Urusi na Ukraine: Afrika inaongoza juhudi za amani- Ramaphosa
Viongozi sita wa Afrika wanatarajiwa kuzuru Urusi na Ukraine katika juhudi za kusuluhisha mzozo huo, rais wa Afrika Kusini ametangaza.
Moja kwa moja
Washukiwa sakata ya vyandarua vya mbu katika shirika la kusambaza dawa Kenya wachunguzwa - KEMSA
Shirika la usambazaji madawa nchini Kenya limesema linawachunguza maafisa wanaohusika na sakata la ufisadi la ununuzi wa vyandarua milioni kumu vya kuzuia mbu vya thamani ya bilioni nne, mradi uliofadhiliwa na Global Fund.
Hii inakuja siku moja baada ya Rais wa Kenya William Ruto amemfuta kazi katibu mkuu wa wizara ya afya Dr Josephine Mburu na maafisa kadhaa wanandamizi wa shirika hilo KEMSA kuhusiana na sakata la ufisadi.
Mwandishi wa BBC Caro Robi alizugumza na mkurugenzi mkuu mtendaji wa shirika la kupambana na ufisadi EACC Twalib Mbarak na kwanza alitaka kufahamu kama wanapanga kuwafungulia watuhumiwa mashitaka.
Maelezo ya sauti, Washukiwa sakata ya vyandarua vya mbu, katika shirika la kusambaza dawa Kenya wachunguzwa Rais Willian Ruto amteua Noordin Haji kuwa Mkuu mpya wa kitengo cha Shirika la Ujasusi Kenya
Rais wa Kenya William Ruto amemteua Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji kuongoza Kitengo cha Ujasusi nchini(NIS), kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Mstaafu Philip Kameru ambaye anaelekea kustaafu.
Bwana Haji anarejea katika kitengo cha NIS baada ya miaka sita.
Aliwahi kuhudumu katika kama naibu mkurugenzi wa idara ya kukabiliana na uhalifu wa kupangwa katika kitengo hicho.
Uteuzi wa Haji unasubiri kuidhinishwa na bunge kabla aanze kuhudumu
Kiongozi wa RSF aapa kumkamata na 'kumnyonga' mkuu wa jeshi Burhani
Maelezo ya sauti, Mzozo wa Sudan:Kiongozi wa RSF aapa kumkamata na 'kumnyonga' mkuu wa jeshi Burhani Kumekuwa na mapigano makali kati ya jeshi la Sudan na Vikosi Maalum vya RSF katika mji mkuu Khartoum na miji jirani ya Omdurman na Bahri,mpaka kuelekea kivuko cha Mto Nile.Kiongozi wa RSF Mohamed Dagalo ametishia kumkamata na kumnyonga mkuu wa jeshi Jenerali Burhani . Yusuf Juma ana maelezo zaidi
Unaweza pia kusoma
Afrika inaongoza juhudi za amani kati ya Urusi-Ukraine - Ramaphosa

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Cyril Ramaphosa alitoa tangazo hilo katika mkutano fupi mjini Cape Town wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong. Viongozi sita wa Afrika wanatarajiwa kusafiri hadi Urusi na Ukraine katika juhudi za kusuluhisha mzozo huo, rais wa Afrika Kusini ametangaza.
Cyril Ramaphosa alisema kuwa mwishoni mwa juma alizungumza na wenzake wa Urusi na Ukraine kwa njia ya simu.
Vladimir Putin wa Urusi na kiongozi wa Ukraine Volodymyr Zelensky walikuwa wamekubaliana na mpango huo, alisema.
"Cha muhimu katika mazungumzo yetu ni juhudi za kutafuta suluhisho la amani kwa mzozo mbaya nchini Ukraine, athari yake katika maisha ya binadamu na athari katika bara la Afrika," Bw Ramaphosa alisema.
"Niliwasilisha mpango huo kwa niaba ya wakuu wa nchi za Afrika kutoka Zambia, Senegal, Congo, Uganda, Misri na Afrika Kusini."
Haijabainika iwapo alikuwa akimaanisha Congo-Brazzaville au Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
"Viongozi hao wawili walikubali kupokea ujumbe na wakuu wa nchi za Afrika, huko Moscow na Kyiv," kiongozi wa Afrika Kusini alisema, akiongeza kuwa mkuu wa Umoja wa Mataifa amepewa taarifa na kukaribisha mpango huo wa Afrika.
Maoni ya Bw Ramphosa, yaliyotolewa mjini Cape Town wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong, yanakuja wakati maafisa wakuu wa kijeshi wa Afrika Kusini wanazuru Urusi.
Kiongozi huyo wa Afrika Kusini amekariri kuwa Afrika Kusini haitashiriki katika vita vya Ukraine.
Hii inafuatia mzozo wa kidiplomasia uliozuka wiki jana wakati balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini alipoishutumu nchi hiyo kwa kutoa silaha na risasi kisiri kwa Urusi.
Bw Ramaphosa amekubali kuchunguza madai hayo lakini anasema hakuna ushahidi thabiti wa kuunga mkono madai hayo.
Ndoa za watu wa jinsia moja zilizofanyika nje ya nchi kutambuliwa Namibia

