Azimio kurejelea maandamano baada ya Ramadhan - Raila Odinga

Kiongozi wa muungano wa Azimio Raila Odinga ametangaza kuwa muungano huo utarejelea maandamano ya kuipinga serikali baada ya Ramadhan.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi and Asha Juma

  1. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu ya leo

  2. DR Congo: Hakuna mazungumzo na waasi wa M23, Rais Tshisekedi

    .

    Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Rais wa Uswizi Alain Berset nchini humo, Rais wa DRC alisisitiza kwamba hakutakuwa na "mazungumzo ya kisiasa" na kundi la waasi la M23.

    Alisema kilichokubaliwa wakati wa mchakato wa amani ni kwamba kundi la waasi lazima liangamizwe huko Kichanga, mji wa Jimbo la Kivu Kaskazini, na kusafirishwa kwa ndege karibu na Kindu, katika Mkoa wa Maniema ambapo waasi lazima watimuliwe na kurejea katika maisha ya kiraia na wanajeshi wa Angola watakaotumwa hivi karibuni.

    Kauli hiyo inawadia siku moja, baada ya Rais Tshisekedi kukutana na João Lourenço, Rais wa Angola na mpatanishi wa Umoja wa Afrika wa mgogoro wa Ukanda wa Maziwa Makuu.

    Kulingana na M23, kundi lenye silaha linalotawaliwa na Wakongo-Watutsi, vuguvugu lao lilianza kujiondoa katika maeneo waliyoyakalia mapema mwezi huu, wakisubiri mazungumzo na serikali.

    Eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lenye machafuko lina makundi yenye silaha yasiyopungua 100.

    Jumuiya ya Afrika Mashariki ilipeleka wanajeshi kutoka nchi nne Kenya, Burundi, Sudan Kusini na Uganda kwa ajili ya kuwaondoa na kurejesha kundi la M23 katika maisha ya kiraia, ambao walianza mapigano tena katikati ya mwaka jana, baada ya miaka kumi uhamishoni.

  3. Bayern Munich yamsimamisha Sadio Mane na kumtoza faini kwa 'kumpiga' mchezaji mwezake

    w

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Bayern Munich imemsimamisha Sadio Mane baada ya kumpiga usoni mchezaji mwenza Leroy Sane kufuatia kichapo cha Jumanne cha Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City.

    Mane pia atapigwa faini na hatakuwa sehemu ya kikosi cha Bayern kwa ajili ya mchezo wao wa nyumbani wa Bundesliga dhidi ya Hoffenheim Jumamosi.

    Sky Germany iliripoti kuwa mdomo wa Sane ulikuwa ukivuja damu baada ya ugomvi huo na wachezaji hao wawili walihitaji kutenganishwa na wenzao kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

    Taarifa kutoka Bayern ilisema: "Sadio Mane, 31, hatakuwepo kwenye kikosi cha FC Bayern kitakachocheza nyumbani dhidi ya 1899 Hoffenheim Jumamosi ijayo.

    Sababu ni utovu wa nidhamu wa Mane baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa FC Bayern dhidi ya Manchester City.

    Aidha, Mane atatoa faini.

    "Sane na Mane walionekana uwanjani wakizozana katika hatua za mwisho za mechi hiyo Jumanne usiku, ambapo City waliwafunga mabingwa hao wa Ujerumani mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Etihad katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

  4. Azimio kurejelea maandamano baada ya Ramadhan - Raila Odinga

    .

    Kiongozi wa muungano wa Azimio Raila Odinga ametangaza kuwa muungano huo utarejelea maandamano ya kuipinga serikali baada ya Ramadhan.

    Alisema ingawa muungano huo unaunga mkono mazungumzo yanayoendelea, utafanya maandamano huku mazungumzo yakiendelea.

    "Mazumgumzo iendelee na maandamano sambamba...dawa ya moto ni moto, kwa hivyo tunaendelea," Raila alisema.

