Mzozo wa Sudan: Mataifa yaendelea kuwaondoa raia wake Sudan huku mapigano yakiendelea
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema kuwa pande zinazohasimiana nchini Sudan zimekubali kusitisha mapigano kwa muda wa saa 72 kuanzia saa nne usiku kwa saa za eneo, siku ya Jumatatu.
Moja kwa moja
Mazungumzo ya amani ya Ethiopia yaanza Visiwani Zanzibar
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Alfred Lasteck
- Nafasi, BBC News, Dar es Salaam

Chanzo cha picha, FACEBOOK/QE'EE OROMOO
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na Oromo Liberation Army (OLA) yameanza Visiwani Zanzibar, nchini Tanzania, kamanda wa waasi ameithibitishia BBC.
Hii ni mara ya kwanza kwa serikali ya Ethiopia kufanya mazungumzo rasmi na OLA baada ya miaka mingi ya mzozo.
Hakuna maelezo yoyote ambayo yametolewa kufikia sasa kuhusu muundo wa mazungumzo hayo au ni nani atakuwa mpatanishi kati ya pande hizo mbili.
Marekani, Norway, Sweden na Kenya zinasemekana zimekuwa zikizisukuma pande hizo mbili kumaliza kwa amani uhasama katika eneo kubwa la Oromia nchini humo ambako wakazi wengi ni Oromos, kabila kubwa zaidi la Ethiopia.
Kundi la OLA limekuwa likipambana na vikosi vya serikali tangu lilipojitenga na kundi la waasi mwaka 2018.
Mazungumzo hayo yanakuja takriban miezi sita baada ya serikali ya Ethiopia kufikia makubaliano ya amani ya kumaliza vita vya miaka miwili vya umwagaji damu katika eneo la kaskazini la Tigray.
Afrika Kusini inatazamia kujiondoa katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Afrika Kusini anasema chama tawala cha African National Congress (ANC) kinataka nchi hiyo kuondoka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Cyril Ramaphosa aliutaja uamuzi huo kuwa wa busara, ikizingatiwa kwamba - kama alivyoiweka - mahakama imezitendea baadhi ya nchi isivyo haki.
Lakini ni mchakato ambao unaweza kuchukua hadi miaka miwili.
Marekebisho yaliyopendekezwa ya sheria yatakuwa wazi kwa maoni kwa Waafrika Kusini wote kabla ya kwenda bungeni kujadiliwa.
Mahakama ya ICC imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vyake dhidi ya Ukraine. Anasemekana kuhusika na uhamishaji haramu wa watoto wa Ukraine na kuwapeleka nchini Urusi.
Kama mwanachama wa ICC, Afrika Kusini itakuwa na wajibu wa kumkamata Bw Putin iwapo atahudhuria mkutano wa kilele wa nchi za Brics Afrika Kusini mwezi Agosti.
Mgogoro Sudan: Familia zinasubiri habari za wapendwa wao

Mwanamke ambaye familia yake imenasa nchini Sudan eneo liliokumbwa na vita anasema "hajaacha kulia" wakati anasubiri habari juu yao.
Sherien Elsheikh kutoka Bristol alisema mumewe, wazazi na dada wamenaswa nchini na hawawezi kutoroka.
Zaidi ya watu 400 wamefariki katika mapigano kati ya makundi hasimu ya kijeshi nchini humo.
Serikali ya Uingereza ilisema inaanza kuwahamisha raia wa Uingereza, lakini kwa Bi Elsheikh anasema uchungu unabaki. "[Mume wangu] amejifungia ndani ya nyumba, hawezi kutoka hata kidogo. Mama yangu, baba yangu na dada zangu - wote wapo, kwa hivyo ninahisi uchungu mwingi. "Mapigano ni karibu nao kiasi kwamba hawawezi kwenda kununua chakula.
Wanaogopa sana. "Sijaacha kulia tangu jana."
Pia kuna mfadhaiko mkubwa. Baada ya kuwasiliana na ubalozi wa Sudan mjini London, na kujaza fomu kwa matumaini kuwa zitasaidia mumewe, alisema hajasikia lolote kutoka kwa maafisa wa serikali. "Barua pepe ya uthibitisho kutoka kwao, ndivyo tu."