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati ndoa za watu wa jinsia moja zikisalia kuwa haramu nchini Namibia, wanandoa wanaofunga ndoa nje ya nchi sasa watatambuliwa nchini humo.
Uamuzi huo wa Mahakama ya Juu ya Namibia unafuatia kampeni za wanaharakati wa haki na wanandoa ambao walikuwa wameadhibiwa na sheria zilizopo.
Chama cha Namibia Equal Rights Movement kilipokea taarifa hiyo kwa kutuma ujumbe kwenye Twitter: "Upendo Unashinda! Asante kwa familia ya Digashu na Sieller-Lilles. Nguvu zenu katika mapambano haya, zimebadilisha taifa hili kwa vizazi vijavyo vya wapenzi wa jinsia moja wa Namibia. #WeBelong."
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kama gazeti la The Namibian linavyoeleza "hukumu ya mahakama inawapa wenzi wasiokuwa Namibia katika ndoa za jinsia moja haki sawa za ukaazi nchini Namibia ambazo zinatolewa kwa wanandoa katika ndoa za jinsia tofauti".
Bado haijabainika wazi uamuzi huu unamaanisha nini kwa sheria za muda mrefu zinapinga uhusiano wa jinsia moja.
Pia unaweza kusoma:
- Ni nchi gani ambazo mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria?
- Zifahamu nchi ambazo wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja hunyongwa
Wizi wa vito vya Dresden: Wanaume watano wapatikana na hatia ya wizi wa 2019

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanaume watano wamepatikana na hatia ya wizi wa vito katika mji wa Dresden nchini Ujerumani.
Wezi hao waliiba vito vya thamani vya euro milioni 98 kutoka kwa jumba la makumbusho la jiji hilo mnamo 2019.
Polisi walipata vito vingi, ikiwa ni pamoja na upanga wa almasi, lakini inahofiwa hazina iliyobakia insipatikane tena.
Wanaume hao, wote wanachama wa mtandao wa uhalifu, wanakabiliwa na kifungo cha miaka minne hadi sita.
Huu ulikuwa ni wizi uliopangwa kwa uangalifu. Genge hilo, lililokuwa likiishi Berlin, lilitembelea eneo hilo mara kadhaa na kutayarisha mahali pao pa kuingia mapema, kwa kutumia mashine ya kukatia maji ili kuona kupitia sehemu za dirisha la ulinzi kabla ya kuzirudisha mahali pake.
Milio ya risasi na milipuko yatikisa Sudan licha ya mazungumzo yanayoendelea

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Mji mkuu na sehemu za Darfur zimeshuhudia vurugu mbaya zaidi Kumekuwa na mapigano makali kati ya jeshi la Sudan na Vikosi hasimu vya kijeshi katika mji mkuu Khartoum na miji jirani ya Omdurman na Bahri, upande wa pili wa Mto Nile.
Wanajeshi wameendelea kufanya mashambulizi ya anga na wakazi wanaojihifadhi katika nyumba zao wanasikia milipuko mikubwa.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu huko Darfur yanasema mapigano katika mji wa el-Geneina katika siku chache zilizopita yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 350.
Kumekuwa na ripoti za wanamgambo wa Kiarabu wanaotii RSF kushambulia, kupora na kuchoma nyumba.
Madaktari wanasema mfumo wa afya huko Darfur umeporomoka kabisa.
Pande hizo mbili zinazozozana zinakusudiwa kuwa zimekuwa zikifanya mazungumzo nchini Saudi Arabia lakini hadi sasa ahadi zote za kulinda raia na kuruhusu ufikiaji wa kibinadamu zimevunjwa.
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Sudan:Jitihada za wapatanishi kutuliza milio ya risasi na kumaliza mapigano
- Mapigano Sudan: Hakuna mazungumzo mpaka mashambulio ya mabomu yakome, Hemedti aiambia BBC
- Mzozo wa Sudan: Mgogoro wa Sudan unaweza kuisha kwa njia hizi tatu
Maafisa wa Kenya wafutwa kazi kutokana na kashfa vyandarua kutoka kwa wafadhili