    Alisema atatangaza hatua inayofuata baada ya mwisho wa mfungo wa Ramadhani ambayo inatarajiwa kuisha Aprili 21.

    Hili linajiri baada ya Kenya kushuhudia utulivu kwa wiki kadhaa tangu kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kutangaza kufutilia mbali maandamano ya kuipinga serikali ili kutoa fursa kwa mazungumzo na upande wa serikali.

    Muungano wa Azimio wakati huo ulisema uko tayari kwa mazungumzo kuhusu masuala walioibua endapo serikali iko itakuwa tayari kufanya majadiliano.

    Baadhi ya mambo muhimu ambayo upinzani ulitaka kushughulikiwa ni pamoja na:

    • Kuundwa kwa tume ya Uchaguzi ya IEBC isioegemea upande wowote
    • Mkurugenzi wa idara ya jinai kusitisha uchunguzi na kukamatwa kwa waandamanaji
    • Kupunguzwa kwa gharama ya maisha
    • Kufunguliwa kwa Seva ya tume ya Uchaguzi IEBC

    Kwa upande wake, Rais wa Kenya William Ruto alichukua hatua na kumtaka kiongozi wa upinzani Raila Odinga kusitisha maandamano na kukubaliana na mojawapo ya matakwa ya Bw Odinga ya ushirikiano wa pande mbili bungeni kuhusu kuundwa kwa tume mpya ya uchaguzi, IEBC.

    Soma zaidi:

  5. Navalny: Mpinzani wa Putin ana ugonjwa wa kushangaza ambao unaweza kuwa sumu ya polepole - msemaji wake

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Alexei Navalny, mwanasiasa mashuhuri wa upinzani nchini Urusi, anapambana na ugonjwa wa kushangaza akiwa jela ambao unaweza kuwa sumu ya polepole na amepungua kilo 8 kwa zaidi ya mbili, msemaji wake amesema.

    Navalny aliitiwa Ambulensi usiku wa siku ya Ijumaa kuamkia Jumamosi hadi koloni ya ulinzi ya juu kabisa ya IK-6 huko Melekhovo, karibu kilomita 250 (maili 115) mashariki mwa Moscow, ambako anazuiliwa, kulingana na achombo cha habari cha Reuters.

    Kira Yarmysh, msemaji wake, alisema katika video kwenye Twitter iliyoambatana na muziki wa asili.

    Alisema malalamiko ya tumbo yalikuwa yameongezeka siku ya Ijumaa na kwamba madaktari wa magereza walimtibu siku za nyuma kwa kumchoma sindano ya dawa ambayo walikataa kuisema.

    "Hatuondoi uwezekano wa kwamba kwa wakati huu Alexei Navalny anatiwa sumu polepole, akiuawa polepole ili watu wasijue," Yarmysh alisema kwenye chapisho la Twitter.

    "Anazuiliwa katika chumba cha adhabu akiwa na maumivu makali bila msaada wa matibabu," alisema.

    Alipoulizwa kuhusu madai kwamba Navalny anaweza kuwekewa sumu polepole, Kremlin ilisema haifuati hali ya afya yake na kwamba ni suala la huduma ya kifungo cha shirikisho.

    Huduma ya wafungwa, ambayo hapo awali ilikanusha madai kwamba wafanyikazi wake walimtendea vibaya Navalny na imesema kila mara amekuwa akipatiwa matibabu inapohitajika, haikujibu mara moja ombi la Reuters la kutoa maoni.

    Navalny, ambaye anatumikia kifungo cha pamoja cha miaka 11-1/2 kwa ulaghai na kudharau mahakama kwa mashtaka ambayo anasema yaliwekwa ili kumnyamazisha, alisema kupitia Twitter siku ya Jumanne kwamba alikuwa amerejeshwa katika kifungo cha upweke na kulazimishwa kuvumilia " hali mbaya sana".

    Yarmysh alisema alipatwa na maumivu kama hayo ya tumbo mnamo Januari baada ya kutibiwa kwa dawa za kuua virusi na alikuwa amepungua tena uzito mwingi.

