Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Polisi Kenya wamkamata kiongozi mwingine anayeshukiwa kuongoza dhehebu tata na kuwaokoa 31

Maafisa wa upelelezi katika Kaunti ya Nakuru nchini Kenya wanamshikilia mwanamke mwenye umri wa miaka 62 anayeshukiwa kuwa kiongozi wa kikundi cha Army Rurwama, ambacho kimewashikilia watu 32 ndani ya nyumba.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa.

  2. Polisi Kenya wamkamata kiongozi mwingine anayeshukiwa kuongoza dhehebu tata, na kuwaokoa 31

    Maafisa wa upelelezi katika Kaunti ya Nakuru nchini Kenya wanamshikilia mwanamke mwenye umri wa miaka 62 anayeshukiwa kuwa kiongozi wa kikundi cha Army Rurwama, ambacho kimewashikilia watu 32 ndani ya nyumba kwa ajili ya ushirika, kufunga na maombi, vimeripot vyombo vya habari nchini humo.

    Watu hao 31, ambao walikuwa katiia nyumba iliyopo katika kijiji cha Kamwene 'B' Kihingo, katika kaunti ndogo ya Njoro , wanasemekana kuwa walikuwa dhaifu baada ya kufunga chakula kwa karibu wiki moja, kulingana na polisi .

    Mshukiwa aliyetambuliwa kwa jina la Hellen Wanjiru Weri alikamatwa katika uvamizi wa Jumamosi, kufuatia ripoti iliyotolewa na mkazi wa Moi's Bridge katika Kaunti ya Uasin Gishu

    Mwanamke huyo anasema kuwa binti yake ambaye alikuwa amepata kazi kama muuguzi wa kijamii katika zahanati , alikataa kuripoti kazinina badala yake alisafirihadi Njoro kwa ajili ya kufanya maombi na kufunga.

    Gazeti la Nation, limesema limeshuhudia ripoti ambapo mwanamke huyo amefungwa katika nyumba ya Bi Wanjiru kwa siku kadhaa, bila kula chakula kwa ajili ya kufanya maombi na kufunga.

  3. Afya: Mtoaji wa mbegu za uzazi za kiume aliyezalisha watoto zaidi ya 550 aamrishwa kukomea hapo

    Mwanaume Mholanzi aliyeshukiwa kwa kuzalisha watoto zaidi ya 550 kote duniani kupitia utoaji wa msaada wa mbegu za kiume za uzazi ameagizwa akomee kapo .

    Mwanaume huyo kwa jina Jonathan, mwenye umri wa miaka 41, anaweza kupigwa faini ya zaidi ya Euro 100,000 (£88,000) iwapo atajaribu tena kutoa msaada wa mbegu zake za uzazi.

    Alikuwa amezuiwa kutoa mbegu za uzazi kwenye klinini ya masuala ya uzazi nchini Uholanzi mwaka 2017, baada ya kufahamika kuwa alikuwa amezalisha watoto zaidi ya 100.

    Lakini badala ya kuacha kuendelea na utoaji wa msaada huo, Jonathan aliendelea kutoa mbegu zake nje ya nchi yake na kwa njia ya mtandao.

    Mahakama ya Uholanzi mjini The Hague imemwambia atoe orodha ya kliniki zote alizotumia na kuziagiza ziharibu mbegu zake.

    Mwanaume huyo inasemekana aliwapotosha wanawake.

    Miongozo ya kliniki ya Uholanzi inasema kuwa mtoaji wa msaada wa mbegu za uzazi za kiume hapaswi kuwa baba wa zaidi ya watoto 25 katika familia 12.

    Kliniki zinaagizwa kupunguza kiwango cha huduma zao, ili kupunguza nafasi ndugu wa damu moja kuoana na kuwa na watoto pamoja.

    Lakini jaji majaji walisema mwanaume huyo amesaidia kuzalisha watoto kati ya 550 na 600 tangu alipoanza kutoa mbegu zake za uzazi mwaka 2007.

    Unaweza pia kusoma:

    • Sababu 5 za kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume duniani
    • Utafiti: Wasiwasi kutokana na kushuka kwa kiwango na ubora wa mbegu za kiume Ulaya na Marekani
    • Utafiti waonesha kuna umuhimu wa kuvuna manii kutoka kwa waliokufa
    • Je kuna hatari gani ya kupata mtoto baada ya kutimu umri wa miaka 40 na zaidi?
  4. Tajiri Jack Ma ' kufundisha katika chuo kikuu cha uongozi cha Rwanda'

    Chuo kikuu cha masuala ya uongozi cha kiafrika- African Leadership University (ALU) kimetangaza kuwa tajiri Mchina Jack Ma ambaye ni muasisi wa kampuni ya biashara ya mauzo ya mtandaoni- Alibaba Group, amechaguliwa kuwa mwalimumgeni katika chuo hicho kilichopo mjini Kigali.

