ufuo wa Queensland imepatikana, lakini watu wanne waliokuwa wameabiri ndege hiyo hawajulikani waliko, polisi wanasema.
Tukio hilo lilitokea wakati wa mazoezi ya Marekani na Australia kwenye Kisiwa cha Lindeman Ijumaa usiku.
Waziri wa Ulinzi Richard Marles alisema shughuli ya utafutaji na uokoaji ilizinduliwa mara moja.
"Wahudumu wanne wa anga bado hawajapatikana," Marles alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumamosi asubuhi.
MRH-90 Taipan ilianguka wakati wa zoezi la Talisman Sabre, ambalo ni mafunzo makubwa ya kijeshi kati ya Australia na Marekani.
Maafisa wa ulinzi walitangaza kusitisha mazoezi ya Talisman Saber, ambayo pia yanajumuisha wanajeshi kutoka Japan, Ufaransa, Ujerumani na Korea Kusini.
Zoezi hilo lilitarajiwa kukamilika Agosti 4.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin wako mjini Queensland kama kushiriki mazungumzo ya kila mwaka ya mawaziri wa Australia na Marekani (AUSMIN).
Trump awaambia wafuasi wa Republican ni yeye pekee anayeweza kushinda uchaguzi wa 2024

Chanzo cha picha, Reuters
Wawaniaji wa urais wa chama cha Republican wameshiriki jukwaa moja kwa mara ya kwanza katika kinyang'anyiro cha Ikulu ya Marekani 2024 kwenye hafla ya kampeni ya Iowa.
Wapinzani wakuu Donald Trump na Ron DeSantis waliongoza hafla ya wa kila mwaka ya chama cha Republican maarufu Lincoln Dinner.
Wagombea wote 13 walipewa dakika 10 za kuzungumza wakati wa hafla hiyo.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa Bw Trump anaongoza kwa wapinzani wake licha ya kukabiliwa na changamoto za kisheria.
Aliwaambia waliohudhuria kuwa yeye ndiye mgombea pekee ambaye anaweza kushinda uchaguzi wa mwaka ujao na kudai kuwa hiyo ndiyo sababu pekee ya yeye kukabiliwa na msururu wa mashtaka ya jinai.
Bw Trump tayari amesisitiza kuwa atawania Ikulu ya White House, hata kama atapatikana na hatia.
Kulikuwa na zaidi ya watu 1,200 katika katika hafla hiyo - wote wana ushawishi mkubwa juu ya nani atateuliwa kupeperusha bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi mkuu wa Marekani.
Maelezo zaidi:
Mapinduzi Niger: Viongozi wa Afrika Magharibi kukutana Jumapili Nigeria

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Bendera ya Urusi imeonekana kwenye maandamano yanayounga mkono mapinduzi Viongozi wa Afrika Magharibi wanatarajiwa kukutana kwa mkutano wa dharura siku ya Jumapili kujadili mapinduzi ya hivi majuzi nchini Niger.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu anatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.
Bw Tinubu kwa sasa ni mwenyekiti wa shirika la Kiuchumi la Kanda ya Afrika Magharibi, Ecowas.
Taarifa kutoka kwa rais ilisema alilaani mapinduzi hayo katika nchi jirani ya Niger na kuahidi kwamba "Ecowas na jumuiya ya kimataifa itafanya kila iwezalo kutetea demokrasia na kuhakikisha utawala wa kidemokrasia unaendelea kukita mizizi imara katika eneo hilo".
Maelezo zaidi:
Kiongozi wa RSF wa Sudan anaonekana kwenye video ya kwanza ya vita

