Vita vya Ukraine: Rais Zelensky atembelea Kisiwa cha Nyoka huku vita kiingia siku ya 500

Volodymyr Zelensky amechapisha video yake akitembelea kisiwa ambacho kilikuja kuwa ishara ya upinzani wa Ukraine - wakati vita vinaingia siku yake ya 500.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa.

  2. Habari za hivi punde, David de Gea: Mlindalango Mhispania athibitisha kuondoka Manchester United baada ya miaka 12

    Mlindalango wa Uhispania David de Gea anasema anaondoka Manchester United msimu huu wa joto, akisema "ni wakati mwafaka wa kukabiliana na changamoto mpya".

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa mchezaji huru kwani kandarasi yake katika klabu hiyo ya Old Trafford ilikuwa imefikia kikomo mwezi uliopita.

    De Gea amekuwa United kwa miaka 12 na alicheza katika mechi 545.

    "Nilitaka tu kutuma ujumbe huu wa kuwaaga mashabiki wote wa Manchester United," aliandika katika chapisho la mtandao wa kijamii.

    De Gea alianza soka lake akiwa Atletico Madrid, lakini alijiunga na United kwa £18.9ml mwaka 2011.

    Aliongeza: "Ningependa kutoa shukrani zangu zisizo na shaka na shukrani kwa upendo wa miaka 12 iliyopita. Tumefanikiwa mengi tangu mpendwa wangu Sir Alex Ferguson aliponileta katika klabu hii.

    "Niliona fahari ya ajabu kila nilipovaa fulana hii, kuiongoza timu, kuiwakilisha taasisi hii, klabu kubwa zaidi duniani ilikuwa ni heshima inayotolewa kwa wanasoka wachache waliobahatika.

    "Kimekuwa kipindi kisichosahaulika na chenye mafanikio tangu nilipokuja hapa. Sikufikiria kutoka Madrid nikiwa kijana mdogo tungefikia kile tulichofanya pamoja.

    "Sasa, ni wakati mwafaka wa kuchukua changamoto mpya, kujisukuma tena katika mazingira mapya.

  3. Kenya: Waandamanaji walirushiwa gesi ya kutoa machozi nje ya kituo cha polisi

    g

    Chanzo cha picha, Twitter

    Polisi nchini Kenya wamefyatua mabomu ya machozi kuwatawanya wanaharakati wa haki za binadamu wanaotaka kuachiliwa kwa makumi ya watu waliokuwa wakizuiliwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali siku ya Ijumaa.

    Kanda za video zinaonyesha moshi wa gesi ya kutoa machozi katika kituo kikuu cha polisi cha Nairobi.

    Miongoni mwa waandamanaji wa leo ni aliyekuwa Jaji Mkuu Willy Mutunga.

    Kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliitisha maandamano ya Ijumaa kupinga kupanda kwa ushuru wa mafuta na gharama ya juu ya maisha.

    Takriban mtu mmoja anaripotiwa kuuawa wakati polisi walipojibu maandamano katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.

    Takriban watu 28 walikamatwa.

  4. Rais anayeshiriki mapenzi ya jinsi moja aapishwa Latvia, akiwa wa kwanza Ulaya

    d

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Katika hotuba yake ya kwanza kama rais, Edgars Rinkevics alisema "mapambano dhidi ya rushwa, uhalifu na makampuni ya biashara lazima yawe kipaumbele cha kitaifa"

    Katika hotuba yake ya kwanza kama rais, Edgars Rinkevics alisema "mapambano dhidi ya rushwa, uhalifu na makampuni ya biashara lazima yawe kipaumbele cha kitaifa"

    Waziri wa mambo ya nje wa muda mrefu wa Latvia Edgars Rinkevics amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa la Umoja wa Ulaya kuwa mpenzi wa jinsi moja wa aliye wazi.

    Bw Rinkevics, ambaye alihudumu kama waziri wa mambo ya nje tangu 2011, ameapishwa kama rais wa Latvia Jumamosi katika mjini Riga.

    Ingawa kwa kwa kawaida cheo chake ni cha hadhi, rais wa Latvia anaweza kupinga sheria na kuitisha kura za maoni.