    Tovuti ya Chuo hicho kikuu inamnukuu, muasisi wake, Dr Fred Swaniker, akisema kuwa amefurahiakuwa wawekezaji vijana wa Afrika wanaosomea katika chuo hicho“sasa watapata fursa ya kufunzwa na mmoja wa wawekezaji wakubwa zaidi duniani”.

    Jack Ma – ambaye wakati mmoja alikuwa ndiye mtu tajiri zaidi nchini China – anaripotiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na uongozi wa Uchina baada ya kukosoa baadhi ya utendaji wake.

    Jack Ma binafsi hajadhibitisha wazi madai ya chuo hiki cha kibinafsi, lakini , hivi karibuni ulitangaza kuwa Ma anarejea tena ‘’kufanya mambo aliyanayoyapenda” – kufundisha – kazi “aliyokuwa akiifanya kabla ya kuanzisha kampuni ya Alibaba”.

  5. Nyumba ya Papa Wemba sasa yawa rasmi makumbusho ya rumba

    Miaka saba baada ya kifo cha Papa Wemba, serikali ya Congo imeamua hatimaye kutekeleza ahadi yake.

    Ijumaa, waziri wa Sanaa na urithi rasmi alikabishinyumba ya nyota huyo wa rumba iliyopo mjini Kinshasa Taasisi ya taifa ya Makumbusho ya Congo, ambayo itaigeuza kuwa nyumba ya ruma ya Congo .

    Studio ya kurekodi pia itawekwa ndani yake, amesema waziri.

    Miaka miwili iliyopita, rumba ya congo ilipata hadhi ya kulindwawakati ilipoongezwa katika orodha Urithi usioshikika wa utamaduni wa binadamuya Unesco.

    Akifahamika kwa jina la jukwani kama Papa Wemba, Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba alikuwa ni mmoja wa waimbaji wa Kicongo ambao waliupekela ladha yamuziki wa Kiafrika wenye ushawishi kwenye jukwa la dunia kutoka kwenye eneo lake la asili, Congo-Brazzaville na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

    Mnamo mwaka 2016 Papa Wemba alifariki akiwa jukwani huku akitumbuiza mashabiki wake Ivory Coast, baada ya kufanya kazi ya muziki kwa miongo minne.

    Kuna ahadi moja ambayo serikali ya Congo bado haijaitimiza – kuweka sanamu ya ukumbusho wa Papa Wemba.

  6. Vita vya Ukraine: Tanki ya mafuta ya Crimea yachomwa moto kwa drone

    Shambulio la droni imesababisha moto mkubwa kuwaka katika hifadhi ya mafuta iliyopo katika jimbo la Crimea, wamesema maafisa wa eneo hilo.

    Picha za mitandao ya kijamii inaonyesha miali ya moto ilitanda katika eneo laSevastopol, mji mku wa Crimea,mapema Jumamosi.

    Baadaye moto ulizimwa na hakuna mtu aliyeumia, alisema gavana aliyeteuliwa na Moscow.

    Ijumaa Urusi ilianzisha wiki la mashambulio ya anga katikamiji kote Ukraine, na kuwauwa takriban watu 25. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa shambulio hilo kufanyika mingikwa kipindi cha miezi .

    Rasi ya Crimean, ambalo lilitwaliwa na Urusi mwaka 2014, ni eneo lenye ngome kuu ya vikosi vya majini ya Urusi iliyopo kwenye ufukwe wa Bahari Nyeusi.

  7. Mapigano Sudan : Hali ya hivi punde kabisa nchini

    Licha ya kuongezwa rasmi kwa muda wa usitishaji mapigano wa saa 72 nyingine, mapigano nchini Sudan yameingia wiki ya tatu.

    • Khartoum: Mji mkuu wa Sudan umekuwa ukipigwa na mashambulio ya anga, vifaru na makombora. Jeshi la Sudan limekuwa likituma ndege aina ya jet au dronikwa mahasimu wao wa vikosi vya dharura- Rapid Support Forces (RSF) , katika maeneo jirani mbali mbali katika mji mkuu, na hivyo kusababisha hali kuwa mbaya zaidi kwa wakazi ambao wana kiasi kidogo cha umeme, mafuta, maji na chakula.
    • Miji iliyopo karibu na Khartoum: Mapigano yanaendelea katika miji iliyopo karibu na mji mkuu Khartoum, mkiwemo Bahri na Ombdurman, kulingana na shirka la habari la Reuters. Katika Omdurman, vikosi vya RSF vimeripotiwa kushutumu jeshi kwa kuvunja mkataba kwa mashambulio kwenye ngome zake zilizo mjini.
    • Darfur: katika jimbo la magharibi la Darfur, jiji la El Geneina limeshuhudia wapiganaji wakipora na kuchoma nyumba na benki. Madaktari wanasema takriban watu 74 wameuawa katika mashambulizi pale wiki hii. Maelfu ya watu wanatoroka jimbo hilo na kuvuka mpaka wakiingia Chad.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mapigano Sudan: Hakuna mazungumzo mpaka mashambulio ya mabomu yakome Hemedti aiambia BBC
    • Mzozo wa Sudan: Mgogoro wa Sudan unaweza kuisha kwa njia hizi tatu
  8. Mapigano Sudan Safari ndefu, ya kuchosha kutafuta usalama

