Mzozo wa Sudan: Jeshi na RSF zalaumiana kwa kutoheshimu makubaliano ya kusistisha vita
Jeshi lilisema lilikuwa linashambulia jiji hilo ili kuwaondoa wapinzani wake wa kijeshi, Kikosi cha (RSF).
Moja kwa moja
Paka aiba vitu vya thamani ya mamia ya pauni kutoka kwa majirani

Chanzo cha picha, DONNA HIBBERT
Mwanamke aliyeaibishwa na paka wake kuiba nguo na chakula mara kwa mara kutoka kwa majirani zake ameingia kwenye Facebook kujaribu kurudisha vitu hivyo.
Paka mwizi, Harry amekuwa akipeleka nyumbani mara kwa mara bidhaa zilizoibwa ikiwa ni pamoja na nguo za ndani, pakiti ya soseji na hata kiatu cha wabunifu katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Katika wiki pekee iliyopita, Harry amechukua vitu sita kutoka kwa majirani huko Darley Abbey, huko Derby. Mmiliki wake, Donna Hibbert, anaamini kwamba Harry anafikiri vitu hivyo ni zawadi.
"Nadhani paka wanapenda kuwaletea wamiliki wao chipsi, hiyo ndiyo saikolojia nyuma yake," alisema. "Mara nyingi ni vitu badala ya ndege au panya."

Chanzo cha picha, DONNA HIBBERT
Anaamini kwamba Harry ameiba takribani vitu vyenye thamani ya pauni 300 kwa miaka mingi. "Kulikuwa na kiatu chekundu, na kilikuwa chapa ya gharama kubwa," alisema. "Sidiria za michezo zinatoka M&S kwa hivyo hazitakuwa nafuu.
"Tulikuwa na mfuko wa fedha siku nyingine lakini hakuna kitu ndani yake." Baadhi ya vitu vimechukuliwa kutoka kwa nyaya, lakini vingine vimechukuliwa kutoka ndani ya nyumba za watu. "Ikiwa anaona fursa, anaichukua," alisema Bi Hibbert. Kakake Harry, Luna, pia huleta vitu vya nyumbani lakini kwa kawaida ni takataka kama vile pakiti nyororo na pakiti za sigara.
Bi Hibbert sasa ameanza kuchapisha vitu vilivyoibiwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Spotted: Darley Abbey. "Nilikuwa na wasiwasi sana kuhusu baadhi ya watu maskini kijijini wakifikiri 'nina uhakika niliweka haya kwenye mstari' au 'nilikuwa na haya nyumbani' na yametoweka," alisema. "Kwenye Facebook jirani yetu aliye karibu nasi aliona chapisho hilo na kusema 'Wao ni vyangu, nilidhani nilikuwa na wazimu'. "Wiki hii tumekuwa na vitu sita tofauti, ambavyo viko kwenye mifuko ya kubebea tayari kurudishwa kwa wamiliki wao."
Rais Ruto:Azimio inafaa kulipa bunge fursa kuendesha mazungumzo

Chanzo cha picha, IKULU YA RAIS KENYA
Rais William Ruto ameutaka Muungano wa Azimio kuepuka ghasia na uharibifu wa mali, huku akitaka timu inayoongozwa na Raila Odinga kukumbatia mazungumzo ya pande mbili bungeni.
Akizungumza wakati wa sherehe za Siku ya Wafanyakazi zilizoandaliwa katika bustani ya Uhuru Gardens Jijini Nairobo Jumatatu,Ruto amesema ni wajibu wake kulinda Haki na mali ya Wakenya wote, akiongeza kuwa ‘hataruhusu uharibifu wa mali’.
“Sitaruhusu uharibifu wa mali kwa sababu kuna mtu anataka tugawanye nchi. Tunataka bora kwa kila mtu. Badala ya vurugu na uharibifu, tuzungumze bungeni. Tunaweza kuwaruhusu wabunge kujadili masuala ya seva,” Ruto ameongeza .
"Tunaheshimu haki za kila mtu. Pia tunaheshimu haki za upinzani na wajibu wao wa kikatiba. Tunajua demokrasia ni nini. Tunajua haki za binadamu ni nini. Sio vurugu,”
Rais pia amesema kazi ya serikali na mashirika ya usalama ni kulinda Haki za Wakenya.
Jana, Kamanda wa eneo la Nairobi aliharamisha maandamano ya muungano wa Azimio la Umoja yaliyopangwa kufanyika Jumanne, Mei 2.
Hata hivyo, muungano huo umethibitisha uamuzi wake wa kuwaongoza wafuasi wake katika maandamano jijini Nairobi, huku wakiwasilisha maombi kwa afisi nne za serikali.
Unaweza pia kusoma
Binti ya Shaquil Barrett, mwenye umri wa miaka miwili afariki kwa kuzama kwenye bwawa la kuogelea, Florida