Chanzo cha picha, @RSFSudan
Maelezo ya picha, Hemedti anasemekana kuonekana mwembamba sana kwenye kipande hicho cha video - picha yake za kwanza ndani ya miezi mitatu Kikosi cha wanamgambo nchini Sudan kimechapisha video ya kiongozi wake kwenye mtandao wa Twitter akiwahutubia wapiganaji - kwa mara ya kwanza tangu mzozo huo kuzuka mwezi Aprili.
Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama "Hemedti", alionekana mwembamba kwenye video hiyo na wachambuzi wanasema mkono wake mmoja unaonekana kana kwamba hauko sawa.
Kumekuwa na uvumi kuwa kamanda huyo ambaye ana umri wa miaka 40 hivi amejeruhiwa katika vita hivyo.
Hotuba yake ilijumuisha matamshi yake ya mara kwa mara dhidi ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa jeshi ambaye anakabiliana naye katika mzozo mkali wa utawala wa nchi hiyo.
Alisema iwapo uongozi wa jeshi hilo utabadilika, atakubali makubaliano ya amani ndani ya saa 72.
Hemedti aliingia madarakani kwa mara ya kwanza kupitia safu ya wanamgambo wa Janjaweed, wanaotuhumiwa kwa mauaji ya kikabila wakati wa mzozo wa Darfur.
RSF iliundwa na Rais wa zamani Omar al-Bashir, ambaye aliondolewa madarakani kufuatia maandamano ya umma mwaka 2019.
Kiongozi wa RSF aliunga mkono kuondolewa kwake kama njia ya kujiingiza katika nafasi yenye nguvu zaidi.
Lakini muungano wake na Jenerali Burhan ulisambaratika vibaya miezi mitatu iliyopita. Tangu vita kuanza RSF imehamia katika maeneo mengi ya makazi ya miji mitatu inayounda Khartoum Kubwa - Bahri, Khartoum na Omdurman - ambayo mara nyingi hukumbwa na mashambulizi ya anga. Katika hotuba yake,
Hemedti alikuwa na tabia mbaya sana kuhusu Yasir al-Atta, afisa wa ngazi ya juu wa jeshi ambaye anaongoza operesheni huko Omdurman.
Aliomba msamaha kwa watu wa Sudan kwa "maafa ya vita", ambayo alishikilia kuwa yamewekwa kwa RSF.
Akiwa amezungukwa na wapiganaji wenye silaha katika kanda hiyo ya video ya dakika tano, pia alikanusha kuwa wale wanaotuhumiwa kwa uporaji mkubwa mjini Khartoum na kwingineko walikuwa wanachama wa RSF.
Makombora ya Urusi yagonga majengo katika mji wa Dnipro nchini Ukraine

Chanzo cha picha, Reuters
Watu tisa wamejeruhiwa wakiwemo watoto wawili baada ya makombora kushambulia majengo mawili katika mji wa Dnipro mashariki mwa Ukraine, maafisa wanasema.
Wanahabari wa BBC waliopo nchini humo wamethibitisha kuwa jengo kubwa la makazi lilikaribia kuharibiwa kabisa katika shambulio hilo la Ijumaa jioni.
Jengo la idara ya usalama ya Ukraine (SBU) pia lilishambuliwa, Rais Volodymyr Zelensky anasema.
Alilaumu "ugaidi wa makombora wa Urusi". Bw Zelensky alichapisha video kwenye Telegram inayoonyesha moshi ukipanda kutoka kwa majengo yaliyoharibiwa na moto katika kiwango cha barabara.
Alisema ameitisha mikutano ya dharura na SBU, wizara ya mambo ya ndani, huduma za dharura na maafisa wa eneo kufuatia tukio hilo.
Mkuu wa mkoa Serhiy Lysak alisema kuwa watoto wawili, wenye umri wa miaka 14 na 17, walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa. Aliongeza kuwa walikuwa wakitibiwa nyumbani.
Hakuna vifo vilivyoripotiwa kufuatia shambulio hilo lililofanyika saa saa mbili unusu usiku kwa saa za Ukraine (17:30 GMT) kulingana na Bw Lysak.
Shambulio hilo la Urusi la hivi punde lilikuwa la tatu dhidi ya jengo la SBU, kulingana na Meya wa Dnipro Borys Filatov.
Majengo yote mawili kwa kiasi kikubwa yalikuwa tupu, alisema, na kuongeza kuwa jengo la makazi lilikuwa limekamilika hivi karibuni na vyumba vilikuwa vikiuzwa.
Vita vya Ukraine: Taarifa zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja leo Jumamosi 29/07/2023
