Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Urusi na Ukraine: Marekani yakadiria vifo vya wanajeshi 200,000 kwa pande zote

Jenerali wa ngazi ya juu wa Marekani anakadiria kwamba wanajeshi kati ya 100,000 na 100,000 wa Ukraine wameuawa au kujeruhiwa katika vita vya Ukraine.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Charlene Ruto: Mjadala watanda kenya kuhusu ufadhili wa mikutano ya mwana huyo wa Rais

    Yeye ni mtoto wa pili wa Rais William Ruto, na anajiita Binti wa Kwanza wa Kenya, lakini watumiaji wa mitandao ya kijamii wanauliza kwa nini Charlene Ruto anaonekana kukutana na mawaziri wengi wa serikali na kusafari nje.

    Miezi kadhaa tangu babake achaguliwe kuwa rais, vyombo vya habari vya humu nchini vinaripoti kuwa Bi Ruto amekutana na maafisa kadhaa wa kaunti kote nchini Kenya pamoja na mawaziri nje ya nchi.

    Wasiwasi kama huo ulizuka wakati Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipochaguliwa kwa mara ya kwanza na binti yake Ivanka alihudhuria mikutano na baba yake kama mshauri asiye rasmi. Bw Trump baadaye alimteua Ivanka katika jukumu rasmi la serikali.

    Mnamo Alhamisi, Charlene Ruto alisema kwenye Twitter kuwa amekutana na waziri wa vijana wa Morocco, Mohammed Mehdi, kwa "mazungumzo na kubadilishana mawazo ambayo yatasaidia sana katika kuunda miradi ya maendeleo ya vijana kwa mataifa yote mawili".

    Baadhi ya Wakenya sasa wanauliza, ni nani anayefadhili mikutano yote hii, na je ni mikutano rasmi ?

  2. Watumishi wa umma Afrika Kusini wagoma wakilalamikia mishahara midogo

    Mamia ya watumishi wa umma nchini Afrika Kusini wameanza mgomo wa nchi nzima wakilalamikia mishahara na mazingira ya kazi.

    Vyombo vya habari nchini humo vimeuelezea kuwa mgomo wa kwanza mkubwa wa watumishi wa umma katika kipindi cha muongo mmoja.

    Unatarajiwa kusababisha usumbufu katika baadhi ya idara za serikali na viwanja vya ndege. Wanachama wa Chama cha Watumishi wa Umma (PSA) kwa muda wa wiki kadhaa walifanya mgomo, lakini sasa wameamua kugoma katika miji yote mikubwa kote Afrika Kusini.

    Hatu hii imekuja baada ya kuvunjika kwa mazungumzo kati ya muungano wa vyama vya wafanyakazi na serikali. Muungano huo unashikilia kidete madai yake ya nyongeza ya 6% ya mishahara, na kukataa toleo la mwisho la serikali la 3%.

    Huduma kama vile utoaji wa pasipoti, vyeti vya kifo na leseni za udereva zitaathirika.

    Wakati huo huo mamlaka ya viwanja vya ndege imeonya kuwa hatua hiyo ya inaweza kusababisha ucheleweshaji wa udhibiti wa pasipoti na imeonya wasafiri kufika kwenye viwanja vya ndege angalau saa nne kabla ya muda wa kuondoka.

  3. Habari za hivi punde, Maeneo 12 yaliokaliwa na Urusi yakombolewa na jeshi la Ukraine – kamanda

    Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine Valery Zaluzhny alikataa kuthibitisha kwamba kweli jeshi la Urusi lilikuwa limeondoka Kherson. Wakati huo huo, kulingana na yeye, katika masaa 24 iliyopita pekee , makazi 12 yalirudishwa chini ya udhibiti wa Ukraine.

    "Madai ya kujiondoa kutoka kwa Kherson ni matokeo ya vitendo vyetu," Zaluzhny alisema. "Moja kwa moja katika mwelekeo wa Kherson, vikosi vya ulinzi vya Kiukreni viliharibu njia za vifaa, mfumo wa msaada, na mfumo wa udhibiti wa adui. Hivyo, hawakuwaachia adui nafasi badala yake akaamua kutoroka .”