Maelezo ya picha, Fadhalraman Mohamed Kama Bi Elsheikh, Fadhalraman Mohamed kutoka Bristol pia ana wasiwasi na habari: "Mke wangu alienda huko takriban siku 25 zilizopita na alikuwa anarudi leo. "Lakini kwa kila kitu [kinaendelea], tunangojea na tunashangaa yuko wapi sasa. "Tuna watoto watano na wana wasiwasi sana. Hata asubuhi hii hawataki kwenda shule. "Kila wakati wanaendelea kutazama habari kuhusu yeye. "Inasikitisha sana na ngumu sana kwangu kufanya kazi, unajua?

Maelezo ya picha, Mohammed Elsharif, Ili kuzisaidia familia, Mohammed Elsharif, kutoka Jumuiya ya Sudan ya Bristol, alisema atatafuta usaidizi kutoka kwa wabunge wa eneo hilo. "Nitawasiliana nao wote. "Nadhani ni kupitia Ofisi ya Mambo ya Nje pekee ambapo mawasiliano yanaweza kutokea na watu hawapati majibu yoyote kutoka kwa ubalozi wa Sudan pia, kwa hivyo hali ngumu sana."

Mgogoro wa Sudan: Kundi la kwanza la raia wa Kenya laondolewa Sudan
Kundi la kwanza la Wakenya kutoka Sudan iliyokumbwa na vita limewasili Nairobi kwa ndege ya kijeshi Jumatatu usiku.
Kundi hilo lilikuwa na Wakenya 19, Wasomali 19 na raia mmoja wa Saudi Arabia ambao wote walisafiri kwa barabara hadi Sudan Kusini ambako walipanda ndege hiyo ya kivita.
Waziri wa Ulinzi Aden Duale, alisema wote walikuwa wanafunzi wanaosoma katika chuo kikuu cha kimataifa nchini Sudan.
"Ninawapongeza watu hawa kwa kufanya safari ndefu na ninashukuru timu zinazohusika katika kuwezesha harakati zao. Serikali imejitolea kuhakikisha kuwa Wakenya wanarejea salama kutoka Sudan," alisema Duale.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni Alfred Mutua alishukuru nchi zilizowaruhusu Wakenya kuvuka mipaka kutoka Sudan na kuruhusu ndege za Kenya kuruka juu ya anga zao kutekeleza zoezi hilo.
Wakimbizi zaidi watasafirishwa kwa ndege hadi Nairobi siku zijazo na timu ya maafisa wa kijeshi ambao wanaongoza zoezi hilo kwa ushirikiano na maafisa wa Masuala ya Kigeni.
Serikali hiyo tayari imetambua Wakenya 3,000 nchini Sudan na inawataka wanaohitaji kuhamishwa kusajili majina yao, maeneo na nambari zao za pasipoti kwenye simu za dharura ili mipango muhimu ifanywe.
Kundi linalofuata la wahamishwaji litajumuisha kundi la wanafunzi 29 waliovuka mpaka na kuingia Ethiopia baada ya kutoroka Sudan.

Habari za hivi punde, Joe Biden athibitisha kuwania tena urais wa Marekani mwaka 2024
Rais wa Marekani Joe Biden amethibitisha kuwa atagombea tena uchaguzi wa Uraisi wa mwaka 2024. Tangazo hilo limetolewa katika video ya matangazo.
Mwishoni mwa wiki, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kwamba Joe Biden amemchagua mshauri wake mkuu wa White House Julie Chavez Rodriguez kama meneja wake wa kampeni.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyoambatana na video ya uzinduzi wa Jumanne, Biden alithibitisha kuchaguliwa kwa Rodriguez, mshirika wa muda mrefu wa Latina Democratic na uhusiano na Rais wa zamani Barack Obama na Makamu wa Rais Kamala Harris.
Quentin Fulks, ambaye hapo awali aliwahi kuwa meneja wa kampeni kwa Seneta wa Georgia Raphael Warnock katika kinyang'anyiro kinachofuatiliwa kwa karibu mwaka jana, atahudumu kama naibu wa Rodriguez.
Wenyeviti-wenza wa kitaifa wa kampeni hiyo - viongozi wa awali ambao watakuwa muhimu kwa maandalizi na juhudi za kujitolea - ni baadhi ya waungaji mkono wa Biden wenye msimamo na wa muda mrefu. Hao ni pamoja na Jim Clyburn, mbunge wa South Carolina ambaye uidhinishaji wake unasifiwa sana kwa kumkuza Biden kwenye uteuzi mnamo 2020; Gavana wa Kidemokrasia wa Michigan Gretchen Whitmer; na Chris Coons na Lisa Blunt Rochester, wabunge kutoka jimbo la nyumbani la Biden la Delaware.
Tangaraju Suppiah: Ahukumiwa kunyongwa kwa kujihusisha na ulanguzi wa bangi