    Muungano wa Ulaya (EU) umewahi kuwa na wakuu wa serikali wapenzi wa jinsi moja hapo awali, lakini haujawahi kuwa na mkuu wa serikali wapenzi wa jinsi moja.

    Katika nchi nyingi, wakuu wa nchi na wakuu wa serikali ni watu tofauti - kwa mfano rais na waziri mkuu. Waziri Mkuu wa zamani wa Ubelgiji Elio di Rupo alikuwa kiongozi wa kwanza wa serikali ya Umoja wa Ulaya ambaye anashiriki mapenzi ya jinsi moja.

    Bw Rinkevics, 49, alijitokeza kwa mara ya kwanza mwaka wa 2014 kutangaza kuwa anashiriki mapenzi ya jinsi moja na amekuwa bingwa wa haki za LGBT tangu wakati huo.

    Ndoa za wapenzi wa jinsi moja ni kinyume cha sheria nchini Latvia, ingawa mahakama ya kikatiba ya nchi hiyo ilitambua ndoa za jinsi moja mwaka jana.

  5. Watoto 494 wamekufa tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Mnamo Juni 4, kumbukumbu ya watoto waliokufa kwa sababu ya mashambulizi ya Urusi iiliadhimishwa mjini Kyiv

    Wakati leo ikiwa ni siku ya 500 tangu vita vya Ukraine vilipoanza, watoto 494 wanaripotiwa kuwa ndio ambao wameuawa hadi sasa, na zaidi ya watoto 1,050 walijeruhiwa, kulingana na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine.

    Watoto wengi waliteseka katika mikoa ya Donetsk, Kharkiv, Kyiv, Kherson, Zaporozhye, Mykolaiv, Dnepropetrovsk, Chernihiv na Lugansk.

    Takwimu hizi sio za mwisho, tunazungumza tu kuhusuwale ambao majina yao yalithibitishwa, sisitiza huko Ukraine.

    Katika mikoa mingi ambapo uhasama unaendelea na katika maeneo yaliyochukuliwa, kuhesabu haiwezekani sasa.

    Zaidi ya watoto 500 walikufa katika siku 500 za vita, kulingana na Umoja wa Mataifa, idadi ya jumla ya raia nchini Ukraine ambao wamekufa tangu mwanzo wa vita, tangu Februari 24, 2022, imepita watu elfu 9, data ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa iliripoti siku moja kabla.

    Umoja wa Mataifa pia unafafanua kuwa kuna watu wengi zaidi waliofariki na kujeruhiwa, takwimu zilizotolewa zimeandikwa na kuthibitishwa wahanga wa vita hivyo.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  6. Edwin van der Sar: Mlindalango wa zamani wa Manchester United na Ajax yuko katika uangalizi maalum

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Edwin van der Sar alijiuzulu wadhifa wake kama mtendaji mkuu wa Ajax mwezi Mei

    Mlinda mlango wa zamani wa Manchester United na Ajax Edwin van der Sar amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuvuja damu kwenye ubongo wake.

    Mzee huyo mwenye umri wa miaka 52 anaripotiwa kutibiwakatika hospitali moja nchini Croatia, ambako amekuwa likizoni.

    Ajax ilisema mchezaji huyo wa zamani wa Uholanzi, ambaye aliichezea nchi yake mechi 130, yuko katika "hali shwari".

    "Kila mtu katika Ajax anamtakia Edwin ahueni ya haraka," klabu ya Eredivisie iliongeza. "Tunawaza wewe."

    Van der Sar alijiuzulu wadhifa wake kama mtendaji mkuu wa Ajax mwezi Mei baada ya timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu kwenye ligi ya Uholanzi na kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 2009.

    Alistaafu kucheza baada ya kuondoka United mwaka 2011 kabla ya kujiunga na bodi ya Ajax mwaka 2012, na baadaye kuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo mwaka 2016.

    Van der Sar alicheza mechi 266 akiwa na Mashetani Wekundu na kuwasaidia kushinda mataji manne ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa 2008.

    Katika taarifa yake, Manchester United ilisema: "Tunatuma upendo na nguvu zetu zote kwako, Edwin."

    Alicheza pia Ligi ya Premia kwa Fulham na Serie A kwa Juventus.

