Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita vya Ukraine: Ukomo wa bei ya mafuta ya Urusi utamuathiri moja kwa moja Putin- Marekani
Ukomo wa bei kwa mafuta ya Urusi utazuia mapato ya Urusi kwa ajili ya "vita vyake dhidi ya Ukraine ", inasema Marekani.
Moja kwa moja
Vita vya Ukraine: ukomo wa bei ya mafuta ya Urusi utamuathiri moja kwa moja Putin- Marekani
Ukomo wa bei kwa mafuta ya Urusi utazuia mapato ya Urusi kwa ajili ya "vita vyake dhidi ya Ukraine ", inasema Marekani.
Ukomo huo, ulioidhinishwa na washirika wa Magharibi Ijumaa, unalenga kuzizuia nchi kulipa zaidi ya$60 (£48) fkwa pipa moja la mafuta ghafi ya Urusi.
Hatua hiyo – inayotarajiwa kutekelezwa kuanzia Jumatatu – inaongeza shinikizo la Magharibi kwa Urusi kuhusiana na uvamizi.
Ukraine ilisema pendekezo la ukomo wa bei la Magharibi linapaswa kupunguzwa kwa kiwango cha nusu. Urusi ilisema haitapeleka mafuta kwa nchi zinazotekeleza azimio hilo.
Ukomo wa bei ya mafuta ya Urusi ulijadiliwa kwa mara ya kwanza katika kikao cha kundi la mataifa ya yenye utajiri zaidi wa viwanda duniani G7 (Marekani , Canada, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Muungano wa Ulaya) kwa lengo la kuathiri uwezo wa Urusi wa kufadhili vita nchini Ukraine.
Katika taarifa ya pamoja, G7, Muungano wa Ulaya na Australia zilisema uamuzi ulichukuliwa ili "kuizuia Urusi kuendeleza vita vyake vya uchokozi dhidi ya Ukraine".
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukrain
Kombe la Dunia 2022: Senegal 'lazima iwe na matamanio' ya kuichapa England katika timu 1616
Senegal lazima ishikilie kanuni zake za mashambulizi iwapo itataka kuichapa England katika kundi la timu 16 za mwisho katika Kombe la Dunia , anasema mchezaji wa kimataifa wa zamani Omar Daf.
Timu hiyo ya magharibi mwa Afrika ilishinda taji lake la kwanza la Afrika mwezi Februari lakini itakabiliana na timu iliyofikika nusu fainali ya Kombe la Dunia la Urusi miaka minne iliyopita na kisha kufika ikashikilia nafasi ya pili katikaKombe la Ulaya mwaka jana.
Yet Daf anataka Teranga Lions wacheze mbele zaidi licha ya kukabiliwa na mashambulizi ya wachezaji wenye vipaji kama vile Murcus Rashford, ambaye ana magoli matatu tayari aliyoyafunga Qatar, na mshindi wa kiatu cha dhahabu mwaka 2018 Harry Kane.
"Senegal ni machampioni wa Afrika kwahiyo ni lazima tuendelee kuwa na matamanio," alisema Daf, mwenye umri wa miaka 45, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Senegal kilichofika katika timu 8 za mwisho katika Kombe la Dunia la mwaka 20222 , nchini Japan na Korea Kusini katika mazungumzo na BBC Sport Africa.
Kampuni ya Marekani yazindua ndege ya makombora ya nyuklia
Kampuni ya Northrop Grumman Corp imezindua ndege yake mpya ya ufyatuzi wa mabomu aina ya B-21 "Raider" aina ya jet, ikiwa ni aina mpya iliyotengenezwa kwa chuma yenye uwezo wa kusafiri angani na kufyatua mabomu ya nyuklia kwa ajili ya kikosi cha anga cha Marekani, Air Force, imeripoti taarifa ya Reuters.
Ndege hiyo B-21 ilizinduliwa katika sherehe ya aina yake iliyofanyika kwenye kiwanda Northrop cha 42, kilichopo katika eneo la Palmdale, California, ili kutoa fursa kwa umma kuitazama kwa mara ya kwanza.
B-21, yenye muundo sawa na ule wa awali B-2 wa "bawa la ndege " itaweza kufyatua silaha za kawaida na zile za nyuklia katika maeneo mbali mbali ya dunia ikiwa pia na uwezo wa kufyatua maeneo yaliyolengwa ya masafa marefu na mafupi angani.
Ndege hiyo ilikadiriwa kugarimu kiasi cha dola zipatazomilioni 550 kila moja katika mwaka 2010, au karibu dola milioni 750 kwa sasa kutokana na mabadiliko ya thamani ya dola.
Air Force inapanga kununua walau ndge za aina hii 100 na kuanza kuzitumia badala ya zile za awali za B-1.
Jenerali Muhoozi Kainerugaba: Kupigana na Rwanda inamaanisha kupigana na Uganda!
Mtoto wa kiume wa rais wa Uganda ameibua mjadala tena kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya kutuma ujumbe wenye utata aliouambatanisha na picha ya zamani ya rais wa Rwanda Paul Kagame.
Katika ujumbe huo, Jenerali Kainerugaba amesema:
‘’Mimi ni Jenerali wa nyota 4 wa UPDF (Jeshi la Uganda). Kuna vitu vichache ambavyo sijaviona katika dunia hii. Lakini ninawahurumia wale wanaomdharau mjomba wangu, Jenerali Kagame. Kupigana na Rwanda inamaanisha kupigana na Uganda!