Chanzo cha picha, TRANSFORMATIVE JUSTICE COLLECTIVE
Singapore inatazamiwa kunyongwa kwa mwanamume kwa kosa la ulanguzi wa bangi, katika hukumu ya hivi punde ya kutatanisha katika jiji hilo.
Wanaharakati wanasema Tangaraju Suppiah alitiwa hatiani kwa ushahidi dhaifu. Mamlaka zinasema alipokea utaratibu uliotazamiwa, na wamepanga kunyongwa kwake Jumatano.
Singapore ina baadhi ya sheria kali zaidi za kupambana na dawa za kulevya, ambayo inasema ni muhimu kulinda jamii.
Katika siku za hivi karibuni wanafamilia wake na wanaharakati waliwasilisha barua kwa rais wa Singapore Halimah Yacob katika ombi la dakika za mwisho la kuhurumiwa, wakati bilionea wa Uingereza Sir Richard Branson ametoa wito wa kusitishwa kwa hukumu hiyo na kuangaliwa upya kwa kesi hiyo. "Ninajua kuwa kaka yangu hajafanya kosa lolote. Ninaiomba mahakama iangalie kesi yake tangu mwanzo," dadake Tangaraju, Leela Suppiah, aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano na wanahabari.
Tangaraju, 46, alipatikana na hatia ya juu ya uwasilishaji wa kilo 1 (35oz) ya bangi kutoka Malaysia hadi Singapore mnamo 2013.
Ingawa hakukamatwa wakati wa kusafirisha, waendesha mashitaka walisema alikuwa na jukumu la kuratibu. Tangaraju alidai kuwa yeye sio mtu anayewasiliana na watu wengine waliohusishwa na kesi hiyo.
Alisema alipoteza simu moja na kukana kumiliki ya pili.
Sheria ya Singapore inaamuru adhabu ya kifo kwa ulanguzi wa dawa za kulevya na ina adhabu ndogo kwa wasafirishaji. Katika rufaa ya mwisho ya Tangaraju, hakimu alikubaliana na upande wa mashtaka kwamba Tangaraju ndiye aliyehusika kuratibu utoaji huo, jambo ambalo lilimfanya asistahili kupewa adhabu ndogo zaidi.
Rwanda inavyotumia ndege zisizo na rubani kupambana na malaria
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Yves Bucyana
- Nafasi, BBC Swahili

Rwanda Nchi ya Kwanza barani Afrika Kutumia teknolojia ya ndege zisizo na rubani katika juhudi za kupambana na malaria.
Ndege hizo zinanyunyiza dawa za kuuwa mbu katika maeneo ya mabonde,kwa mujibu wa Taasisi ya Taifa ya Afya (RBC).
Tangu kuanzishwa kwa matumizi ya teknolojia hiyo mwaka 2021, ugonjwa wa malaria ulipungua kwa zaidi ya asilimia 90% katika maeneo yanayofanyiwa majaribio.
Bwana Kamali Paul, ambaye ni msimamizi wa ugonjwa wa malaria katika kampuni ya Charis, anasema wanatumia ndege hizo kwa sababu teknolojia yake inaruhusu kunyunyiza dawa katika eneo kubwa sana na kwa muda mfupi
''kabla ya kunyunyiza dawa kwanza ndege hii inatengeneza ramani ambayo inatusaidia kujua hasa sehemu yenye maji machafu yenye mayai ya mbu.sehemu hii ya kilimo cha mpunga huwa ni kiini cha mbu unaosababisha malaria.tukishapata picha hiyo inaturahisishia kazi ya kunyunyiza dawa.halafu inanyunyiza katika eneo kubwa na kwa muda mchache’’alisema
Kampeini ya kunyunyiza dawa za kukabiliana na mbu imeleta hali ya afueni miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo waliozungumza na BBC waliokuwa wamezongwa na malaria.
''Malaria sasa ni historia kwangu.Mimi pamoja na watoto tulikuwa tumezongwa na malaria.Binafsi nilikuwa naugua malaria kama mara tatu ndani ya mwezi moja lakini tangu waanze kunyunyiza dawa,sijaugua ama kuuguza malaria tena imepita miezi mitatu sasa.’’Alisema Bi Musabyima.

Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Afya (RBC), maeneo ambayo hunyunyiziwa dawa za kukabilia na mbu unaosababisha malaria huchaguliwa kwa sababu ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Kwa takwimu, Dk Emmanuel Hakizimana, ambaye anasimamia udhibiti wa malaria katika wizara ya afya anasema kuwa vita dhidi ya Malaria kwa kutumia ndege zisizo na rubani vinaleta matokeo ya kuridhisha katika maeneo ''tunayofanyia majaribio''
‘’Kwa kweli mafanikio ni makubwa –kwanza mbu unaosababisha malaria ulipungua kwa zaidi ya asilimia 85 kadhalika malaria ilipungua kwa zaidi ya asilimia 90.
Hakika matumizi ya ndege zisizo na rubani yamekuja kusaidia sana mkakati tuliokuwa nao wa kunyunyiza dawa kwenye majumba ya watu na pia matumizi ya vyandarua'' alisema Dk Hakizimana
Wizara ya afya ya Rwanda imesema inapanga kupanua kampeini ya kunyunyiza dawa dhidi ya mbu unaosababisha malaria kwa kutumia ndege zisizo na rubani katika wilaya nyingine tano zinazokabiliwa na ugonjwa huo.
Kenya: Waziri wa usalama kutembelea msitu walipozikwa wafuasi wa kanisa tata lililowaagiza waumini kufunga hadi kufa

Chanzo cha picha, REX/SHUTTERSTOCK
Waziri wa usalama nchini Kenya Kithure Kindiki anatarajiwa kutembelea msitu wa Shakahola hii leo ambako miili 26 zaidi ilifufuliwa. Polisi na mashirika ya kutetea haki za binadamu wanahofia kuwa idadi ya miili itaendelea kuongezeka.
Kiongozi wa dhehebu tata, Paul Makenzie Nthenge ambaye kwa sasa yuko mahabusu, huku akisubiri kesi yake, aliwaagiza wafuasi wake wafunge kula chakula hadi kufakama ''njia ya moja kwa moja ya kwenda kwa mumba wao kwa haraka.
Jumla ya miili 73, ya wafuasi wa dehebu la Paul Makenzie, imekwishafufuliwa.
Mwandishi wa BBC aliyeko katika mji wa pwani ya Kenya wa Malindi, Dorcas Wangira anasema inaaminiwa pakubwa kwamba bado kuna watu zaidi katika msitu wa heka 800 wa Shakahola na wanaendelea kufunga kula chakula.
Eneo hilo la msitu limetangazwa kuwa eneo la tukio la uhalifu na uchunguzi unaendelea leo.
Polisi wanamchunguza zaidi mshiriki mwingine wa uhalifu ambaye walikamatwa jana. Walimtambua kama msaidizi wa kiongozi wa dhehebu tata.
Anashutumiwa kuizika miili na kuwaziba pumzi ya kupumua watoto.
Hifadhi ya maiti iliyopo karibu, ya hospitali ya Kaunti ndogo ya Malindi kwa sasa haina uwezo wa kupokea miili zaidi.
Unaweza pia kusoma:
- Paul Makenzi:Mhubiri huyu alianzaje safari tata ya kuwashawishi watu kufunga hadi kufa?
Hali ya utulivu Sudan huku makundi hasimu yakiheshimu makubaliano ya usitishaji mapigano