Chanzo cha picha, Getty Images
Binti wa miaka miwili wa mchezaji wa Tampa Bay Buccaneers NFL alizama kwenye kidimbwi cha kuogelea kwenye nyumba ya familia hiyo Jumapili, mamlaka ilisema.
Maafisa wa polisi waliitikia wito kwamba Arrayah, binti mdogo wa Shaquil Barrett, alianguka kwenye kidimbwi cha maji mwendo wa 09:30 saa za ndani (14:30 BST).
Alipelekwa hospitalini huko Tampa, Florida, na kutangazwa kuwa amefariki.
Mchezaji huyo aliyeshinda Super Bowl akiwa na Buccaneers, Bw Barrett, 30, na mkewe wana watoto wengine watatu.
The Buccaneers ilitoa taarifa juu ya habari "ya kutisha" na "ya kuhuzunisha".
"Ingawa hakuna maneno yanayoweza kutoa faraja ya kweli kwa wakati kama huu, tunatoa msaada na upendo wetu wanapoanza kushughulikia hasara hii kubwa ya kumpoteza Arrayah wao mpendwa."
Polisi walisema uchunguzi unaendelea lakini kifo hicho hakikuaminika kuwa cha kutiliwa shaka.
Bw Barrett anaingia mwaka wake wa tano na Tampa Bay Buccaneers, baada ya kutumia misimu minne ya kwanza ya uchezaji wake na Denver Broncos.
Kwa sasa anauguza jeraha la ililomuweka benchi katika kipindi cha pili cha msimu uliopita.
Maurizio Cattelan: Kazi ya sanaa ya ndizi yaliwa na mgeni wa jumba la makumbusho la Seoul

Chanzo cha picha, getty
Mwanafunzi wa sanaa wa Korea Kusini alikula ndizi ambayo ilikuwa sehemu ya usakinishaji wa msanii Maurizio Cattelan, akisema alikuwa na "njaa" baada ya kukosa kifungua kinywa.
Mchoro uitwao "Mcheshi", sehemu ya onyesho la Cattelan "WE", ulijumuisha ndizi mbivu iliyobandikwa ukutani katika Jumba la Makumbusho la Sanaa la Leeum la Seoul.
Baada ya kula ndizi, mwanafunzi, Noh Huyn-soo, alibandika ganda ukutani.
Jumba la makumbusho baadaye liliweka ndizi mpya katika sehemu moja, vyombo vya habari viliripoti.
Tukio hilo lililochukua zaidi ya dakika moja lilirekodiwa na rafiki wa Bw. Noh.
Jumba la Makumbusho ya Sanaa la Leeum halikujibu barua pepe ya BBC.Hata hivyo, iliambia vyombo vya habari kwamba haitadai fidia dhidi ya mwanafunzi huyo.
Ndizi inayoonyeshwa inaripotiwa kubadilishwa kila baada ya siku mbili au tatu.
Katika video zilizochapishwa mtandaoni, kelele za "samahani" zinaweza kusikika wakati Bw Noh akiondoa ndizi hiyo ukutani.Haitikii na kuanza kula huku chumba kikiwa kimya.
Kisha anafunga ganda hilo ukutani na kusimama kwa muda kabla ya kuondoka.
Mgogoro wa Sudan: Mashambulio ya anga yaikumba Khartoum licha ya kuwepo makubaliano ya kusitisha vita

