Binti wa mshirika wa Putin auawa katika shambulio la Moscow

Inadhaniwa babake, mwanafalsafa wa Kirusi Alexander Dugin ambaye anajulikana kama "Ubongo wa Putin," huenda ndiye aliyelengwa na shambulio hilo.

Moja kwa moja

  1. Tunakomea hapo hadi kesho kwaheri.

  2. Uvamizi wa hoteli Somalia: Kwa nini ilichukuwa muda mrefu?

    The attack on Hayat hotel

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kama tulivyokuarifu hapo awali zaidi ya 20 waliuawa katika shambulio la al-Shabab dhidi ya Hoteli ya Hayat nchini Somalia.

    Mchambuzi wa masuala ya usalama wa Somalia Ahmed Kaboole, ambaye, ameambia BBC Idhaa ya Kisomali kwamba kundi lililoshambulia hoteli hiyo huenda lilichunguza eneo hilo kwa muda kabla ya kutekeleza mashambulizi hayo.

    "Muda uliochukuliwa na majeshi ya serikali kukomesha uvamizi huo unaashiria kuwa kundi lililoingia kwenye hoteli hiyo lilikuwa limejipanga vyema au huenda kuna uwezekano tayari lilikuwa limemeingiza vilipuzi ndani ya jengo la hoteli," alisema.

    "Walikuwa wakifanya kazi na wakazi wa eneo hilo au watu wa ngazi za chini waliokuwa pale kwa sababu hawakuweza kupata mahali pa kujificha kutokana na milio ya risasi ya jeshi, ambayo sauti yake ilisikika mjini."

    Aliongeza kuwa kulingana na eneo la hoteli hiyo, ilikuwa rahisi kwa watu wengi kuingia humo bila kupitia vizuizi vya usalama.

    "Eneo la Hayat liko nje kidogo ya eneo la udhibiti wa uwanja wa ndege. Liko wazi kwa jiji zima. Ilikuwa rahisi kwa watu kuingia na kuifikia jengo hilo kwa miguu bila kupitia sehemu zilizo na vizuizi vya usalama."

    Hoteli hiyo iliharibiwa vibaya baada ya vikosi vya usalama kukabilia vikali na wavamizi ho Ijumaa na Jumamosi usiku, huku picha zikionyesha moto na moshi ukifuka kwenye paa la hoteli hiyo.

    “Makundi haya huwa yanatafuta mwanya wa kuvuruga jamii iwe maeneo ya biashara au mikusanyiko wanatafuta mwanya wa kuwanyanyasa wananchi walipata fursa hiyo mahali hapo kwa sababu serikali ilikuwa katika kipindi cha mpito,” alisema Bw Ahmed Kaboole.

  3. Mwendesha mashtaka wa kimataifa arejea Sudan kuhusu Darfur

    Karim Khan first went to Sudan in August 2021

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa jinai (ICC)y uko nchini Sudan kwa ziara ya tatu kama hiyo tangu mwaka 2019.

    Mara ya kwanza ilikuwa mwaka mmoja uliopita, wakati mmiliki wa ofisi ya sasa Karim Khan alipofanya mazungumzo kuhusu hati bora za kukamatwa kwa uhalifu uliofanywa wakati wa vita huko Darfur mwaka 2003.

    Mmoja wa wanaosakwa ni Rais wa zamani Omar al-Bashir, ambaye alitimuliwa madarakani miaka mitatu iliyopita na kuzuiliwa mjini Khartoum.

    Anatafutwa kwa mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

    Sudan imekuwa ikikabiliwa na machafuko makubwa baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka jana.

  4. 377A: Singapore kuondoa marufuku ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja

    Kila mwaka makumi ya maelfu ya watu huhudhuria mkutano wa haki za LGBT wa Pink Dot nchini Singapore

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Singapore inatarajiwa kubatilisha sheria inayopiga marufuku ngono ya wapenzi wa jinsia moja.

    Uamuzi huo uliotangazwa na Waziri Mkuu Lee Hsien Loong kwenye televisheni ya taifa, unakuja baada ya miaka mingi ya mjadala mkali.

    Jimbo la jiji linajulikana kwa maadili yake ya kihafidhina, lakini idadi ya watu wanaotaka sheria hiyo ya enzi ya ukoloni ya 377A ikomeshwe imeendelea kuongezeka.

    Singapore ni nchi ya hivi punde zaidi barani Asia kuzingatia haki za wapenzi wa jinsia moja baada ya India, Taiwan na Thailand.

