Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marekani yawawekea vikwazo maafisa wakuu wa Mali kutokana na uhusiano wa Wagner
Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya maafisa watatu wakuu wa Mali wanaosemekana kuratibu kuenea kwa kundi la Wagner katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Moja kwa moja
Makamu wa Rais wa seneti ya Rwanda aomba msamaha kwa Kagame kwa kuhudhuria mkutano wa ukoo
Makamu wa rais wa seneti ya Rwanda ameshirikisha ujumbe kwenye Twitter akiomba kwa Rais Paul Kagame baada ya kushiriki katika hafla ya kumtambulisha kiongozi wa ukoo.
Espérance Nyirasafari alisema "amefanya jambo la kutisha" kwa kushiriki katika hafla hiyo, kitendo ambacho chama tawala cha RPF kilisema "kinatishia umoja wa Wanyarwanda wote".
Wanachama wengine wa chama walioshiriki pia wameomba radhi.
Naibu mmoja wa meya alijiuzulu Jumatatu usiku kufuatia tukio hilo.
Kiongozi wa ukoo ambaye alitambulishwa kwenye hafla iliyofanyika mapema mwezi huu, pia aliomba msamaha.
Suala kuhusu ukabila nchini Rwanda bado ni nyeti, karibu miongo mitatu baada ya mauaji ya halaiki ambapo Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa katika siku 100.
Kuomba radhi hadharani sio jambo geni kwa RPF na upinzani unasema lengo lao ni kuwaaibisha viongozi ambao vinginevyo wangetoa mawazo tofauti kuhusu sera.
Ugiriki yathibitisha marubani wawili walifariki katika ajali ya ndege
Wizara ya ulinzi ya Ugiriki imethibitisha marubani wawili wa jeshi la anga la Ugiriki walifariki dunia wakati ndege yao ilipoanguka walipokuwa wakizima moto katika kisiwa cha Evia
Wametajwa kama Kamanda Christos Moulas mwenye umri wa miaka 34 na rubani mwenzake Pericles Stefanidis mwenye umri wa miaka 27.
Waziri wa Ulinzi Nikos Dendias alisema walipoteza maisha yao "wakiwa kazini... walipokuwa wakijaribu kulinda maisha na mali ya raia, pamoja na mazingira ya nchi yetu".
"Tunaungana na familia zao na wafanyakazi wenzao, kuwasilisha rambirambi zetu za dhati."
Wapiganaji wa Kipalestina wauawa katika eneo la Ukingo wa Magharibi
Wapalestina watatu wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kuwafyatulia risasi wanajeshi wa Israel karibu na Nablus katika eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu, jeshi la Israel limesema.
Wanajeshi walikuwa wakiwalinda Wasamaria, jumuia ndogo ambayo inaanzia kwenye makabila ya kibiblia ya Waisraeli.
Picha za kamera za usalama zinaonyesha mtu akiwafyatulia risasi wanajeshi wawili waliofyatua risasi kabla ya mapigano ya dakika mbili.
Inakuja huku kukiwa na mvutano kati ya Waisraeli na Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, zaidi ya Wapalestina 160 - wanamgambo na raia - wameuawa na vikosi vya Israel au walowezi katika Ukingo wa Magharibi, Jerusalem Mashariki na Ukanda wa Gaza.
Kwa upande wa Israel, takriban watu 30 - ikiwa ni pamoja na wageni wawili na mfanyakazi wa Kipalestina - wameuawa katika mashambulizi au mashambulizi ya wazi ya Wapalestina.
Wote walikuwa raia isipokuwa mwanajeshi mmoja aliyekuwa nje ya kazi na mwanachama wa vikosi vya usalama vya Israel.
Katika tukio hilo la Jumanne asubuhi, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema wanajeshi hao walifyatuliwa risasi wakiwa kwenye gari. Ilisema kuwa wanajeshi walirudisha risasi "bila kuwajali magaidi".
Shirika rasmi la habari la Wafa la Palestina limesema wanajeshi wa Israel waliichukua miili ya watu hao ambao ilisema walikuwa na umri wa kati ya miaka 32 na 43 na gari lao.
Eneo ambalo tukio hilo lilitokea ni makazi ya Wasamaria, jamii inayoaminika kuwa chini ya 900, nusu yao wanaishi Israel na nusu nyingine chini ya utawala wa Wapalestina nje ya Nablus.
Katika hali isiyo ya kawaida, wanachama wake wana uraia wa Israeli na Palestina. Wanafuata dini ambayo ina mizizi katika Uyahudi lakini ina hadhi yake rasmi, mila na seti za imani.