    Serikali ya Ujerumani ilisema Jumatano ina wasiwasi mkubwa juu ya hali mbaya ya kiafya ya Navalny.

    Hata hivyo, Reuters imesema kuwa haikuweza kuthibitisha kwa uhuru hali ya afya ya Navalny.

    pia unaweza kusoma zaidi kilichowahi kutokea Navalny:

  6. Mahakama ya Marekani yaruhusu upatikanaji wa dawa ya kutoa mimba ya mifepristone kwa sasa

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Dawa ya mifepristone imeidhinishwa kutumika nchini Marekani kwa miongo miwili

    Mahakama ya rufaa ya Marekani imezuia kwa muda uamuzi wa jaji wa Texas wa kusitisha kibali cha serikali cha upatikanaji wa dawa ya kutoa mimba inayotumiwa sana.

    Mifepristone - moja ya dawa mbili zinazotumiwa kutoa mimba - iliidhinishwa na Utawala wa Chakula na Dawa na imeruhusiwa kwa zaidi ya miaka 20.

    Vidonge vya kuavya mimba sasa ndiyo njia ya kawaida ya kuavya mimba, inayotumiwa katika zaidi ya nusu ya utoaji mimba wote nchini Marekani.

    Uamuzi huu unamaanisha ufikiaji wake utadumishwa lakini kwa vizuizi kadhaa.

    Zinajumuisha hitaji la kutembelea daktari ili kupata dawa na kupunguza matumizi yake hadi wiki saba za kwanza za ujauzito kutoka kwa 10 za sasa.

    Wakosoaji wa uamuzi wa Jaji wa Texas Matthew Kacsmaryk wanasema utafungua mlango wa changamoto kwa dawa zingine zilizoidhinishwa nchini Marekani na pia inaweza kukandamiza maendeleo ya dawa za siku zijazo.

    Katika uamuzi wake wa Aprili 8, Jaji Kacsmaryk aliamuru kuondolewa kwa dawa ya mifepristone sokoni katika muda wa siku saba, akisema FDA ilikuwa imekiuka sheria za shirikisho ambazo ziliruhusu idhini ya kuharakishwa ya baadhi ya dawa.

    Agizo hilo lilipangwa kuanza kutekelezwa siku ya Ijumaa.

    Idara ya Haki na mtengenezaji wa dawa za kulevya waliomba kusitishwa kwa dharura kwa uamuzi huo Jumatatu, wakiiomba mahakama isitishe uamuzi wa hakimu.

    Idara ya Haki na mtengenezaji wa dawa za kulevya waliomba kusitishwa kwa dharura kwa uamuzi huo Jumatatu, wakiiomba mahakama isitishe uamuzi wa hakimu.

    Uamuzi wa jaji wa Texas - ambaye aliteuliwa na Rais wa zamani Donald Trump - uliwadia baada ya Mahakama ya Juu kuondoa ulinzi wa kikatiba wa utoaji mimba mwaka jana, na kusababisha wimbi la marufuku ya serikali kwa jimbo.

    Soma zaidi:

  7. Sudan yatiwa hofu na kutumwa kwa wanajeshi 'hatari'

    .

    Chanzo cha picha, Anadolu Agency via Getty Images

    Hali ya wasiwasi imetanda nchini Sudan baada ya jeshi kushutumu kikosi chenye nguvu cha kijeshi kwa kukusanya wanajeshi katika mji mkuu, Khartoum na miji mingine, na kupeleka wanajeshi bila idhini ya uongozi wa vikosi vya jeshi.

    Mzozo kuhusu kuunganishwa kwa Vikosi vya (RSF) katika jeshi umezidisha mzozo wa kisiasa nchini Sudan, miaka minne baada ya jeshi kumpindua rais wa muda mrefu Omar al-Bashir.