Ujumbe wa Bw Muhoozi ulifuatiwa na hisia tofauti za watumiaji wa mtandao wa Twitter:
Kauli hii inajiri huku mzozo kuhusu wapiganaji wa kundi la M23 ukiendelea kutokota baina ya Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo na Rwanda.
Congo inaishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi wa M23 walioyateka maeneo mashariki mwa nchi hiyo, madai ambayo Rwanda inayakanusha.
Kwa upande mwingine inaishutumu DRC kwa kushindwa kutimiza ahadi ya kuwarejesha nyumbani waasi wa Rwanda wa kundi la FDLR walioko mashariki mwa DRC inaowashutumu kuhatarisha usalama wa Rwanda.
Hivi karibuni pande mbili zilirushiana cheche za maneno, kila upande ukielezea uwezekano wa kuingia vitani iwapo usalama wake utayumbishwa.
Hii si mara ya kwanza kwa Jenerali Muhoozi kutuma jumbe zenye utata kupitia mtandao wa kijamii kuhusu uhusiano wa nchi yake na nchi jirani, ambazo mara nyingi huibua gumzo mtandaoni, huku baadhi wakijiuliza ni vipi mtu wa kaliba yake anaweza kutoa jumbe za aina hiyo. Katika jumbe zake huwaelezea viongozi wa nchi jirani kama, makaka, na wajomba zake.
Unaweza pia kusoma:
- Muhoozi Kainerugaba: Kutoka ‘kumposa’ Waziri Mkuu wa Italia hadi kutishia kuivamia Kenya
- Muhoozi Kainerugaba - Jenerali mashuhuri wa Uganda mwenye 'uchu' wa madaraka
- Muhoozi Kainerugaba: Je, tunajua nini kuhusu tangazo la kustaafu la mtoto huyu wa Rais Museveni?
Abiria wa ndege katika Muungano wa Ulaya wataweza kupiga simu wakiwa safarini
Wasafiri wanaotumia ndege katika Muungano wa Ulaya (EU) hivi karibuni wataweza kutumia simu zao za mkononi kikamilifu.
Tume ya Muungano huo imesema kuwa mashirika ya ndege yanaweza kutoa teknolojia ya 5G ndani ya ndege, pamoja na simu za mkononi zinazotumia data polepole zaidi.
Hii inamaanisha kuwa wasafiri wa safari za ndege, hawatahitaji tena kuweka simu zao katika, hali ya ndege (airplane mode), licha ya kwamba haijabainika wazi ni vipi teknolojia hii mpya itakavyotekelezwa.
Siku ya mwisho ya nchi wanachama wa Muungano wa Ulaya kukamilisha uwepo wa masafa ya 5G kwa ajili ya ndege ni tarehe 30 Juni 2023.
Hii itamaanisha kuwa watu wanaweza kutumia simu zao kwa ukamilifu katika kati ya safari ya ndege – na kuwawezesha kupiga simu kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na kupakua programu zao nzito za muziki na video.
Wanaoshiriki ngono nje ya ndoa kufungwa jela Indonesia
Bunge la Indonesia linatarajiwa kupitisha sheria ya uhalifu mwezi huu itakayowaadhibu watu wanaoshiriki ngononje ya ndoa kwa kifungo cha hadi mwaka mmoja.
Mwanasiasa nchini humo -Bambang Wuryanto, ambaye alihusika katika utungaji wa sheria hiyo, alisema kuwa inaweza kuidhinishwa wiki ijayo.
Iwapo sheria hiyo itapitishwa, itawaadhibu rai awa Indonesia pamoja na rai awa kigeni.
Adhabu hiyo ya uasherati inaweza kutekelezwa tu iwapo kuna watu watakaowasilisha malalamiko kwa mamlaka.
Kwa walie ambao wameoana, mmoja wao ana haki ya kuwasilisha malalamiko kama mshitakiwa ni mume au mke.
Sheria hiyo pia inawaruhusu wazazi wa watu ambao hawajaolewakuwaripoti kwa kufanya ngono.
Kuishi kama mume na mke kabla ya ndoa pia kutapigwa marufuku na wale watakaopatikana na hatia wanaweza kukabiliwa na hukumu ya kifungo cha miezi sita jela.
Bilionea wa Urusi: Ni wakati wa kuwaonyesha Magharibi nguvu za kijeshi za Urusi
Mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa wanaounga mkono uamuzi Vladimir Putin wakuivamia Ukraine mwenye jumri wa miaka 71, Yuri Kovalchuk, amesema kuwa vita vinaweza kuonyesha uthabiti wa Urusi kwa nchi za Magharibi . Bilionea Kovalchuk, ameyasema hayo katika Makala ndefu ya jarida Wall Street.
Nchini za Magharibi ni dhaifu na muda umefika kwa Urusi kuonyesha nguvu zake za kijeshi kwa kuivamia Ukraine, alinukuliwa na vyanzo mbali mbali vya habari vya Marekani, akisema .
Mara kwa mara amekuwa akikutana na Putin kabla vita vya Ukraine havijaanza, na pia amekuwa akizungumza naye kwa njia ya simu na video.
Kovalchuk, ambaye aliwekewa vikwazo mwaka 2014, ni mfanyabiashara anayemiliki kampuni ya habari - yenye vituo vya TV, magazeti, mitandao ya kijami inayounga mkono utawala wa Urusi.
Wakati vita vya Ukraine vilipoanza, vyombo vyake vya habari vilikuwa muhimu sana kwa utawala Kremlin kwa kueneza propaganda za utawala wa Urusi, limesema jarida la Wall street.
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukrain
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo Jumamosi tarehe 3 Disemba