Chanzo cha picha, ANADOLU AGENCY VIA GETTY IMAGES
Mashambulizi ya anga yameathiri mji mkuu wa Sudan, Khartoum, licha ya mapatano yaliyolenga kuwaruhusu raia kukimbia hadi maeneo salama.
Jeshi lilisema lilikuwa linashambulia jiji hilo ili kuwaondoa wapinzani wake wa kijeshi, Kikosi cha (RSF).
Mapigano hayo yalizidi kupamba moto huku pande zinazozozana zikisema kwamba zitaongeza muda wa makubaliano hayo kwa siku tatu nyingine.
Zaidi ya vifo 500 vimeripotiwa huku idadi halisi ya majeruhi ikiaminika kuwa kubwa zaidi.Mamilioni ya watu bado wamenaswa mjini Khartoum.
Kamanda wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na mkuu wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana zaidi kama Hemedti, wanawania mamlaka - na hawakubaliani hasa kuhusu mipango ya kujumuisha RSF katika jeshi.
Majenerali hao walikubali kusitisha mapigano kwa sababu za kibinadamu baada ya juhudi kubwa za kidiplomasia za nchi jirani, Marekani, Uingereza na Umoja wa Mataifa.Makubalino hayo hata hivyo hayajapelekea kusistishwa kwa vita .
Hata hivyo, bado haijafahamika ni nini watafanya katika hatua inayofuata ya makubaliano yaliyofikiwa na upatanishi wa Marekani na Saudi, kulingana na jeshi.
Nchi hiyo sasa inapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe, anasema mfanyabiashara na Mhisani wa Sudan Mo Ibrahim, na mzozo wake haufai kuruhusiwa kuenea katika nchi jirani .
"Hatutaki Syria nyingine," aliambia BBC, na kuongeza kuwa ilikuwa vigumu kwa kila upande kushinda moja kwa moja.
Unaweza pia kusoma:
- Mapigano Sudan: Hakuna mazungumzo mpaka mashambulio ya mabomu yakome, Hemedti aiambia BBC
- Omar al-Bashir: Hivi ndivyo Sudan inavyolipa gharama za mateso ya miaka 30 ya utawala wake
- Mgogoro wa Sudan: Majenerali wanaopigania hatima ya Sudan
Vita vya Ukraine : Urusi yafanya shambulio la pili la makombora ya masafa usiku kwa siku ya tatu

Chanzo cha picha, SERHIY LYSAK
Urusi imefanya msururu wa mashambulio ya makombora ya masafa dhidi ya Ukraine, likiwa ni shambulio la pili la usiku wa manane kwa siku ya tatu.
Mtu mmoja ameuawa katika jimbo la Kherson na watu wengine 25, wakiwemo watoto watatu – wamejeruhiwa jimbo la Dnipropetrovsk.
Vikosi vya Ukraine vilisema kuwa makombora 15 kati ya 18 yaliyofyatuliwa yalizuiwa na mifumo ya ulinzi ya nchi hiyo.
Moja ya maeneo yaliyolengwa ulikuwa ni mji wa Pavlohrad katika Dnipro – alisema afisa mmoja aliyeteuliwa na Urusi ambaye aliongeza kuwa raslimali za mashambulio za Ukraine zilipigwa.
Akiandika kwenyeujumbe wa Telegram wenye ishara ya kidole gumba juu, Vladimir Rogov alisema kuwa makombora yalilenga reli na hifadhi za mafuta ya petroli.
Jengo la gorofa kumi na tisa, nyumba 25 za kibinafsi, shule sit ana shule za chekechea pamoja na maduka matano viliharibiwa.
Kwa muda mrefu jeshi la Ukraine limekuwa likizungumzia kuhusu mashambulio ya ulipizaji kisasi – bila kuelezea ni wapi na ni lili yatafanyika.
Urusi imefanya msururu wa mashambulio ya makombora ya masafa dhidi ya Ukraine, likiwa ni shambulio la pili la usiku wa manane kwa siku ya tatu.
Mtu mmoja ameuawa katika jimbo la Kherson na watu wengine 25, wakiwemo watoto watatu – wamejeruhiwa jimbo la Dnipropetrovsk.
Vikosi vya Ukraine vilisema kuwa makombora 15 kati ya 18 yaliyofyatuliwa yalizuiwa na mifumo ya ulinzi ya nchi hiyo.
Moja ya maeneo yaliyolengwa ulikuwa ni mji wa Pavlohrad katika Dnipro – alisema afisa mmoja aliyeteuliwa na Urusi ambaye aliongeza kuwa raslimali za mashambulio za Ukraine zilipigwa.
Akiandika kwenyeujumbe wa Telegram wenye ishara ya kidole gumba juu, Vladimir Rogov alisema kuwa makombora yalilenga reli na hifadhi za mafuta ya petroli.
Jengo la gorofa kumi na tisa, nyumba 25 za kibinafsi, shule sita na shule za chekechea pamoja na maduka matano viliharibiwa.
Kwa muda mrefu jeshi la Ukraine limekuwa likizungumzia kuhusu mashambulio ya ulipizaji kisasi – bila kuelezea ni wapi na ni lili yatafanyika.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
'Uzani wangu mwili haukunizuia kuwa mwanamitindo wa mavazi'

Chanzo cha picha, Jennifer Enujiugha
Kila mara wanapozungumzia kuwa ‘modellling’ au kuonyesha urembo wa mitindo ya mavazi , kinachokuja akilini ni mwanamke mwenye umbo jembamba na uzani mdogo wa mwili.
Hatahivyo sivyo Jennifer Enujiugha ameamua kuonyesha kuwa sio lazima iwe hivyo wakati wote.