    Katika taarifa iliyotolewa mapema leo kwenye Shirika la Habari la Sudan (Suna), Jeshi la Sudan (SAF) lilionya kwamba kutumwa kwa kikosi cha RSF "ni ukiukaji wa wazi wa sheria" na "bila shaka kutasababisha migawanyiko na mivutano zaidi ambayo inaweza kusababisha kuharibika kwa usalama wa nchi”.

    Jeshi liliongeza kuwa uwepo mkubwa wa kikosi cha RSF "ulizua hofu na wasiwasi miongoni mwa raia, kuzidisha hatari za usalama, na kuongeza mvutano kati ya vikosi vya kawaida".

    Maendeleo hayo yanazua hofu ya makabiliano ya kijeshi kati ya jeshi na RSF yakichochewa na mzozo wa madaraka kati ya kiongozi wa jeshi la wanamgambo Jenerali Mohamed Hadan Dagalo na kiongozi wa mapinduzi ya Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

    Jana, jeshi la SAF liliripotiwa kuizuia kikosi cha RSF kusimama katika eneo karibu na Uwanja wa Ndege wa Merowe kaskazini mwa Sudan, ambao ni mwenyeji wa Jeshi la Anga la Sudan.

  8. DR Congo: Yasitisha kampuni ya uchimbaji madini ya China huku 16 wakikamatwa

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    DR Congo imesitishata shughuli za kampuni ya uchimbaji madini ya China katika Mkoa wa Tshopo kaskazini na kuwakamata wafanyakazi 16 huku kukiwa na mapitio ya shughuli za uchimbaji madini nchini humo.

    "Xing Jiang Mining ilikuwa na leseni ya kufanya uchunguzi wake lakini haikuwa na kibali cha kuendesha shughuli za uchimbaji madini. (...) Lakini kwa bahati mbaya, tuligundua kuwa kampuni hii ilikuwa inaendesha shughuli za uchimbaji madini na ndiyo maana tukaiita uendeshaji shughuli haramu."

    Waziri wa Madini wa Mkoa, Annelle Kamba alinukuliwa akisema na Radio Okapi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.

    Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi hivi karibuni alitoa wito wa kuangaliwa upya kwa mkataba wa uchimbaji madini na China.

    Pia unaweza kusoma:

  9. Nigeria yasema Tinubu ataapishwa licha ya kesi mahakamani

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri wa Habari wa Nigeria Lai Mohammed anasema rais mteule Bola Tinubu ataapishwa tarehe 29 Mei licha ya kesi mahakamani kupinga ushindi wake.

    Makundi ambayo hayajaridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 25 Februari yanaitisha serikali ya mpito huku Rais anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari akiondoka madarakani rasmi mwezi Mei.

    Bw Mohammed alisema "hakuna msingi" wa katiba ya serikali ya mpito.Alisema vyama vya siasa vya upinzani vina haki ya kupinga uchaguzi wa urais mahakamani

    Wagombea wanne wa urais waliwasilisha mapingamizi ya kisheria tarehe 21 Machi dhidi ya ushindi wa Bw Tinubu, kwa madai kuwa kulikuwa na wizi wa kura na udanganyifu .

    Inachukua takriban miezi minane kwa mahakama kuamua ombi la uchaguzi wa urais.Ombi lazima lisikilizwe ndani ya siku 180 tangu siku lilipowasilishwa.

    Mlalamishi anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama katika Mahakama ya Rufaa ndani ya siku 21 kutoka tarehe ya uamuzi.

    Iwapo walalamikaji hawajaridhika na uamuzi wa mahakama ya rufaa, unaotolewa ndani ya siku 60, wana siku 21 za kukata rufaa katika Mahakama ya Juu, ambayo uamuzi wake ni wa mwisho.

  10. Mahakama ya kijeshi ya Uganda yawahukumu kifungo cha miaka 10 Wakenya 32

    g

    Chanzo cha picha, Col.Deo Akiiki/Twitter

    Raia 32 wa Kenya wamehukumiwa kifungo cha miaka10 na mahakama ya kijeshi yenye makao yake katika wilaya ya kaskazini mwa Uganda ya Moroto.

