Mzozo wa Ukraine: Zelensky asema mji wa Bakhmut umeharibiwa huku Urusi ikidai ushindi
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema mji wa Bakhmut umeharibiwa kabisa – lakini akakanusha kuwa Urusi imepata ushindi katika vita vya kuudhibiti mji huo.
Moja kwa moja
Vita vya Ukraine: ICC 'haijazuiwa' na waranti ya kukamatwa kwa mwendesha mashtaka mkuu

Chanzo cha picha, reut
Maelezo ya picha, Karim Khan wa ICC alihusika katika kutoa hati ya kukamatwa kwa Vladimir Putin mwezi Machi. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu inasema "haijazuiliwa" na Urusi kumweka mwendesha mashtaka wake mkuu kwenye orodha inayotafutwa.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu inasema "haijazuiliwa" na Urusi kumweka mwendesha mashitaka wake mkuu kwenye orodha inayotafutwa.
Hii inakuka miezi miwili baada ya Karim Khan wa ICC kutoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Katika taarifa siku ya Jumamosi, mahakama ilisema hatua hiyo ni jaribio la kuhujumu "mamlaka yake halali ya kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji kwa uhalifu mbaya zaidi".
Urusi, ambayo si mwanachama wa ICC, hapo awali ilielezea waranti dhidi ya Bw Putin kuwa "batili".
Bw Khan, wakili wa Uingereza, alitoa hati ya kukamatwa kwa Rais Putin mwezi Machi.
Alidai kuwa anahusika na uhalifu wa kivita, na alielezea madai yake juu ya uhamishaji haramu wa watoto kutoka Ukraine hadi Urusi.
Hati pia ilitolewa kwa kamishna wa haki za watoto wa Urusi Maria Lvova-Belova kwa mashtaka sawa na hayo.
Katika taarifa yake Jumamosi, ICC yenye makao yake The Hague ilisema "inafahamu na ina wasiwasi mkubwa kuhusu hatua zisizostahiliwa na zisizo na sababu za kulazimisha zilizoripotiwa kuchukuliwa dhidi ya maafisa wa ICC".
Ikiashiria hatua hizo "zisizokubalika", mahakama ilisema haitazuiliwa kuendelea "kutekeleza wajibu wake huru".
Bw Khan bado hajatoa maoni yake kuhusu hatua dhidi yake.
Vita vya Ukraine: Alichosema Rais Zelensky katika mkutano wa G7 Hiroshima

Chanzo cha picha, hoto by Louise Delmotte/POOL/EPA-EFE/REX/Shutterstock
Baada ya rais wa Marekani Joe Biden kufanya mkutano na waandishi wa habari, ilikuwa ni zamu ya Volodomyr Zelensky. Aliusifu mji wa Hiroshima kwa kuonesha rushirikiano na Ukraine
Haya ndio aliyoyasema zaidi :
- Mji uliokumbwa na mapigano wa Ukraine, Bakhmut "haujatwaliwa na Urusi ", anadai.
- Picha za Hiroshima ikiwa mogofu baada ya kurushiwa bomu la atomiki mwaka 1945 inamkubusha siku ya leo katika Bakhmut
- Ana "uhakika" Ukraine itapokea ndege za mapigano za F-16 lakini hajui ni ngapi
- Zelensky aliongeza kuwa Urusi itayahisi mashambulio ya ulipizaji kisasi ya Ukraine yatakapowadia
Je kuna yeyote anayeweza kuzuia ushindi wa Pep Guardiola?

Taji la sita la Primia Ligi la Manchester City katika kipindi cha miaka sita na kwa namna lilivyopatikana lazima inatuma ujumbe wa hofu kwa wale wanaotaka kuchukua ukbingwa huu ambao sasa umezoeleka wa Pep Guardiola.
Hamu ya City ya kuendeleza ubabe wao inaonekana kuongezeka , badala ya kutoa ishara yoyote kwamba kuna siku moja mahasimu wao watawapokonya taji.
Manchester City ni timu ya kwanza kushinda Primia Ligi kwa misimu mitatu tangu Manchester United ilichukue 2006-07, 2007-08 na 2008-09.
Bila shaka kuna ushindi wa United wa1999 ambao uliwawezesha kuwa timu pekee ya Uingereza, kupata taji wakati huo , halafu wakashinda Kombe la FA na Championi Ligi.
Urithi wa Guardiola kama meneja wa City umeijenga timu kuwa kikosi imara zaidi. City ni mashine ambayo haina mapungufu dhahiri ambayo iliundwa na mmoja wa mameneja bora zaidi katika soka kuwahi kushuhudiwa.
Bakhmut: Zelensky asema mji umeharibiwa huku Urusi ikidai ushindi