      • Author, Lyse Doucet
      • Nafasi, Mwandishi Mkuu wa Kimataifa, akiripoti kutoka Jeddah

    Amanah ni boti la hivi karibuni kuwasili katika ngome ya kijeshi ya King Faisal Naval iliyopo Jeddah kama sehemu ya juhudi kubwa za kuwaokoa watu kutoka Sudan.

    Imekuwa ni safari ndefu, nay a kuchosha ya saa 12 kuvuka Bahari Nyekundu kutoka Port Sudan kwa wasafiri wote zaidi ya 2000 kutoka mataifa 80 – wakiwemo Wasaudia na Wairan.

    Lakini imekuwa ni mapito ya kufikia usalama katika chombo hiki kilichowabeba raia chenye chapa ya jeshi la Saudi Arabia.

    Wasafiri wanapunga mkono na kutabasamu kwa juu juu tu. Wanaosubiri kwenye sehemu ya chini ni wanadiplomasia wanaosubiri kuwapokea raia wao wakiwa na mabasi ya kifahari na vikosi vya Saudia vya kuwasindikiza.

    Kuna maua ya kuwakaribisha lakini pia viti vya magurudumu na magari ya kuwabebea wagonjwa waliojeruhiwa na kuugua waliotoroka vita vya Sudan.

    Sawa na nchi nyingine katika kanda hii, Saudi Arabia ina maslahi ndani ya Sudan lakini kwa sasa dola zenye nguvu zaidi duniani zinakusanyika kwa pamoja kuzungumza kwa kauli moja – kwa dharura kili kumaliza vita.

    Unaweza pia kusoma:

    • Mapigano Sudan: Hakuna mazungumzo mpaka mashambulio ya mabomu yakome Hemedti aiambia BBC
    • Mzozo wa Sudan: Mgogoro wa Sudan unaweza kuisha kwa njia hizi tatu
  9. Rais wa Brazil Lula azitambua hifadhi 6 za wazawa

    Rais wa Brazil Luiz Inácio Lula da Silva ameidhinisha hifadhi mpya sita za jamii ya wazawa , na kuzuia uchimabi wa madini na kuweka masharti ya biashara y kilimo pale.

    Ardhi- hiyo ni pamoja na eneo kubwa ya msitu wa mvua wa Amazon – unaochukua eneo la hekta zipatazo 620,000 (sawa na mita milioni 1.5).

    Viongozi wa wazawa wameafiki hatua hiyo, lakini wakasema maeneo zaidi yanahitaji ulinzi.

    Lula, ambaye aliingia mamlakani Januari, ameahidi kuondoa sera za mtangulizi wake wa mrengo wa kulia Jair Bolsonaro, ambaye aliendelea uchimbaji wa madini karika ardhi za wazawa asilia wa Brazil. Umati wa wazawa walikusanyika katika mji mkuu Brasília, kushuhudia tukio la kurudishiwa kwa ardhi yao.

  10. Vita vya Ukraine: idadi ya vifo vilivyotokana na mashambulio ya Urusi katika Uman yaongezeka

    Wafanyakazi wa huduma za tahadhari nchini Ukaine (GSChS) cwanaendela kusaka miili ya watu na kuondoa vifusi vya jengo la gorofa lililopigwa na kombora la Urusi Ijumaa.

    Taasisi ya huduma za dharura iliripoti kwamba moto uliwaka kwenye paa la nyuma tena – na moto huo ulisambazwa zaidi na upepo. Waokoaji wanafanya kazi ya kuudhibiti moto, kulingana na ripoti za gazeti la "Suspilne.

    Idadi ya watu waliofariki imefikia 23. Wakati huo huo, wakat iwa utambuzi wa miili ya watu waliokufa, iligundulika kuwa kulikwa na watoto watano miongoni mwao, ilieleza wizara ya mambo ya nje ya Ukraine.

    Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  11. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yate ya mubashara ya leo Jumamosi tarehe 29.04.2024