    Naibu msemaji wa jeshi la Uganda Kanali Deo Akiiki amethibitisha taarifa hii.

    Walipatikana na hatia ya kumiliki bunduki na risasi kinyume cha sheria, makosa yanayoshtakiwa katika Mahakama ya kijeshi nchini Uganda.

    Kila kosa lina adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela. Mahakama iliamuru Jumatano kuwa watatakiwa kutumikia kifungo kwa wakati mmoja.

    Wakenya wote ni wakazi wa kaunti ndogo ya Orum iliyopo katika wilaya ya Lodwar, katika Kaunti ya Turkana na walipatikana na hatia baada ya kukiri wenyewe.

    Watatumikia kifungo hicho katika gereza la serikali la Moroto.

    Walikuwa ni miongoni mwa washtakiwa zaidi ya 100 waliokamatwa tarehe 8 Aprili kutoka kwenye maficho yao katika kijiji cha Lokeriaut kilichopo katika kaunti ndogo ya Nanduget wilayani Moroto Uganda.

    Jeshi limepata bunduki haramu 31 na risasi zipatazo 751 wakati wa operesheni ambayo ni sehemu ya zoezi la msako wa kuwapokonya silaha watu wanaozimiliki kinyume cha sheria.

  11. Watoto 17 miongoni mwa watu waliopotea katika mkasa wa boti nchini Malawi

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Malawi ilikabiliwa na kimbunga kilichosababisha maiaji mwezi uliopita

    Watu 17, wakiwemo watoto, hawajulikani walipo baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama katika mto siku ya Jumatano katikati mwa nchi ya Malawi.

    Polisi inasema kikundi cha watu 22 kilikuwa kikivuka Mto Rusa kikielekea kwenye shughuli ya mazishi katika wilaya ya Mchinji.

    Watu watano walifanikiwa kuogelea hadi ufukweni.

    Kamanda wa polisi wa eneo, John Nkhoma, ameiambia tovuti ya habari ,Zodiak Online kwamba boti hiyo ilikuwa dogo ukilinganisha na idadi ya watu waliokuwa ndani yake.

    Waokoaji zaidi wanatarajiwa kuanza kufanya msako kwa ajili ya watu waliotoweka hii leo Alhamisi.

    Wakati huo huo, maafisa katika wilaya wanawashauri watu kuepuka kusafiri katika mito iliyofurika.

    Malawi iliathiriwa na kimbunga cha kitropiki mwezi uliopita ambacho kiliwaua wawatu 511 na kusababisha wengine 533 kupotea.

    g
  12. 'Mbakaji wa Facebook ' arejeshwa Afrika Kusini baada ya kutoroka gerezani

    Thabo Bester alirejeshwa nyumbani pamoja na mpenzi wake

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Thabo Bester alirejeshwa nyumbani pamoja na mpenzi wake

    Mbakaji wa Afrika Kusini na muuaji ambaye alitoroka gereza amesafirishwa kwa ndege hadi katika nchi yake ya asili mapema asubuhi Alhamisi kufuatia kukamatwa kwake nchini Tanzania.

    Thabo Bester alitoroka kutoka gerezani mwezi mei mwaka jana kwa kutunga taarifa za kifo chake katika ajali ya moto na kuweka mwili bandia katika cumba chake cha gereza.

    Alikamatwa pamoja na mpenzi wake, ambaye ni daktari maarufu Nandipha Magudumana.

    Wawili hao waliwasili kwa ndege katika uwanja wa ndege uliopo viungani mwa mji wa kibiashara wa Johannesburg.

    Watawekwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, afisa wa ngazi ya juu amemwambia mwandishi wa BBC wa Afrika Kusini Pumza Fihlani.

    Mipango inaendelea kwa ajili ya kumrejesha Bw Bester katika gereza lenye ulinzi wa hali ya juu ili atumikie kifungo chake cha maisha kwa mauaji, pamoja na maandalizi kwa ajili ya mashtaka mapya pamoja na mpenzi wake kwa kutoroka gerezani.

    Bw Bester anafahamika kama "mbakaji wa Facebook " kwa kutumia mtandao huo wa kijami kuwalaghai watu.

    Alipatikana na hatia mwaka 2012 kwa kumbaka na kumuua mpenzi wake aliyekuwa mwanamitindo Nomfundo Tyhulu.

    Mwaka mmoja kabla ya hapo , alipatikana na hatia ya kuwabaka na kuwaibia wanawake wengine wawili.

  13. Tazama:Ndege zatatizika kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow kutokana na upepo mkali

    Maelezo ya video, Tazama:Ndege zatatizika kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Heathrow kutokana na upepo mkali

    Ndege ya abiria ya United Airlines ilishindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Heathrow kutokana na upepo mkali ulioletwa na Kimbunga Noa.

    Chaneli ya YouTube ya Big Jet TV ilinasa wakati huo mubashara ambao pia ulionesha ndege nyingine kadhaa zikijitahidi kutua katika hali ngumu ya hewa.

    Dhoruba ya Noa inaenea kote Uingereza, kwa zaidi ya kasi ya 60mph (96.5km/h) ikirekodiwa kwenye Visiwa vya Scilly. Ofisi ya utabiri wa hali ya anga imetabiri kasi ya upepo ya hadi 70mph (113km/h).

  14. Times: Maisha ya Waingereza yamo hatarini kutokana na kuvuja kwa nyaraka za siri za Pentagon

    G

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Pentagon

    Maisha ya raia wa Uingereza yamo hatarini kutokana na kuvuja kwa taarifa za marekani za ujasusi, limeandika gazeti la Times nchini Uingereza, likiinukuu Kamati ya Ulinzi ya bunge la Uingereza.

    Awali, vyombo vya habari viliripoti kuwa kuvuja kwa waraka tarehe 23 Machi, ambao ulidai kwamba v wanajeshi wa kikosi maalumu wa Uingereza hadi 50 walitumwa nchini Ukraine pamoja na vikosi vingine maalum kutoka nchi za Magharibi.

    Waraka huo hauonyeshi ni wapi vikosi hivi vilipo na ni nini vinafanya.

    "Sehemu kubwa ya maudhui ya ripoti hizi ni uongo, zimebadilishwa, au zimefanyiwa yote ," Times lilimnukuu msemaji wa wizara ya ulinzi ya Uingereza "Tunashauri kwamba mtu yeyote asichukulie kwa umakini madai haya kuwa yenye thamani."

    Huku Pentagon ikijaribu kutafuta chanzo cha uvujaji mkubwa wa taarifa zake za siri, maafisa wa Uingereza, wa kijeshi na ujasusi hawachukulii kirahisi uvujaji wa taarifa hizi.

    "Pentagon haijui ni nini kingine kinaweza kutokea," chanzo cha usalama kililiambia gazeti la Times. "Inatia wasi wasi kusema kweli, na kunaweza kuwa na uvujaji zaidi kabla ya kufichwa."

    Kamanda wa kikosi maalumu cha zamani na ambaye kwa sasa ni mbunge wa chama cha LabourDan Jarvis aliliambia gazeti kwamba operesheni ya aina hiyo inayohusisha kikosi maalumu cha Uingereza kwa kawaida huwa ininafanyika kwa siri.

    "Kupatikana kokote kwa taarifa za siri kuhusiana na mahala walipo au idadi yo, sio jambo linaloaibisha tu , bali ni hasara kijeshi. Inahatarisha usalama na ufanisi wa operesheni hizi na inaweza kuyaweka maisha hatarini," alisema.