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Walikusudiwa kununua vyandarua milioni 10 Rais wa Kenya William Ruto amemfuta kazi katibu mkuu anayesimamia afya ya umma na kuvunja bodi nzima ya taasisi ya kununua vifaa vya matibabu kutokana na kashfa ya ufisadi.
Ulaghai huo unahusisha zabuni ya usambazaji wa vyandarua vya thamani ya dola milioni 27 vilivyotolewa na wafadhili kwa lengo la kukabiliana na mbu wanaosababisha malaria.
Hazina ya Global Fund ilikuwa imeagiza Mamlaka ya Ugavi wa Dawa nchini (Kemsa) kununua zaidi ya vyandarua milioni 10 ambavyo vingetolewa kwa watu walio na mapato ya chini katika kaunti kadhaa zinakabiliwa na ugonjwa wa malaria.
Lakini Global Fund ilighairi zabuni hiyo - ikishutumu Kemsa kwa makosa ya kudaiwa kupendelea kampuni moja ambayo nyaraka zake hazikuwa katika mpangilio na kuwafungia nje wengine
Mnamo 2020, Kemsa iliangaziwa tena kutokana na madai ya matumizi mabaya ya mamilioni ya dola yaliyokusudiwa kununua vifaa vya kinga wakati wa janga la Covid.
Maafisa wa Kyiv: shambulio katika mji mkuu lilikuwa la kipekee katika ukubwa wake

Chanzo cha picha, STATE EMERGENCY SERVICE OF UKRAINE
Shambulio la usiku la mjini Kyiv lilihusisha ndege nane katika mji mkuu wa Ukraine tangu mapema mwezi Mei.
Kulingana na mkuu wa utawala wa kijeshi wa mji wa Kyiv, Sergei Popko, "shambulio baya lilifanyika kutoka maeneo mbali mbali kwa wakati mmoja, kwa kutumia, silaha kama UAVs, makombora ya masafa yanayoongozwa kulenga eneo, na labda makombora ya ballistic."
Popko analiita shambulio "la kipekee kwa ukubwa wake -likijumuisha mashambulio ya makombora mengi ya masafa kwa pamoja kwa wakati mfupi ."
Kulingana naye, kulingana na taarifa za awali, mengi kati ya makombora yaliyofyatuliwa yaliangamizwa.
Kwa mujibu wa Meya Kyiv Mayor Vitaliy Klitschko, vipande vya roketi vilinguka katika maeneo tofauti yam ji mkuu – katika wilaya za Obolonsky, Shevchenkovsky, Solomensky na Darnitsky- pamoja na hifadhi ya Wanyama ya Kiev.
Popko alisema kuwa uharibifu mkubwa ulionekana katika wilaya ya Solomensky – kulikuwa na moto katika makazi yasiyokaliwa na watu na magari kadhaa yaliungua.
Meya wa Kyiv Mayor Vitaliy Klitschko aliripoti awali kuwa, kulingana na taarifa za awali, kulikuwa na watu watatu waliouawa katika wilaya ya Solomensky.
Mzozo wa Sudan: Waziri wa mambo ya ndani wa Sudan afutwa kazi huku nchi ikikabiliwa na mzozo