    Msimamo wa awali wa serikali ulikuwa ni kudumisha sheia ya 377A lakini pia iliahidi kutotekeleza sheria hiyo, kama njia ya kutuliza pande zote mbili.

    Lakini usiku wa Jumapili saa za huko, Bw Lee alisema watakomesha sheria hiyo kwani "Ninaamini hili ni jambo sahihi kufanya, na jambo ambalo wananchi wengi wa Singapore watakubali," alisema.

    Alibainisha kuwa "wapenzi wa jinsia moja sasa wanakubalika katika jamii" na kufuta sheria ya 377A kutaleta uwiano wa sheria za nchi kulingana na "maadili ya sasa ya kijamii, na ninatumai italeta ahueni kwa wapenzi wa jinsia moja wa wa Singapore".

    Lakini pia alisema serikali itahakikisha ulinzi bora wa kisheria kwa tafsiri ya ndoa kuwa moja kati ya mwanaume na mwanamke.

    Hii itafanya iwe vigumu kwa ndoa za wapenzi wa jinsia moja kuhalalishwa.

    Alisema Singapore inasalia kuwa jamii ya kitamaduni yenye watu wengi wanaopenda kudumisha kanuni za familia na kijamii.

    Singapore ilirithi sheria 377A kutoka kwa Waingereza na ikachagua kuihifadhi baada ya uhuru mnamo 1965.

    Ingawa sheria kitaalam inaharamisha ngono kati ya wapenzi wa jinsia moja inaonekana kama marufuku dhidi ya watu walio kwenye uhusiano wa jinsia moja.

    Soma:

  5. Maharashtra: Msichana aliyepotea na kupatikana baada ya miaka tisa asimulia masaibu

    Msichana

    Chanzo cha picha, BBC NA POLISI MUMBAI

    Baada ya takriban miaka tisa, Pooja Gaud mwenye umri wa miaka 16 hatimaye anaweza kuegemeza kichwa chake kwenye mapaja ya mama yake.

    Pooja alitoweka tarehe 22 Januari 2013 alipokuwa na umri wa miaka saba.

    Anasema alichukuliwa kutoka nje ya shule yake katika jiji la Mumbai katika jimbo la magharibi mwa India la Maharashtra na wanandoa ambao walimvutia kwa ice-cream.

    Tarehe 4 Agosti, alipatikana katika kile kinachoelezwa kama "kutoroka kwa kimiujiza".

    Mama yake, Poonam Gaud, anasema anamshukuru Mungu kwa furaha.

    "Nilikuwa nimekata tamaa ya kumpata binti yangu. Lakini miungu imekuwa yenye fadhili kwangu," anasema.

    Polisi wamedai kuwa mtoto huyo alitekwa nyara na Harry D'Souza na mkewe, Soni D'Souza, kwa sababu wapenzi hao hawakuwa na mtoto wao. Wamemkamata Bw D'Souza.

    Kabla ya kutoweka, Pooja aliishi na kaka zake wawili na wazazi katika nyumba ndogo katika eneo la makazi duni.

    Siku ambayo alipotea, alikuwa ametoka kwenda shule na kaka yake mkubwa, lakini wawili hao walikosana ndipo kaka yake alimuacha na kuingia shuleni kwani alikuwa anaelekea kuchelewa.

    Hapo ndipo wanandoa hao inadaiwa walimchukua na kuahidi kumnunulia ice-cream.

    Pooja anasema kwamba wanandoa hao hapo awali walimpeleka Goa na kisha Karnataka, majimbo ya magharibi na kusini mwa India, na kutishia kumuumiza ikiwa angelia au kupiga nayowe.

    Tangu Pooja arejee nyumbani, majirani zake wamekuwa wakiingia kumlaki

    Chanzo cha picha, COURTESY OF RAFIQ

    Anasema aliruhusiwa kuhudhuria shule kwa muda mfupi, lakini baada ya wenzi hao kupata mtoto wao wenyewe, alitolewa shuleni na wote wakahamia Mumbai.

    Pooja anasema unyanyasaji huo ulizidi baada ya mtoto kuzaliwa. "Walikuwa wakinipiga kwa mkanda, kunipiga teke, kunipiga ngumi.

    Wakati mmoja walinipiga vibaya sana hadi mgongo wangu ukaaanza kutokwa na damu.

    Pia nililazimishwa kufanya kazi za nyumbani kwa saa 12 hadi 24 katika mazingira magumu."