Maelezo ya picha, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (kushito) akizungumza na Rais wa Marekani Joe Biden katika kikao cha G7 cha wiki hii Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema mji wa Bakhmut umeharibiwa kabisa – lakini akakanusha kuwa Urusi imepata ushindi katika vita vya kuudhibiti mji huo.
Alipoulizwa Jumapili kuhusu iwapo vikosi vyake vina udhibiti wa mji wa huo wa mashariki mwa Ukraine, Bw Zelensky alisema: "inasikitisha, ni mkasa, lakini kwa leo Bakhmut ipo mioyoni mwetu tu."
Baadaye ofisi yake ilifafanua kuwa hakuwa amesema kwamba mji umeangukia mikononi mwa Urusi .
Kikundi cha wanajeshi wa Urusi cha Wagner kilidai kuukamata mji huo Jumamosi.
Katika video muasisi wa kundi hilo, Yevgeny Prigozhin - akiwa amesimama na baadhi ya wapiganaji wake – alisema kuwa vikosi vyake vinaudhibiti mji wote, ingawa serikali ya Ukraine ilikanusha haraka, huku ikikiri kuwa haliilikuwa "mbaya".
Jumapili, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kwamba Urusi imeshinda vita vya kuudhibiti mji wa Bakhmut, na kwamba vikosi vyote ambavyo vilifanya kazi nzuri vitapata zawadi ya kitaifa.
Lakini naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine, Ganna Malyar, alisema baadaye kwamba vikosi vya Ukraine bado vinadhibiti sehemu yam ji na vinaendela kusonga mbele pamoja.
Walikuwa wameizungira sehemu ya Bakhmut, na kufanya hali kuwa "ngumu sana" kwa wanajeshi wa Urusi, alisema katika mitandao ya kijamii.
Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Dhehebu la kufunga hadi kufa Kenya: Serikali kupanua msako wa miili hadi mbuga ya Tsavo

Chanzo cha picha, Reuters
Msako wa wa manusura na miili ya watu waliokufa kutokana na mfungo katika thehebu ‘tata’ la msitu wa Shakahola , Kilifi nchini Kenya utapanuliwa hadi katika Mbuga ya Wanyama ya taifa ya Tsavo East, Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Kithure Kindiki , amenukuliwa na vyombo vya habari Jumamosi akisema.
Amesema kuwa serikali itatumia droni kusaidia juhudi za wachunguzi wanaofanya msako wa miili ardhini huku mchakato wa kufukua miili katika makaburi ya pamoja uliwa umesimamishwa ili kuruhusu uchunguzi wa maiti ufanyike .
"Msako wa manusura na miilindani yam situ wa Shakahola na katikaChakama Ranch kwa ujumla utaendelea bila kuvurugwa na utapanuliwa hadi ndani ya mbuga ya Wanyama ya taifa-Tsavo East National Park katika siku zijazo kwa msako wa ardhini na wa anga kwa kutumia droni," alisema wazir Kindiki katika taarifa yake.
Ijumaa watu zaidi waliokolewa katika msitu wa Shakahola, na hivyo kupelekea idadi ya watu waliookolewa katika tukio ambapo mchungaji Paul Mackenzie Nthenge wa kanisa la Good News International aliripotiwa kuwaagiza wafuasi wake kufunga hadi kufa ili ‘’kukutana na Yesu’’ kufikia 90.
Miili zaidi ya 230, tayari imefukuliwa na idadi ya miili zaidi inatarajiwa kufukuliwa, kulingana na maafisa.
Shughuli ua kufukua miili ilisitishwa Alhamisi ili kutoa fursa ya uchunguzi wa miili , na inatarajiwa kuanza tena Jumatano wiki ijayo.

