Habari za hivi punde, Mzozo wa Ukraine: Urusi yaamua kuwaondoa wanajeshi wake mjini Kherson
Urusi imeamua kuondoka Kherson - Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu ametoa amri ya kufanya mbele ya kamera za runinga ya taifa la Urus.
Kamanda wa jeshi la Urusi nchini Ukraine, Jenerali Sergei Surovikin, akiripoti kwa Sergei Shoigu mbele ya kamera za runinga ya Urusi kuhusu hali ilivyo katika mstari wa mbele, alisema kuwa chini ya hali ya sasa, Kherson na makazi ya jirani "hayawezi kusambaziwa zana kikamilifu ili jeshi kuendelea na kazi," na kwa hivyo jeshi linajitolea kuchukua ulinzi kwenye ukingo wa kushoto wa Mto Dnieper (Kherson ipo upande wa kulia).
"Ninaelewa kuwa huu ni uamuzi mgumu sana, wakati huo huo tutahifadhi kitu muhimu - maisha ya wanajeshi, "Surovikin alisema, akiongeza kuwa askari waliopo katika upande wa kulia wa ukingo wa mto huo wataondolewa katika siku za usoni.
Shoigu alijibu: "Nakubali. Endelea na uondoaji wa askari."