    Wakati huo huo, Zaluzhny amesema kuwa sasa hawezi kudhibitisha au kukataa habari kuhusu kujiondoa kwa wanajeshi wa Urusi kutoka Kherson. Kulingana na yeye, Jeshi la Ukraine liliendeleza mashambulikzi kulingana na mipango

    Tangu Oktoba 1, kulingana na yeye Ukraine, imefikia kilomita 36.5 ndani ya maeneo yaliokaliwa na adui na kwamba jumla ya eneo wailokomboa linafikia mita za mraba 1381. km, huku udhibiti wa makazi 41 pia ukirejeshwa.

    Mamlaka ya Ukraine hadi sasa imejibu kwa kujizuia ikisema hadi sasa hawajaona dalili za kuondoka kwa wanajeshi na kwamba kundi la Urusi kwenye ukingo wa kulia lilikuwa limejenga mahandaki tayari kujilinda.

    Katika hali ya vita, BBC haiwezi kuthibitisha mara moja madai yaliyotolewa na maafisa wa kijeshi.

  4. ATCL kupunguza baadhi ya safari zake kwasababu za kiufundi

    Shirika la ndege Air Tanzania limesema kuwa litapunguza miruko na kufuta baadhi ya safari zao kulingana na idadi ya ndege zilizopo.

    Katika taarifa ya Shirika hilo, imeelezwa kuwa kutokana na changamoto za kiufundi kote duniani za injini aina ya PW1524G-3 zinazotumika katika ndege za Airbus A220-300 kumekuwa na uchaleweshaji wa ndege za shirika hilo wakati changamoto hiyo ikitafutiwa ufumbuzi.

    Mkurugezi wa Shirika la ndege, ATCL, Ladislaus Matindi akiongea na BBC amesema Shirika huu ni uamuzi wa muda mfupi ili kutoa muda kwa watengenezaji wa injini za ndege hizo kushughulikia matatizo yaliyopo.

    ''Injini si kuwa inatengenezwa ina makosa, kuna mengine yanakuja kutokea baada ya matumizi na hawa watengenezaji watawashauri

    Amesema kwa kawaida huwa injini zinatolewa kisha huletewa injini nyingine lakini kwa bahati mbaya mahitaji yamekuwa makubwa wamekuwa na ndege nyingi hawana uwezo huo wa kuleta injini kwa ajili ya kurekebisha kwa hiyo lazima zirudishwe kiwandani zikafanyiwe marekebisho.

    ''Faida tulizonazo sasa hivi kuendelea kufumbia macho hili jambo kutegemea leo tutafanya kazi kesho hatufanyi linaleta matatizo makubwa sana kwa abiria wetu... kwa hiyo ni lazima tuhakikishe kuwa hapa sasa hivi tuna uwezo huu kutokana na tatizo la hizi ndege, kwa hiyo basi tuwe na safari ambazo zinaendana na uwepo wa ndege zilizopo''.

    Amesema kwa shirika ni tatizo kwa kuwa wanapoteza mapato, lakini kwa abiria inakuwa vigumu kwao kuwa na uwanda mpana wa kuchagua safari kwa kuwa ratiba nazo zinakuwa zimepungua.

    Bado haijajulikana itatengamaa lini lakini Shirika hilo limesema kuwa halitakuwa tatizo la muda mrefu.

    ''Hatujajua bado, tunaendelea kuzungumza nao lakini nina uhakika halitakuwa tatizo la muda mrefu, ndege zetu zina rekodi nzuri sana kwahiyo tunaposema kuna tatizo, kuna tatizo dogo ambalo linatakiwa kushughulikiwa, lisiende likawa tatizo kubwa ambalo linaweza kuleta ajali, ndiyo maana yetu. Alisema Bw.Matindi.

  5. Mahakama yatupilia mbali kesi ya ufisadi dhidi ya Naibu Rais wa Kenya

    Mahakama ya Kenya imeruhusu ombi la upande wa mashtaka kuondoa kesi ya ufisadi ya shilingi bilioni 7.4 ($60m; £53m) dhidi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua na wengine tisa.

    Katika uamuzi huo, hakimu Victor Wakumile alikubali ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) lakini akawaonya washtakiwa kwamba wanaweza kukamatwa tena iwapo wapelelezi watapata ushahidi wa kuwashutumu.

    Ofisi ya DPP ilituma maombi ya kufuta kesi hiyo kwa sababu ya ukosefu wa ushahidi, na kuwalaumu wapelelezi wa polisi kwa kutokamilisha uchunguzi.

    Mwendesha mashtaka wa umma hivi karibuni amekosolewa kwa kuondoa kesi za ufisadi dhidi ya watu mashuhuri, wakiwemo mawaziri.