Chanzo cha picha, Jennifer Enujiugha
Bi Enujiugha ana umbo kubwa la mwili, lakini pia ni mwanamitindo anayeonyesha mavazi, katika kitengo cha maonyesho ya mitindo ya mavazi, ambacho Waingereza wanakiita ‘’Plus size modelling’’.

Chanzo cha picha, Jennifer Enujiugha
Akizungumza na BBC Bi Jennifer alielezea jinsi alivyopitia matusi mengi, na kukosolewa sana katika makuzi yake kwasababu alikuwa mnene.
Nilikuwa ninapenda kuwa mwanamitindo wakati wote, lakini nilihisi kukosa kujiamini’’, alisema.

Chanzo cha picha, Jennifer Enujiugha
Hatahivyo baadaye anasema alipata kampuni iliyokuwa inawatafuta wanawake wanene au ‘Plus size model’, ikamuajiri.
‘’Kwa sasa nahisi kana kwamba siwezi kuishi bila kuwa mwanamitindo wa mavazi’’.
Bi Jeniffer ana maono ya kuanzisha kampuni ya maonyesho ya mitindo ya mavazi na kuwaajiri wanawake wanene, ili kuwapatia fursa ya kuwa wanamitindo.
Anawashauri wanawake wanene kutokuwa na hofu ya kubadili maumbile yao na badalake wajivunie walivyooumbwa.
Francisco Oropeza: FBI inamsaka mshukiwa 'mwenye silaha na hatari’ aliyehusika na shambulio la risasi Texas

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wakala wa FBI alimtaja Francisco Oropeza, 38, kama mshukiwa "mwenye silaha na hatari". Shirika la upelelezi la Marekani FBI limesema kuwa linamsaka mwanaume mmoja anayeshutumiwa kuwauwa watu watano katika eneo moja la Texas baada ya mabishano kuhusu kitendo chake cha kufyatua risasi katika eneo jirani.
Mshukiwa huyo Francisco Oropeza, 38, ana "silaha na ni hatari", amesema wakala wa FBI agent.
Anadaiwa kuwafyatulia risasi majirani zake baada ya kumuomba aache kufyatua risasi kwasababu walikuwa wakijaribu kumlaza mtoto wao mchanga.
Wahanga walikuwa wote kutoka Honduras, na alikuwemo mtoto wa miaka minane miongoni mwao.
Kwa sasa wametambuliwa kama Sonia Argentina Guzman, 25; Diana Velazquez Alvarado, 21; Julisa Molina Rivera, 31; Jose Jonathan Casarez, 18; and Daniel Enrique Laso, 8.
"Yuko kule nje, ni tisho kwa jamii," Wakala maalumu wa FBI Houston James Smith aliwaambia waandishi wa habari.
Vita vya Ukraine: Makombora 18 yanayosafiri yalifyatuliwa Ukraine; 15 kati yake yalidunguliwa- APU

Chanzo cha picha, RUSSIAN DEFENCE MINISTRY WEBSITE
Maelezo ya picha, jaribio la kombora linaloongozwa akulenga eneorlikifyatuliwa katika eneo la ncha ya kaskazini ya Urusi (picha ya maktaba) Jeshi la Ukraine limethibitisha kwamba katika usiku wa Mei 1, jeshi Urusi lilishambulia Ukraine kwa ndege za kimkakati na kufyatua 18 X-101/X-555 makombora ya anga yanayoongozwa kulenga shabaha.
Kulingana na taarifa ya mkuu wa majeshi ya Ukraine aliyoiandika kwenye mtandao wa Facebook, shambulio hilo lilianza usiku wa saa nane unusu na vilipuzi vya mabomu aina ya Tu-95 vilitumiwa katika jimbo la Olenegorsk region , na vingine aina ya Tu-160s viliwekwa katika eneo la Bahari ya Caspian.
"Vikosi vya Ukraine kwa kutumia njia za ulinzi wa anga viliangamiza makombora 15!" – kulingana na wavuti wa Zaluzhny.
Awali, utawala wa Kyiv uliripoti kwamba maroketi yote yaliyofyatuliwa katika mji huo mkuu yalidunguliwa.
Wizara ya ulinzi ya Urusi bado haijatoa kauli yoyote kuhusiana na shambulio la lao la makombora nchini Ukraine.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Anayeshukiwa kuwa mkuu wa kundi la Islamic State Qurayshi auawa ndani ya Syria, Uturuki yasema