    Nyumba aliyokuwa akiishi D'Souza ilikuwa karibu kabisa na familia yake - lakini, anasema, hakuwa na ufahamu wa barabara, alikuwa akitazamwa kila mara na hakuwa na pesa wala simu, na hakuweza kutafuta msaada au kujaribu kumtafuta. njia ya nyumbani.

    Lakini siku moja, Pooja alifanikiwa kushika simu ya wanandoa hao walipokuwa wamelala na kuandika jina lake kwenye YouTube.

    Alipata video na mabango yanayotaja utekaji nyara wake na nambari ambazo angeweza kupiga ili kupata usaidizi.

    “Hapo ndipo nilipoamua kutafuta msaada na kutoroka,” anasema.

    Lakini ilimchukua miezi saba kabla ya kupata ujasiri wa kutosha kuijadili na Pramila Devendra, 35, msaidizi wa nyumbani ambaye alifanya kazi katika nyumba moja ambapo Pooja alifanya kazi kama mlezi wa watoto.

  6. Kyiv yakanusha kuhusika na mauaji ya binti wa Dugin

    Eneo la tukio

    Chanzo cha picha, Sledcom RF / TASS

    Ofisi ya Rais wa Ukraine imeangazia mlipuko wa gari uliotokea usiku wa kuamkia jana katika mkoa wa Moscow, ambapo binti wa mwanafalsafa wa Urusi, mwana itikadi wa "ulimwengu wa Urusi" Alexander Dugin aliuawa.

    "Ninasisitiza kwamba Ukraine, haina uhusiano wowote na hili, kwa sababu sisi sio taifa la uhalifu kama Urusi linaloendeshwa chini ya serikali ya kigaidi," Mikhail Podolyak, mshauri wa Mkuu wa Ofisi ya Rais, alisema katika kituotelethon ya kitaifa.

    Kwa maoni yake, mauaji haya yanashuhudia mapambano ya madaraka na ushawishi wa makundi mbalimbali ndani ya Urusi.

    Kulingana na ripoti zingine, mlengwa wa shambulio hilo labda alikuwa Dugin mwenyewe, ambaye waliamua kutumia gari lingine dakika za mwisho badala ya kuandamana na binti yake.

  7. Binti wa mshirika wa Putin auawa katika shambulio la Moscow

    Alexander Dugin anasifiwa kwa kuunda mtazamo wa ulimwengu wa Rais Vladimir Putin
    Maelezo ya picha, Alexander Dugin anasifiwa kwa kuunda mtazamo wa ulimwengu wa Rais Vladimir Putin

    Binti ya mshirika wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin ameuawa katika mlipuko unaoshukiwa kuwa kwenye gari.

    Darya Dugina alikufa baada ya mlipuko kwenye barabara nje ya Moscow, kamati ya uchunguzi ya Urusi ilisema.

    Inadhaniwa babake, mwanafalsafa wa Kirusi Alexander Dugin ambaye anajulikana kama "Ubongo wa Putin," huenda ndiye aliyelengwa na shambulio hilo.

    Bw Dugin ni mwana itikadi mashuhuri wa uzalendo na anaaminika kuwa karibu na rais wa Urusi.

    Alexander Dugin na binti yake walikuwa wakihudhuria tamasha katika shamba moja karibu na Moscow, ambapo mwanafalsafa huyo alitoa hotuba.

    Tamasha la "Utamaduni" linajielezea tukio hilo kama la familia kwa wapenzi wa sanaa na hufanyika katika shamba la Zakharovo ambapo mshairi wa Kirusi Alexander Pushkin aliwahi kuishi.

    Binti wa Dugina

    Chanzo cha picha, Mitandao ya Kijamii

    Wawili hao walipaswa kurejea kutoka lwa tamasha hilo Jumamosi jioni kwa gari moja kabla ya Bw Dugin kuripotiwa kufanya uamuzi dakika za mwisho kusafiri tofauti na bintiye.

    Picha ambazo hazijathibitishwa zilizochapishwa kwenye mtandao wa Telegram zinaonekana kumwonyesha Bw Dugin akitazama kwa mshtuko wakati huduma za dharura zikifika katika eneo la tukio.

    BBC haijaweza kuthibitisha video hiyo.

    Wachunguzi walithibitisha kuwa Bi Dugina alifariki katika eneo la tukio karibu na kijiji cha Bolshiye Vyazemy.

    Unaweza pia kusoma

  8. Hujambo na karibu.