    Awali Naibu Rais alikuwa amekanusha mashtaka yaliyotolewa dhidi yake alipokuwa mbunge akisema kuwa yalichochewa kisiasa.

  6. Waasi wa DRC waua watu wawili na kuwateka nyara wengine 10

      • Author, Richard Kagoe
      • Nafasi, BBC News, Nairobi

    Watu wawili wameuawa na wengine 10 kutekwa nyara na wapiganaji wa Allied Democratic Forces katika eneo la Kabasha karibu na mji wa Beni kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Haya yanajiri baada ya mashambulizi ya anga yaliyofanywa na wanajeshi wa Congo yakilenga makundi ya wanamgambo katika maeneo ya Runyoni, Musangati, Chanzu na Bunagana katika eneo la mashariki lenye machafuko.

    Kuna ripoti kwamba vijiji kadhaa vilivyotekwa na waasi huko Rutshuru vimewaacha wakazi bila kupata chakula na huduma za dharura.

    Zaidi ya watu 90,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano mapya katika eneo hilo katika miezi michache iliyopita, kulingana na mashirika ya misaada.

    Serikali ya DR Congo imeishutumu nchi jirani ya Rwanda kwa kuunga mkono kundi la M23 kwa kuwapa msaada wa vifaa na kifedha.

    Rwanda imekanusha mara kwa mara madai hayo. Rais Félix Tshisekedi wiki iliyopita aliwataka vijana kuunda vikundi vya tahadhari na kujiunga na jeshi ili kulinda nchi dhidi ya uvamizi wa nje wa makundi yenye silaha.

  7. Habari za hivi punde, Nathan Jones: Southampton wamteua kocha wa Luton kama meneja mpya

    Klabu ya Southampton imethibitisha kumteua Nathan Jones kama meneja wao mpya baada ya kutimuliwa kwa Ralph Hasenhuttl.

    Mchezaji wa Wales Jones, 49, ameondoka kwenye klabu ya Championship ya Luton Town na kuchukua jukumu hilo kwa kandarasi ya miaka mitatu na nusu.

    Hasenhuttl, ambaye aliongoza kwa takriban miaka minne, alifutwa kazi siku ya Jumatatu baada ya kufungwa 4-1 na Newcastle siku ya Jumapili

    "Ninajivunia sana kupewa nafasi hii," alisema Jones.

  8. Ajali ya ndege Ziwa Viktoria: Uwanja wa ndege wa Tanzania wafunguliwa tena baada ya ajali

      • Author, Alfred Lasteck
      • Nafasi, BBC News, Dar es Salaam

    Uwanja wa ndege wa Bukoba kaskazini - magharibi mwa Tanzania umefunguliwa tena kufuatia ajali iliyosababisha vifo vya watu 19.

    Ndege hiyo ya abiria ilianguka katika Ziwa Victoria ilipokuwa ikijaribu kutua kwenye uwanja huo Jumapili.

    Afisa utawala katika mji huo ameiambia BBC kwamba ndege ya kwanza ya abiria inatarajiwa kutua kwenye uwanja wa Bukoba leo Alhamisi.

    Washauri wa kiufundi kutoka kwa watengenezaji wa ndege, ATR, wameanzisha uchunguzi kuhusu ajali hiyo.

    Wataalamu wa Ufaransa wa usalama wa safari za ndege pia wamepelekwa nchini humo.

    Ndege hiyo ilikuwa ni ya kampuni ya Precision Air - kampuni kubwa zaidi ya kibinafsi ya safari za ndege za abiria nchini Tanzania.

    Imekuwa ikiendesha safari zake kutoka Dare es salaam - Bukoba tangu mwaka 1994.

    Unaweza pia kusoma:

    • Ifahamu aina ya ndege iliohusika na ajali Tanzania
    • Waliopoteza maisha kwa ajali ya ndege Tanzania waagwa
    • 'Rubani aliwasha taa wakati tunaokoa watu tukaambiwa ndege inaweza kulipuka'- shuhuda
  9. Urusi na Ukraine: Marekani inakadiria vifo vya wanajeshi 200,000 kwa pande zote

    Jenerali wa ngazi ya juu wa Marekani anakadiria kwamba wanajeshi kati ya 100,000 na 100,000 wa Ukraine wameuawa au kujeruhiwa katika vita vya Ukraine.