G7: Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema kuwa China inasababisha "changamoto kubwa ya kizazi chetu"

Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema kuwa China inasababisha "changamoto kubwa ya kizazi chetu" kuhusu usalama wa dunia na mafanikio, na inaendela kuwa ya kiimla zaidi ndani ya nchi na nje yake".
Katika mkutano wa wiki hii, viongozi wa nchi zenye utajiri wa kiviwanda zaidi duniani G7 wameweka wazi misimamo yao kuhusu masuala yakiwemo ya Indo-Pacific na Taiwan.
Huku viongozi wa nchi zenye utajiri wa kiviwanda zaidi duniani G7 wakituma ujumbe mkali kwa Urusi kwa kumkaribisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika mkutano wao wa Hiroshima, hasimu wao pia alikuwa akilini mwao - China.
Na katika taarifa zao mbili, viongozi wa nchi tajiri zaidi duniani wameweka wazi msimamo waokuhusu masuala yanayoleta mgawanyiko kama vile lile la Indo-Pacific na Taiwan. Lakini sehemu muhimu zaidi ya ujumbe wao ilikuwa juu ya kile kinachoitwa "vitisho vya kiuchumi".
Ni suala gumu kwa G7. Chumi za biashara zao zimekuwa zikitegemea China, lakini ushindani na utawala wa Beijing umeongezeka na hawakubaliani juu ya mambo mengi likiwemo suala ya haki za binadamu. Na sasa, wanahofia kuwa watashikwa mateka kiuchumi na China.

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Katika mkutano wa wiki hii, viongozi wa G7 wameweka wazi misimamo yao kwa Beijing kuhusu masuala mkiwemo lile la Indo-Pacific na Taiwan Muungano wa Ulaya ulitahadharishwa hasa baada ya China kuzuia mauzo ya nje ya Lithuania baada ya Baltic kuweka ubalozi Taiwan nchini humo.Kwahivyo sio jambo la kushangaza kwamba G7 wangelaani kile wanachokiona kama "kuongezeka kwa usumbufu" wa "kutumia uchumi kama silaha kwa nchi ambayo haijiwezi vyema kiuchumi".
Tisho hili la China , wanasema linalenga ku ''kushusha hadhi ya sera za kigeni na za ndani ya nchi wanachama wa G7 pamoja na washirika wao kote duniani ".
Hatahivyo kwa kiasi kikubwa lugha yao ya kiuchumi kuhusiana na hili hawakuitaja China, katika jaribio la kidiplomasia la kuepuka kuinyooshea kidole moja kwa moja serikali ya Beijing.
Mzozo wa Sudan: Pande zinazopigana zakubaliana kusitisha mapigano kwa siku saba, Marekani yasema

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Zaidi ya watu milioni wanakadiriwa kuzikimbia nyumba zao tangu vita vianze Pande mbili zinazopigana nchini Sudanzimeafikiana kusitisha mapigano kwa muda baada ya mapigano hayo kuendela kwa wiki ya sita.
Makubaliano ya awali ya jeshi na kikundi cha wanajeshi wa dharura -Rapid Support Forces (RSF) yamekuwa yakikiukwa katika kipindi cha dakika chache kabla ya utekelezaji wake kuanza.
Lakini mkataba mpya utaimarishwa na "mpango wa ufuatiliaji wa usitishaji wa mapigano," kulingana na taarifa ya Marekani na Saudi Arabia.
Kama sehemu ya siku saba za usitishaji huo wa mapigano wa kibinadamu , maafisa wa Sudan wamekubaliana kurejesha huduma muhimu.
Mapigano baina ya pande mbuili yameliingiza taifa katika limbi la ghasia tanfu yalipoanza mwezi uliopita, huku zaidi ya watu milioni wakidhaniwa kuyakimbia makazi yao.
Akiba za chakula, pesa na huduma muhimu vimepungua kwa haraka na makundi ya misaada yamekuwa yakilalamika mara kwa mara kuwa yameshindwa kutoa usaidizi wa kutosha katika mji mkuu wa SudanKhartoum, ambako kuna ghasia zaidi
- Mapigano Sudan: Hakuna mazungumzo mpaka mashambulio ya mabomu yakome, Hemedti aiambia BBC
- Mzozo wa Sudan:Mahasimu wa Sudan wakubaliana 'kimsingi' kusitisha mapigano kwa wiki moja
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara ikiwa leo ni Jumapili tarehe 21.05.2023