    Unaweza pia kusoma:

    • Nyaraka za Pentagon: Jinsi faili za siri zilivyosambazwa, kisha zikatoweka
    • Vita vya Ukraine: Nani alivujisha nyaraka za siri za Marekani kuhusu vita Ukraine-na kwa nini?
  15. ‘Tunawaambia Watanzania wasitumie poda ya Johnson &Johnson kwa sasa’- Mkurugenzi wa TBS

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Shirika la Viwango nchini Tanzania(TBS) limewataka Watanzania kuacha kutumia poda ya Johnson & Johnson hadi uchunguzi kuhusu poda hiyo utakapokamilika.

    Juma lililopita ilifahamika kuwa Shirika la viwango Tanzania, linachunguza poda aina ya Johnson inayouzwa katika maduka mbalimbali nchini humo na kwingineko duniani.

    Uchunguzi huo unatokana na kampuni inayotengeneza bidhaa hiyo, Johnson & Johnson ya Marekani kukubali kulipa fidia ya dola za Marekani bilioni 8.9 kwa sababu ya kesi zaidi ya elfu 38 za madai kuwa madini ya talcum yaliyomo kwenye poda hiyo ya watoto na bidhaa nyingine yanasababisha saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi kwa watumiaji.

    Akizungumza na BBC, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athumani Yusuph Ngenya amesema

    Poda hiyo ina madhara ambayo yamepigwa marufuku.

    ‘’Kitu chochoe kinachozungumzwa kwamba kina madhara ni bora na ni busara kukiweka kando mpaka uchunguzi ukamilike’’ , alisema na kusisitiza kuwa:’’Tunawaambia Watanzania wasitumie poda ya Johnson & Johnson’’ iliyopo madukani hadi uchunguzi utakapokamilika.

    Bw Dkt. Athumani Yusuph Ngenya, amesema uchunguzi kuhusiana na poda ya Jojnson &Johnson ambayo kwa sasa ipo madukani, nchini humo utakamilika katika kipindi cha wiki mbili au wiki tatu zijazo.

  16. Vitu sita tulivyojifunza kutokana na mahojiano na Elon Musk

    H
    Maelezo ya picha, Elon Musk (kushoto), katika mahojiano ya nadra na mwandishi wa BBC wa masuala ya teknolojia James Clayton

    Elon Musk alitetea jinsi anavyoendesha Twitter katika mahojiano ya nadra na yaliyohusu masuala mbali mbali na BBC.

    Mwanaume huyo ambaye ni tajiri wa pili zaidi duniani alihojiwa kwa karibu saa moja na mwandishi wa BBC wa masuala ya teknolojia James Clayton katika makao makuu ya Twitter yaliyopo San Francisco.

    Haya ni mambo sita tuliyojifunza kumuhusu:

    1.Anakanusha kauli za chuki katika Twitter zimeongezeka

    Be Musk alikataa kukubali kuwa kulikuwa na maudhui ya chuki zaidi kwenye jukwaa hilo tangu achukue umiliki wa mtandao wa Twitter.

    2.Alimpigia kura Joe Biden

    Karibu nusu ya nchi ilimpigia kura Bw trump katika uchaguzi wa urais uliopita nchini Marekani, Bw Musk alisema , lakini aliongeza kuwa: "Sikuwa mmoja wao. Nilimpigia kura Biden."

    Katika sehemu nyingine ya mahojiano, alitetea kmwisho wa marufuku ya matumizi ya Twitter dhidi ya Bw Trump ambaye aliondolewa mwaka 2021 kwenye mtandao ho wakati jukwaa hilo lilipomshutumu kwa uchochezi wa ghasia.

    3.Anasema Twitter inaipiku bots katika vita juu ya kupambana na taarifa gushi

    Bw Musk alidai kuwa juhudi zake za kufuta akauti zinazojiendesha zimepunguza taarifa za upotoshaji kwenye Twitter baada ya kuinunua.

    ‘’Uzoefu wangu ni kwamba kuna taarifa chache za upotoshaji kuliko zaidi ," alimwambia mwandishi wetu.