    Jenerali Mark Milley, ambaye ni mwenyekiti wa muungani wa wakuu wa majeshi, pia amesema kuwa takriban raia 40,000 waliuawa baada ya kujipata katika mzozo.

    Makadirio hayo ni ya juu zaidi kutolewa na afisa mwingine wa magharibi.

    Lakini alisema dalili kwamba Ukraine ina utashi wa kurejea tena katika mazungumzo ilitoa "fursa" kwa ajili ya mazungumzo.

    Katika siku za hivi karibuni, Ukraine iliashiria utashi wa kufanya baadhi ya mazungumzo na Urusi, baada ya Rais Volodymyr Zelensky kuachana na shiniko la kutaka Vladimir Putin, aondolewe madarakani kabla ya kufufuliwa kwa mazungumzo.

    Lakini akizungumza mjini New York, Jenerali Milley aliongeza kwamba kwa mazunguzo kuwa ya mafanikio, nchi zote mbili Urusi na Ukraine zitatakiwa kufikia"utambuzi wa pande zote" kwamba ushindi wa vita" huenda usipatikane kwa njia za kijeshi, na kwa hiyo unahitaji kutumia mbinu nyingine".

    Jenerali huyo wa ngazi ya juu – ambaye anahudumu kama mshauri wa ngazi ya juu zaidi wa Rais Biden wa masuala ya kijeshi - alisema kiwango cha vifo na majeruhi kinaweza kuishawishi Urusi na Ukraine kwa pamoja kuhusu haja ya kufanya mazungumzo katika kipindi cha miezi ijayo ya majira ya baridi, wakati ambapo mapigano yanaweza kupungua kutokana na baridi kali.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  10. Tazama: Wafugaji wa Kenya wanavyouza mifugo wao kwa 'bei ya kutupa'

    Kila wiki siku ya Jumanne mjini Kimana viungani mwa mbuga ya wanyamapori ya Amboseli, wakati huu wa kiangazi umekuwa na changamoto sana kwa wafugaji wa mifugo kwani kuuza mifugo iliyodhoofika ni kama kukwea mlima.

    Video: @judith_wambare

  11. Félicien Kabuga: Mfungwa wa mauaji ya kimbari Rwanda amshutumu kwa kuhamasisha mauaji ya Watutsi

    Shahidi katika kesi ya Félicien Kabuga anayeshitakiwa kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda amemshutumu kwa kuhamasisha mauaji ya Watutsi.

    Shahidi huyo alitoa ushahidi wake kwa mahakama ya kimatafa ya jinai (ICC) ambako kesi ya Bw Kabuga inaendelea, kwa njia ya video kutoka kwenye kitengo cha mahakama ya Umoja wa Mataifa mjini Arusha.

    Jina na sauti yake vilibadilishwa ili kulinda utambulisho wake.

    Jumanne mawakili wa Bw kabuga walimhoji maswali shahidi - mengi ya maswali yaliulizwa faraghani ili kuepuka kutambulika kwa utambulisho wake.

    Shahidi huyo ambaye amefungwa kwa miaka baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kimbari, alisema kuwa alipewa mafunzo kama mwanamgambo wa Interahamwe (kundi lililotekeleza mauaji ya kimbari) mwaka 1993, akiwa pamoja na kundi lingine – na wote walikuwa ni wa jamii ya Wahutu.

    Shahidi huyo aliiambia mahakama ya The Heague kuwa alikutana na Bw Kabuga mara nne na kila mara Kabuga alikuwa akiwahamasisha kutoa msaada wa kununua silaha za kulisaidia jeshi katika vita vya kuwazuia watutsi kuchukua mamlaka ya nchi.

    Unaweza pia kusoma:

    • Félicien Kabuga: 'Huo wote ni uongo, sikumuua Mtutsi yeyote'
    • Felicien Kabuga: Mawakili wake wanataka mteja wao kushtakiwa the Hague na sio Tanzania
    • Mauaji ya Rwanda: Jinsi Felicien Kabuga alivyojificha kwa miaka 26
  12. Wananchi wa Liberia wazua hasira juu ya mpango wa siku tisa wa Kombe la Dunia wa rais George Weah

    Rais wa Liberia George Weah amelifahamisha baraza la seneti kuwa anapanga kukaa siku tisa nchini Qatar kutazama mechi za kombe la dunia .

    Bw Weah - mwanasoka wa zamani - aliondoka nchini wiki iliyopita kwa ziara kadhaa za kigeni, lakini sio mipango yake yote imefichuliwa.

    Mwanawe Timothy, ambaye ni Mmarekani, atakuwa katika kikosi cha Marekani katika mashindano ya Kombe la Dunia, yatakayong'oa nanga tarehe 20 Novemba.

    George Weah alichezea timu kubwa za Ulaya, zikiwemo AC Milan na Chelsea.

    Rais huyo mwenye umri wa miaka 56 alibadili kazi na kuchaguliwa kuwa rais wa Liberia mwaka wa 2017.

    Habari za mipango ya safari ya nje ya rais zimewakasirisha raia wengi wa Liberia, wengine wametumia vipindi vya kupiga simu kwenye redio na kwenye mitandao ya kijamii kumkosoa.

    Wanasema itakuwa ni kutotilia maanani hali ya wananchi kwa rais kwenda Qatar wakati ambapo watu wengi walikuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la chakula, pamoja na kutokuwa na uhakika kuhusu mwenendo wa sensa ya watu iliyocheleweshwa sana, ambayo Bw Weah aliiahirisha hivi majuzi kwa mara ya sita.

    Wafanyakazi wa Bw Weah - ambao hawajajibu maswali kuhusu gharama ya safari hiyo - wamejibu wakosoaji wake, wakisema ziara za nje za rais "zitazaa faida kubwa" kwa nchi.

  13. Tuzo ya amani ya Nobel ya rais wa zamani wa Afrika Kusini FW de Klerk iliibiwa

    Medali ya Tuzo ya Amani ya Nobeli yar ais wa zamani wa Afrika Kusini FW de Klerk iliibiwa kuoka nyumbani kwake mwezi Aprili, wakfu wake umeithibitishia BBC.

    Haukutoa maelezo zaidi, lakini vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuwa medali hiyo ilichukuliwa wakati wa wizi uliofanyika katika nyumba yake yamjini Cape Town.

    Bw De Klerk alishinda tuzo hiyo pamoja na Rais Nelson Mandela mwaka 1993 kwa juhudi zao za kumaliza mfumo wa ubaguzi wa rangi.

    Vyombo vya habari vya Afrika Kusini vimeripoti kuwa polisi hawajamkamata yeote kuhusiana na wizi huo wala kupata medali.

    Akizungumza na wavuti wa habari News24, mjane wa Bw de Klerk , Elita, alisema kuwa alirejea nyumbani kutoka safarini Ulaya akakuta sanduku la "liko karibu tupu".

    "Niligundua kuwa tulikuwa tumeibiwa mwezi Aprili mwaka huu. Tarehe 5 Aprili, nilikwenda kwenye sanduku na sanduku lilikuwa wazi. Nilikuwa nimerejea kutoka safari ya mng'ambo, kwahiyo ninakumbuka tarehe. Kwa bahati mbaya, sanduku lilikuwa karibu tupu ," alisema.

    "Vito vingi vilikuwa vimechukuliwa – ni vigumu kuelezea thamani yake kwani vile vilivyochukuliwa nilipewa kama zawadi zaidi ya miaka 50 iliyopita, katika nyakati mbali mbali, pia nilikuwa na kipuli nilichorithi kutoka kwa mama yangu," aliongeza.

    Alisema kuwa hana matumaini kwamba vitu vilivyoibiwa vitapatikana.

    Unaweza pia kusoma:

    • FW de Klerk: Rais wa mwisho mweupe wa Afrika Kusini
    • Je, FW de Klerk alikuwa shujaa aliyemaliza ubaguzi wa rangi au alipaswa kushtakiwa?
  14. Ufaransa: Kadinali Ricard ni miongoni mwa maaskofu 11 wanaoshutumiwa kuwanyanyasa watoto

    Kadinali Mfaransa Jean Pierre Ricard alitajwa na Kanisa katoliki kama mmoja wa Maaskofu 11 wanaowanyanyasa au waliowanyanyasa watoto.

    Katika taarifa aliyoitoa, Kadinali Jean Pierre Ricard alikiri kuwa alimnyanyasa kingono mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 alipokuwa padre wa parokia miaka 35 iliyopita, na kwa sasa anaweza kutoa siri hiyo.

    Mwaka mmoja uliopita jopo la uchunguzi lilitangaza kuwa kuna maelfu kwa maelfu ya watu waliowanyanyasa kingono watoto, katika Kanisa Katoliki nchini Ufaransa kwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita.

    Baadhi ya maaskofu hao 11 wanachunguzwa na mahakamani na kupewa adhabu na Kanisa Katoliki.

