Vita vya Ukraine: Urusi yaharibu hospitali katika shambulio la hivi punde la kombora
Takriban watu wawili wameuawa na zaidi ya 30 kujeruhiwa katika shambulizi la kombora la Urusi kwenye hospitali katika mji wa Dnipro mashariki mwa Ukraine, maafisa wa Ukraine wamesema.
Watoto wawili wavulana wenye umri wa miaka mitatu na sita pia walikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa, mkuu wa mkoa Serhiy Lysak alisema.
Rais Volodymyr Zelensky alielezea shambulio hilo kama "ukatili mtupu".
Mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine yameongezeka katika wiki za hivi karibuni kabla ya shambulio linalotarajiwa la Ukraine.
.Bw Zelensky alichapisha video ya kliniki iliyoharibika ambayo ilionyesha wazima moto kwenye eneo la tukio na moshi ukifuka kutoka kwa jengo hilo.
"Magaidi wa Urusi kwa mara nyingine tena wanathibitisha hali yao ya wapiganaji dhidi ya kila kitu cha utu na uaminifu," alisema.
Hapo awali, Bw Lysak alisema eneo hilo lilikumbwa na "mashambulizi makubwa...kwa makombora na ndege zisizo na rubani" Alhamisi usiku.
"Ulikuwa usiku mgumu sana. Ilikuwa ni sauti kubwa," alisema. "Dnipro ameteseka."
Katika eneo la tukio, wazima moto walikuwa wakikata miti ili kupata bomba lililowekwa karibu na moto ambao ulikuwa umeshika jengo kubwa la ghorofa tatu.
Wakati huo huo, katikati ya vifusi, timu za uokoaji zilikuwa zikiwasaka watu wawili waliopotea.
Mamlaka ya Ukraine ilisema ilirusha makombora 17 na ndege zisizo na rubani 31 zilizorushwa kutoka Urusi usiku kucha.
Ndege zisizo na rubani na makombora kadhaa zililenga shabaha huko Dnipro na mji wa mashariki wa Kharkiv, pamoja na ghala la mafuta.
Mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, pia ulilengwa na maafisa walisema vipande vya ndege zisizo na rubani zilizonaswa zilianguka juu ya paa la kituo cha biashara, huku nyumba na magari kadhaa yakiharibiwa.
Nchini Urusi, mlipuko uliharibu jengo la makazi na ofisi katika mji wa kusini wa Krasnodar siku ya Ijumaa asubuhi.
Mashambulio ya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine