Vita vya Ukraine: Mashambulio ya Urusi " yaliwaacha watu milioni 6 gizani "

Ukraine inasema watu milioni 6 hawana umeme baada ya mashambulizi ya Urusi

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa

  2. DRC yatangaza tarehe ya uchaguzi wa urais

    g

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Félix Tshisekedi, alishinda uchaguzi uliopita, lakini matokeo yalipingwa

    Uchaguzi wa urais katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo utafanyika tarehe 20 Disemba mwaka ujao ,tume ya uchaguzi imetangaza.

    Kwa sasa, hali ya usalama inayoyakumba maeneo ya mashariki mwa nchi huku waasi mbali mbali wakisababisha ukosefu wa usalama.

    Jaribio la kulitaka kundi la waasi wa M23 kusitisha mapigano nilnaonekana kugonga mwamba.

    Shirika la habari AFP linaripoti kuwa tume ya uchaguzi imekiri kuwa "kuna ukosefu wa usalama unaoendelea katika baadhi ya maeneo ya nchi " ambao unaweza kuzuiwa kufanyika kwa uchaguzi "huru, wa kidemokrasia na wa uwazi’’ unaoweza kuwa changamoto kwa shughuli ya upigaji kura.

    Lakini maafisa wameazimia kuzingatia ratiba.

    "Sio suala la majadiliano kuhusu ukomo uliowekwa na katiba, ni swala la sisi kuheshimu katiba na demokrasia yetu ," msemaji wa serikali Patrick Muyaya amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema.

    Anakadiria kuwa uchaguzi utagarimu karibu dola milioni 600, Reuters imeripoti.

    Rais wa sasa President Félix Tshisekedi, ambaye aliingia kwa mara ya kwanza madarakani Januari 2019, tayari amekwishasema atagombea tena muhula wa pili, kulingana na AFP.

    Alichukua mamlaka kutoka kwa Joseph Kabila – ambapo ilikuwa na mara ya kwanza kwa marais wa Congo kukabidhiana mamlaka kwa amani.

    Unaweza pia kusoma:

    • Makundi ya waasi bado yanahatarisha maisha ya watu wa mashariki mwa Jamuhuri ya Congo
    • Mzozo wa DRC: Je inawezekana kuyamaliza makundi ya wapiganaji Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo?
  3. Kombe la Dunia 2022: Cristiano Ronaldo 'mwenye fikra kamili za kiakili’ kwa kushinda penati ya Ureno – Fifa

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Cristiano Ronaldo ameitwa "mwenye fikra kamli za kiakili’ kamili na Fifa kwa jinsi alivyoshinda bao la penati ya Ureno katika ushindi wao katika mechi Kombe la Dunia dhidi ya Ghana.

    Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 alikuwa mtu wa kwanza kufunga magoli ya penati katika mashindano Matano tofauti ya Kombe la Dunia, baada ya kufunga bao kwa mkwaju wa penati.

    Ureno ilishinda 3-2, lakini kutolewa kwa penati kulimghadhabisha menja wa Ghana Otto Addo, ambaye alisema "haikuwa penati ".

    Katika mkutano wa wandishi wa habari mjini Doha, mjumbe wa Kikundi cha Fifa cha kiufundi(TSG) , Sunday Oliseh alisema washambuliaji "wanakuwa bora zaidi".

    TSG, ambayo inaongozwa na meneja wa zamani wa Arsenal manager Arsene Wenger, hutazama kila mechi na kutoa tathmini ikiwa ni pamoja na data za ubora wa uchezaji na mitindo ya mchezo.

  4. Vita vya Ukraine: Ukraine na Urusi zatangaza kubadilishana tena wafungwa wa kivita

    G

    Chanzo cha picha, Andrey Ermak/BBC RUSSIAN

    Vyanzo vya habari kutoka Urusi na Ukraine vinaripoti kuhusu kubadilishana tena kwa wafungwa wa kivita.

    Mkuu wa ofisi ya Rais wa Ukraine, Andriy Yermak, ameandika kwenye chaneli ya Telegram kwamba wafungwa 12 wa Ukraine waliachiliwa , na wizara ya ulinzi ya Urusi ilitangaza kuwarejesha nyumbani wanajeshi wanane wa ukrainne waliokamatwa .

