Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Shambulio la sinagogi Jerusalem: Saba wauawa katika shambulio la risasi
Watu saba wamepigwa risasi na kufa katika sinagogi lililopo mashariki mwa mji wa Jerusalem, ikiwa ni idadi kubwa ya watu waliouliwa katika shambulizi la aina hii kwa miaka.
Moja kwa moja
Olaf Scholz: Ujerumani inaisaidia Ukraine ili vita visije karibu na mpaka wake
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amechapisha video ya ujumbe ambapo anazungumzia msimamo wa Berline wa kisiasa kwa Urusi na vita vya Ukraine, na akasisitiza kwamba anazingatia tu sio kuiunga mkono Ukraine, bali pia hofu za usalama za nchi yake.
Kipaumbele cha maafisa , kulingana na Scholz, kimebakia kuwa usalama wa Ujerumani . "Lengo letu liko wazi- Urusi haipaswi kupanua mipaka yake kwa nguvu - ," alisema. Scholz aliongeza kuwa Wajerumani wanataka "amani katika Ulaya na kwamba vita visije karibu."
Kulingana na Kansela huyo, sera ya kigeni ya Ujerumani ina misingi mitatu - ubinadamu, fedha na usaidizi wa teknolojia ya kijeshikwa Ukraine; kuzuia kupanuka kwa mzozo, ni kupanuka kwa vita na kuwa vita baina ya Urusi na Nato, uratibu wa karibu wa nji zote zenye ushirika na urafiki unaoongozwa na Marekani
Scholz alisema tangu mwanzoni mwa mashambulio ya Urusi dhidi ya Ukraine, serikali ya Ujerumani imekuwa ikichukua maamuzi baada ya taarifa , ambazo kila mara huafikiwa katika ngazi ya kimataifa. Alikumbuka kwamba "vita vibaya, vya ukatili na visivyo na maana" nchini Ukraine vilichochewa na Rais wa Urusi.
Wakati huo huo, kulingana na jarida la Wall Street Journal, likikariri vyanzo vyake , linasema Olaf Scholz, ambaye amekuwa akikosolewa kwa kusita kuhusu kupeleka vifaru Ukraine, alifanya jukumu muhimu katika kubadili miiko isiyo rasmi katika upelekaji wa silaha hizimiongoni mwa nchi za Magharibi .
Kulingana na jarida hilo, ilikuwa ni Bw Scholz, ambaye alimshawishi rais wa Marekani Joe biden kuhusu haja ya Marekani kupeleka vifaru vyake, ambao walikuwa na mashaka iwapo hili linafaa kufanyika.
Nemes Tarimo: Mazishi ya Mtanzania aliyeuawa vitani Ukraine yafanyika kijijini kwao
Ndugu, jamaa na marafiki wa Mtanzania, Nemes Tarimo wamekusanyika kijijini kwao katika wilaya ya Tukuyu Nyada za juu kusini kwa ajili ya mazishi yake.
Nemes Tarimo alienda nchini Urusi kwa ajili ya masomo ya juu kabla ya kupatwa na umauti wake.
Mapema wiki hii serikali ya Tanzania ilithibisha kijana huyo kuuawa vitani Ukraine mara baada ya kufungwa kwa uhalifu nchini Urusi na baadae kujiunga na kundi la mamluki wa Urusi, Wagner.
Mamia ya watu wamehudhuria mazishi ya marehemu Nemes Tarimo kijijini kwao:
Unaweza pia kusoma:
- Serikali ya Tanzania: Mtanzania aliyekufa Ukraine alifungwa na baadaye kujiunga na Wagner
- Familia yathibitisha kifo cha raia wa Tanzania vitani nchini Ukraine
Fulana ya Pele kuuzwa hadi pauni 30,000
Fulana ambayo alikuwa ametengenezewa mchezaji maarufu wa soka wa Brazil Pele kabla ya kucheza mchezo wake wa mwisho wa kimataifa inatarajiwa kupigwa mnada na kuuzwa kwa hadi pauni 30.000.
Fulana hiyo ni moja ya jezi mbili zenye nambari 10 ambazo alikuwa ametengenezewa ili azivae katika mechi kati ya Brazili na Yugoslavia mwaka 1971 , kulingana na taasisi inayopiga mnada fulana hiyo, Hansons Auctioneers.
Pele hakuweza kuvaa fulana hiyo, na badala yake alimpatia mtu ambaye alikwa akiwachua wachezaji wa timu ya Brazil.
Baadaye fulana hiyo ilinunuliwa na kituo cha kihistoria cha Shropshire nchini Uingereza ambaye anasema alitarajia kuwa itahifadhiwa katika jumba la makumbusho ya mpira wa miguu.