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Hakuna taarifa za mashambulio ya bunduki na mitaa ya Khartoum imesalia kuwa tulivu kwa kiasi kikubwa Hali ya utulivu imeendelea kushuhudiwa katika mji mkuu wa Sudan Khartoum huku makubaliano ya usitishaji mapigano ya saa 72 yakizingatiwa baina ya vikosi vya serikali - Sudanese Armed Forces (SAF) na kundi la kijesjhi la Support Forces (RSF).
Televisheni ya Saudia- Al-Arabiya TV Jumanne asubuhi ilisema kuwa mkataba huo umeheshimiwa hadi sasa na ‘’ hakuna malalamiko ya ukiukwaji".
Hapakuwa na taarifa za milio ya bunduki na mitaa ya Khartoum imebaki mitupu.
Watu saba waliripotiwa kuuawa katika shambulio la ndege kusini mwa mji mkuu, kabla ya kutangazwa kwa makubaliano hayo, shuhuda aliuambia mtandao wa habari wa Darfur 24 kwamba makumi ya watu walijeruhiwa kutokana na shambulio la ndege lililolenga eneo la makazi la Kalakla.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepanga kukutana Jumanne kujadili mzozo wa Sudan huku serikali za kigeni zikiendelea kuwaondoa kwa ndege raia wake nje ya nchi.
Unaweza pia kusoma:
- Wagner: Mamluki wa Urusi wamekuwa wakifanya nini Sudan?
- Mgogoro wa Sudan: Kwa nini Misri ipo katika njia panda juu ya mapigano Sudan?
Sudan: Serikali ya Uingereza kuanza kuwahamisha raia wake

Uingereza itaanza kuwahamisha Waingereza kutoka Sudan, serikali imetangaza. Familia zilizo na watoto, wazee na watu walio na hali ya kiafya zitapewa kipaumbele.
Vikosi vya kijeshi vya Uingereza vitatekeleza "operesheni hiyo tata," alisema Waziri Mkuu Rishi Sunak.
Makundi hasimu ya kijeshi yalikubali kusitishwa kwa mapigano kwa saa 72 kuanzia Jumatatu usiku nchini humo, ambapo takriban watu 400 wameuawa katika mapigano tangu tarehe 15 Aprili.




Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza James Cleverly alisema maafisa wameanza kuwasiliana na raia wa Uingereza. Mawaziri wamezidi kushinikizwa kusaidia takriban raia 2,000 kukimbia mapigano makali.
Bw Sunak alielezea uhamishaji huo kama "mkubwa" na alitoa pongezi kwa wanajeshi ambao wanatekeleza operesheni hiyo kuanzia Jumanne.
Takriban raia 4,000 wa Uingereza wanafikiriwa kuwa nchini Sudan na 2,000 kati yao tayari wameomba msaada, waziri wa mambo ya nje Andrew Mitchell alisema Jumatatu.
Siku ya Jumapili, Uingereza iliwasafirisha kwa ndege wanadiplomasia na familia zao kutoka Sudan katika operesheni ya kijeshi.
Unaweza pia kusoma:
- Wagner: Mamluki wa Urusi wamekuwa wakifanya nini Sudan?
- Mgogoro wa Sudan: Kwa nini Misri ipo katika njia panda juu ya mapigano Sudan?
Rais Ndayishimiye azungumza na marais wastaafu

Chanzo cha picha, NTARE RUSHATSI
Maelezo ya picha, Kuanzia kushoto: Domitien Ndayizeye, Evariste Ndayishimiye na Sylvestre Ntibantunganya Katika tukio lisilo la kawaida, marais wa zamani wa Burundi Sylvestre Ntibantunganya na Domitien Ndayizeye wamefanya mazungumzo na Rais Evariste Ndayishimiye kuhusu maendeleo na uongozi wan chi, vimeripoti vyombo vya habari vya Burundi.
Ni nadra kwa kiongozi aliyeko madarakani nchini Burundi, na katika baadhi ya mataifa ya maziwa makuu kufanya mazungumzo na watanguli wake.