Senegal: Miili 17 yapatikana baada ya boti kuzama
Miili ya watu 17 imepatikana baada ya boti kuzama katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, kulingana na maafisa wa eneo hilo.
Idadi kamili ya watu waliokuwemo kwenye boti hiyo bado haijabainika, lakini watu wawili waliokolewa wakiwa hai huku miili 17 ikipatikana.
Miili hiyo ilipatikana na jeshi la wanamaji mapema Jumatatu asubuhi na inaaminika kuwa wahamiaji kwa sababu ya aina ya mashua waliyokuwa ndani, alieleza Meya wa kitongoji cha Ouakam, Ndeye Top Gueye.
Kikosi cha wazima moto na wapiga mbizi kilikuwa kikiendelea kutafuta miili katika eneo hilo Jumanne mchana.
Wakati hii ikiwa ni mara ya kwanza miili kusombwa na maji katika kitongoji hicho, vifo vya wahamiaji baharini vinazidi kuwa vya kawaida nchini Senegal.
Haikuwa wazi watu hao walikuwa wanatoka wapi, walikuwa wa mataifa gani, au hata walikokuwa wakienda.
Lakini njia ya uhamiaji ya Atlantiki ni mojawapo ya njia mbaya zaidi duniani, na karibu watu 800 wanakufa au kutoweka katika nusu ya kwanza ya 2023 kulingana na shirika la misaada la Uhispania la Walking Borders.
Operesheni za utafutaji pia zimefanyika hivi karibuni nchini Uhispania, kutafuta boti za wahamiaji kutoka Senegal ambazo zimepotea, zikiwa na zaidi ya watu 300, kulingana na NGO ya Caminando Fronteras.
Qin Gang: China yamuondoa waziri wa mambo ya nje miezi kadhaa baada ya kuteuliwa
China imemuondoa Qin Gang kama waziri wa mambo ya nje chini ya miezi saba baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Jukumu hilo litachukuliwa na mkuu wa maswala ya kigeni wa Chama cha Kikomunisti, Wang Yi, ambaye hapo awali alikuwa waziri wa mambo ya nje.
Kutoweka kwa Bw Qin kwa muda mrefu kutoka kwa umma - na ukimya wa wizara yake kumhusu - kumechochea uvumi mkali.
Mara ya mwisho kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 57 alionekana hadharani ilikuwa tarehe 25 Juni. Aliyeteuliwa katika wadhifa wake Desemba mwaka jana, Bw Qin alionekana kama msaidizi wa karibu wa Rais Xi Jinping wa China.
"Bunge la juu la China lilipiga kura kumteua Wang Yi kama waziri wa mambo ya nje," shirika la habari la serikali Xinhua lilisema.
"Qin Gang aliondolewa kwenye wadhifa wa waziri wa mambo ya nje." Hakuna sababu iliyotolewa ya kuondolewa kwa Bw Qin, lakini ripoti hiyo ilisema Rais Xi alitia saini amri ya kuidhinisha hatua hiyo.
WHO yaonya juu ya kuongezeka kwa mzozo wa kibinadamu nchini Sudan
Shirika la Afya Duniani (WHO) linaonya kuhusu kuongezeka kwa mgogoro wa kibinadamu nchini Sudan ambapo zaidi ya theluthi mbili ya hospitali za nchi hiyo hazina huduma.
Ripoti zinazoongezeka za mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na wafanyakazi.
Kulingana na WHO, milipuko ya magonjwa - ikiwa ni pamoja na malaria, surua na dengue - ambayo ilikuwa imedhibitiwa vyema kabla ya mzozo wa sasa, inaongezeka kutokana na kukatizwa kwa huduma za msingi za afya ya umma.
Pia inasema kuna ripoti zinazoongezeka za unyanyasaji wa kingono na kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana.
Juhudi kadhaa za mazungumzo ya amani zimefanywa lakini hazijafanikiwa kusitisha vita.
WHO imetoa wito kwa pande zote zinazopigana kuwalinda raia, watoaji huduma za kibinadamu na vituo vya afya.
Pia unaweza kusoma:
Kiongozi wa upinzani Kenya kuzindua hazina ya kufadhili wahanga wa maandamano
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, anasema anapanga kuzindua hazina ya kusaidia "familia zilizopoteza wapendwa wao na wale ambao bado wamelazwa hospitalini wakipokea matibabu" baada ya kujeruhiwa katika maandamano.