ISW: Putin anajianda kwa shambulio kubwa dhidi ya Ukraine
Rais wa Urusi Vladimir Putin anajiandaa kwa mashambulio mapya makubwa ambayo yanaweza kuanza mapema mwezi Februari au Machi 2023, kulingana na rioti kutoka taasisi ya Marekani ya stadi za kivita (ISW)
Wandani wa utawala wa Urusi -Kremlin waliliambia shirika la habari la Bloomberg kwamba Putin anaimani kwamba uvumilivu wa Urusi baada ya kupoteza maeneo iliyokuwa imeyateka kijeshi Ukraine utaiwezesha kushinda vita baada ya muda mrefu, licha ya mapungufu.
Kulingana na matazamio ya ISW, Urusi huenda inajitayarisha kwa opreresheni za kimkakati – na hasa ni katika jimbo la Luhansk zaidi – katika kipindi cha miezi sita ijayo
Mashambulio machache ya hivi karibuni ya ardhini ya Urusi katika Zaporozhye huenda yanalenga kuvipotosha vikosi vya Ukraine na kujiandaa kwa ajili ya mashambulizi katika jimbo la Luhansk, wanasema wataalamu wa ISW .
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:
- MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Marekani kuwarahisishia wapenzi wa jinsia moja wa kiume kutoa msaada wa damu
Taasisi ya udhibiti wa viwango vya chakula na madawa nchini Marekani (FDA) imetangaza kuwa itabadilisera ya hivi karibuni inayozuia wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kutoa damu kwa miezi mitatu.
Sheria ya sasa inaruhusu uitaoaji wa damu tu kama mwanaume hajafanya tendo la ngono na mwanaume mwingine kwa kipindi cha miei mitatu.
Chini ya sheri mpya inayopendekezwa "ya msingi wa hatari ya kibinafsi" , watu wote wanaoweza kutoa msaada wad amu wataulizwa kuhusu wapenzi wapya au wapenzi wengi walioshiriki nao ngono kwa kipindi cha miezi mitatu, kabla ya kukubaiwa kutoa msaada wa damu.
FDA inatumai kuwa kubadilishwa kwa sheria hii kutawatia moyo watu wengi kujitolea kutoa zaidi usaidizi wa damu.
"Pendekezo hili kwa tathmini ya mtu binafsi, bila kujali jinsia au hali yake ya kingono , itatuwezesha kuendelea kutumia sayansi bora " kuhakikisha usambazaji wa haraka wad amu salama, alisema kamishna wa FDA Robert Califf katia taarifa yake ya Ijumaa.
Makundi ya kutetea maslahi ya wapenzi wa jinsia moja kwa miaka mingi yamekuwa yakiyaita masharti hayo ya kutoa msaada wad amu waliyowekewa kama ubaguzi dhidi ya jamii ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia kwani wanasema teknolojia za kisasa zinaweza kuchunguza dam una kubaini iwapo ina maambukizi au la.
Unaweza pia kusoma:
- Papa Francis akosoa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja kuwa "sio haki" lakini ni 'dhambi'
- Maaskofu wa Kanisa la England wakataa kuunga mkono ndoa za watu wa jinsia moja
- Jinsi sheria mpya inavyowabana wapenzi wa jinsia moja Urusi
Shambulio la sinagogi Jerusalem: Saba wauawa katika shambulio la risasi
Watu saba wamepigwa risasi na kufa katika sinagogi lililopo mashariki mwa mji wa Jerusalem, ikiwa ni idadi kubwa ya watu waliouliwa katika shambulizi la aina hii kwa miaka ya hivi karibuni.Takriban watu watatu zaidi wamejeruhiwa.
Tukio hilo limetokea katikaeneo la mji wa Jerusalemu linalofahamika kama Neve Yaakov majira ya saa mbili na robo kwa saa za eneo.
Polisi imemuelezea mshambuliaji kama "gaidi" na kuongeza kuwa ameuawa.
Vyombo vya habari vimemtambua mshambuliaji kama mwanaume Mpalestina kutoka Jerusalem Mashariki.
Polisi wa Israel wamesema Jumamosi kwamba wamewakamata watu 42 kuhusiana na ufyatuaji wa risasi.
Akisungumza katika eneo la shambulizi, kamanda wa polisi wa Israeli Kobi Shabtai aliita "moja ya mashambulio mabaya zaidi ambayo tumekabiliana nayo katika miaka ya hivi karibuni ".
Waumini wa Israeli walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya maombi katika mwanzo wa sabato ya Wayahudi katika sinagogi katika makazi ya Wayahudi na walikuwa wanaondoka wakati mtu mwenye silaha alipoanza kuwafyatulia risasi. Police inasema kuwa baadaye maafisa walimpiga risasi ya kichwani akafa.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo Jumamosi 28.01.2023