Chanzo cha picha, NTARE RUSHATSI
Maelezo ya picha, Kuanzia kushoto: Pascasie Minani,Mke wa Ntibantunganya, Angeline Ndayishimiye na Oda Ndayizeye Picha ya wake wa marais hawa watatu wakiwa pamoja pia ilichapishwa kwenye mitandano ya kijamii ya ofisi ya rais wa Burundi.
Mazungumzo ya Rais Evariste Ndayishimiye na marais wa zamani yalirekodiwapamoja na picha zaona kutangazwa Jumatatu.
Walizungumza kuhusu ‘’utawala bora na maendeleo ya wananchi’’
Kulingana naorodha ya kiwango cha maendeleo cha Umoja wa Mataifa (HDI) , Burundi ni miongoni mwa nchi tano masikini zaidi duniani, lakini serikali ya Gitega haikubaliani na hilo.
Rais Evariste Ndayishimiye alisikika akiwaambia wananchi kuwa “Burundi ni moja ya nchi zinazoitunza dunia sana”, na kwamba “hawahitaji dola ”
Vyama vya upinzani nchini Burundi vinalaumu utawala wa chama tawala cha CNDD-FDD kwa kutokubali hali halisi ya wananchi na kuitafutia suluhu, na badala yake dkuonyesha picha nzuri ambayo sio halisi.
Politico: White House inahofia athari za kushindwa kwa mashambulio ya Ukraine ya ulipizaji kisasi kwa Urusi

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Jeshi la Ukraine linapewa mafunzo na wakufunzi kutoka nchi tofauti. Lakini hakuna anayejua ni nini watakachofanya Gazeti la Politicoto leo la Marekani Jumatatu lilichapisha data zake kuhusu jinsi Ikulu ya Marekani White House ina wasiwasi wa mashambulio ya Ukraine ya kulipiza kisasi kwa Urusi, na jinsi wanavyojiandaa kuyafanya iwapo yatashindwa.
Wakosoaji wanawalaumu maafisa wa sasa wa Marekani kwa hilo.
Kwa sasa Rais Joe Biden ametoa hakikisho la wazi la usaidizi wa silaha na wa kiuchumi kwa Ukraine hadi watakapokuwa hawauhitaji tena.
Lakini kama operesheni ijayo ya Ukraine ya kuyachukua tena maeneo yaliyonyakuliwa na Urusi haitazaa matunda, utawala wa Biden utalazimika kushughulikia athari zake nyumbani (Marekani), limeandika gazeti la Politico.
Kwa upande mmoja, White House itashambuliwa na wakosoaji ambao watamshutumu rais kwa kutoipatia Ukraine silaha za kutosha.
Na kwa upande mwingine, wanaounga mkono usitishaji mapigano wa mapema, watasema haiwezekani kuifukuza Urusi kabisa kutoka kwenye maeneo iliyoyatwaa kwa muda mfupi.
Na hili hata halikuzingatia jinsi washirika wa Marekani wa Ulaya watakavyojibu.
Maafisa wa utawala wanasisistiza kuwa wanafanya kila liwezekanalo kuisaidia Ukraine kufanikiwa katika mashambulio ya kukabiliana na uvamizi wa Urusi.
“Tumetimiza karibu kila maombi ambayo Ukraine imetuomba kwa ajili ya silaha na vifaa muhimu,” mmoja wa maafisa ambaye hakutajwa jina alituma ujumbe. Lakini nyuma ya pazia, kuna hofu kuhusu ni kwa kiwango gani jeshi la Ukraine ni imara inapokuja katika masuala ya mikakati, aliongeza
Wakati huo huo, mwezi Machi Rais Zelensky alisema kuwa mashambulio dhidi ya Urusi hayakuanza kwasababu Ukraine haikuwa na vifaru na risasi za kutosha
Politico lilirejelea hofu za hivi karibuni kutoka kwa maafisa wa Marekani ambazo zilitambuliwa kutokana na kuvuja kwa nyaraka za siri za pentagon ambazo zilionekana kwenye intaneti baada ya kuvuja.
Walisema kwamba, kulingana na ujasusi wa Marekani, jeshi la Ukraine linaweza kupata mafanikio fulani katika maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi, lakini hakuna uwezekano mkubwa wa kufikia mengi ya malengo yake.
Kwa kuzingatia nyaraka, Marekani inashuku kwamba jeshi la Ukraine litaweza kuvunja vizuizi vya kuelekea Crimea, lakini wana matumaini kuwa jeshi la Ukraine litaharibu mifumo ya usambazaji wa silaha ya Urusi.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Mzozo wa Ukraine: Iran inatuma makombora na risasi Urusi kwa njia ya bahari - Wall Street Journal