Akizungumza na wanachama wa Chama cha Kimataifa cha Wanahabari Afrika Mashariki Jumanne asubuhi, kiongozi huyo wa muungano wa Azimio aliongeza kuwa hazina hiyo itakuwa wazi kwa wengine pia kuchangia .
Maandamano zaidi yalikuwa yamepangwa kufanyika Jumatano kuanzia saa kumi na mbili asubuh hadi saa kumi na mbili jioni lakini, katika taarifa yake kwenye Twitter, Bw Odinga ametaka aina tofauti ya maandamano yafanyike badala yake alisema watafanya mikesha ya kuwakumbuka wahanga wa ukatili wa polisi katika maeneo mbalimbali nchini kote.
"Tunatoa pole zetu kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na ndio sababu tulisitisha maandamano," aliongeza.
Polisi nchini Kenya wamekuwa wakipambana na waandamanaji katika maandamano ya hivi punde ya upinzani kupinga kupanda kwa gharama ya maisha na kupandishwa kwa kodi.
Maelezo zaidi:
'Nahodha hawezi kufanya kazi peke yake' - Ten Hag
Erik ten Hag anasema Bruno Fernandes "hawezi kufanya hivyo peke yake" na anaamini viongozi wengine wanaweza kusonga mbele Manchester United.
Kiungo huyo wa kati wa Ureno alikabidhiwa jukumu la unahodha baada ya Ten Hag kuchukua jukumu hilo kutoka kwa Harry Maguire wiki iliyopita na kocha huyo wa United ameeleza kwa nini alimchagua namba nane wa United.
"Nahodha ana jukumu la kuimarisha uhusiano wa timu," alisema. "Anahitaji mtazamo sahihi, ujuzi wa kutia moyo, mamlaka na uelewa wa mchezo ili kuhamisha sheria na kanuni kutoka kwa meneja wake.
"Lakini nahodha hawezi kufanya hivyo peke yake. Nimeeleza kuwa timu inahitaji viongozi na kikosi hiki kina viongozi wengi ambao wataisaidia na kuipeleka timu katika mwelekeo sahihi."
Kwa ajili hiyo, Ten Hag amemnasa Jonny Evans kwa mkataba wa muda mfupi na anasema mlinzi huyo wa zamani wa Leicester City anafaa.
"Ungeweza kuona wiki iliyopita wakati wa mechi yao [dhidi ya Lyon] jinsi Jonny alivyokuwa akiwashauri wachezaji wachanga na kuwasukuma kwa kiwango cha juu," Ten Hag aliongeza.
"Anatusaidia. Anataka kubaki fiti, bado ana kazi na anatusaidia kusimamia mzigo wa wachezaji."
Marekani yawawekea vikwazo maafisa wakuu wa Mali kutokana na uhusiano wa Wagner
Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya maafisa watatu wakuu wa Mali wanaosemekana kuratibu kuenea kwa kampuni ya kijeshi ya Urusi ya Wagner katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Maafisa hao ni waziri wa ulinzi wa Mali, mkuu wa jeshi la anga na naibu mkuu wa majeshi, anasema waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken.
Anasema vifo vya raia vimeongezeka mara tatu tangu vikosi vya Wagner kutumwa Mali mnamo Desemba 2021, akiongeza "vingi vya vifo hivyo vilitokana na operesheni zilizofanywa na wanajeshi wa Mali pamoja na wanachama wa kundi la Wagner".
Washington na washirika wake kwa miaka kadhaa wameliwekea vikwazo kundi la Wagner na wafuasi wake, wakilishutumu kundi hilo la kijeshi kwa ukiukaji wa haki na kueneza habari potofu. Mnamo Januari, Washington ililiteua kundi la Wagner kama "shirika la uhalifu la kimataifa".
Wiki iliyopita, Uingereza iliwawekea vikwazo watu 13 wenye uhusiano na Wagner katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mali na Sudan.
Tangu wanajeshi wa Ufaransa waondoke nchini Mali mwezi uliopita wa Agosti na kutaka kuondoka kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa huko, jeshi la kijeshi la Mali, ambalo lilichukua mamlaka mnamo Mei 2021, limezidi kumgeukia Wagner.
Wagner inadhaniwa kuwa na takriban wanajeshi 1,000 katika taifa la Sahel ambalo limekuwa kitovu cha machafuko ya jihadi na machafuko ya kisiasa kwa miaka mingi.