  7. Kylian Mbappé 'ni heshima' kuwa Cameroon

    f

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Kylian Mbappé alizaliwa huko Paris kwa baba wa Cameroon

    Nyota wa soka wa Ufaransa Kylian Mbappé anasema "anaheshimika" kuzuru Cameroon, nchi yake "ya asili".

    "Nina furaha sana kuwa hapa," aliongeza, akisema kwamba watu wamemwonyesha "mapenzi" mengi.

    Hapo awali, mashabiki wa kandanda walielezea kwa BBC msisimko walionao kuhusu safari hiyo.

    "Sote tumekuwa tukingojea wakati na hatimaye imefika," mtu mmoja aliambia kipindi cha redio cha BBC Newsday

    "Ni msaada mkubwa kwa Cameroon, sio tu kwa Cameroon lakini kwa bara zima," shabiki huyo aliongeza. "Kuwa naye karibu kunaonyesha kuwa nyumbani ni nyumbani - lazima urudi nyumbani kwako."

    Nahodha huyo wa kandanda wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 na mshambuliaji wa PSG - ambaye alizaliwa Paris, Ufaransa, kwa baba Mcameroon - pia alikutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Joseph Ngute siku ya Ijumaa, pamoja na maafisa wengine.

    Ni safari yake ya kwanza nchini Cameroon tangu akiwa kijana.

    v

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Nyota huyo wa kandanda alizingirwa na mamia ya mashabiki waliokuwa na shauku alipowasili Cameroon siku ya Alhamisi

    Nyota huyo wa kandanda alizingirwa na mamia ya mashabiki waliokuwa na shauku alipowasili Cameroon siku ya Alhamisi

    Nyota huyo wa michezo pia amekuwa akikutana na wanamichezo wengine wa Cameroon, kama vile nyota wa MMA Francis Ngannou, ambaye alipigwa picha naye akitabasamu.

    Pia alicheza mpira wa kikapu na nyota wa zamani wa Chicago Bulls, Joakim Noah kwenye uwanja wa Noah, ambapo alipigwa picha na umati wa watu waliokuwa wakifuatilia mchezo huo.

    Baadaye alicheza soka dhidi ya timu ya Cameroon Vent d'Etoudi FC, Reuters inaripoti.

    Mbappé pia anafanya kazi ya kibinadamu katika safari yake kwa niaba ya taasisi yake, ambayo inataka kuwasaidia vijana kufikia malengo yao.

  8. Vita vya Ukraine: Rais Zelensky atembelea Kisiwa cha Nyoka huku vita kiingia siku ya 500

    g

    Chanzo cha picha, Telegramu

    Maelezo ya picha, Rais Zelensky alikiita Kisiwa cha Nyoka "mahali pa ushindi" ambao hautawahi kutekwa tena

    Volodymyr Zelensky amechapisha video yake akitembelea kisiwa ambacho kilikuja kuwa ishara ya upinzani wa Ukraine - wakati vita vinaingia siku yake ya 500.

    Mwanzoni mwa vita, askari wa Ukraine wanaotetea Kisiwa cha Nyoka walikaidi amri kutoka kwa meli ya kivita ya Urusi ya kujisalimisha.

    Kisiwa hicho kilichopo kwenye Bahari Nyeusi kilitekwa na Urusi lakini baadaye kikarudishwa na Ukraine.

    Katika video, rais wa Ukraine akiita "mahali pa ushindi" ambapo haikutaweza kutekwa tena.

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kisiwa cha Nyoka ni muhimu kimkakati katia Vita vya Ukraine, na nchi mbili zimekuwa ziking'ang'ana kukidhibiti

    Katika video ambayo haikuonyeshwa tarehe iliyochukuliwa, iliyotumwa kwenye Telegram, Bw Zelensky alielezea kama dhibitisho kwamba Ukraine itarudisha kila inchi ya eneo lake lililochukuliwa na Urusi tangu vita vilipoanza tarehe 24 Februari 2022.

    "Ninataka kushukuru kutoka hapa, kutoka mahali hapa pa ushindi, kila mmoja wa askari wetu kwa siku hizi 500," Bw Zelensky alisema kwenye video, ambayo alionyeshwa akiwasili kisiwani kwa mashua na kuacha maua kwenye eneo la kumbukumbu.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  9. Hukambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara ya leo Jumamosi tarehe 08.07.2023