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Jenerali Burhan awali alimfuta kazi gavana wa benki kuu Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amemfuta kazi kaimu waziri wa mambo ya ndani, Anan Hamed Mohammed Omar, ambaye pia ni mkuu wa polisi.
Katika taarifa yake, Jenerali Burhan alimtaja Khalid Hassan Muhyi al-Din kama mkurugenzi mkuu mpya wa polisi.
Hakuna sababu iliyotolewa ya kumfuta kazi lakini Jenerali Burhan awali alimfuta kazi kwa agizo kama hilo, gavana wa benki kuu na mawaziri wawili wa kigeni wanadiplomasia.
Poli imekuwa haifanyi kazi katika maeneo yaliyokumbwa na mzozo, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Khartoum, tangu mapigano yalipoibuka tarehe 15 Aprili. Matokeo yake, vitendo vya ukikaji wa sheria, ukiwemo uporaji na wizi, vimekuwa vikiripotiwakatika maeneo haya.
Mapiganno ya mwezi mmoja baina ya makundi hasimu ya kijeshi yanaonekana kutomalizika hivi karibuni kufuatia kuvurugika kwa mazungumzo ya amani yaliyoandaliwa na Marekani na Saudi Arabia.
Unaweza pia kusoma:
- Mzozo wa Sudan:Jitihada za wapatanishi kutuliza milio ya risasi na kumaliza mapigano
- Mapigano Sudan: Hakuna mazungumzo mpaka mashambulio ya mabomu yakome, Hemedti aiambia BBC
- Mzozo wa Sudan: Mgogoro wa Sudan unaweza kuisha kwa njia hizi tatu
Laporta: Tutafanya 'tuwezalo kumsajili' tena Messi

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Laporta: Barca ni nyumbani kwa Messi Rais wa Barcelona Joan Laporta anasema klabu hiyo ni "nyumba" ya Messi huku wakitarajia kumsajili tena fowadi huyo msimu huu wa joto.
Mkataba wa Muargentina huyo katika klabu ya Paris St-Germain unamalizika mwezi Juni, huku ripoti zikimhusisha na Saudi Arabia.
Lakini katika mahojiano na shirika la utangazaji la Uhispania TV3, Laporta alisema Barcelona inaweza kushindana na mtu yeyote kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35.
"Historia inatuunga mkono, hisia ni kali sana, tuna mashabiki milioni 400 duniani kote pia," alisema.
Messi aliondoka kwa wababe hao wa Catalan miaka miwili iliyopita baada ya miaka 21 katika klabu hiyo lakini amekuwa na wakati mgumu katika misimu yake miwili nchini Ufaransa, huku mashabiki wakimzomea baada ya ushindi wao wa 5-0 dhidi ya Ajaccio wikendi.
Laporta alisema kumekuwa na "mazungumzo ya kimapenzi" kati ya wawili hao na kwamba alimpongeza Messi kwa kushinda Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka jana.
"Yeye ni mchezaji wa Paris St-Germain na tunapaswa kusubiri hadi mwisho wa msimu, hadi umalizike, na ndipo tunaweza kuzungumza kwa utulivu zaidi kuhusu hili," Laporta aliongeza.
"Kwa heshima zote kwa Saudi Arabia, Barca ni Barca, na ni nyumbani."
Matamshi hayo yanakuja baada ya Barcelona kushinda taji lao la kwanza la La Liga ndani ya miaka minne kwa ushindi wa 4-2 dhidi ya Espanyol Jumapili.
Laporta alionekana kujizuia zaidi kuliko wakati wa usiku wa manane wa Twitch baada ya ushindi huo, ambapo anaripotiwa kusema kuwa klabu hiyo itafanya "kila linalowezekana" kumsajili Messi.
Mwanamke mwenye umaarufu wa Ghana ashitakiwa kwa utapeli wa kimapenzi Marekani