Zaidi ya viongozi 20 wa Afrika kukutana Tanzania
Wakuu wa nchi na serikali kutoka nchi 21 za Afrika wamethibitisha kushiriki katika mkutano maalumu wa kujadili rasilimali watu, Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Dkt. Mwigulu Nchemba ameiambia BBC.
Safari ya mkutano huo ilianza tangu Mei 19,2023 na unatarajiwa kufungwa tarehe 26 Julai, 2023 na Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Akifafanua ajenda ya mkutano, Waziri Nchemba amesema nchi washiriki zitaweka nia ya pamoja ya kuongeza uwekezaji katika eneo la rasilimali watu ili kuongeza tija ya uzalishaji.
Mkutano huo ulioratibiwa na Benki ya Dunia, unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na Tanzania ikiwa ndiye mwenyeji wake.
Nyoka aliyeonekana kwenye treni awashtua abiria Uingereza
Abiria wa treni walilazimika kubadilisha mabehewa baada ya nyoka wa urefu wa mita 1.5 (futi 5) kuonekana ndani ya treni katika eneo la Yorkshire Uingereza.
Treni ya Northern alisema nyoka huyo mwenye rangi ya kung'aa lakini asiye na madhara alipatikana kwenye treni ya inayosafiri kutoka Skipton hadi Leeds.
Picha na video za msafiri huyu asiye wa kawaida asiye na sumu zilishirikiwa kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kuondolewa kweney treni baada ya kuwasili Leeds.
Nyoka huyo, ambaye sasa anaitwa Noodles, alichukuliwa na mamlaka ya kuhifadhi Wanyama RPSCA na sasa anatunzwa na mtaalamu.
Nyoka wa mahindi ana asili ya Amerika Kaskazini na ni moja ya wanyama wanaopendwaambao wanaofugwa sana nchini Uingereza.
Kwa sasa haijulikani jinsi nyoka huyo aliachiliwa na kuishia ndani ya treni siku ya Jumamosi, huku baadhi ya abiria wakisemekana kubadili njia zao za treni baada ya kupatikana kwa nyoka huyo.
Kamata kamata baada ya mwanamume kushambuliwa kingono kwenye treni Uingereza
Mwanamume mmoja alinajisiwa kwenye treni baada ya kutukanwa kwa maneno machafu, polisi wanasema.
Tukio hilo lilitokea karibu majira ya saa sita na dakika 50 mchana mnamo tarehe 1 Julai, kwenye treni kutoka Aberdare hadi Cardiff Central.
Muathiriwa alipita kundi la watu kabla ya mtu anayedaiwa "kumtolea maneno machafu".
Polisi walisema mwanamume huyo kisha alimnyanyasa kingono muathiriwa.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 40 alikamatwa baadaye akihusishwa na shambulio hilo kabla ya kuachiliwa kwa dhamana.
Polisi wa Usafiri wa Uingereza (BTP) wanawaomba mashahidi walioshuhudia tukio hilo kujitokeza kutoa ushahidi katika kesi kuhusu tukio hilo.
Mamluki wa PMC "Wagner" watatoa mafunzo kwa askari wa vikosi maalum vya Wizara ya Mambo ya ndani ya Belarusi
Mkutano kuhusu mada hii ulifanyika baina ya PMC ‘Wagner’’na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Belarus Ivan Kubrakov, imeripoti wizaraya mambo ya ndani ya Berarus.
Ripoti inasema kwamba "maswala ya mwingiliano na kampuni ya kijeshi ya kibinafsi na mafunzo ya wapiganaji wetu na wakufunzi wake yaliwekwa kwenye ajenda."
"Vyama vimeunda mpango wazi wa utekelezaji, kubadilishana maoni juu ya matumizi ya aina fulani za vifaa," kulingana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani
Siku ya Alhamisi, jeshi la Belarusi liliripoti kwamba vitengo vyake, pamoja na Wagner PMC, vitashughulikia kazi za mafunzo ya mapigano katika uwanja wa mazoezi wa Brestsky kusini magharibi mwa Belarusi ndani ya wiki moja.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Mpishi wa Obama Tafari Campbell afariki katika ajali ya majini
Mpishi wa kibinafsi wa rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amefariki dunia wakati wa ajali kwenye safari ya kupiga kasia karibu na nyumba ya Obamailiyopo Massachusetts.
Tafari Campbell, 45, alifanya kazi katika Ikulu ya White House kabla ya kukaa na familia ya Obama baada ya Bw Obama kuondoka mamlakanimwaka 2016.
Siku ya Jumapili, alipotea ndani ya maji katika eneo la Edgartown Great ,kwenye bwawa la shamba la Mizabibu la Martha.