    Askofu mkuu wa Ufaransa Eric de Moulins-Beaufort aliwaambia waandishi wa habari kuwa miongoni mwa maaskofu hao ni pamoja na Askofu wa Creteil Michel Santier ambaye alistaafu mwaka jana ambaye anashutumiwa kwa unyanyasaji wa kingono miaka ishirini iliyopita.

    Unaweza pia kusoma:

    • Unyanyasaji kingono ndani ya kanisa katoliki watu waanza kufunguka
    • Kwa nini mnyanyasaji bado anafanya kazi kama kasisi?
    • Makasisi wa kikatoliki wafungwa jela kwa kuwanyanyasa watoto viziwi Argentina
  15. Diana Toebbe: Hukumu kali zaidi kwa mke wa jasusi aliyepatikana na hatia nchini Marekani

    Mhandisi wa zamani wa Jeshi la Wanamaji la Marekani na mkewe wamefungwa huko West Virginia kwa kujaribu kuuza siri za kijeshi kwa nchi ya kigeni ambayo haijatajwa.

    Jonathan Toebbe, 42, alikuwa amefanya kazi katika ofisi ya mkuu wa operesheni za wanamaji na alinaswa akitoa siri kuhusu manowari zinazotumia nyuklia.

    Alifungwa jela kwa miaka 18, huku mkewe Diana akipokea miaka 21 - hukumu kali zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

    Hakimu alipendekeza mke, 42, ndiye aliyekuwa akisimamia oparesheni hiyo

    Nyaraka za mahakama zilifichua kwamba mwalimu huyo wa zamani alikuwa mlinzi wa mumewe alipoacha habari kwenye katika maeneo ya siri mara moja akificha kadi ya data ndani ya mkate wa siagi .

    Awali waendesha mashtaka walikuwa wakitaka kifungo cha hadi miaka 17.5 kwa Toebbe na miaka mitatu kwa mke wake. Lakini msimu huu wa joto, Jaji wa Marekani Gina Groh alisema alizingatia miongozo hiyo haitoshi.

    "Pengine ni Bi Toebbe ambaye alikuwa akiendesha shughuli nzima," hakimu alisema. "Alikuwa sehemu ya njama hiyo."

    "Madhara kwa taifa hili ni makubwa, na hizi ni nyakati za kutisha tunazoishi," hakimu alisema katika kikao cha hukumu huko Martinsburg.

    Jaji Groh pia alieleza kukerwa na tabia ya mke huyo ambaye alinaswa akipitisha barua kwa mumewe huku wote wawili wakiwa mahabusu akimtaka kufuata mpango wao na kumuondolea lawama.

    "Alitaka [mumewe] aseme uongo," hakimu alisema

  16. Uchaguzi wa Marekani : Udhibiti wa bunge dogo wachukuliwa na Republicans, kuna mchuano kwa ajili ya Senate

    Nchini Marekani, uchaguzi wa nusu muhula umefanyika, ambapo Bunge la wawakili na theluthi ya maseneta wanachaguliwa upya pamoja na magavana wa majimbo muhimu na wabunge.

    Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea, na hatma ya makumi kadhaa makumi kadhaa ya viti vya bunge la Congress itatoa mwelekeo kuhusu ni majimbo gani yanapaswa kuangaziwa zaidi na ni kwanini.

    Hesabu za awali zimethibitisha ubashiri wa kampuni ya televisheni ya CBS nchini humo, kituo washirika na BBC, kwamba udhibiti wa bunge la wawakilishi utachukuliwa na Warepublican. Kwa sasa, mabunge yote ya Congress yanadhibitiwa na chama cha Rais Joe Biden cha Democrats.

    Rais wa Marekani binafsi tayari ameashiria kwamba yupo "wazi kwa mapendekezo yote mazuri" na yuko tayari kufanya kazi na Warepublican walio wengi katika Bunge la wawakilishi na Seneti, lakini hataunga mkono miswada yoyote anayoamini kuwa itawaumiza wafanyakazi, mkiwemo kupunguza kodi kwa matajiri.

    Unaweza pia kusoma:

    • Uchaguzi wa Marekani : Warepublican wana matumaini ya ushindi katika Bunge la Wawakilishi
    • Uchaguzi Marekani 2018: Uchaguzi wa katikati ya muhula ni kama kura ya maoni kuhusu Donald Trump
  17. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 10.11.2022