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Vikosi vya Uturuki vinaendesha operesheni dhidi ya makundi ya Jihadi kaskazini mwa Syria Vikosi vya Uturuki vimemuua mtu anayeshukiwa kuwa ni kiongozi wa kikundi cha Islamic state(IS) nchini Syria, ametangaza Rais Recep Tayyip Erdogan
Abu Hussein al-Quraysh inasemekana kuwa alikuwa amechukua uongozi wa kikundi hicho baada ya mtangulizi wake kuuawa mwaka jana.
Bw Erdogan ameliambia shirika la utangazaji la uturuki TRT Turk kwamba kiongozi wa IS ali "sawazishwa’’ katika operesheni iliyofanywa na shirika la ujasusi la Uturuki MIT siku ya Jumamosi.
IS haijatoa kauli yake hadi sasa kuhusiana na operesheni iliyotangazwa.
BBC bado haijathibitisha kuhusu dai la Rais Erdogan.
Shirika la ujasusi la Uturuki MIT limekuwa ikimfuatilia Qurayshi kwa "muda mrefu", alisema Bw Erdogan.
"Tutaendelea na mapambano yetu na mashirika ya ugaidi bila ubaguzi wowote," aliongeza, bila kutoa taarifa zaidi.
Vyanzo vya habari vya Syria vilivyonukuliwa na Shirika la habari la Reuters vilisema kuwa operesheni hiyo ilifanyika katika mji wa kaskazini wa Jandaris, karibu na mpaka wa Uturuki.
Mwezi Novemba mwaka jana kundi la hilo la jihad lilitangaza kifo cha kiongozi wake, Abu al Hassan al-Hashemi al- Quraysh.
Marekani ilisema kuwa aliuliwa katika operesheni iliyotekelezwa na waasi wa Syria kundi la kijeshi la Syria-Free Syrian Army, kusini -magharibi mwa nchi hiyo mwezi wa Oktoba mwaka 2022.
Mzozo wa Ukraine: Papa Francis asema anashiriki katika mpango wa upatikanaji wa amani nchini Ukraine

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Papa alifanya mkutano na waandishi wa habari akiwa ndani ya ndege Papa francis amesema kuwa Vatican inashiriki katika majaribio ya kupata amani nchini Ukraine.
Baada ya ziara yake nchini Hungary, kiongozi huo wa Kanisa Katoliki aliwaambia waandishi wa habari kuhusi hayoakiwa ndani yandege kuelekea Itali. Papa alisema ni vigumu kujadili hali katika Ukraine na waziri mkuu wa Hungury Viktor Orban.
“Unaweza kufikiria kwamba wakati wa mikutano hii hatukuongelea kuhusu tu mambo madogo ya kawaida. Tulijadili mambo yote,” alisema Papa. “Kila mtu ana nia katika njia ya amani. Kazi inaendelea, lakini bado haijawekwa wazi kwa umma. Nitawafanhamisha wakati itakapokuwa wazi kutangazwa kwa umma.
Jumanne, Papa Francis alikutana na Waziri mkuu wa Ukraine Denys Shmyhal mjini Vatcan.
Kulingana na mkuu wa serikali ya Ukraine , walijadili"formula ya amani" ya Rais Volodymyr Zelensky, ambayo, miongoni mwa mambo mengine, inahusisha ukombozi wa maeneo yote yaliyotwaliwa na Urusi, adhabu ya wahali wa kivita na fidia kwa uharibifu uliosababishwa kwa nchi na Urusi.
Shmyhal pia alisema kuwa alimualika Papa aizuru Kyiv.
Jumamosi, Papa alikutana na wakimbizi katikamji mkuu wa Hungury Budapest, ambao wengi wao walikuwa ni Waukraine. Ijumaa , pia alitoa wito wa "kubuniwa kwa ujenzi wa juhudi za amani" nchini Ukraine, lakini hakuelezea hasa nini alichokimaanisha.
Papa Francis akisisitiza mara kwa mara kuhus amani nchi nchini Ukraine na kuiita nchi ya mashahidi .
Hatahivyo, baadhi wanamkosoa kwa kutowahi hata mara moja kuilaani moja kwa moja Urusi kwa uvamizi, mauaji ya maelfu ya watu na kuiangamiza nchi Jirani.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Mapigano Sudan :Tawi la benki Kuu ya Sudan likiungua moto
Video imeonekana ikionyesha tawi la Benki kuu ya Sudan likiungua moto huku mapigano yakiendelea kote mjini Khartoum.
BBC haijaweza kuthibitisha tarehe ambayo picha hii ya video ilichukuliwa.
Jumapili, mashambulio ya anga yaliongezeka katika mji huo licha ya kufikiwa kwa makubaliano yaliyolenga kuwaruhusu raia kukimbia.
Jeshi lilisema kuwa linaushambulia mji ili kuwatimua mahasimu wao wa jeshi la dharura - Rapid Support Forces (RSF).
Maelezo ya video, Khartoum branch of Sudan Central Bank in flames Unaweza pia kusoma:
- Mapigano Sudan: Hakuna mazungumzo mpaka mashambulio ya mabomu yakome, Hemedti aiambia BBC
- Omar al-Bashir: Hivi ndivyo Sudan inavyolipa gharama za mateso ya miaka 30 ya utawala wake
- Mgogoro wa Sudan: Majenerali wanaopigania hatima ya Sudan
Mzozo wa Sudan: Vurugu katika bandari huku maelfu wakiharakisha kuondoka nchini
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Lyse Doucet
- Nafasi, Mwandishi mkuu wa kimataifa