Chanzo cha picha, Hajia4Real/Instagram
Maelezo ya picha, Montrage anadaiwa kuwa sehemu ya biashara ya uhalifu katika Afrika Magharibi Mwanamuzi mwenye ushawishi wa Ghana ambaye pia ni maarufu sana kwenye miytandao ya kijamii Mona Faiz Montrage, al maarufu Hajia4Real, amesafirishwa hadi nchini Marekani kushitakiwa katika utapeli wa kimapenzi wa dola milioni 2 ($1.6m)
Biashara ya uhalifu anaypdaiwa kuhusishwa nayo inasemekana kuwalenga wanaume wa Kimarekani wenye upweke pamoja na wanawake na wakati mmoja kujifanya kuwa ameolewa na mmoja wa waathiriwa ili kuendeleza utapeli wake.scheme.
Shirika la ujasusi la Marekani (FBI) katika taarifa yake lilionyesha kuwa ameshitakiwa kwa mashitaka kadhaa, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kutekeleza wizi na utakatishaji wa pesa.
Anaweza kupewa hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela kwa kila kosa iwapo atapatikana na hatia.
Alishitakiwa kwa kusaidia katika kupokeana kutoa hundi za pesa zilizoibiwa, uhalifu unaoweza kumfunga jela kwa miaka mitano na kumi.
Mona mwenye umri wa miaka 30, alikamatwa tarehe 10 Novemba mwaka jana nchini Uingereza na kusafirishwa hadi Marekani Ijumaa.
Alikana mashitaka yote alipofikishwa mahakamani mbele ya majaji Jumatatu.
Maafisa wa Marekani wameelezea hofu yao kuhusu ulaghai wa kimapenzi unaowalenga wazee binafsi na kuelezea haja ya kuwawajibisha wahusika.
Montrage anadaiwa kuwa sehemu ya mtandao wa uhalifu katika Afrika magharibi, wakiwemo matapeli wa kimapenzi nchini Marekani kati ya mwaka 2013 na 2019.
Zaidi ya watu 20 hawajulikani walipo baada ya kiboko kugonga boti yao kusini mwa Malawi

Chanzo cha picha, Malawi Broadcasting Corporation/Facebook
Maelezo ya picha, Hadi sasa watu 13 wameokolewa Takriban watu 20 hawajulikani wlipo baada ya boti walilokuwa wakisafiria kugongwa na kiboko na kuzama katika Mto Shire uliopo katika jimbo la kusini mwa nchi hiyo la Nsanje.
Afisa wa ngazi ya juu katika wilaya ya Nsanje, Robert Nayeja, amesema kuwa boti hiyo ilikuwa imewabeba watu 37 ambao walikuwa wanaelekea kwenye mashamba yao upande wa Msumbiji, televisheni ya taifa MBC imeripoti.
Mwili wa mtoto mchanga, ambaye alikuwa miongoni mwa wasafiri, umeopolewa.
Afisa wa ngazi ya juu wa polisi Agnes Zalakoma, aliliambia shirika la habari la VOA kwamba idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka kwani timu ya uokozi inawasaka watu waliozama. Hadi sasa watu 13 wameokolewa.
Mbunge wa eneo hilo alisema kuwa mto huo una mamba na viboko wengi na maboti yanayoendeshwa pale huwa sio maboti yanayotumia injini.
Ajali hiyo ya boti ni ya tatu kutokea katika mto huo katika kipindi cha miaka miwili.
Malawi ilikabiliwa na kimbunga kibaya cha kitropiki mwezi Machi kilichowauwa watu 511 na 533 kutoweka.
Urusi na Ukraine: Mji wa Kyiv waamkia mashambulizi makali kutoka kwa Urusi

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mshambuliai ya Urusi Kyiv Kuna ripoti za idadi kubwa ya milipuko katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, na ving'ora vya mashambulizi ya anga vimekuwa vikilia.
Katika video kwenye mitandao ya kijamii, mifumo ya ulinzi wa anga inaweza kuonekana ikirusha makombora yanayoshukiwa kuwa ya Kirusi.
Jumbe za serikali zilionya watu kujiepusha na madirisha huku vifusi vya makombora yaliyozuiwa vikianguka kutoka angani.
Meya wa jiji Vitali Klitschko alisema baadhi ya vifusi vya roketi vimeanguka katika wilaya za kati, ikiwa ni pamoja na bustani ya wanyama ya jiji.
Kuna ripoti za majeruhi.
Shambulio hilo tata, ambalo lilitumia ndege zisizo na rubani na makombora, lilielezewa kuwa "la kipekee katika msongamano wake" na afisa mmoja wa Kyiv.
Serhiy Popko, mkuu wa utawala wa kijeshi wa mji mkuu wa Ukraine, alielezea shambulio hilo kuwa na "idadi ya juu zaidi ya makombora ya mashambulizi katika kipindi kifupi zaidi cha muda".
"Kulingana na taarifa za awali, idadi kubwa ya malengo ya adui katika anga ya Kyiv yaligunduliwa na kuharibiwa," aliongeza.
Urusi na Iran kupanua ushirikiano wa kijeshi - Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais Putin na Raisi wa Iran Marekani inaona dalili zinazoongezeka kwamba Urusi na Iran zinapanua ushirikiano wa kiulinzi ambao ungeisaidia Moscow kurefusha vita vya Ukraine na pia kuwa tishio kwa majirani wa Iran, Ikulu ya White House ilisema.
"Tunatumia zana tulizonazo kufichua na kusimamisha shughuli hii na tuko tayari kufanya zaidi," John Kirby, mratibu wa kimkakati wa mawasiliano katika Baraza la Usalama la Kitaifa la White House, aliwaambia waandishi wa habari.
Msingi wa usaidizi wa kijeshi wa Iran ni ndege zisizo na rubani, ambazo Urusi hutumia kikamilifu kushambulia eneo la Ukraine, pamoja na makombora ya vifaru na risasi za vifaru . Zaidi ya ndege 400 zisizo na rubani zimewasilishwa tangu Agosti mwaka jana, Kirby alisema.
Kulingana naye, katika siku za usoni Marekani itaweka vikwazo dhidi ya wale wanaohusika na ushirikiano wa kijeshi kati ya Urusi na Iran.
Afrika Kusini na Urusi kuimarisha ushirikiano wa kijeshi – Tass