    4.Anapinga marufuku dhidi ya TikTok

    Bw Musk anasema hatumii app hiyoinayopakuliwa zaidi nchini Marekani lakini anapinga hatua zozote za kuifunga.

    Marekani inaangalia uwezekano wa kuipiga marufuku kutokana na hofu za kiusalama kuhusu Tiktok inayomilikiwa na Chin. Baadhi yan chi nyinginezimeipiga marufuku kwenye simu za wafanyakazi wake wa serikali.

    "Kwa ujumla ninapiga kupiga marufuku vitu," alisema Bw Musk, ingawa anasema marufuku itaipatia faida Twitter kwasababu itamaanisha kuwa watu wengi zaidi watatumia muda katika jukwaa lake.

    5. Anaweza kukataa kupokea dola bilioni 44

    Awali Bw Musk alidai katika mahojiano kwamba kama mtu fulani atajitolea kununua Twitter sasa hivi kwa pesa aliyoinunua , angekataa.

    Anasema iwapo ataiuza, itakuwa muhimu zaidi kumpata mnunuzi ambaye anapenda’’ukweli’’ kuliko ni kiasi gani atainuynua, anasema : "Sijali kuhusu pesa ."

    6.Ataondoa jinsi BBC ilivyotambulishwa

    Bw Musk alithibitisha kuwa atabadilisha nembo ya BBC kwenye Twitter kutoka kwa"inayodhaminiwa na serikali" na kuwa "inayodhaminiwa na umma "baada ya mzozo wa wiki iliyopita, na saa kadhaa baada ya mahojiano mabadiliko haya yalifanyika.

  17. Kuvuja kwa nyaraka za Pentagon: Marekani inadhani mkuu wa Umoja wa Mataifa Guterres anaipendelea sana Urusi

    Antonio Guterres (katikati) alitembelea eneo lililoathiriwa na vita la Ukraine Aprili mwaka jana

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Antonio Guterres (katikati) alitembelea eneo lililoathiriwa na vita la Ukraine Aprili mwaka jana

    Serikali ya Marekani inaamini kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifayuko tayari kuyapokea sana maslahi ya Urusi, kulingana na taarifa za siri zilizovuja kwenye mtandao.

    Faili mpya zilizovuja za nyaraka hizo zinaonyesha kuwa serikali ya Marekani mjini Washington imekuwa ikimfuatilia kwa karibu Antonio Guterres.

    Nyaraka kadhaa zinaelezea mawasiliano ya kibinafsi yanayomhusisha BwGuterres na naibu wake.

    Ni taarifa za hivi karibuni kutoka katika uvujaji wa nyaraka za siri, ambazo maafisa wa zamani wanahangaika kujua ni vipi zilivuja.

    Nyaraka hizo zinaonyesha ukweli wa maoni ya Bw Guterres kuhusu vita nchini Ukraine na viongozi kadhaa wa Kiafrika.

    Nyaraka zilizovuja zinaangazia mkataba wa nafaka wa Bahari Nyeusi, uliofikiwa baina ya Umoja wa Mataifa na Uturuki mnamo mwezi Julai kufuatia mzozo wa chakula wa dunia.

    Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Bw Guterres alikuwa makini sana kunusuru mkataba kiasi kwambaalikuwa tayari kuafiki maslahi ya Urusi.

    "Guterres alisisitizia juhudi zake za kuboresha uwezo wa Urusi wa mauzo ya nje ," unasema waraka, "hata kama hilo litahusisha makampuni ya Urusi na watu binafsi waliowekewa vikwazo."

    Unaweza pia kusoma:

    • Vita vya Ukraine: Nani alivujisha nyaraka za siri za Marekani kuhusu vita Ukraine-na kwa nini?
    • Urusi huenda ndio waliohusika na kuvuja kwa nyaraka za siri kwenye mitandao ya kijamii
  18. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara leo ikiwa ni Alhamisi tarehe 13.04.2023