Chanzo cha picha, AFP VIA GETTY IMAGES
Maelezo ya picha, Waliookolewa wakiwa wamepumzika njiani huku meli ya kikosi cha Majiniya Saudia ikisafiri kutoka bandari ya Port Sudan kuelekea Jeddah Port Sudan inaendelea kuwa bandari muhimu katikati ya mzozo wa Sudan. Mwandishi mkuu wa BBC wa kimataifa Lyse Doucet amejiunga na shuhghuli ya hivi karibuni ya uokoaji wa watu wa hivi karibuni kutoka Sudan hadi Jeddah
Katika usiku wa manane,huku meli ya HMS Al Diriyah ikikaribia mwambao wa Sudan, maafisa wa Saudia wanawasha taa ili kuwasaka na kuwaokoa wasafiri kwa kutumia meli yao ya kivita ambayo ilibadilishwa haraka kuwa chombo kikuu cha uokozi na cha shughuli za kibinadamu katika mzozo unaendelea kuongezeka wa Sudan.
Ingawa ilikuwa nis aa nane usiku meli nyingine mbili pia zilikuwa zinatia nanga kwenye mwambao katika bandari ya Port Sudan, ni bandari kubwa zaidi, zikisubiri muda wao katika juhudi hizi za kimataifa za uokozi.
"Ninajihisi kuwa mwenye ahueni lakini pia nahisi huzuni kuwa sehemu ya historia hii," ananiambia Hassan Faraz kutoka Pakistan, huku akionekana kutetemeka. shaken.
Tuifika Saudia mwisho wa safari iliyotuchukua saa 10- katika safari iliyokuwa ya usiku mzima katika meli ya HMS Al Diriyah kutoka bandari ya mji wa Saiudia wa Jeddah.
Kikundi kidogo cha waandishi wa habari wa kigeni kilipewa fursa ya nadra ya kuingia ndani yan chi iliyokumbwa na vita ya Sudan, mwa muda mfupi.
"Watu watakuwa wakizungumza kuhusu matukio haya kwa miaka mingi inayokuja," Faraz alikumbuka, huku msururu mrefu wa watu waliojipangakwa ajili ya ukajguzi wa paspoti zao kwa ajili ya kuingia Saudia.
Mara hii walikuwa wengi ni vijana wafanyakazi kutoka Kusini mwa Asia ambao walisema wamekuwa wakisubiri hapa kwa siku tatu - baada ya wiki mbili ngumu wakiwa ndani ya mapigano.
Mapigano ambayo yaliibuka katika wiki za hivi karibuni nchin Sudan, yameendelea licha ya pande zinazohasimiana kuweka muda wa kusitisha mapigano.

Unaweza pia kusoma:
- Mapigano Sudan: Hakuna mazungumzo mpaka mashambulio ya mabomu yakome, Hemedti aiambia BBC
- Omar al-Bashir: Hivi ndivyo Sudan inavyolipa gharama za mateso ya miaka 30 ya utawala wake
- Mgogoro wa Sudan: Majenerali wanaopigania hatima ya Sudan
Hujambio na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 01.05.2023