Chanzo cha picha, IRANIAN ARMY/GETTY IMAGES
Katika kipindi cha miezi sita, Iran ilituma makombora 300,000 na risasi kar*ibu milionikutoka kwenye bandari zake katika Bahari ya Caspian kuelekea Urusi, limeandika gazeti la Wall Street Jumatatu.
Gazeti hilo la Marekani, limeelezea kuwa vyanzo vyake vya taarifa hii vilikuwa ni vya Mashariki ya Kati ambavyo viliwaonyesha waandishi wa habari nyaraka zinazothibitisha taarifa hii.
Hadi sasa, vyombo vya habari vinaripoti kuhusu usafirishaji wa silaha kuelekea Urusi vingi vikiangazia zaidi droni zilizosafirishwa na ndege, lakini pia kumekuwa na usafirishaji wa silaha kwa njia ya Bahari ya Caspian – kama gazeti la WSJ linavyosema, kulikuwa na ripoti hizo kwa mfano katika kituo cha televisheni cha Uingereza cha Sky News.
Kulingana na gazeti hilo, mzigo wa makombora ulitumwa kutoka kwenye bandari ya Iran ya Bandar Amirabad kuelekea Astrakhan mapema mwezi wa Machi: meli ya mizigo ya Urusi Rasul Gamzatov tilisafirisha makombora 2,000 kupitia maeneo mbali mbali ya Bahari ya Caspian.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Mzozo wa Sudan: Pande zinazohasimiana zakubaliana kusitisha mapigano

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Msichana akisubiri kuondoka Khartoum Waziri wa mambo ya nje wa Marekan Antony Blinken amesema kuwa pande zinazohasimiana nchini Sudan zimekubali kusitisha mapigano kwa muda wa saa 72 kuanzia saa nne usiku kwa saa za eneo, siku ya Jumatatu.
Hii ni mara ya tatu kutangazwa kwa usitishaji wa mapigano tangu ghasia zilipoibuka nchini humo mwezi huu lakini haujawahi kutekelezwa hata mara moja.
Bw Blinken alisema kuwa makubaliano yamefikiwa baina ya jeshi la kundi la wanajeshi la Rapid Support Forces (RSF) baada ya saa 48 za mazungumzo.
Takriban watu 400 wameuawa tangu mapigano yaibuke tarehe 15 Aprili.
Pande zote zimetangazauhusika wake katika usitishaji wa mapigano.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametahadharisha kuwa ghasia nchini Sudan zina hatari ya kusababisha"janga la moto" ambalo linaweza kusambaa katika kanda yote na nje yake.
Tangu ghasia zianze, wakazi wa mji ulikokumbwa na mapigano wa Khartoum wamekuwa wakiambiwa wakae majumbani mwao, na maji na chakula vimekuwa vikipungua.
Makombora yamepiga miundombinu muhimu kama vile mifumo ya maji, ikimaanisha kuwa baadhi ya watu wamelazimika kunywa maji kutoka Mto Nile.
Kutakuwa na matumaini kuwa usitishaji wa mapigano utawawezesha raia kuondoka katika mji mkuu.
Serikali za kigeni pia zitakuwa na matumaini kwamba zitaweza kuendelea kuwaondoa watu wake nje ya Sudan.
Unaweza pia kusoma:
- Wagner: Mamluki wa Urusi wamekuwa wakifanya nini Sudan?
- Mgogoro wa Sudan: Kwa nini Misri ipo katika njia panda juu ya mapigano Sudan?
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo, tarehe 25.04.2023