Chanzo cha picha, Getty Images
Maafisa wa ngazi ya juu wa kijeshi kutoka Afrika Kusini na Urusi wamekubaliana kuimarisha ushirikiano, na kuongeza utayari wa mapambano dhidi ya maadui zao, katika mazungumzo yaliyofanyika mjini Moscow, imenukuliwa wizara ya ulinzi ya Urusiikisema kama ilivyonukuliwa na shirika la habari linalomilikiwa na taifa hilo -Tass.
Mazungumzo ya ngazi ya juu yanakuja siku kadhaa baada ya balozi wa Marekanimjini Pretoria, Reuben Brigety, Afrika Kusini kwa kuipatia Urusi silaha na risasi, licha ya kusema kuwa haiegemee upande wowote katika vita vya Ukraine.
Kamanda wa vikosi vya ardhini wa Afrika Kusini Luteni Jenerali Lawrence Mbatha, aliongoza mazungumzo na mwenzake wa Urusi , Oleg Salyukov, mjini Moscow, limeripoti shirika la habarila Tass.
"Pande mbili zimejadili masuala ya ushirikiano wa kijeshi, na utekelezaji wa miradi ambayo inalenga kuimarisha utayari wa vita wa majeshi ya nchi mbili.
"Mkutano ujao kati ya makamanda ulifikia makubaliano kuhusu upanuzi zaidi wa ushirikiani wa vikosi vya ardhini katika maeneo mbali mbali ," ilinukuliwa wizara ya ulinzi ya Urusi ikisema.
Wiki iliyopita, Afrika Kusini ilijipata katikati ya mzozo wa kidiplomasia na Marekani baada ya Bw Brigety kusema kuwa anaamini kwamba silaha na risasi vilipakiwa katika meli ya Urusi katika ngome ya vikosi vya majini katika mji wa Capetown mwezi Disemba.
Afrika Kusini ilisema kuwa haina rekodi ya mauzo ya silaha, lakini RaisCyril Ramaphosa ameagiza uchunguzi kuchunguza madai hayo.
Katika chapisho lake la kila wiki Jumatatu, Bw Ramapphosa alisema kuwa Afrika Kusini iko chini ya"shinikizo lisilo la kawaida" la kuwa na upande inayouunga mkono katika vita vya Ukraine, lakini haitafanya hivyo katika kile ambacho ni "athari za mashindano kati ya Urusi na Magharibi".
Vikosi vya ulinzi vya Afrika Kusini (SANDF) vimethibitisha kuwa maafisa wa ngazi ya juu wako Moscow kwa sasa.
"Ni lazima ifahamike kuwa Afrika Kusini ina uhusiano wa ushirikiano nan chi mbali mbali barani na nje ya bara," SANDF kilisema katika taarifa, na kuongeza kuwa, safari hiyo ya Urusi ilipangwa vyema kabla.
Muungano mkuu wa upinzani Democratic Alliance (DA) ulisema kuwa ziara ya hivi karibuni ni mfano wa hivi karibubi wa serikali ya Afrika Kusini wa kuonyesha uungaji mkono wake kwa Urusi ‘’bila aibu’.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 16.05.2023