    Kulingana na Yermak, miongoni mwa Waukraine waliokombolewa ni wanajeshi wanne wa vikosi vya majini, walinzi wawili wa taifa na walinzi wa mpaka wawili, mmoja kutoka kikasi cha ulinzi wa kieneo na raia watatu : mke na mume wake, ambao walitangazwa kutoweka. "Miongoni mwa wanajeshi kuna maafisa wawili, pamoja na wanajeshi wa cheo cha Private na Sajenti ," mtandao wa Yermak umeandika

    Kulingana na Yermak, "wapiganaji wa msituni ambao walilinda hususan, Mauripol, mtambo wa nyuklia wa Chernobyl na Kisiwa cha Nyoka- Snake Island wanaenda nyumbani."

    Wakati huo huo, Waziri wa ulinzi wa Urusi amesema kuwa kurejea kwa wanajeshi tisa kumetokana na ubadilishanaji wa wafungwa wa vita.

    Kwa kipindi cha wiki iliyopita, Ukraine ana Urusi zimekwishabadilishana wafungwa kadhaa .Mkuu wa ofisi ya Rais wa Ukraine amesema kuwa waukraine 98 tayari wamerejea Kyiv wiki hii kutoka upande wa Urusi.

  5. Vita vya Ukraine: Mashambulio ya Urusi " yaliwaacha watu milioni 6 gizani "

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Mitaa ya Kyiv usiku

    Ukraine inasema watu milioni 6 hawana umeme baada ya mashambulizi ya Urusi

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema katika kwamba hali ni mbaya ni ngumu.

    "Tangu jioni hii, ukosefu wa umeme, unaendelea katika majimbo mengi na katikaKyiv."

    Urusi ilianza shambulia kwa makombora maeneo mabali mbali ya Ukraine tangu wiki iliyopita.

    Jimbo la Odessa iliyopo katika , Lviv iliyopo magharikbi naDnepropetrovsk mashariki ni miongoni mwa majimbo yaliyoathiriwa zaidi na mashambulio ya roketi.

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Maafisa wanatoa wito kwa watu kubana matumizi ya umeme.

    Wanatahadharisha kuwa mashambulizi ya Warusi yanayolenga miundombinu ya Ukraine inaweza kusababisha mzozo wa afya kabla ya majira ya baridi .

    Ijumaa, gavana wa jimbo la Kherson alisema kwamba wagonjwa wamekuwa wakihamishwa kutokana "mashambulio ya Warusi yanayoendelea".

    Ukraine na washirika wake wa Magharibi wamerudia mara kwa mara kusema kuwa Urusi inatekeleza uhalifu wa kivita kwa kulenga miundombinu ya raia, shutuma ambazo Urusi inazikanusha.

  6. Msafiri wa Meli akolewa baharini baada ya kupotea kwa zaidi ya saa 15

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Msafiri alianguka kutoka ndani ya meli ya Carnival Valor, inayoonekana hapa kwenye picha

    Msafiri aliyepotea kutoka kwenye meli kubwa katika Ghuba ya Mexico ameokolewa baada ya saa zaidi ya 15 akiwa baharini, walinzi wa mwambao wa Marekani wasema.

    Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 28 alikwenda kwenye baa katika meli hiyo Carnival Valor pamoja na dada yake Jumatano usiku, lakini hakuweza kurejea tena baada ya kuondoka kwenda haja.

    Wahudumu kasha wa uokozi walisaka eneo Several rescue crews na hatimaye mwanaume huyo alionekana Alhamisi jioni, umbali wa takriban maili 20 (30km) kutoka kwenye mwambao wa Louisiana. Anasemekana kuwa yuko katika hali nzuri.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  7. Ujasusi wa Uingereza: Urusi inatumia makombora ya zamani dhidi ya Ukraine

    G

    Ripoti ya hivi karibuni ya ujasusi inasema kuwa jeshi la Urusi mamombora ya kupaa yanayoongozwa dhidi ya Ukraine ambayo yameundwa kwa ajili ya kufyatua makombora ya nyuklia.

    Kulingana na Wizara ya ulinzi ya Uingereza, vifyatuzi vya nyuklia kwanza vinaondolewa halafu makombora yanafyatuliwa bila vichwa.

    "Picha zilizopigwa na vyanzo huru zinaonyesha mabaki yakifyatuzi cha kombora la anga cha AS-15 Kent [ ambayo NATO inayafahamu kama makombora ya aina ya Kh-55 ], ambayo yalidunguliwa," ilisema ripoti.

    Kulingana na kumbukumbu ya Ujasusi wa Uingereza, makombora hayo yalibuniwa miaka ya1980 kama njia ya kufyatua silaha za nyuklia. Wakati huo huo, vifuniko vya makombora hayo ambayo yalitumiwa wakati wa mashambulizi ya Ukraine viliondolewa na, huenda, badala yake kiliwekwa kitu kingine kizito cha kushikilia kombora.

    Kulingana na ujasusi wa Uingereza, Urusi "ilikuwa na matumaini kuwa makombora aina hiyo yanaweza kusaidia kukwepa mifumo ya ulinzi ya mashambulio ya anga."

    Urusi na Ukraine: Mengi zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  8. Kwa picha: Mashindano fainali ya mbio za punda Kenya

    G

    Mashindano maarufu ya mbio za punda yanafanyika leo katika mjiwa Lamu pwani ya Kenya.

    Mashindano hayo maarufu ambayo hufanyika kila mwaka yanahudhuriwa na mamia ya mashabiki wakiwemo wenyeji, wageni na waralii na mgeni rasmi wa mashindano ya leo ni Waziri kiongozi wa Kenya Musalia Mudavadi.

    Mji wa Lamu ndio mji mkongwe zaidi nchini Kenya, ukiwa na mitaa myembambainayokaliwa na wenyeji wenye tamaduni za uswahili na Kiarabu . Kutokana na wembamba wa mitaa ya Lamu, Punda wamepata umaarufu mkubwa kwani hutegemewa na wenyeji kuwasafirisha katika maeneo mbali mbali yam ji huo.

    Hizi ni baadhi picha za mashindano ya punda ya Lamu:

    g
    d
    g

    ‘’Sherehe hizi zimeandaliwa kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa janga la corona hatua ambayo inewafurahusha wenyeji wa hapa’’, anasema mwandishi wa BBC Robert Kiptoo, aliyeko mjini Lamu.

    Biashara ambazo zilikuwa zimefungwa kutokana na janga la Corona zimefunguliwa tena. Miongoni mwa mwa shughuli nyingine zitakazofanyika hii leo ni pamoja na mashindano ya mashua na uvuvi na maonyesho mengine ya tamaduni za watu wa pwani.

    g
    Maelezo ya picha, Mashindano ya mashua ni moja ya shughuli zinazofanyika katika sherehe za maonyesho ya utamaduni wa Lamu
    G
  9. Neymar kukosa mechi mbili zijazo akiuguza jeraha la mguu

    G

    Chanzo cha picha, Reuters

    Neymar hatashiriki mechi mbili zijazo za Brazil za Kombe la Dunia baada ya kupata jeraha la mguu wa kulia, anasema daktari wa timu yao.

    Mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 30 aliondolewa uwanjani dakika ya 80 ya mchezo wa siku ya Alhamisi ambapo Brazil waliichapa Serbia 2-0 baada ya kukabiliwa vikali na Nikola Milenkovic.

    Neymar aliketi huku uso wake ukiwa umefunikwa wakati alipokuwa akipata matibabu na picha zilionyesha fundo lake la mguu wa kulia likiwa limevimba.

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Neymar aliondoa kiatu chake kuonyesha mguu wa kulia uliovimba vibaya baada kuondolewa uwanjanikaribu na mwisho wa mechi ambayo Brazil ilipata ushindi dhidi ya Serbia.

    Alielezea jeraha lake kama "moja ya nyakati ngumu zaidi katika kazi yangu ".

    "Nimejeruhiwa, ndio sio vizuri, itaniumiza lakini nina uhakika nitakuwa na fursa ya kurejea tena kwasababu nitafanya kila liwezekanalo kuisaidia nchi yangu, timu yangu na mimi mwenyewe."

  10. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo tarehe 26.11.2022