Obama na mkewe walitoa taarifa wakisifu vipaji vyake ndani na nje ya jiko.
"Tafari alikuwa sehemu pendwa ya familia yetu. Tulipokutana naye kwa mara ya kwanza, alikuwa mpishi wa mpishi hodari katika Ikulu ya White House - mbunifu na mwenye shauku ya mapishi ya chakula, na uwezo wake wa kuleta watu pamoja," Bw Obama na aliyekuwa mke wa rais wa zamani Michelle Obama walisema Jumatatu.
"Katika miaka iliyofuata, tulimfahamu kama mtu mchangamfu, mwenye furaha, na mkarimu sana ambaye alifanya maisha yetu yote kuwa angavu kidogo."
Bw Campbell alikuwa akitembelea kisiwa cha Massachusetts kutoka nyumbani kwake huko Virginia wakati alipokutana na mauti yake. Polisi wanasema familia ya Obama haikuwa nyumbani wakati wa ajali hiyo.
Msako ulianza siku ya Jumapili usiku kumtafuta "mwanaume mpiga kasia ambaye alikuwa ameingia ndani ya maji, alionekana kuhangaika kwa muda kukaa juu ya maji na kisha kuzama na hakuibuka tena," kulingana na ripoti ya polisi.
"Mpiga kasia mwingine alikuwa kwenye bwawa pamoja naye wakati huo na kumwona akizama chini ya maji," iliongeza.
Siku ya Jumatatu, mwili wake ulipatikana "takriban futi 100 (mita 30) kutoka ufuo kwenye kina cha futi nane".
Kuchoma Quran Denmark : Mataifa ya Kiislamu yalaani kitendo cha kundi la mrengo wa kulia
Iraq na baadhi ya nchi zenye Waislamu wengi zimelaani vikali kuchomwa moto kwa Qur'ani siku ya Jumatatu na kundi liitwalo "Danish Patriots" nje ya ubalozi wa Iraq mjini Copenhagen.
Kundi hilo la mrengo wa kulia lilitangaza moja kwa mojamaandamano kama hicho kwenye Facebook siku ya Ijumaa.
Takriban waandamanaji 1,000 mjini Baghdad walijaribu kufikia ubalozi wa Denmark baada ya tukio hilo.
Wiki iliyopita, umati wa watu waliuchoma moto ubalozi wa Uswidi mjini Baghdad baada ya mpango wa kuchomwa kwa Quran mjini Stockholm.
Katika tukio la Jumatatu nchini Denmark, waandamanaji wawili wanaopinga Uislamu walikanyaga kitabu hicho kitakatifu na kukichoma kwenye trei ya karatasi ya bati karibu na bendera ya Iraq iliyokuwa chini.
Wizara ya mambo ya nje ya Iraq ilisema vitendo kama hivyo viliruhusu "virusi vya itikadi kali na chuki" kuleta "tishio la kuishi pamoja kwa amani katika jamii".
Waislamu wanaichukulia Quran kuwa ni neno la Mwenyezi Mungu na wanaona uharibifu wowote wa kimakusudi au kuonyesha kutoiheshimu kuwa ni maudhi sana.
Udhalilishaji wa hivi punde wa kitabu hicho katika mji mkuu wa Denmark pia ulisababisha maandamano ya maelfu ya waandamanaji katika mji mkuu wa Yemen Sanaa, ambao walionyesha hasira kwa Denmark na Sweden kwa kuruhusu vitendo hivyo.
Uturuki imelitaja tukio hilo kuwa ni "shambulio la kuchukiza" dhidi ya Qur'ani, huku wizara ya mambo ya nje ya Algeria ilimwita balozi wa Denmark na idara ya masuala ya Uswidi kulaani vitendo hivyo.
Raia wa Iran pia iliandamana siku ya Jumamosi kutokana na udhalilishaji wa kitabu hicho jitakatifu wa awali. Vyombo vya habari nchini Qatar viliripoti kuwa soko kubwa zaidi la nchi hiyo, Souq Al Baladi, limeondoa bidhaa za Uswidi kufuatia maandamano hayo.
- Malkia wa Sheba:Kwa nini wanawake wa nchi hizi wanajihusisha na mwanamke anayetajwa katika Biblia na Quran?
- Maonyesho ya Dubai 2020: Mfahamu rais wa zamani wa Marekani aliyeweka Korani ofisini kwake
Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara, ikiwa leo ni tarehe 25.07.2023